Mkuu uko sahihi kabisa. Hilo linawezekana kama wataamua kufanya hivyo.Hamna cha kulalamika. Huu ni wakati wa CHADEMA kufanya fund raising, ili kufungua kituo chetu cha habari.
La sivyo, unyanyasaji huu utaendelea. And its advantage kwa CCM. Hata wakifanya maovu hakuna mtu atayejua. Either wachache walioshuhudia hilo jambo
Taarifa ya TBC1 kuhusu kukatwa mapanga na mashoka kwa Mbunge wa Ilemela na yule wa Ukerewe imetuacha na maswali mengi. Tukio hilo ni kubwa na la aina yake kutokea katika nchi hii tokea tupate uhuru. Inakuwaje TV ya taifa waripoti swala hili kama tukio la kawaida lisilo na uzito wowote katika jamii? Au kwa vile ni wabunge waupinzani? Nchi inayojitapa kuwa ya amani na utulivu na wabunge wanapigwa mapanga na mashoka tunaenda wapi? Hoja jee kituo cha TV cha taifa kinapo dharau jambo kama hili maana yake nini katika mustakabali wa Taifa?
Sifa kubwa ya wafuasi wa CHADEMA ni kulalamika hata pasipo na sababu ya kulalamika! Hivi ingekuwa wewe ndio muhisika pale TBC1, unge-include nini ili ionekane umeipa uzito habari hiyo?! Ukiangalia, taarifa za tukio lile limechukua takribani tatu.....Highness Kiwia amehojiwa na wala hakukatizwa alichotaka kuongea! Zitto Kabwe amehojiwa na ameyasema aliyokusia kuyasema bila kukatizwa. RPC nae amehojiwa na amesema bila kukatizwa! Wametoa picha za pale Bugando Hospital hadi Muhimbili! Nini cha ziada ambacho ungependa kionekane kwenye taarifa hiyo?! Ulitaka kuwe na live coverage?!
Mkuu bila ya kujali itikadi za chama, hivi inaingia akili kweli kwamba Mbunge anaweza akakatwa MAPANGA na Serikali yetu tukufu ikaona hilo ni jambo la kawaida KWELI? Mimi sikuwahi kuangalia TBC kwa hiyo siwezi kutoa maoni katika hilo.
Mimi nataka kulikumbusha jeshi la POLISI kwamba mambo ya RWANDA yalianza kidogo kidogo mwishowe likaja kuwa janga la kitaifa, Watanzania tusije kujidanganya kwamba hili aliwezi kutokea HAPA, tukumbuke hatuishi kwenye kisiwa.