Serikali yatishia kulifungia gazeti la Mwananchi

Wakizuwia gazeti la mwananchi litatokea linginelo na kueleza wananchi ukweli wa mambo!
Mabadiliko ya mienendo yao ndio itakayobadilisha uandishi, na si kutumia makaripio!
 
Mwananchi ndio gazeti linaloongoza kwa kuwa balanced and fair.

Sasa serikali yetu baada ya kuona mwananchi wamekataa kuvaa majacket ya CCM press na kupelekeshwa kama magazeti mengine (jina kapuni) linaamua kutafuta visingizio ili kulipunguzia makali, Mimi ni mwanahabari mzuri tu na nakuhakikishia hawawezi kulifungia kwa sababu hawana ground yoyote wnakurupuka tumwananchi sio kijigazeti kinachoamka tu na kuanza kutunga tunga habari ili kiuzwe.

Mwananchi ni gazeti makini lenye waandishi makini wenye elimu ya kutosha! Kwa mfano rafiki yangu Kagashe, Mgalula, lugongo, Mkinga ,Poyo, Kimboy si watu wa elimu ya uchochoroni pamoja na degree zao bado walipelekwa Nairobi kupata mafunzo kwa mwaka mzima unaweza kuona ni jinsi gani chombo hichi ni makini . Naona baada ya kushindwa kutimiza majukumu yao na kuona joto la uchaguzi liko juu wanaanza kutafuta wa kulaumu leo naona wametoa tena tishio kwa Tamwa.

Kwa mara nyingine tena nawapongeza Mwananchi kama gazeti pekee lisilo na kuegemea upande wote nawapenda sana. Walinza na HakiElimu wakawashindwa kisha wakaja na Policy forrum sasa Tamwa na Mwananchi hawa jamaa vipi? Nashukuru sana Jamaa (Rostam) kishauza Share zako zote aende huko huko mtanzania na RAI.

Mtanishagaza sana kama mtatishiwa nyau na hawa bwana wadogo hongera Mhariri kwa quick response
 
Nilijua tu CCm itaanza kutumia mabavu kupitia serikali na ni DALILI ZA KUOGOPA KUSHINDWA. Kuandika habari hasi dhidi ya CCM na serikali yake eti ndiyo sababu ya kulifungia gazeti!!! Hawana habari au hawaoni jinsi magazeti yao -- Uhuru, Mzalendo, D. News na yale yanayomilikiwa/yanayofadhiliwa na wahindi wanne mafisadi kama vile Mtanzania, Rai, Sauti ya Umma, Tazama, Changamoto yanavyowatukana wapinzani hasa Chadema. Kweli Mkuki kwa Nguruwe.
 
Al Hudaaa Oyeeeeeee!!! Kazi ipo mwaka huu, ukiona mkuwa anastuka na kuanza kukimbia bila sababu,ujue kuna jambo....
 
Watafungia gazeti hawawezi kufungia mawazo

kabisa hawa serikali n wapuuzi sana sana,,na wataishia na mikwara hiyohiyo..naona mkuchika kaona tripu hii awatumie watu mpuuzi kwelikweli yule baba,,alifungie aone
 
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, achilia mbali ya ujio wa vyama vingi, CCM imeanza ku-PANIC!!! HA HA HA!!!! Hii kali kweli kweli!! Magazeti yanayotishiwa kufungiwa Mwananchi na Mwanahalisi ndiyo magazeti pekee yenye kuchapisha nakala nyingi kuliko yote, ukiachia yale ya akina Shigongo (ya udaku).

Mengineyo mengi hasa yale yanayoitetea CCM na ufisadi wake hakuna mtu anayeyataka, hubakia kupauka kwenye meza za mauzo na huishia kuuzwa kwa kilo kwa ajili ya kufungia mandazi.

C-mon CCM. Be a man as you claim to be. Pingana na hoja za magazeti hayo kwa hoja, siyo kwa vitisho. Tatizo lako CCM ni kwamba sera yako unayoonyesha ya kuwatetea mafisadi imekwama kwenye matope kwa sababu inawanufaisha wachache tu. Ondokana na wahindi hao, wanakupoteza bure na kutaka kuleta vurugu nchini.
 
You can fool the people for sometime but you cant fool all the people all the time.awake tanzania the time is now and not no more sleep.
 
Kweli linaleta uchochezi, Very GOOD serikali imeliona

itakuwa vizuri kulifungia

Ina maana wewe ndiye Hokororo/Mshana nini? Mbona unarudia makosa yale yale ya kusema gazeti linaleta uchochezi bila kueleza ni habari ipi hasa inayoleta huo uchochezi. Hebu tuwekee hapa hiyo habari tuione basi!!!!! La sivyo, ni bora ukakaa kimya!!!

Tiba
 
Kweli Serikali ya JK na CCM wamechanganyikiwa.

Mimi ni msomaji nambari wani wa MWANANCHI na gazeti lake dada linalotolewa kwa Kiingereza,The Citizen.
Hawa CCM na JK wake hawataki chombo cha habari kinachoandika habari za UKWELI kuhusu CCM na serikali yake.
Ndiyo maana wameshindwa kuainisha ni habari zipi za UCHOCHEZI zilizoandikwa na MWANANCHI. Hawawezi na hawataweza kutaja hata habari moja yenye kuichafua CCM au JK wake! Wenyewe wanaona aibu na ndiyo maana wameshindwa kutamka. Ni aibu saana kwa JK na CCM yake. Hii ni sawa na kumpeleka mtu mahakamani wakti hana hatia! Ni upuuzi na ujinga ambao haukubaliki hata kidogo.

Hizi chokochoko hazianja leo.Walianza kwa kumshusha kwenye gari la msafara wa Kampeni za CCM mwandishi wa gazeti la MWANANCHI huko Kagera kwa kisingizio kuwa haiandiki vizuri CCM kwenye kampeni zake. Kwa hiyo sasa ndiyo wameamua kuweka mambo hadharani.

LAKINI CCM NA SERIKALI YAO WASIFIKIRI KUWA SISI WATANZANIA NI MAJUHA TUSIOJUA MBELE WALA NYUMA,TUSIOJUA HABARI ZA KWELI NA ZA UONGO,TUSIOJUA MAANA YA MAENDELEO NA UMASKINI.

HEBU KWANZA WATUELEZE GAZETI LA SERIKALI LINALOTOLEWA KWA LUGHA YA KIINGEREZA,THE DAILY NEWS(NOISE) LINALOTOLEWA KILA SIKU LIMECHUKULIWA HATUA GANI BAADA YA KUANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI KUHUSU MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHADEMA DR.WILBROAD PETER SLAA KUWA KASISI AU PADRI HUYU HATAINGIA IKULU HATA AKIFANYA NINI NA WAKAENDA MBALI ZAIDI KWA KUSEMA KUWA WANACHOANDIKA NI UHAKIKA NA VYOMBO VYA HABARI VIWANUKUU HIVO!!!


Sasa mchochezi hapa ni nani kati ya MWANANCHI na THE DAILY NOISE??????????????????????????????????

Ninawaomba SERIKALI na CCM wakome kabisa kutuona sisi wananchi ni wajinga tusiojua nini kinachoendelea kwenye nji hii.
 
CCM sumu ya uhuru wa vyombo vya habari,si wange quote habari moja ya kichochezi
 
Wanataka tusome magazeti ya Uhuru,mzalendo,daily news na Habari leo bila kusahau Mtanzania!Hapo ndiyo watajisikia raha mstarehe!Hawataki kukosolewa,kazi kwelikweli!
 
Serikali inafanya mambo yakitoto na aibu kabisa. wa nini isilifungie gazeti lake la D. News kwa kutaka kuleta uchochezi wa dhahiri? Ni lazima CCM ipigane kiume -- hoja kwa hoja, na siyo kukimbilia kuokota jiwe. Hivi habari zinazoandikwa na magazeti tunayoyasoma yakiwaponda akina Dr Slaa na hata kuingilia masuala yake binafsi, siyo habari hasi kwake? Kwa nini serikali inatafsiri neno 'hasi' kwa habari dhidi yake tu?

Kwanza wao (serikali) ni nani? Sasa hivi s imekuwa ni genge la mafisadi tu linalofadhiliwa na wahindi wachache? Watanzania wangapi wasiolijua hilo?
 
You can fool the people for sometime but you cant fool all the people all the time.awake tanzania the time is now and not no more sleep.

As the massage refers to all Tanzanian but its directly to Government mean the CCM the ruling party.

Khaaa hawa jamaa yaani hawapendi kukosolewa kama kilicho andikwa na ndicho mricho bolonga msiambiwe haya basi jitawaleni nyie wenyewe basi khaa kwani mwataka kutuambia nyie mko Perfect machoni pa binadamu wote?

Hizo chochezi mzidaizo zimetokana na hao viongozi kuvurunda sasa wanaanza walaumu magazeti khaa

 
hakuna haja ya kuchekeana kama serikali yao inavyofanya, ametoa shutuma aseme! na afungie kabisa gazeti hilo.

Serikali itoe ufafanuzi kwamba Gazeti la Mwananchi katika toleo lipi liliandika taarifa hasi, vilevile Gazeti la HabariLeo nalo kama limeandika taarifa hasi dhidi ya wagombea wengine nako lifungiwe! Isije ikawa mkuki kwa nguruwe...........!
 
Wanataka tusome magazeti ya Uhuru,mzalendo,daily news na Habari leo bila kusahau Mtanzania!Hapo ndiyo watajisikia raha mstarehe!Hawataki kukosolewa,kazi kwelikweli!
 
Hawa Mwananchi waombee Dr. Slaa ashinde; uhuru wao kwenye habari hautadumu hata mwaka mmoja.

JK amevipa vyombo vya uhabari uhuru mkubwa sana na inabidi walitambue hilo.
 
Kwa mara nya kwanza katika historia ya nchi hii, achilia mbali ya ujio wa vyama vingi, CCM imeanza ku-PANIC!!! HA HA HA!!!! Hii kali kweli kweli!! Magazeti yanayotishiwa kufungiwa Mwananchi na Mwanahalisi ndiyo magazeti pekee yenye kuchapisha nakala nyingi kuliko yote, ukiachia yale ya akina Shigongo (ya udaku).

Mengineyo mengi hasa yale yanayoitetea CCM na ufisadi wake hakuna mtu anayeyataka, hubakia kupauka kwenye meza za mauzo na huishia kuuzwa kwa kilo kwa ajili ya kufungia mandazi.

C-mon CCM. Be a man as you claim to be. Pingana na hoja za magazeti hayo kwa hoja, siyo kwa vitisho. Tatizo lako CCM ni kwamba sera yako unayoonyesha ya kuwatetea mafisadi imekwama kwenye matope kwa sababu inawanufaisha wachache tu. Ondokana na wahindi hao, wanakupoteza bure na kutaka kuleta vurugu nchini.

Imebidi nikugongee senksi ndugu yanu. Kweli katika hii final straight CCM imeanza ku-panic, tena ile mbaya -- na tutayaona mengi tu bado. CCM ni chama kisichojua ushindani wa halali na haki, inapenda kuwaburuza tu wananchi, na ndo maana wahudhuriaji wa mikutano yao husombwa kwenye malori kama kondoo -- kwa kuogoipa kukuosa watu!!

Eti uchochezi!!! Uchochezi gani huo? Tayari wameshakaa kimahakama na kuamua hivyo? Hawa watu nawachukia kweli kweli mie!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom