Gazeti la Mwananchi liombe radhi Serikali na walimu Tanzania

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Katika toleo la leo tarehe 4 Januari 2024 gazeti kubwa nchini Tanzania limeibua hoja ya wizi wa mitihani unaondeshwa na kusimamiwa na Baraza la mitihani Tanzania

Hili gazeti kwa taarifa hii wamechafua serikali na taasisi zake zinazosimamia ufanyikaji wa mitihani Tanzania na ikumbukwe elimu ndo injini namba moja Tanzania na Taifa lingine katika kuendesha mambo ya kitaalamu

Madhara yake ni nini kwa kashifa hii kwa Taifa

1, Wataalamu waliopo Tanzania ni wa kubumba( hawana vigezo bali kwa wizi wa mitihani) kwa habari hii nchi za nje wanaweza kudharau Wataalamu kutoka Tanzania

2,Wananchi wataanza kupoteza imani na serikali iliyopo madarakani kwa kutosimamia mitihani ipasavyo na matokeo yake ni mapinduzi kwa serikali iliyopo madarakani

3,Walimu wataonekana wanakula mishahara bure kwamba hawafundishi badala yake wanasubiri kuiba mitihani ili wanafunzi wafaulu

4,Kwamba Wataalamu wetu hawataaminika kwa kile wanachokifanya, kwamba si Wataalamu bali ni utaalamu wa wizi wa mitihani (Wataalamu fake)

Kwa matinki hiyo hili gazeti lilipaswa kufanya yafuatayo

Mtihani ni siri kwa Taifa na ndicho kipimo cha kupata Wataalamu katika Taifa hivyo Mwananchi angeandika waraka wa Siri kwa mamlaka husika ili kukamata mtandao huo na wangekuja na kichwa cha habari "Jinsi Mwananchi alivyosaidia kukamata mtandao unaochafua Baraza la mitihani"

Kwa mantiki hii naomba gazeti hili lifute hiyo habari mtandaoni na kuomba radhi wananchi, serikali na walimu
1704353527907.jpg
 
Ukweli ukiandikwa mnataka ukanushwe, inawezekana bosi huyu wa NECTA ni legelege, wezi wa mitihani wanajiibia watakavyo. Ndalichako alidhibiti vikali wizi wa mitihani na alijua wapi i
 
Ukweli ukiandikwa mnataka ukanushwe, inawezekana bosi huyu wa NECTA ni legelege, wezi wa mitihani wanajiibia watakavyo. Ndalichako alidhibiti vikali wizi wa mitihani na alijua wapi i
Si kwamba ni NECTA tu ndo wasimamizi wa mitihani kuna idara zingine kama TAKUKURU NA TISS
 
Katika toleo la leo tarehe 4 Januari 2024 gazeti kubwa nchini Tanzania limeibua hoja ya wizi wa mitihani unaondeshwa na kusimamiwa na Baraza la mitihani Tanzania

Hili gazeti kwa taarifa hii wamechafua serikali na taasisi zake zinazosimamia ufanyikaji wa mitihani Tanzania na ikumbukwe elimu ndo injini namba moja Tanzania na Taifa lingine katika kuendesha mambo ya kitaalamu

Madhara yake ni nini kwa kashifa hii kwa Taifa

1, Wataalamu waliopo Tanzania ni wa kubumba( hawana vigezo bali kwa wizi wa mitihani) kwa habari hii nchi za nje wanaweza kudharau Wataalamu kutoka Tanzania

2,Wananchi wataanza kupoteza imani na serikali iliyopo madarakani kwa kutosimamia mitihani ipasavyo na matokeo yake ni mapinduzi kwa serikali iliyopo madarakani

3,Walimu wataonekana wanakula mishahara bure kwamba hawafundishi badala yake wanasubiri kuiba mitihani ili wanafunzi wafaulu

4,Kwamba Wataalamu wetu hawataaminika kwa kile wanachokifanya, kwamba si Wataalamu bali ni utaalamu wa wizi wa mitihani (Wataalamu fake)

Kwa matinki hiyo hili gazeti lilipaswa kufanya yafuatayo

Mtihani ni siri kwa Taifa na ndicho kipimo cha kupata Wataalamu katika Taifa hivyo Mwananchi angeandika waraka wa Siri kwa mamlaka husika ili kukamata mtandao huo na wangekuja na kichwa cha habari "Jinsi Mwananchi alivyosaidia kukamata mtandao unaochafua Baraza la mitihani"

Kwa mantiki hii naomba gazeti hili lifute hiyo habari mtandaoni na kuomba radhi wananchi, serikali na walimu View attachment 2861542
Wewe mwizi wa mitihani tulia tunajua kila kitu
 
Hilo gazeti liombe radhi kwa kosa lipi wakati mwalimu ndio kafichua. Yaani huyo aliyefichua anaisaidia serikali na watumishi wake (NECTA) wajirekebishe.
Uliyesema gazeti liombe radhi ni chawa na pia wewe ni zao la wizi wa mitihani.
 
Duh mkuu mimi nimwalimu,kukaata uwepo wa tatizo hakufanyi tatizo hilo kutokuwepo,mimi ni mwalimu nimesimamia mitihani ya taifa mara kadhaa,ila hatari na wizi wa mitihani kwa asilimia 80 uko shule za msingi

Huko shule za msingi ukisema wewe sio muumini wa kuvujisha mitihani utashambuliwa sana,mwaka jana nikiwa nawalimu wenzangu tikisuhiri kupelekwa kwenye vituo vya kusimamia iliibuka hoja hii ya wizi wa mitihani,nilipinga sana kuhusu kuwapa watoto majibu,nilichokiona mimi nilionekana kituko ikabidi kunyamaza.Nilipofika kituoni siku ya kwanza mwalimu mkuu akawa anajichekesha chekesha,sura yangu huwa inaogopesha kidogo kwa mtu akiniona at first sight,mwalimu mkuu hakuniambia kitu.

Siku ya pili ikabidi aniambie kuwa nimsaidie kupitisha vibomu darasani ili watoto wake wafaulu nikakataa,akasema basi niwasaidie mimi mwenyewe nikakubali nikamwambia sawa,kilichomkuta hatosadiki,darasa la watoto 25 waliofaulu ni 7 tu kwa wastani wa C na ndo watakaoenda sekondari.

Nadhani hii hojan ni kweli,mimi napambana nayo sana ,na ili kuwa sehemu salama nimeamua kutojihusisha na usimamimizi wa hii mitihani iki kutoharibu kibarua changu kwani watu wengi wanaamini katika wizi .

Niukweli usiopingika kuwa mitihani inaibwa sana huku,sio haja yakukanusha bali baraza lijipange kukomesha hali hii.
 
Back
Top Bottom