Serikali yatishia kulifungia gazeti la Mwananchi

magazeti yanayoongoza kwa uchochezi wa kidini huku vikiutukuza serikali ni;
  • uhuru
  • mzalendo
  • rai
  • habari leo
na hasa gazeti la rai limekuwa likiongoza kwa kuhamasisha;
  • ukabila
  • dini
  • rangi
hasa likielekeza mashambulizi yake kwa chadema; hata hivyo serikali imekaa kimya.
 
Hicho kijarida cha mwananchi ni cha kipuuzi kinataka kuleta machafuko kama walivofanya kule kwao kenya,washindwe na walegee wana mapepo hao mwananchi.Hata kikifutwa hakitakuwa na impact yoyote kwani kijarida cha nje ya nchi ni sawa na kutumbukiza kijiko cha sukari katika bahari ya hindi.Wafutiliwe mbali hao mavuvuzela,hawana sera zaidi ya uchonganishi na uzushi kama mgombea wanaomshabikia aliyeshindwa kabla ya upigaji wa kura ,ni yule mwenye sura ya kisomali na anayeongea kama amekula chura,aliyeanguka bafuni akip...............
we ma....... yako! $%%$$#@@##$$$##@##$# zako!
 
Tafadhali fuatilia habari hii;
Mwandishi Wetu
SERIKALI imetishia kulifunga au kulifutia usajili gazeti la Mwananchi kwa madai kwamba linaandika habari za uchochezi dhidi ya serikali ya awamu ya nne.Barua ya serikali yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/76 iliyoandikwa kwa mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, inaonya kwamba kama gazeti hili litaendelea kuandika habari ambazo imeziita za uchochezi dhidi yake, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hata hivyo, barua hiyo haijaweka bayana habari hizo ilizozielezea kuwa ni za mtazamo hasi dhidi ya serikali na ambazo imedai kuwa ni za uchochezi.

“Kwa barua hii unatakiwa kuacha mara moja tabia ya kuandika habari za uchochezi na kuidhalilisha nchi na serikali kwa kisingizio cha uhuru wa habari na uhuru wa kutoa mawazo ulioanishwa katika katiba ya nchi yetu," inaeleza barua hiyo ya Oktoba 11 iliyosainiwa na Raphael Hokororo kwa niaba ya Msajili wa Magazeti.

"Aidha ukiendeleza tabia hiyo, serikali haitasita kuchukua hatua stahiki za kulifungia gazeti lako au kulifutia usajili kwa mujibu wa sheria za nchi.”

Barua hiyo, ambayo imebeba kichwa cha habari kisemacho "Karipio kali kwa kuandika habari zenye mwelekeo wa uchochezi wa kudhalilisha", ni mwendelezo wa barua nyingine iliyoandikwa na mkurugenzi wa Idara ya Habari, Clement Mshana kwenda kwa mhariri wa gazeti hili Septemba 24, 2010.

Katika barua hiyo ya Mshana, serikali imedai kuwa gazeti la Mwananchi limekuwa na mtazamo hasi dhidi ya serikali na ikamtaka mhariri ajieleze.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/70, bila ya kutoa mifano, inadai kuwa Mwananchi imekuwa ikiandika habari hasi tu kana kwamba serikali haina zuri linalofanywa kwa wananchi wake na kutaka maelezo.

“Katika kipindi kirefu sasa, na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Habari hizo zimekuwa zikidhalilisha serikali iliyo madarakani ya awamu nne,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Katika majibu ya barua hiyo ya kwanza, Mwananchi Communications Ltd (MCL), ilieleza kuwa baada ya kutafakari kwa kina ilishindwa kuelewa msingi wa tuhuma hizo ambazo hazina mifano yoyote ya habari inayodaiwa kuwa ni hasi kwa serikali.

“Baada ya kupitia barua yako na kuitafakari, imetuwia vigumu kuelewa msingi wa tuhuma zako kwa gazeti hili kuhusu mtazamo hasi dhidi ya serikali bila hata kutoa mifano ya habari ambazo zinabeba tuhuma zako kwa gazeti hili hasa unaposema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi,” inasema barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCL/RN/09/VOL.1.27 iliyoandikwa na mhariri mtendaji wa MCL, Theophil Makunga.

Barua hiyo ya MCL inaeleza kuwa kimsingi habari za kampeni za uchaguzi katika kipindi hiki zinahusu vyama vya siasa na kuhoji sababu za serikali kujiona inaandikwa vibaya na Mwananchi wakati ni vyama ndivyo vinavyoshiriki kwenye kampeni.

Mhariri wa Mwananchi anaeleza katika barua hiyo kuwa kwa sasa gazeti lake linaandika habari za wagombea uongozi kutoka vyama mbalimbali na sera zao ili wananchi wafanye uamuzi siku ya kupiga kura na hakuna chama kilichoandika barua ya malalamiko.

“Kwa taarifa yako tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi Agosti 21, 2010, gazeti la Mwananchi halijawahi kupata malalamiko kutoka chama chochote cha siasa kinachoshiriki katika kampeni hizo juu ya kuandikwa vibaya. Kimsingi Mwananchi linachofanya ni kuripoti wanachosema wagombea wa vyama mbalimbali au kufanyiwa katika mikutano ya kampeni,” inasema barua hiyo ya MCL kwenda kwa Msajili wa Magazeti.

Katika barua hiyo, MCL inaiomba serikali kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kuhusika kwa serikali katika kampeni za uchaguzi hadi gazeti hili lionekane lina mtazamo hasi.

“Kwa msingi huo, tunaomba ufafanuzi zaidi hapa; serikali inahusika vipi katika kampeni mpaka Mwananchi ionekane ina mtazamo hasi kwa serikali wakati vinavyoshiriki katika kampeni ni vyama vya siasa na wagombea wake,” inasema barua hiyo.

Baada ya barua hiyo, Msajili wa Magazeti alijibu kwamba majibu yaliyotolewa na MCL hayaridhishi na hivyo ofisi yake haikuridhika na utetezi huo.

“Kama tulivyoeleza kwenye barua yetu kwako kuwa katika kipindi kirefu sasa na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Gazeti lako sasa limeamua kufanya ‘house style’ yake ya kuandika habari zenye uchochezi na kudhalilisha nchi na serikali iliyopo madarakani,” inasema barua hiyo.

Katika onyo lake, serikali inasema kwamba picha, habari zinazopewa kipaumbele katika ukurasa wa kwanza wa gazeti zinatiwa chumvi kwa lengo la kuchochea wananchi waione serikali yao haijafanya chochote kwa maendeleo yao.

Akiongelea hatua hiyo ya serikali, Makunga alisema kwamba MCL imeshtushwa na karipio hilo ambalo halikuonyesha ni habari ipi ambayo gazeti la Mwananchi limekosea.

“Msajili hakunukuu hata sheria moja ya vyombo vya habari kuonyesha jinsi gani gazeti limekosea wala habari au kichwa cha habari chenye mtazamo hasi kwa serikali,” alisema Makunga.

Alisema Mwananchi imechukulia hatua hiyo ya msajili kuwa inatishia uhuru wa vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi ambacho kinahitaji uvumulivu baina ya taasisi mbalimbali katika jamii.

Makunga alisema kwa kuwa Mwananchi na msajili inaonekana kutokubaliana katika suala hilo, wameamua kupeleka taarifa Baraza la Habari Tanzania (MCT) liweze kufanya uchunguzi kwa mujibu wa katiba yao.

Alisema msimamo wa sera ya uhariri ya MCL inasimamia kwenye ukweli na weledi pasipo kushurutishwa na vikundi vyovyote vya nje na ndani.Makunga alisema Mwananchi itaendelea kuandika habari za ukweli bila ya kumuonea mtu au taasisi yoyote kwa maslahi ya Tanzania.

Hii thread imeshawekwa humu JF, hivyo bora uiondoe
 
Acha kukurupuka wewe

huyo JK wa ukweli sijui ana nini kichwani mwake, yaaani watu wanafuata mkumbo kama bendera ifuatavyo upepo hata kama wewe niccm fanya reasoning hata kidogo, Hata mimi hapa kipindi Kikwete anaingia madarakani nilikuwa na imani nae sana, tumemshauri hasikiiiiii, tumetoa maoni hasikiiii, sasa unategemea nini?
 
Serikali sasa yatishia kulifuta Mwananchi
Wednesday, 20 October 2010 07:52
0
digg

Send to a friend Wednesday, 20 October 2010 07:52 0diggsdigg

bmwana.jpg
Mwandishi Wetu
SERIKALI imetishia kulifunga au kulifutia usajili gazeti la Mwananchi kwa madai kwamba linaandika habari za uchochezi dhidi ya serikali ya awamu ya nne.Barua ya serikali yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/76 iliyoandikwa kwa mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, inaonya kwamba kama gazeti hili litaendelea kuandika habari ambazo imeziita za uchochezi dhidi yake, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hata hivyo, barua hiyo haijaweka bayana habari hizo ilizozielezea kuwa ni za mtazamo hasi dhidi ya serikali na ambazo imedai kuwa ni za uchochezi.

"Kwa barua hii unatakiwa kuacha mara moja tabia ya kuandika habari za uchochezi na kuidhalilisha nchi na serikali kwa kisingizio cha uhuru wa habari na uhuru wa kutoa mawazo ulioanishwa katika katiba ya nchi yetu," inaeleza barua hiyo ya Oktoba 11 iliyosainiwa na Raphael Hokororo kwa niaba ya Msajili wa Magazeti.

"Aidha ukiendeleza tabia hiyo, serikali haitasita kuchukua hatua stahiki za kulifungia gazeti lako au kulifutia usajili kwa mujibu wa sheria za nchi."
Barua hiyo, ambayo imebeba kichwa cha habari kisemacho "Karipio kali kwa kuandika habari zenye mwelekeo wa uchochezi wa kudhalilisha", ni mwendelezo wa barua nyingine iliyoandikwa na mkurugenzi wa Idara ya Habari, Clement Mshana kwenda kwa mhariri wa gazeti hili Septemba 24, 2010.
Katika barua hiyo ya Mshana, serikali imedai kuwa gazeti la Mwananchi limekuwa na mtazamo hasi dhidi ya serikali na ikamtaka mhariri ajieleze.
Barua hiyo yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/70, bila ya kutoa mifano, inadai kuwa Mwananchi imekuwa ikiandika habari hasi tu kana kwamba serikali haina zuri linalofanywa kwa wananchi wake na kutaka maelezo.
"Katika kipindi kirefu sasa, na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Habari hizo zimekuwa zikidhalilisha serikali iliyo madarakani ya awamu nne," inasema sehemu ya barua hiyo.
Katika majibu ya barua hiyo ya kwanza, Mwananchi Communications Ltd (MCL), ilieleza kuwa baada ya kutafakari kwa kina ilishindwa kuelewa msingi wa tuhuma hizo ambazo hazina mifano yoyote ya habari inayodaiwa kuwa ni hasi kwa serikali.
"Baada ya kupitia barua yako na kuitafakari, imetuwia vigumu kuelewa msingi wa tuhuma zako kwa gazeti hili kuhusu mtazamo hasi dhidi ya serikali bila hata kutoa mifano ya habari ambazo zinabeba tuhuma zako kwa gazeti hili hasa unaposema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi," inasema barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCL/RN/09/VOL.1.27 iliyoandikwa na mhariri mtendaji wa MCL, Theophil Makunga.
Barua hiyo ya MCL inaeleza kuwa kimsingi habari za kampeni za uchaguzi katika kipindi hiki zinahusu vyama vya siasa na kuhoji sababu za serikali kujiona inaandikwa vibaya na Mwananchi wakati ni vyama ndivyo vinavyoshiriki kwenye kampeni.
Mhariri wa Mwananchi anaeleza katika barua hiyo kuwa kwa sasa gazeti lake linaandika habari za wagombea uongozi kutoka vyama mbalimbali na sera zao ili wananchi wafanye uamuzi siku ya kupiga kura na hakuna chama kilichoandika barua ya malalamiko.
"Kwa taarifa yako tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi Agosti 21, 2010, gazeti la Mwananchi halijawahi kupata malalamiko kutoka chama chochote cha siasa kinachoshiriki katika kampeni hizo juu ya kuandikwa vibaya. Kimsingi Mwananchi linachofanya ni kuripoti wanachosema wagombea wa vyama mbalimbali au kufanyiwa katika mikutano ya kampeni," inasema barua hiyo ya MCL kwenda kwa Msajili wa Magazeti.
Katika barua hiyo, MCL inaiomba serikali kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kuhusika kwa serikali katika kampeni za uchaguzi hadi gazeti hili lionekane lina mtazamo hasi.
"Kwa msingi huo, tunaomba ufafanuzi zaidi hapa; serikali inahusika vipi katika kampeni mpaka Mwananchi ionekane ina mtazamo hasi kwa serikali wakati vinavyoshiriki katika kampeni ni vyama vya siasa na wagombea wake," inasema barua hiyo.
Baada ya barua hiyo, Msajili wa Magazeti alijibu kwamba majibu yaliyotolewa na MCL hayaridhishi na hivyo ofisi yake haikuridhika na utetezi huo.
"Kama tulivyoeleza kwenye barua yetu kwako kuwa katika kipindi kirefu sasa na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Gazeti lako sasa limeamua kufanya ‘house style' yake ya kuandika habari zenye uchochezi na kudhalilisha nchi na serikali iliyopo madarakani," inasema barua hiyo.
Katika onyo lake, serikali inasema kwamba picha, habari zinazopewa kipaumbele katika ukurasa wa kwanza wa gazeti zinatiwa chumvi kwa lengo la kuchochea wananchi waione serikali yao haijafanya chochote kwa maendeleo yao.
Akiongelea hatua hiyo ya serikali, Makunga alisema kwamba MCL imeshtushwa na karipio hilo ambalo halikuonyesha ni habari ipi ambayo gazeti la Mwananchi limekosea.
"Msajili hakunukuu hata sheria moja ya vyombo vya habari kuonyesha jinsi gani gazeti limekosea wala habari au kichwa cha habari chenye mtazamo hasi kwa serikali," alisema Makunga.
Alisema Mwananchi imechukulia hatua hiyo ya msajili kuwa inatishia uhuru wa vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi ambacho kinahitaji uvumulivu baina ya taasisi mbalimbali katika jamii.

Makunga alisema kwa kuwa Mwananchi na msajili inaonekana kutokubaliana katika suala hilo, wameamua kupeleka taarifa Baraza la Habari Tanzania (MCT) liweze kufanya uchunguzi kwa mujibu wa katiba yao.

Alisema msimamo wa sera ya uhariri ya MCL inasimamia kwenye ukweli na weledi pasipo kushurutishwa na vikundi vyovyote vya nje na ndani.Makunga alisema Mwananchi itaendelea kuandika habari za ukweli bila ya kumuonea mtu au taasisi yoyote kwa maslahi ya Tanzania.
 
Hicho kijarida cha mwananchi ni cha kipuuzi kinataka kuleta machafuko kama walivofanya kule kwao kenya,washindwe na walegee wana mapepo hao mwananchi.Hata kikifutwa hakitakuwa na impact yoyote kwani kijarida cha nje ya nchi ni sawa na kutumbukiza kijiko cha sukari katika bahari ya hindi.Wafutiliwe mbali hao mavuvuzela,hawana sera zaidi ya uchonganishi na uzushi kama mgombea wanaomshabikia aliyeshindwa kabla ya upigaji wa kura ,ni yule mwenye sura ya kisomali na anayeongea kama amekula chura,aliyeanguka bafuni akip...............

Utabaki kuwa mbea tu....nani kakwambia hicho ni kijarida..FYI ni gazeti linaloongoza kwa daily circulation zaid ya hata UHURU+DAILY NEWS+MTANZANIA combined....na si la wakenya...ni la Agha Khan kama humjiui
 
Tatizo ni kwamba hiyo idara ya habari au MAELEZO inaongozwa na vilaza ambao ni waoga na hawajiamini. Hawa wakitishwa na CCM kidogo tu wanaanza kuhangaika ovyo na kutishia kuyafungia magazeti. Ukweli ni kwamba CCM ina wasiwasi sana na magazeti yanayowaeleza wananchi ukweli wa mambo kwani wanajua wakierevuka watafanya maamuzi sahihi Oktoba 31, ndio maana wanahaha kuhakikisha kwamba wanayaziba mdomo magazeti kama Mwananchi na Mwanahalisi.
Nimependa majibu ya Mhariri Mtendaji wa Mwananchi kwa Msajili wa Magazeti (Maelezo) alipotaka ufafanuzi kwamba serikali inahusika vipi katika kampeni mpaka gazeti la Mwananchi lionekane lina mtazamo hasi kwa serikali wakati vinavyoshiriki katika kampeni ni vyama vya siasa na wagombea wake?
Mimi nadhani akina January Makamba na Kinana walienda kuwatisha hawa vilaza wa Maelezo ili watoe vitisho kwa magazeti haya. Inabidi hawa wakurugenzi wa maelezo wajiuzulu mara moja kwa ujinga huu waliouonyesha.
Kama hawa Maelezo wangekuwa wanajua kazi yao wangeanza kulifungia DAILY NEWS kwa kuandika ile tahariri ya kipumbavu kuhusu Dr Slaa, halafu wangelifungia gazeti la MTANZANIA kwa kuandika taarifa za uchochezi kwamba kuna kiongozi katishia kumwaga damu, na magazeti mengine ya kidini(majina yake nimeyasahau kwa sababu huwa siyasomi - Sijui AL HUDA au kitu kama hicho) yanayowagawa Watanzania kwa misingi ya kidini.
 
Asante mkuu habari yako niyapili nasiho breaking news namuomba mod aunganishe hii story.
 
Hii yanikiumbusha kitabu cha marehemu Seith Chachage kiitwacho "Makuadi wa soko huria" kuna pahala hadithi zake zafanana na hii, hii ni dalili ya mfa maji, magazeti yanayoandika uchochezi wanayajua wanayaacha wanarukia yanayoandika ukweli!!!! huu ni undumilakuwili wa ajabu sana, mi nilidhani labda leo ni April Fool kumbe ni Oktoba!!

wengi waliokuwa undecided voters nadhani sasa wanaweza kuchambua pumba na mchele kwa haya yanayoendela na hivyo kufanya maamuzi sahihi, si ajabu pia wale waliokuwa washaamua kupiga kura kwa mazoea sasa wanaona mwanga na kubadili maamuzi yao kabla ya Oktoba 31,

Najiuliza hali itakuwaje hadi tarehe hiyo ya uchaguzi, nahisi arufu kama hautafanyika siku hiyo, kuna kaarufu fulani nakahisi, sina hakika nako,
but as they say "ONLY TIME WILL TELL"
 
Habari ndiyo hiyo

Kwa mtazamo wa huyu mtu aliyeandika hii barua inaelekea ameshinikizwa na nguvu fulani kwani hizi barua mbili hazina vielelezo vya kutosha ni vipi Mwananchi inachochea vurugu. Kama ingelikuwa inachochea vurugu ni akina nani wamelalamikia? Kama wamelalamika je mwananchi imechukua hatua gani? Kama hawakuchukua hatua (mwananchi) je serikali imechukua hatua gani dhidi yao? Hizi barua zimekaa kibabe zaidi kama bwana maguvu anapomtishia kimbaumbau (Betina na zena kama umesoma sani wakati ule!!!) kwamba ukileta mchezo nitakutandika pasina kueleza kwanini unataka kunitandika? Binafsi hizi siasa za kibabe na kidikteta na pia naziona na ni moja ya kampeni za CCM kuwabadilisha mawazo wananchi kwani ufisadi unawaumiza kiasi kwamba kila wanapoenda wanajikuta hawana la kujibu sasa ili kuwabadilisha mawazo wanacreate distraction kama unafatilia matukio wameanza na kashfa za Dr Slaa, wakaja na suala la udini, sasa wanakuja na sensitization of media ili wananchi wasahau ufisadi but mie ni mmoja kati ya ambao sitadanganyika na hilo!!!!
 
Huku ni kutapa tapa kweli kweli! Tatizo la msajili ni kwamba ni biased ile mbaya. Mbona magazeti kama Al-Hudda yanaandika habari za uchochezi kabisa tena kiasi cha kuweza kuleta hatari katika Taifa hatujasikia wanakaripiwa hata kidogo? Mwananchi inatoa habari jinsi zilivyo hata kama ni mbaya kwa CCM au chama kingine.
 
Hata hivyo kuna haja ya Serikali kuwa wazi ni mada ipi yenye mtazamo hasi iliyoandikwa na gazeti hili, ndipo haki itendeke.
 
Hicho kijarida cha mwananchi ni cha kipuuzi kinataka kuleta machafuko kama walivofanya kule kwao kenya,washindwe na walegee wana mapepo hao mwananchi.Hata kikifutwa hakitakuwa na impact yoyote kwani kijarida cha nje ya nchi ni sawa na kutumbukiza kijiko cha sukari katika bahari ya hindi.Wafutiliwe mbali hao mavuvuzela,hawana sera zaidi ya uchonganishi na uzushi kama mgombea wanaomshabikia aliyeshindwa kabla ya upigaji wa kura ,ni yule mwenye sura ya kisomali na anayeongea kama amekula chura,aliyeanguka bafuni akip...............

Tayari mmeanza!!!!! Unataka na gazeti litangaze sera zake?. Kweli mmepauka kimawazo hadi mabango mkatengeneze nje ya nchi ili muonekane kung'aa! Sera gani hizo?

HAPA PATAMU KWELI

“Katika kipindi kirefu sasa, na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Habari hizo zimekuwa zikidhalilisha serikali iliyo madarakani ya awamu nne,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Katika majibu ya barua hiyo ya kwanza, Mwananchi Communications Ltd (MCL), ilieleza kuwa baada ya kutafakari kwa kina ilishindwa kuelewa msingi wa tuhuma hizo ambazo hazina mifano yoyote ya habari inayodaiwa kuwa ni hasi kwa serikali.

“Baada ya kupitia barua yako na kuitafakari, imetuwia vigumu kuelewa msingi wa tuhuma zako kwa gazeti hili kuhusu mtazamo hasi dhidi ya serikali bila hata kutoa mifano ya habari ambazo zinabeba tuhuma zako kwa gazeti hili hasa unaposema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi,” inasema barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCL/RN/09/VOL.1.27 iliyoandikwa na mhariri mtendaji wa MCL, Theophil Makunga

Chama twawala bwana! VOTE FOR DR. SLAA

Kwa CCM na serikali habari za uchochezi ni kuandika "UKWELI"Hii inadhihilisha ni kiasi gani CCM mambo sio swali>Na hiyo aliotoa onyo inaonekana ametoa kauli zake kwa shinikizo la CCM na serikali.Kwani kauli yake haina uthibitisho nia ya jumla ,hii inaonesha ya kwamba amefuata maneno ya viongozi wa CCM na hakutaka kufanya uchunguzi,na hata kama atafanya uchunguzi hatapata uthibitisho kwa madai hayo.Anadai ya kua gazeti linaandika habari hasi!Kama hakuna habari chanya wazipike?kamazilvyojaribu kufanya baadhi ya taasisi katika kura ya maoni?Gazeti la WANANCHI ni gazeti pekee litolewalo kila siku linalotoa habari zilizo balanced na zilizo andikwa kwa umakini.CCM na serikali chukuweni habari zinazoandikwa na MWANANCHI kama kioo nazinaweza kuwasaidia kujirekebisha na kutofanya makosa.MAWANANCHI KIOO CHA JAMII MSITISHIKE TUKO NYUMA YENU MUNGU IBARIKI TANZANIA/
Huyu Mhariri wa MWANANCHI yuko sahihi kabisa, Serikali ieleze ni habari ipi ilikuwa hasi na inayoleta uchochezi badala ya kuelezea jumla jumla! Gazeti la MWANANCHI msiogope chochote endeleeni na kutujulisha habari kama zilivyo! After all mimi sioni zuri lililofanywa na Serikali ya awamu ya nne ambalo linastahili kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti, hata la udaku!
 
mh ujue serikali yetu haipendi watu waujue ukweli wa mambo ndio mana gazeti lolote linalosema ukweli lazima lifungiwe au lipewe vitisho.kama wanafanya vitu vizuri kwa nini waogope na kutishia vyombo vya habari?
 
Serikali ifungie kwanza magazeti ya UHURU, MTANZANIA, DAILY NEWS na HABARI LEO maana ndiyo magazeti ambayo bila kificho yanavidhalilisha vyama vya kisiasa. Hivi habari iliyoandikwa na DAILY NEWS tena kwenye ukurasa wa mbele kwamba Dr. Slaa kamwe hawezi kuwa rais wa Tanzania ingekuwa imeandikwa na gazeti la MWANANCHI ingekuwaje?

Ama kweli mwaka huu, sisi m itashika matawi yote lakini mwisho wake ndiyo umefika. Lazima chama hiki kiondoke.
 
Sasa maji ya shingo yako wapi? ni nani yuko kwenye hayo maji ya shingo wasomaji au wachapishaji gazeti? tuwe makini jamani na hizi titles
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom