Serikali yapewa nafasi ya mwisho kesi vigogo wa bandari

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa nafasi ya mwisho kwa Serikali kabla ya kutoa uamuzi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande na wenzake watano.

Hatua hiyo inatokana kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2022 kutoendelea katika hatua nyingine, licha ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika, huku jalada halisi ya kesi hiyo likielezwa kuwa lipo Dodoma, makao makuu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS).

Mbali na Kipande, washtakiwa wengine ni Peter Gawile (58) aliyekuwa Ofisa Rasilimali Watu wa TPA na mkazi wa Mianzini na Casmily Lujegi (65) aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi wa TPA.

Wengine ni Mashaka Kisanta (59) Mkurugenzi wa Idara ya Ununuzi, Kilian Chale (51) na Andrew John.

Katika keis ya msingi, wa washtakiwa wandaiwa kati ya Oktoba Mosi, 2014 na Oktoba Mosi 2020 Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa la kuisababishia TPA hasara ya Sh4.2 bilioni.

Leo Julai 11, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemarila ametoa ahirisho la mwisho, baada ya kukubaliana na maombi ya mawakili wa upande wa utetezi walioomba Serikali ipewe siku 30 ili wakamilishe kulifanyia kazi jalada hilo.

"Kesi hii imefikishwa mwaka mmoja sasa tangu washtakiwa walipofikishwa mahakamani hapa, bila kuendelea na hatua nyingine, hivyo natoa ahirisho la mwisho leo," amesema hakimu Rugemalira na kisha kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 3, 2023 itakapoitwa kwa ajili ya kitajwa.

Awali mawakili wa Serikali, Mosia Kaima na Glory Kilawi, wamedai kuwa shauri hilo liliitwa kwa ajili ya kutajwa na jalada halisi lipo Dodoma na bado hawajawasilisha nyaraka muhimu Mahakama Kuu.

Kaima baada ya kueleza hayo, upande wa utetezi ulidai kuwa Serikali ndio inatakiwa kutoa taarifa wamefikia wapi kuhusiana na kesi hiyo.

Akijibu hoja hiyo, Mosia amedai kuwa taarifa aliyopewa na kiongozi wake ndio hiyo amewasilisha mahakamani hapo.

Kutokana na hali hiyo, mawakili hao wa utetezi wakiongozwa na Fabian Mruge, Peter Kibatala na Kilian Mutasa, wameomba Mahakama iwapa mwezi mmoja upande wa mashtaka ili tarehe ijayo waje na majibu kuhusiana na kesi hiyo.

"Mheshimiwa hakimu, tuwape muda wa mwezi mmoja ili waje na majibu maana ameshasema hana jalada halisi la kesi hii na amesema jalada lipo Dodoma, tuwape huo muda ili tarehe ijayo waje watupe majibu wamefikia wapi," amesema Wakili Mruge.

Hakimu Rugemalira baada ya kusiliza hoja za pande zote mbili, amekubalina na upande wa utetezi na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 3, 2023 itakapotajwa.

MWANANCHI
 
Wasitutoe kwenye mstari

Wahaini ni wale waliouza bandari kwa vipande vya pesa kwa waarabu

Hizi case zingine zisubiri tu

Rudisheni Bandari za Tanganyika
 
Ila kwa wizi majina hayo hamjambo.

Huwa wanapiga kubwa kubwa tu ila kuleni tu mtaziacha na dhambi juu
 
Back
Top Bottom