Jaji atishia kutoa hati ya kuwakamata vigogo wawili wa ardhi Dar walioidharau Mahakama

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Jaji Mahakama kuu divisheni ya Ardhi jaji Hemedi ametoa onyo kali na kutishia hati ya kuwakamata washtakiwa wawili ambao ni Joanita Kazinja pamoja na Hadija Kalulu kwa kosa la kudharau amri ya mahakama

Hatua hiyo imekuja baada ya washtakiwa kutokufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yao msingi ya kubadilisha hati kinyune na utaratibu kwa Mfanyabiashara maarufu Matunda

Hata hivyo wakili wa Kamishna wa ardhi Dar es Salaama kupitia kwa wakili wake aliomba huruma yake mahakama kupitia jaji kwamba atawaleta tarehe itakayopangwa

Pamoja na hayo kamishna anadaiwa kuendelea kukiuka na kuzuia (SEARCH) ya kujua nani ni mmiliki halali wa eneo hilo licha ya Matunda kuwa ameshalipia lakini hadi hivi sasa hawajapewa

Katika hatua nyingine Pingamizi lililokuwa limewekwa upande wa Mwanasheria wa serikali kwamba kesi imefunguliwa kimakosa na nakutaka mwanasheria mkuu wa serikali aongezwe mahakamani jaji amesema hajaona kishawishi kinachofanya pingamizi hilo kukubaliwa nakuamua kulitupilia mbali

Ikumbukwe kuwa kesi inayowakaili Anita Kazinja na Hadija Malulu ni kesi ya kudharau amri ya mahakama iliyotolewa Tarehe 24.10.2023 ya kuzuia tilte namba isifanyiwe kitu chochote lakini inadaiwa walikiuka nakufyatua hati nyingine 7.11.2023 baada ya amri hiyo

Jaji huyo aliahirisha kesi hiyo hadi April 15 2024 nakutaka kamishna wa Ardhi kufika mahakamani au kuwa na mwakilishi nakusema wasipofika atatoa hati ya kuwakamata washtakiwa hao
IMG-20240313-WA0019.jpg
 
Ofisi ya kamishna wa Ardhi msaidizi wa daslam inahusika kwenye kutoa hati juu ya hati.

Hakuna raia mwenye uwezo wa kupata hatimiliki ,ofisi ya kamishna wa Ardhi msaidizi Kanda husika na msajili isipohusika.

Hilo ni deal la ndani, la watumishi wa ofisi za Ardhi Daslam,ndomana hata hao kina joanita na mariam wanadharau wito wa hakimu.

Wizara ya Ardhi imeoza,Kuna uchafu mwingi unaohusisha Maafisa Ardhi direct,inatakiwa kufanya overhaul ya watumishi hasa waliokaa kituo kimoja zaidi ya miaka mi5.

Hata hivyo ni ngumu kufanya hivyo kwakua watumishi wengi maeneo hayo wanawekwa na wakubwa Wenye interests zao,hivyo kuwa ni untouchables.
 
Back
Top Bottom