Jalada kesi ya vigogo wa Bandari TPA mbioni kusajiliwa Mahakama Kuu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kuwasilisha taarifa muhimu Mahakama Kuu katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (66) na wenzake watano.

Kipande na wenzake hao wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Dola za Marekani 1.85 milioni sawa na Sh4.2.bilioni.

Leo Jumatatu Machi 27, 2023 Wakili wa Serikali, Mosie Kaima ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa, baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika.

Wakili Kaima ametoa meelezo hayo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira anayesikiliza shauri hilo.

" Kesi imeitwa kwa ajili ya kujatwa na upelelezi umekamilika, nimeelezwa kutoka makao makuu Dodoma kwa DPP, kuwa jalada la kesi hii lipo huko na wapo katika hatua za mwisho kusajili taarifa muhimu Mahakama Kuu, hivyo kutokana na maelezo haya, tunaomba utupangie tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama nyaraka hizo zimeshasajiliwa," amedai Kaima.

Kaima baada ya kumaliza kutoa maelezo hayo, mmoja wa mawakili wa utetezi, Mruge Fabian aliomba upande wa mashtaka wajitahidi kusajili taarifa hizo kwa haraka ili kesi iweze kuendelea.

Hakimu Rugemalira baada ya kusikiliza maelezo, ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 25, itakapotajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Mbali na Kipande, washtakiwa wengine ni Peter Gawile (58) aliyekuwa Ofisa Rasilimali Watu wa TPA na mkazi wa Mianzini; Casmily Lujegi (65) mkazi wa Mbezi Juu na Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi wa TPA, Mashaka Kisanta (59) Mkurugenzi wa Idara ya Manunuzi, Kilian Chale (51) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano pamoja na Andrew John.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2022 wanadaiwa kati ya Oktoba Mosi, 2014 na Oktoba Mosi 2020 Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa la kuisababishia TPA hasara.

Shtaka la pili, kati ya Januari Mosi, 2015 hadi Februari 17, 2015 washitakiwa kwa pamoja wakiwa maofisa wa TPA, walitumia madaraka yao vibaya kwa kutangaza zabuni namba AE/016/2014-15/CTB/G/39 kwa nia ya kujipatia dola za Marekani 1,857,908.04 .

Shtaka la tatu, inadaiwa kati ya Oktoba Mosi 2014 na Oktoba Mosi, 2020 maeneo ya TPA na maeneo mengine ya Dar es Salaam, washtakiwa kwa makusudi walitangaza zabuni ya Enterprises Planning Resources (ERP) bila kupata kibali cha Bodi ya Zabuni ya mamlaka hiyo na kushindwa kufuata kanuni za zabuni hivyo kutoa malipo ya awali ya asilimia 40 bila idhini ya bodi hiyo, jambo lililosababisha TPA hasara ya Dola za Marekani 1.8milioni ambazo ni sawa na Sh4.2bilioni.

MWANANCHI
 
Casmily Lujegi (65) mkazi wa Mbezi Juu na Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi wa TPA, Badala ya kutulia na wajukuu nyumbani utakuta mtu alishazidi umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria bado unang'ang'ania teuzi ndo unakutwa na dhahama uzeeni.
 
Back
Top Bottom