Serikali yaongeza bajeti ya elimu bila ada kwa asilimia 15

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Elimu bila ada kwa shule za shule za msingi na sekondari imeongezewa kwa asilimia 15.34 kwa mwaka ujao wa fedha 2023/24 ikilinganishwa na bajeti iliyoidhinishwa katika mwaka wa fedha wa unaomalizika wa 2022/23.

Hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023 /24 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki imeonesha hilo.

Kairuki ameliomba Bunge liidhinishe Sh bilioni 399.64 kwa mwaka 2023/24 kwa ajili ya elimu bila ada ambazo kati yake, Sh bilioni 157.79 zimetengwa kwa shule za msingi na Sh bilioni 241.85 kwa sekondari.
Bajeti hiyo ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 53.15 ambayo ni sawa na asilimia 15.34


Ongezeko hilo limeelezwa kuwa linatokana na wanafunzi wa kidato cha tano na sita kujumuishwa katika Mpango wa Elimu Bila Ada.

Katika hatua nyingine, Kairuki amesema serikali itaendelea na mpango wa ujenzi wa matundu ya vyoo katika vituo shikizi ambako Sh bilioni 5.74 zimetengwa kwa ujenzi wa matundu 5,218 ya vyoo.

Aidha, zimetengwa Ujenzi wa mabweni 61 ya wanafunzi wenye mahitaji maalum umetengewa Shilingi bilioni 7.86
 
Elimu bila ada ila wazazi mtaani wananyooka na michango ya shule,

Kwa mwezi mzazi anajikuta katoa kama 50,000 kabisa...
 
Serikali iwekeze kwenye elimu bora watu walipie, asiyetaka lipa akae nyumbani na mwanae.
Elimu bure ila watoto wanafika shule ya Upili hawajui soma na kuandika
 
Serikali iwekeze kwenye elimu bora watu walipie, asiyetaka lipa akae nyumbani na mwanae.
Elimu bure ila watoto wanafika shule ya Upili hawajui soma na kuandika
Watoto wa maskini wakae nyumbani sio
 
Back
Top Bottom