Serikali yakimbia bungeni, yaogopa mapigo ya upinzani, spika ainusuru kwa kuahirisha Bunge

onembuya

Member
Apr 16, 2012
18
3
Leo katika historia ya Bunge la Tanzania, kumetokea kituko Bungeni. Kituko namba moja ni kutowasilishwa kwa hati mezani (Finance Bill) na kituko cha pili ni kutosomwa kwa Finance Bill kama ilivyokuwa imeoneshwa kwenye ORDER PAPER YA LEO.

Kuna tetesi kwamba Serikali ilimwomba Spika ailinde kwa kutoruhus mswada huo kuwasilishwa bungeni kwa kuwa ulikuwa na mapungufu mengi sana na kwa maana hiyo ungepondwa sana na Upinzani jambo ambalo limeiogopesha Serikali na hivyo kutafuta EXIT kwa Spika.

Ijulikane kwamba kwa kuahirisha bunge hadi saa kumi ni kwamba sasa wabunge hawatapata tena nafasi ya kutosha kujadili mswada huo kwa kuwa bunge litamaliza shughuli zake na kuahirishwa hadi Novemba leo jioni.

Pata Picha jinsi Spika anavyoikingia serikali dhidi ya makombora ya Upinzani. TUTAFIKA KWA STYLE HII?
 
Wanajimaliza bahati nzuri wananchi wanaelewa nini kinaendelea wasubiri tu mwisho wao unakaribia
 
sIJUI WATAKIMBIA MPAKA LINI? SHEM ON YOU LIWALO NA LIWE WEWE SI NDIO KILANJA WAO? AIBU PIA KWA SPIKA BI. KIROBOTO
 
Hahahaha, kweli hatuna viongozi ila ni wachumia tumbo tu!! Haiwezekani wakati watu hawalali kwa kunusuru uchumi wa nchi zao, wenzetu ndiyo kwanza wanakuwa busy kupindisha mambo ili waonekane wasafi wakati wanayoyasema hata hawayafanyi!!. Kusema kweli hawa viongozi wetu wanatuchelewesha mno!! Come guys, you are tired, leave your post hamuendani na karne ya 21 ambapo ni vichwa smart tu ndiyo vinatakiwa kubebeshwa kazi za kusaidia watanzania maskini.
 
mzee cheyo kapiga biti ya kwamba ina maana sheria ya mbegu bora ni SUKUMALAND??????? Spika kaona wakajipange upya
 
download

Serikali ya walevi
 
Wanatapatapa tu, muda wao wa kuchinjiwa baharini unawadia sasa!
 
Jana usiku walikaa Caucus ya chama chao na kukubaliana kuwa sheria ya kodi ambayo wanaiwasilisha hawataeleweka kwa watanzania na hivyo wataendelea kuwapa credit CDM kwani walikuwa wanaenda kuongeza kodi kwenye maji ya kunywa kwa asilimia 17, kodi ya VAT kwenye maziwa, kusamehe kodi ya VAT kwenye bidhaa zote zinazotumiwa na makampuni ya madini nchini nk.

Hali ni mbaya sana ndani ya CCM hasa wakati huu wanapokua wanaelekea kwenye uchaguzi wa chama chao ,
 
serikali inamtawala spika, inatawala polisi na mahakama, inatawala wafanyakazi wa umma wasidai haki yao...kwenye katiba mpya jamani waweke kua spika asiwe na chama chochote awe ni mtu independent bungeni mana namna hii hatutafika
 
Leo katika historia ya Bunge la Tanzania, kumetokea kituko Bungeni. Kituko namba moja ni kutowasilishwa kwa hati mezani (Finance Bill) na kituko cha pili ni kutosomwa kwa Finance Bill kama ilivyokuwa imeoneshwa kwenye ORDER PAPER YA LEO.
Kuna tetesi kwamba Serikali ilimwomba Spika ailinde kwa kutoruhus mswada huo kuwasilishwa bungeni kwa kuwa ulikuwa na mapungufu mengi sana na kwa maana hiyo ungepondwa sana na Upinzani jambo ambalo limeiogopesha Serikali na hivyo kutafuta EXIT kwa Spika.
Ijulikane kwamba kwa kuahirisha bunge hadi saa kumi ni kwamba sasa wabunge hawatapata tena nafasi ya kutosha kujadili mswada huo kwa kuwa bunge litamaliza shughuli zake na kuahirishwa hadi Novemba leo jioni.
Pata Picha jinsi Spika anavyoikingia serikali dhidi ya makombora ya Upinzani. TUTAFIKA KWA STYLE HII?

Hatufiki kwa kuwa na watu kama wewe. Unaanzisha thread, unaonyesha problem basi hata kama huna solution omba wachangiaji wanaofuata wachangie kutoa solution. Badala ya kufanya unaanza kuelekeza malalamiko na thread nzima ijae malalamiko badala ya kujaa solution.
 
Sasa tunaoneshwa wazi kuwa hakuna mgawanyiko wa mihimili mitatu katika serikali ya tz kwani kiongozi wa bunge amedhihirsha hilo kwa kuaccep the gvt command.
 
Back
Top Bottom