BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesema kupanda kwa bei ya nondo na misumari kumetokana na uhaba wa chuma ghafi na chakavu ambavyo ndio malighafi inayotumika kutengenezea bidhaa hizo.
Kigahe alibainisha hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi aliyehoji sababu za kupanda kwa bei ya bidhaa hizo.
Naibu Waziri huyo alisema kupanda kwa bei kunategemeana na soko la chuma duniani, akiwa na ufafanuzi kwamba viwanda vingi kwa sasa vinategemea chuma ghafi toka nje ya nchi.
"Bei hizi ni za kimataifa, ndio maana unaona bei inaongezeka, ndio maana tumeruhusu hata chuma chakavu kutoka nje kuuzwa hapa (nchini) ili kusaidia (kukabili) huo upungufu.
"Tunajitahidi kutoa taarifa sahihi kwa wakati kwamba kuna changamoto hizo na mpango wa serikali ni upi katika kuhakikisha bei inashuka.