Serikali na BOT, mbali na watumishi kukatwa mishahara kulipa mikopo yao, watumishi waruhusiwe pia kulipa wao wenyewe waweze kumaliza madeni yao mapema

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,022
144,379
Katika vitu ambavyo huwa naviona haviko sawa kwa watumishi, ni hili la Mtumishi kutakiwa kusubiri mpaka makato yote ya mkopo yaishe ndio amalize mkopo wake au kama anataka kumaliza mkopo wake mapema, basi ni kwa mfanyakazi husika kulipa kwa mkupuo mmoja deni lote lililobaki(outstanding balance).

kwa lugha nyingine, mbali na mfanyakazi kuendelea kukatwa mdshahara wake, mfanyakazi hana option ya kulipa deni lake kidogo kidogo kwa kutumia mapato yake mengine ili amalize mkopo kwa haraka zaidi pale anapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo na kama anataka kumaliza deni lake, basi ni shartiti alipe deni lote lililobaki kwa mkupuo mmoja.

BOT na mabenki ya kibiashara hapa nchini, kwanini hamuoni umuhimu wa kuruhusu wafanyakazi kulipa madeni yao kidogo kidogo(mfano kwa installments kadhaa) kwa kutumia mapato yao mengine pale Mtumishi anapotaka kufanya hivyo ili amalize mkopo wake mapema? Nini kinashindikana?

Swali ninalojiuliza ni kama inawezekana kwa wafanyabiashara, kwanini isiwezekane kwa waajiriwa?

Mbona katika taasisi nyingine za kifedha zikiwemo SACCOS ambapo malipo hufanyika kwa mwezi, wakopaji wanaruhusiwa kulipa zaidi ili tu wamalize mapema mikopo yao mapema?

Je, hii si mbinu ya kuwabana watumishi wakae na madeni muda mrefu ili mabenki yatengeneza faida?

Serikali kupitia BOT, tunaomba utaratibu huu upitiwe upya ili kama inawezekana, kuwe na utaratibu utaoruhusu mabenki na wafanyakazi kukaa pamoja na kukubaliana ni namna gani mtumishi anaetaka kutumia mapato yake mengine kuhudumia deni lake hata kama hawezi kulipa deni lote lililobaki kwa mkupuo mmoja.

Sababu mojawapo inayochangia ugumu wa maisha na umasikini wa watu katika nchi hii, ni wenye mamlaka kukosa ubunifu, kutowaza sawa sawa na kushindwa kuvaa viatu vya watawaliwa.
 
Katika vitu ambavyo huwa naviona haviko sawa kwa watumishi, ni hili la Mtumishi kutakiwa kusubiri mpaka makato yote ya mkopo yaishe ndio amalize mkopo wake au kama anataka kumaliza mkopo wake mapema, basi ni kwa mfanyakazi husika kulipa kwa mkupuo mmoja deni lote lililobaki(outstanding balance).

kwa lugha nyingine, mbali na mfanyakazi kuendelea kukatwa mdshahara wake, mfanyakazi hana option ya kulipa deni lake kidogo kidogo kwa kutumia mapato yake mengine ili amalize mkopo kwa haraka zaidi pale anapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo na kama anataka kumaliza deni lake, basi ni shartiti alipe deni lote lililobaki kwa mkupuo mmoja.

BOT na mabenki ya kibiashara hapa nchini, kwanini hamuoni umuhimu wa kuruhusu wafanyakazi kulipa madeni yao kidogo kidogo(mfano kwa installments kadhaa) kwa kutumia mapato yao mengine pale Mtumishi anapotaka kufanya hivyo ili amalize mkopo wake mapema? Nini kinashindikana?

Swali ninalojiuliza ni kama inawezekana kwa wafanyabiashara, kwanini isiwezekane kwa waajiriwa?

Mbona katika taasisi nyingine za kifedha zikiwemo SACCOS ambapo malipo hufanyika kwa mwezi, wakopaji wanaruhusiwa kulipa zaidi ili tu wamalize mapema mikopo yao mapema?

Je, hii si mbinu ya kuwabana watumishi wakae na madeni muda mrefu ili mabenki yatengeneza faida?

Serikali kupitia BOT, tunaomba utaratibu huu upitiwe upya ili kama inawezekana, kuwe na utaratibu utaoruhusu mabenki na wafanyakazi kukaa pamoja na kukubaliana ni namna gani mtumishi anaetaka kutumia mapato yake mengine kuhudumia deni lake hata kama hawezi kulipa deni lote lililobaki kwa mkupuo mmoja.
Yamekukuta
 
Hii nchi ina mifumo ya hovyo Sana ndio maana utasikia ma-bank yakitangaza faida kubwa na muda huo huo wananchi wakibaki kwenye umasikini wa kutupwa
 
Back
Top Bottom