Hebu tujikumbushe Hali ilikuwaje huko nyuma kwa mawaziri wa fedha na Marais wao walipandishaje mishahara. Tuangalie hawa wa tgts:

Mwaka 2005 ... Ilikuwa 24.32% Hadi 8.34%
Mwaka 2008.. waliongeza kati ya 25% na 30%
Mwaka 2014 kwenye kundi Hilo nyongeza ilikuwa kati ya 7.58% na 9.73%
Angalia nyaraka za utumishi kipindi hicho.
Na hapakuwepo na mbwembwe na matangazo kama tuliyoshuhudia mwaka huu!!!
 
Haijalishi unamchukukia kiasi gani , she is your president, Hadi mwaka 2030,jiandae kisaikolojia,

By the way mtu hawezi ishi na kuwa na Maisha Bora kwa kutegemea vitu vya kupesa, mshahara ni sawa na kitu Cha kupewa, hivyo hata ukilipwa milioni Saba bado utalalamika.

Kwa kilichoweka kinatosha, tusubiri mwaka kesho Mungu akipenda.
No one know tomorrow, hata jiwe aliamin atatawala milele Leo hii hatunaye
 
Tatizo la Serikali/CCM ni kupenda sifa za kijinga, na tatizo hili linachangiwa na uwepo wa kundi kubwa la wajinga ndani ya Serikali na Chama husika.
Watumishi wenu walinyamaza siku ile Rais alipokataa kutoa kiasi cha nyongeza hadharani. Sasa wajinga wakajitafutia sifa wakaja na ahadi ya 23%, Sasa hapa mmewapa watu matumaini wakaanza kupanga mipango yao kwenye mishahara kumbe mnajua hili jambo ni gumu kutekelezeka.
Ufafanuzi mnaotaka kuwapa watumishi hauna maana yoyote, kama ni kufafanua mngefanya hivyo wakati mnatoa tangazo ili kuweka angalizo.
Wale wanaomkumbuka Magufuli muwaache wafanye hivyo kwani yanayoendelea ni fedheha.
 
Mara ngapi afedheheke kinachomkera wameongeza posho wao wakubwa huku chini maumivu ubinafsi wa Hali yajuu aa Hawa viongozi, waogope jamani, tozo Kila Kona, gharama za maisha zimepanda. Kwani si angekaa tu kimya kuliko Nye Nye Nye nyingi afu unakuta 12600 upuuzi mtupuu!!

Nimemchukia huyu maza na vibaraka wake!!
Ndugu kwakweli hawajafanya vizuri Mimi hata shilingi hamsin sijapata na mshahara wangu ni mdogo daah! Tutafute vingine vya kufanya mtumishi wa Umma Hana thamani.
 
Wakati wa mei mosi kuna mtumishi nilikula kwa furaha ya ongezeko la mshahara nadhani huko alipo akifikilia kuliwakaliwa na mshahara 20000 Ila yote heri
 
Wapo bize kutenga billion 700 kwa ajili ya kuwang'oa wamasai ngorongoro!!! Pesa ya kuongeza mishahara sio priority kwao... au kuna ufafanuzi zaidi ???
 
IMG-20220725-WA0013.jpg

Ninajiuliza mambo mengi sana kuandika nashindwa nianzie wapi, ngoja tusubiri kesho.
 
View attachment 2303405
Ninajiuliza mambo mengi sana kuandika nashindwa nianzie wapi, ngoja tusubiri kesho. Naona kama kikundi cha wenye lao moja wanakaa kutengeneza jibu moja.
Wanakutana kujadili nini mjadala ulisha anza kwa magufuli huko hadi leo hauishi? Buying time strategy

Litapigwa tukio moja hapa katikati na kila mtu atasahau habari za nyongeza za mishahara. Siunajua watanzania wanaishi kwa matukio? Kuna njemba zipo jikoni zinaandaa tukio
 
Itoshe kusema kuwa, Mhe. SSH Rais wa JMT anayo dhamira njema ya kuondoa kero ya muda mrefu ya kutoongezwa mshahara Watumishi wa Umma lakini kwa ongezeko hili, dhamira yake hii inedhulumiwa! Haiwezekani Mtumishi hajapandishwa mshahara wa kisheria (Annual Increment) wala ongezeko la mshahara kwa ridhaa ya Rais kwa miaka takriban saba halafu leo unampatia ongezeko la 20,000.00!!!

Hapa Mama aitishe kwa mara nyingine washauri wake na wamweleze sababu hasa za kuja na pendekezo hili ambalo halina uhalisia. Ni sawa tu na kutoongezwa mshahara kabisa. Mbaya zaidi ni namna baadhi ya washika dau (Wachechemuzi) walivyolipaisha suala hili kwa kusema "Mama kaupiga mwingi na kshangaza Kimataifa"!!! Wengi walijawa na shauku ya kufahamu hili ongezeko la kushangaza Kimataifa, lkn ilipofika tarehe ya malipo ya mshahara mpya, kila mmoja ameshangazwa na naamini hata Rais wetu Mpendwa pia ameshangazwa na namna Watumishi walivyolipokea.

Ni imani yangu kuwa Viongozi wa TUCTA na Serikali watakutana kesho na kufikia muafaka utakaowaondolea Watumishi kero hii ya kutoongezwa mshahara kwa miaka 7 huku gharama za maisha zikipaa siku hadi siku.
 
Back
Top Bottom