Sintofahamu Nyongeza ya Mishahara: Serikali Kukutana na TUCTA 26/07/2022

Thabit Karim

JF-Expert Member
Sep 3, 2012
375
682
Serikali kupitia ukurasa wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali imesema itakutana na viongozi wa TUCTA kuhusu suala la nyongeza ya mishahara. Taarifa hiyo imesema hivi:

Ndugu wafanyakazi, Jumanne tarehe 26 Julai, 2022 Serikali itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara katika mishahara ya Julai, 2022.

======

Haya sasa sijui Serikali ijataka kusema nini

IMG_1321.jpg
 
Hao viongozi wa TUCTA wakitoka kupigwa sound wanakuja kuwapa moyo wafanyakazi, then from there hizi hasira za siku mbili zinayeyuka maisha yanaendelea na nyongeza zinazoeleka.

Katiba Mpya [Rasimu ya Warioba ] ndio dawa ya matatizo mengi yanayoikumba jamii yetu, angalau pawepo na sheria zitakazowalazimu watawala kuzifuata, wasipozifuata ni mahakamani.

Kuwa na taasisi imara ni muhimu sana, mfano hao TUCTA wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hii, lakini kwa udhaifu wao wamewekwa mfukoni na watawala.

Vyama kama TUCTA nchi nyingine vinaheshimiwa sana na serikali zao kwa sababu ya nguvu waliyonayo, ajabu hapa kwetu walimu nao hutumika kwenye kuiba kura ili hao watawala wanaowaonea waendelee kubaki madarakani!.
 
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter msemaji mkuu wa serikali ametoa taarifa ya wao serikali kukutana na viongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) kwa ajili ya ufafanuzi na maongezi zaidi, "Ndugu wafanyakazi, Jumanne tarehe 26 Julai, 2022 Serikali itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara katika mishahara ya Julai, 2022.


IMG_20220724_131651.jpg
 
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter msemaji mkuu wa serikali ametoa taarifa ya wao serikali kukutana na viongozi wa shirikisho ...
Zaidi ya watu 500 wamekusanyika na kuandamana wakilalamikia gharama za maisha kuwa kubwa Jijini Kuala Lumpur Nchini Malaysia yakihusisha wanasiasa vijana wa upinzani ambapo pia walipata nafasi ya kutoa hotuba.

Sehemu ya madai ya waandamani ni kudhibiti ongezeko la bei za bidhaa, usalama wa chakula na kutoa misaada kwa Wananchi.

Maandamano hayo yalihusisha watu kutoa taasisi tofauti ambapo Polisi waliweka vizuizi na kueleza kuwa hawakuwa na taarifa juu ya maandamano hayo kama inavyotakiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria.

ED3BE041-7AF2-4C75-A640-70D45695B998.jpeg
 
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter msemaji mkuu wa serikali ametoa taarifa ya wao serikali kukutana na viongozi wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) kwa ajili ya ufafanuzi na maongezi zaidi, "Ndugu wafanyakazi, Jumanne tarehe 26 Julai, 2022 Serikali itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara katika mishahara ya Julai, 2022.


View attachment 2302219
 

Attachments

  • F9C589F6-183D-4BC2-AF67-BDF805436C71.jpeg
    F9C589F6-183D-4BC2-AF67-BDF805436C71.jpeg
    75.4 KB · Views: 4
Serikali kupitia ukurasa wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali imesema itakutana na viongozi wa TUCTA kuhusu suala la nyongeza ya mishahara. Taarifa hiyo imesema hiv...
Hi I kumbe ni kufadanua na siyo kuongeza Hela? Ufafanue Nini wakati tuliambiwa asilimia 23.3?
Kama haiwezekani acheni tu sisi hayo matatizo tumeshazoea.

Kama tumevumilia miaka Saba Kuna Nini tena hapo.Lamsingi serikali itambue kuwa haijatutendea haki,inatuonea na imetulaghai jambo ambalo siyo zuri.

Wao wanaishi vizuri Kwa Kodi zetu halafu sisi wanatutesa, kosa letu Nini hasa? Kikotoo nacho kimejaa uonevu tu. Shida Nini lakini? Tumeshachoka na propaganda za serikali
 
Kesho ni sikukuu ya mashujaa na itaadhimishwa nchi nzima ni siku najua serikali itamwaga wanajeshi katika miji yote kutukumbusha kuwa huyu MAMA ni ameshika nchi kwa ridhaa ya JW, tukileta fyoko tu wanatunyokoa , na wale wastaafu kama Warioba, Msuya wanaotaka katiba mpya nao watawekwa kiti moto baada ya sherehe huko chamwino
 
Hapo itakuwa ufafanuzi tu, kuwa barua ilisema nyongeza kwa kiwango cha chini
 
Wananchi tumechoshwa na UONGO!

Mlisema Bei ya mafuta itashuka KWA kukopa billion 100 dollar kutoka IMF na haijashuka Hadi leo!!

Mmewaahidi watumishi 23.3% Lakini hola!!

Sasa hatutaki dana dana fanyeni hivi;-

"Samiah jiuzulu Sasa nchi imeshakushinda, ulambaji asali umekuponza"!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!
 
Kuwa na taasisi imara ni muhimu sana, mfano hao TUCTA wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hii, lakini kwa udhaifu wao wamewekwa mfukoni na watawala.
Udhaifu wa taasisi na uwepo wa katiba mbovu ni matokeo ya udhaifu wa jamii nzima (watanzania wote tu dhaifu). Sri Lanka raia wameiwajibisha serikali.

Hapa kwetu raia bado wamelala ndiyo maana aasisi zipo tu kama koti la babu. Raia ni dhaifu ndiyo maana katiba mbovu inakumbatiwa na chama tawala lakini tumetoa machobtu kama Mazombie.

Hakuna kitakachofanyika nq hqo TUCTA zaidi ya kupewa naagizo na serikali wawashughulikie wafanyakazi ama watapewa lugha ya kuja kuwalainisha wafanyakazi
 
Siku ele nilisikia sauti madaraja ya mseleleko yapo,ni lini Sasa? Mbona hatuyaoni Wala kusikia Tena? Au siku hizi uongo ni hadharani tu?
 
Ni upuuzi kusema, "serikali itakutana na TUCTA kutoa ufafanuzi"

Nilitegemea aseme;

"....serikali imekiri kuwa kuna makosa ya kikotozi cha mshahara yamefanyika, nserikali inawaomba radhi wafanyakazi wote na wawe watulivu wakati marekekebisho yakifanyika..."

Huu ndiyo ungekuwa uungwana...
 
Tucta hii iliyotuuza kwenye kikokotoo ndo itajadili nini na serikali. Tucta hii iliyojaa makada wa CCM itajenga hoja zipi na serikali ya CCM?
Kikundi cha Vijana Wachumia Tumbo. Vyama vya Wafanyakazi Nchi hii having Meno Tena. Kikokotooo wameuchuuza Wazee Wastaafu Ili wafe Maskini. Sina Hamu na hili kundi najuta kukatwa Mchango Kwa ajili Yao.
 
Back
Top Bottom