Da Womanizer
JF-Expert Member
- May 24, 2010
- 1,577
- 148
....
Change begins with YOU
Do u really mean this??? I mean are you implementing the same??
....
Dah wakati mwingine inashangaza kuona JF ni sehemu ya kulalamika na kulialia juu ya kila uamuzi wa serikali. Ni serikali ipi duniani haikopi?
Serikali ina njia kadhaa ya kupata fedha, borrowing is among them. Wanaosema kwamba serikali haifanyi bihashara ni dhahiri kwamba elimu yao haijai kiganjani; serikali inauza na kununua securities takriba kila juwa linapochomoza. Kabla hatujaendeleza "tamaduni" ya kulalamika na kukemea ni bora tukarejea darasani kidogo na kuangalia mahusiano ya shughuli za serikali, benki, na uchumi wa nchi. Vinginevyo wanaotusoma hapa JF (including the Mkulos) wanatuona kana kwamba akili zetu ni mchanyato wa ubongo na togwa.
Dhahabu bado hiko juu usd 1241.00/ounce na TZ ni nchi ya Tatu kwa uzalishaji Africa....
Tunaongozwa na CCM na CCM ingekua na uwezo wa kupambanua mambo Tanzania ingeshaendelea siku nyingi.Sawaaa, lakini hata kama ukiambiwa ukope kwani na wewe ndio huna akili ya kupambanua?
Kwanini tusitumie rasilimali zetu kibao kwa ajili ya bajeti na matumizi yetu? Sijui tunaenda wapi na ni nani atatuongoza
Mtalalamika sana but nothing will change mpaka mtakapoacha kulalama na ku-take things into your own hands.
Nadhani ndugu yangu una uhuru wa kusema kama sie tulivyo na uhuru wa kusema. But unapotuhukumu kuwa sie tuna mtindio wa akili kwakweli unakuwa umetukosea haki kwani tunatumia haki yetu ya kikatiba kuzungumza lile tunaloliona. Sasa ngoja nikupe darasa kwanini sie tunalalamika maana umetwambia hatuendi darasani.
Serikali inapokopa kwa kukutumia T-bills, au government bonds ni kwamba zile ni securities ambazo inazitumia kuraise liquidity (mkusanyiko wa fedha). Lakini tofauti yake na mkopo ni kwamba serikali inatangaza gawio au interest inayotaka kulipa kwa kuazima hizo pesa hivyo basi unakuta maranyingi interest hiyo haiwi kubwa kulinganisha na mkopo wa kawaida. Vile vile Serikali inakuwa na discretion ya lini italipa hizo pesa mfano kuna 90 days bills, 180 days, 360 days, 1 year bond, 2 year, 5 year etc. Lakini unapokuwa umekopa katika mabenki mfano overdraft facility kila siku wanakuwa wana charges zinazoambatana na mkopo huo. Vilevile ile overdraft inachajiwa interest in accordance to the prevailing market rates.
Sasa kwa Tanzania interest katika loanable funds ni 18-23% kama haijabadiilika kuzidi. Wakati interest kwenye Tbills ni lower zaidi ya hiyo kwa akili ya mtu wa kawaida unadhani inamake sense kwenda kuchukua mkopo wenye riba ya juu ukaacha mkopo wenye riba ya chini unless uwe umekunywa pombe. Na kwanini wasiissue securities kuraise more capital? Unakuta kwamba serikali imekwama with liquidity shortage na sasa inatafuta a quick alternative ya kuraise cash.
Sasa katika bank njia rahisi ya kupata cash ni kuchukua overdraft facility ambayo ni mara moja kuipata kama wewe mteja mkubwa. Hatari iliyopo ni charges zinazoambatana na facility hiyo na interest inayochagiwa. Vilevile kama serikali ikishindwa kulipa inamaana serikali itakuwa imeweka collateral (rehani) rasilimali fulani ambazo sijui bunge lina taarifa nazo au la? Sasa kimkopo kama serikali yetu iko makini sio tatizo but kama serikali yetu haina misingi mizuri ya usimamiaji wa kodi matumizi ya mabovu ya pesa ni hatari kwasababu hizi pesa zinatakiwa kulipwa on time na ukichelewa deni linaongezeka.
Sasa usifikiri watu tunapayuka kama wendawazimu bali tuna akili zetu na vilevile tumeshaona vyanzo vyote unavyovitazama wewe tukaona kwamba hili linaweza kusababisha a sovereign debt crisis kama iliyopo Greece na Spain. Na vilevile hatulalamiki ila tunaleta changamoto kwasababu nchi ikishatawaliwa na mabenki ndio hatuna sauti wananchi zaidi ya kukubali mabadiliko hivyo kabla hatujafika huko tusema tusije tukaambiwa mlikuwa wapi wakati tunafanya maamuzi.
Kuna maswali matatu naomba niwaulize Mkulo na wenzie:
a. Wameshindwa nini kuraise funds kwenye capital market (soko la mitaji) kwa kuuza hisa za serikali mfano bonds?
b. Wameshindwa nini kwenda kukopa katika development banks kama World Bank, IMF, ADB, EADB kuna ishu gani inaendelea?
c. Wameshindwa nini kupunguza fiscal policy budget instead budget ya serikali inakua kila siku? Hawajui kuwa mtu ukiwa huna kitu unapunguza matumizi yako kuweza kusave kiasi kidogo cha pesa?
Interesting analysis Mdondoaji.
Serikali, kama msimamizi na mchochezi wa shughuli za uchumi wa nchi, inapokopa kutoka kwenye benki za ndani uchumi wetu una athirika vipi? Serikali ikiuza bonds vs kukopa benki uchumi wetu unaathirika vipi?
Hatuwezi kulinganisha maesabu ya mfanya biashara wa kawaida na yale ya serikali katika kukuza uchumi na kuchochea maendeleo. Biashara ambazo hazina tija kwa mfanya bihashara wa kawaida zaweza kuwa na tija kwa uchumi na mendeleo ya nchi. Kwa mantiki hii mawazo yako kwamba serikali ikwepe riba ya juu hayana maana kwa serikali endapo inakopa ndani ya nchi yake. Serikali ni baba wa uchumi kamwe haogopi kutozwa riba ya juu kutoka kwa mtoto wake.
Kusema ati serikali ikakope kutoka World Bank, IMF, ADB, EADB nikutuzamisha zaidi kwenye umasikini, mana huko tumekuwa tukikopa tangu tupate uhuru na bado umaskini tunao...riba za huko tutaendelea kuzilipa hadi vizazi 15 vijavyo. Mdondoaji utakuwa mchumi wa kwanza ku suggest tukakope nje hali tunaweza kukopa ndani na hivyo kuongeza harakati za shughuli za uchumi.
Sasa naona unachanganya mambo hapa. Kupunguza fiscal policy kunatatua vipi tatizo la mkopo in the short-run? Serikali inahitaji fedha leo, impact ya kupunguza matumizi ya serikali inakuja in medium au in long-run! Yani nikija kwako kukopa badala ya kunipa mkopo utaniambia nipunguze matumizi? Kwanini nimekuja kukukopa in the first place?
Ah nilisahau kujibu tofautisha between government bonds, tbills na commercial loans. Government bonds ni promissory note ya kulipa pesa huitaji kuweka collateral kukopa. Similar to Tbills. Mkopo mzee lazima pawepo na collateral hata kama wewe ni Bill Gates. Sasa mengine utajaza mwenyewe kuhusu athari zake kwa nchi yetu.
Dah wakati mwingine inashangaza kuona JF ni sehemu ya kulalamika na kulialia juu ya kila uamuzi wa serikali. Ni serikali ipi duniani haikopi?
Serikali ina njia kadhaa ya kupata fedha, borrowing is among them. Wanaosema kwamba serikali haifanyi bihashara ni dhahiri kwamba elimu yao haijai kiganjani; serikali inauza na kununua securities takriba kila juwa linapochomoza. Kabla hatujaendeleza "tamaduni" ya kulalamika na kukemea ni bora tukarejea darasani kidogo na kuangalia mahusiano ya shughuli za serikali, benki, na uchumi wa nchi. Vinginevyo wanaotusoma hapa JF (including the Mkulos) wanatuona kana kwamba akili zetu ni mchanyato wa ubongo na togwa.
Pamoja na matatizo mengine, hili pia nimeliona. Ikimweka Mkulo aongee na hawa donors, kwa kweli huyu mtu anapwaya. Hawa wafadhili wanapokutana na mtu anayeweza kujieleza, kuwavutia na mwenye msimamo mambo huwa yanakwenda. Lakini wanapokutana na huyu Mkulo wanatuona kama watu wasio na mwelekeo..Viongozi wetu nao wanatupoza. Kama Mkulo unapitia hapa, naomba mara nyingine deligate someone who can do the job!