Serikali Iwasimamie Wasafirishaji wa Mizigo Kutoka Nje ya Nchi ili Ipate Kodi Halisi Kutoka kwa Wafanyabishara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE JULIANA MASABURI AISHAURI SERIKALI IWASIMAMIE WASAFIRISHAJI WA MIZIGO ILI KUPATA KODI HALISI KWA WAFANYABIASHARA​

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa Mhe. Juliana Didas Masaburi tarehe 23 Juni 2023 amechangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023-2024 na kutoa mapendekezo Mbalimbali kuhusu TRA na makusanyo ya kodi halisi.

"Naungana na Wabunge wenzangu kumpongea Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Nampongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba. Wote mnastahili Maua" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Napenda kuchangia kwenye mambo matatu; Cargo (Wasafirishaji wa mizigo), Kusajiliwa kwa Store na Mfumo wa FD Mashine" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Kuna tatizo kwenye wasafirishaji wa mizigo ambao wafanyabiashara wakienda China 🇨🇳, Uturuki, Marekani na nchi zingine. Wafanyabiashara wengi wanatumia wasafirishaji wa mizigo ambao kazi yao kubwa ni kukusanya mizigo ya wafanyabiashara wengi na kuweka kwenye Shehena moja" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Mwezi mmoja uliopita ulitokea mgogoro Kariakoo. Hawa wasafirishaji mizigo ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo na kuingiza nchini mfumo huu Serikali ilikuwa na nia njema lakini mfumo huu unasababisha kukosa kodi halisi" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Mfanyabiashara anapoenda nchi yoyote anaenda kununua mzigo na anapewa risiti ya manunuzi yake. Msafirishaji anachukua mzigo kwa nia ya kumsafirishia mpaka nchini kwake na kuuingiza kwenye forodha kwa pamoja" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Kwenye ulipaji wa kodi hawa wasafirishaji wanakwepa mbinu za kulipa kodi halisi. Kwa Kamishna wa TRA kodi za ndani wakiwa wanakaguliwa wanaingiza mizigo kwa majina yao au kampuni zao wanalipia mizigo wao wenyewe TRA wanaenda nje kwenye maghala yao mizigo ikishatoka na kuwapa wafanyabiashara mizigo bila kuwapa risiti zao" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Tatizo linakuja, Afisa TRA anapenda Kariakoo kukagua mahesabu ya wafanyabiashara au mizigo anawakuta hawana risiti halisi. Ndiyo maana wanapokisia kodi wanasema wanaonewa kwasababu kiukweli wanakuwa hawana kumbukumbu ya risiti maana zinabaki kwa msafirishaji" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Sababu hiyo inafanya ulipaji wa VAT uwe mgumu kwasababu kodi ya VAT ni Input Tax na Output Tax. Bila kuwa na VAT uliyolipa wakati unaingiza mzigo huwezi kutoa risiti kwa minajili ya kulipia VAT wakati ukiuza ndiyo maana kuna bei ya bila risiti na bei ya risiti" - Mhe. Abbas Talimba, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni

"Suala la wasafirishaji unaona hata wafanyabiashara hawalalamiki kwasababu wanapata faida sana, pale Kariakoo sijamsikia mtu akiwalalamikia wasafirishaji maana wanapata faida mara tatu" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Nashauri kuwepo na hawa wasafirishaji maana hawezi kuepukika kwaajili ya urahisi wa kusafirisha mizigo ya wafanyabiashara lakini Wizara ya Fedha na Mipango na TRA waone njia sahihi ya kuwasimamia hawa wasafirishaji wa mizigo" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa

"Napendekeza mfanye kama Bonded Warehouse ya Magari, mizigo ikifika kila mfanyabiashara akafuate mzigo wake mwenyewe apewe risiti zake akalipe kodi mwenyewe. Hii itasababisha Serikali kupata kodi halisi na wafanyabiashara hawataogopa mlolongo wa watu. Lazima kila mfanyabiashara alipe kodi kwasababu ya mahesabu ya kampuni yake na Biashara yake kuwa safi na sahihi" - Mhe. Juliana Didas Masaburi, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-06-24 at 12.56.38.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-24 at 12.56.38.jpeg
    43 KB · Views: 6
Hawa wabunge wanatia hasiraaa hivi serikalini kuna watu wangapi wanapoteza mabilioni ya hela lakini hawaoni ila kuumiza wafanya biashara kwa kuwabana mikodi.Harafu huyo ni mbunge ni kijana lakini ana roho ya kwa nn.Wapige kelele kwanza kwenye mabilioni yanayopotea hata sisi tutalipa kodi kwa amani.
 
Back
Top Bottom