Wabunge Watoa Hoja Kuishauri Serikali Juu ya Wakulima Kuuza Mazao Nje ya Nchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

WABUNGE WATOA HOJA KUISHAURI SERIKALI JUU YA WAKULIMA KUUZA MAZAO NJE YA NCHI

Mbunge wa Jimbo la Momba, Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe amewaongoza wabunge wanaotokea maeneo ya wakulima na wafanyabiashara kutoa hoja ya kuishauri Serikali namna nzuri ya kuwasaidia wakulima wanaouza mazao nje ya nchi

"Serikali haijatoa katazo ila imetoa maelekezo yanayofanya wakulima na wafanyabiashara wapate changamoto ya kutoa mazao nje ya nchi. Changamoto itapelekea bei za Mahindi kushuka. Lakini mpaka sasa NFRA hawajaanza kununua Mahindi kwenye vituo" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Wazo la Serikali ni jema lakini masharti waliyoyaweka yanafanya wakulima wasiweze kusafirisha nje ya nchi (Export) mazao kwa wakati na NFRA kwenye vituo siyo rafiki kumfanya mkulima auze mazao. Mazingira ni magumu kwa wakulima" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"NFRA wana vigezo vingi, unaweza kupeleka Mahindi tani 500 wakachukua Tani 10 na kufanya wakulima wasipate mahali pa kuuza Mahindi. Wachukuzi wa kawaida wanachukua Mahindi madam wananchi wananunua" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Tunaomba tutoe hoja ili wabunge tunaotokea kwenye maeneo ya wakulima wa mazao na wafanyabiashara tujadili ili tuweze kuishauri Serikali juu ya kuuza mazao au Mahindi nje ya nchi na NFRA" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Waraka wa Waziri aliotoa tarehe 23 Mei, 2023 kuelezea mchakato wa kutoa mazao nje ya nchi unaonekana una tija kwa Serikali na una tija kwa wananchi lakini changamoto ipo kwasababu ametoa jambo hili ghafla sana, siyo rafiki kwa mazingira yetu" - Mhe. Condester Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Waraka unasema, Wafanyabiashara na wanunuzi wanatakiwa kuwa na nyaraka zote muhimu ikiwemo utambulisho wa mlipa kodi (TIN), Certificate of Clearance, Leseni ya biashara (Export License), Namba za NIDA na Wamiliki wa Makampuni" - Mhe. Condester Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"TASAF pekee yake watu wanakosa kwasababu hawana NIDA, leo ndani ya mwezi mmoja mtu ataweza kupata namba ya NIDA aweze kufanya hilo jambo? Siyo uhalisia. Jambo aliloleta Mheshimiwa Waziri ni rafiki lakini haliendani na Mazingira" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Biashara ya Mazao ni ya msimu. Zambia 🇿🇲 imefunga mipaka yake kupeleka chakula Democratic Republic of Congo. Tanzania 🇹🇿 ni fursa. Kama Waziri amelileta hili Hatuwezi kufikia mahitaji ya Kongo. Tunaomba mambo haya yaanze Januari 2024" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Kama Waziri anataka jambo hili liendelee awe rafiki aseme mambo yote yanayotakiwa Mwananchi anaweza kuyapata ndani ya wiki moja ili aweze kuendana na mahitaji (demand) ya wakati huo, Waziri awe kiungo kwenye hizo taasisi zingine" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Waziri anaongelea lazima upate Export Permit na Faito Sanitary Certificate na wameweka Tovuti (Link) Wizara ya Kilimo ambayo unapaswa kuomba kutumia mfumo wa mtandao. Lakini hapa mfumo unaonesha upo kwenye matengenezo (System Under Maintenance), Mwananchi ataomba kitu gani?" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Nia ya Serikali ni njema lakini ndani ya muda mfupi wameweka masharti lukuki ambayo hata hao wafanyabiashara na Watanzania bado hayawasaidii, tunaomba Waziri wa Kilimo alegeze masharti kwa lengo la kuwasaidia wakulima" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-06-24 at 12.56.38(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-24 at 12.56.38(2).jpeg
    39.3 KB · Views: 8
Back
Top Bottom