DOKEZO Serikali itusaidie Wanafunzi Chuo cha Mbeya Training College, Chuo hakijasajiliwa kinatoa vyeti feki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Sisi Wanafunzi wa Chuo cha Mbeya Training College kilichopo Uyole Mkoani Mbeya ambacho kinatoa Kozi 4 ambazo ni Laboratory Assistant, Secretary, Business Operator na Hotel Management.

Mwaka jana (2022) wakati tunajiunga na chuo hiki ada ilikuwa ni Shilingi Milioni 1.36 na mmiliki wa chuo anaitwa Joseph Asajile akatuahidi kuwa mtihani wa NACTVET tungefanya Novemba 2022.

Ulipofika muda huo akasema tutafanya mtihani Januari 2023 kwa kuwa kuna hitilafu imetokea kati ya chuo na NACTVET, ilipofika Januari akaanza na ratiba nyingine kisha akatangaza ongezeko la ada kuwa Shilingi Milioni 13.8.

Masomo yakaendelea kama kawaida huku kukiwa hakuna mitihani, inapofika pia muda wa field anatupeleka kama kawaida, amekuwa na kawaida ya kufanya mipango yeye mwenyewe hasa katika taasisi binafsi.

Wachache ambao wanaenda kufanya field kwenye Taasisi za Serikali wamekuwa wakienda kwa maombi maalum lakini hawapeleki yeye.

Baada ya kwenda field akasema tukirejea tutafanya mitihani ya NACTVET, tulipoona danadana nyingi tukaenda NACTVET Mbeya wakasema chuo chetu hakijasajiliwa na kuwa kipo kwenye mchakato.

Pia wenzetu waliohitimu mwaka jana wakatutafuta na kusema kuwa vyeti vyao walivyokabidhiwa havitambuliki na hawajapata ajira.

Tukaanza kuripoti kuanzia ngazi ya chini kuhusu suala letu lakini kote hatujapata msaada, tukafika hadi Polisi tukaripoti Mmiliki hayupo ni kama amekimbia, anadai yupo Dodoma kwenye vikao.

Mwalimu wa Academy alishikiliwa siku moja na Polisi baada ya hapo akaachiwa na hatujui kinachoendelea kwa kuwa hakuna majibu rasmi.

Mtendaji wa Kata ndio amechukua maamuzi, alitaka kufunga chuo tukakataa, hivyo akaamua kusitisha masomo lakini tuendelee kwenda chuo kama kawaida tukisubiri hatima yetu, ikiwezekana waturudishie gharama zetu na ada tulizolipa.

Naomba Serikali iingilie kati itusaidie sisi Wanafunzi kwa kuwa, uwezo wa vyuo kama hiki inawezekana ni vingi, pia uwepo wake unamaanisha mamlaka zinafanya nini?

Taarifa tulizonazo ambazo si rasmi inadaiwa chuo hiki kilifungwa na Waziri Mwaka 2019 kwa kujiendesha bila kujisajili, Mwaka 2020 masomo yakarejea kumbe tabia za mmiliki ni zilezile.

Kozi za hapa zipo za mwaka mmoja na miaka miwili, hivyo kuna Wanafunzi wengi wamepigwa kama tunavyoelekea kupigwa sisi ambao kwa sasa tupo takribani 120.
 
inakuaje mwanafunzi bila kujali ngazi ya elimu kutokuwa makini? Hapo wa kulaumiwa ni wewe kutofanya tafiti ili kujirizisha kama upo mahala salama au lah na sio wazazi.Wazazi walio wengi jukumu lao ni kukutafutia ada na wewe ni kufanya tafiti ili usije choma pesa zao.Dunia ya sasa manamba ya taasisi za serikali zipo wazi kwanini usichukue na kuhakiki kwanza kabla ya kujiunga?
 
Back
Top Bottom