Taarifa kwa Wizara ya Afya, Nactevet na Serikali kwa ujumla

Antibiotics

New Member
Jan 30, 2021
3
3
TAARIFA KWA WIZARA YA AFYA, NACTEVET,SERIKALI NA WANANCHI WOTE KUHUSU CHUO CHA ST.ALVIN INSTITUTE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCE KILICHOPO MOROGORO MANISPAA.


Nikiwa kama mdau wa elimu napenda kueleza mambo mchache juu ya mwenendo mzima wa chuo cha ST.ALVIN INSTITUTE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCE, kilichopo MOROGORO MJINI,KATA YA KIHONDA ,POST CODE 67128,MTAA WA BARABARA MPYA ,PLOT NUMMBER 121,BLOCK C NA CHENYE USAJIRI (REG/HAS/193P) ili kusaidia serikali kuwa na wasomi wenye tija lakini pia kuokoa upotevu wa fedha za wazazi zinazo haribiwa na chuo hiki.

MAMBO HAYO NI KAMA YAFUATAYO


1.UKOSEFU WA MAKTABA NA MAABARA


Chuo hiki kimepewa ithibati ya ubora lakini hakina hata kozi moja yenye vitabu wala chumba cha maktaba/library mbaya zaidi kuna wanafunzi wa UTABIBU (CLINICAL OFFICER) ambao wanatakiwa waje wahudumie afya za watu lakini wana LAB ambayo haina vifaa NA IMEJAANVUMBI TU

Sasa kwa mwenendo huu tunapata wasomi wa aina gani? Na vipi kuhusu wazazi ambao wanapoteza fedha zao na watoto hawa kufeli ovyo, ombi langu naomba mamlaka husika ichukue hatua ili kuboresha haya mapungufu mana ndio jukumu lenu kubwa kwenye swala la elimu.

2.UWEPO WA KOZI ISIYO SAJILIWA KWA MIAKA 3 NA WANAFUNZI WANAHITIMU

Kwa miaka MITATU sasa chuo hicho kimekuwa kikitoa kozi hewa ya MAABARA NA UGUZI pamoja na kuwa danganya wanafunzi kwa kuwapa vyeti feki wakiomba kazi vyeti vinagoma kwa kuwa kozi haija sajiliwa hivo wahusika lioneni hili kwa maslahi ya taifa na wazazi pia kozi hii haijasajiliwa na wapo wanafunzi wanao soma nivyema mkawasaidia hawa ili kuleta tija katika elimu yao.

3.UWEPO WA WANAFUNZI AMBAO KWA MWAKA WA KWANZA AMBAO HAWAPO KWENYE MFUMO

Nikosa kisheria kwa chuo kuendelea na mwanafunzi ambaye hayupo kwenye mfumo wa NACTEVET lakini kwa chuo hiki kime kaa na wanafunzi hawa mpaka sasa na wamelipa ada lakini hawapo kwenye mfumo wa NACTEVET

4.UNYANYASAJI WA WAFANYAKAZI KUFUKUZA BILA MPANGILIO,KUCHELEWESHEWA NA KUTOLIPWA MISHAHARA ZAID YA MIEZI MITATU HADI MITANO.

Kumekuwa na utawala ambao unakiuka sheria ya kazi ya mwaka 2004 kuanzia kwenye masaa ya kazi, leave za watumishi, overtime,extra duty hata mishahara lakini pia mfumo wa kumwachisha mtumishi kazi, Hali inayopelekea walimu kutokufundisha kwa morali na kupelekea taaluma kuwa chini na wanafunzi kufeli

5. CHUO KUISHI BILA BODI

Chuo hakina bodi na kazi za bodi katika chuo , bodi ndio chombo pekee kilicho pewa mamlaka ya kuendesha chuo bila upendeleo na kulinda mslahi ya wadau na ina muda wa kufika ukomo, lakini katika chuo hicho toka chuo kianze bodi haijawahi kuwa na bodi maamuzi yanafanywa na ndugu

6. CHUO KUTO LIPA STAHIKI ZA WAFANYAKAZI ZA KISHERIA KAMA VILE ,NSSF, NA nk

Kwa mujibu wa sheria chuo kinatakiwa ki abide na taratibu zote za kiserikali kama vile kodi,NSSF, payee, wcf, loan bodi lakini hapa imekuwa tofauti kitu ambacho kina hujumu uchumi wa serikali kuna fedha za watumishi kwenye WCF, LOAN BOARD, NSSF ,kwa kifupi hakuna mtumishi ambae amesaunganishwa na huduma hizo

7. CHUO HAKINA WALIMU KUTOKANA NA WALIMU WENGI KUACHA KAZI KWA KUTOLIPWA MISHARA

Kutokana na walimu kutokulipwa mishahara yao wengi wao wameacha kazi hivyo kupelekea wanafunzi kukaa madarasani pasipo kufundishwa na mpaka sasa hawajafanya mitihan CAT 1 hasa mwaka wa kwanza

BINAFSI NAOMBA MAMLAKA HUSIKA ZICHUKUE HATUA HARAKA ILI KUNUSURU WANAFUNZI HAWA
 

Attachments

  • IMG_20231214_112528_769@1046305599.jpg
    IMG_20231214_112528_769@1046305599.jpg
    616.3 KB · Views: 11
  • IMG_20231214_112533_431@-1458656847.jpg
    IMG_20231214_112533_431@-1458656847.jpg
    605.2 KB · Views: 11
  • IMG_20231214_112627_909@-1634926137.jpg
    IMG_20231214_112627_909@-1634926137.jpg
    637.1 KB · Views: 12
  • IMG_20231214_112632_656@388729526.jpg
    IMG_20231214_112632_656@388729526.jpg
    851 KB · Views: 11
  • IMG_20231214_112757_034@957220596.jpg
    IMG_20231214_112757_034@957220596.jpg
    1.7 MB · Views: 8
  • IMG_20231214_112810_344@-1890224492.jpg
    IMG_20231214_112810_344@-1890224492.jpg
    1.6 MB · Views: 10
Back
Top Bottom