benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,505
- 3,038
Hadi kufikia mwaka 2023 jumla ya mashine za mionzi (X-ray) za kisasa za kidijitali 213 zimesimikwa huku vipimo vya Utra sound 67 vimesambazwa na kusimikwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya msingi nchini.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk Charles Mahera ameeleza kwenye kikao kazi cha wadau kujadili rasimu ya mtaala wa astashahada ya radiolojia
Vifaa tiba vingine vilivyosambazwa ni pamoja na X-ray zinazohamishika 108 ambazo zitatoa huduma kwenye majengo ya dharura yaliyojengwa kwenye halmashauri 80 nchini na majengo 28 ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
Aidha, alisema katika mwaka wa fedha 2022 / 23, Tamisemi ilifanya upembuzi yakinifu na kujiridhisha kuwa kufikia mwaka 2032 jumla ya wataalamu 13,178 wanahitajika kutoa huduma za radiolojia katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi nya msingi