Serikali inashirikiana na matapeli kuwaibia wananchi?

Mazima1

Member
Dec 31, 2020
20
47
Habari wakuu,

Naandika kidogo hapa maana mambo ni mengi,jana wakati naangalia taarifa ya habari nikaona habari kuwa kuna watu wametapeli wananchi zaidi ya milioni 900 kwa kuwauzia ardhi ambayo ni pori la serikali huko maeneo ya Bagamoyo, hadi muda huu wananchi hao wamekwishajenga na ndipo imetoka kauli ya serikali kuwa wananchi wabomoe nyumba hizo kwa mikono yao wenyewe kabla serikali haijachukua hatua.

Mbaya zaidi viongozi wa kampuni iliyowauzia ardhi wametokomea kusikojulikana na bado wanasakwa.

Ninachojiuliza hadi watu wanauziwa maeneo hayo hadi inafika hiyo milioni 900 Wizara ya ardhi iko wapi? Jeshi la polisi liko wapi? Wale jamaa wa makumbusho ambao wakishalewa wanauliza unaniju mi ni nani wako wapi?je baadhi ya viongozi wakubwa wa serikali wanashiriki katika mipango ya aina hii?
 
Kuna wengine kule Morogoro maeneo ya kwa Makunganya walikuwa hadi wamejenga ofisi ya ccm na bendera juu, wanauzia watu maeneo na kuwalipisha na mchango wa shule na kuwapa hati ya kimila......baadaye wakaambiwa ni eneo la msitu wa serikali, nchi hii wananchi wanapata taabu sana...
 
Inatisja na kuogofya, hasa kwa watu wa kipato duni kuambiwa umetapeliwa kiwanja ulichopata kwa jasho na damu la familia nzima!!!!!!
 
Habari wakuu,naandika kidogo hapa maana mambo ni mengi,jana wakati naangalia taarifa ya habari nikaona habari kuwa kuna watu wametapeli wananchi zaidi ya milioni 900 kwa kuwauzia ardhi ambayo ni pori la serikali huko maeneo ya bagamoyo,hadi muda huu wananchi hao wamekwishajenga na ndipo imetoka kauli ya serikali kuwa wananchi wabomoe nyumba hizo kwa mikono yao wenyewe kabla serikali haijachukua hatua.

Mbaya zaidi viongozi wa kampuni iliyowauzia ardhi wametokomea kusikojulikana na bado wanasakwa.

Ninachojiuliza hadi watu wanauziwa maeneo hayo hadi inafika hiyo milioni 900 Wizara ya ardhi iko wapi?jeshi la polisi liko wapi?wale jamaa wa makumbusho ambao wakishalewa wanauliza unaniju mi ni nani wako wapi?je baadhi ya viongozi wakubwa wa serikali wanashiriki katika mipango ya aina hii?
Huko Bagamoyo huko wamepigwa mpaka top layers
Wabunge
Mawaziri
Majaji
Mawakili wa serikali
Makatibu wakuu Nknk
Ila wakaogopa kulalamika popote kwakuwa baadhi ilikuwa uwekezaji wa siri wa michepuko pesa za rushwa nknk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo hapo wizara ya ardhi ijue ina watu wasiostahili kuwepo. Kama nakumbuka vizuri,kuna hotba aliwahi kutoa waziri mkuu,akiwataka watu kutonunua maeneo bila kushilikisha ngazi za uongozi wa juu,unaohusika na ardhi. Labda,hawa walikuwa wameshanunua. Ila sasa, ina maana kitengo hicho hakikupata malalamiko? Je,nchi hii, mtu anapoteleaje kusikojulikana! Mbona wakiamua kumtafuta tu ni masaa kadhaa wanae!
Harafu,kwa nini isitungwe sheria, ili tapeli au fisadi,ajue,ikibainika mali alizopata maelezo hayajitoshelezi, atafilisiwa. Sidhani kama wangeacha familia zao ziteseke.
Je,kama kiongozi,una raia aanyonge hivi, watakuelewa kweli? Je,swali la kujiuliza. Mtu hakuja na kuanza kuuza ardhi,lazima alishirikiana na watu. Itakuwaje watu hao hawajulikani walipo? Bila badhi ya watu kuwajibishwa,lazima mtindo ni huo huo.
 
Habari wakuu,naandika kidogo hapa maana mambo ni mengi,jana wakati naangalia taarifa ya habari nikaona habari kuwa kuna watu wametapeli wananchi zaidi ya milioni 900 kwa kuwauzia ardhi ambayo ni pori la serikali huko maeneo ya bagamoyo,hadi muda huu wananchi hao wamekwishajenga na ndipo imetoka kauli ya serikali kuwa wananchi wabomoe nyumba hizo kwa mikono yao wenyewe kabla serikali haijachukua hatua.

Mbaya zaidi viongozi wa kampuni iliyowauzia ardhi wametokomea kusikojulikana na bado wanasakwa.

Ninachojiuliza hadi watu wanauziwa maeneo hayo hadi inafika hiyo milioni 900 Wizara ya ardhi iko wapi?jeshi la polisi liko wapi?wale jamaa wa makumbusho ambao wakishalewa wanauliza unaniju mi ni nani wako wapi?je baadhi ya viongozi wakubwa wa serikali wanashiriki katika mipango ya aina hii?
Watumishi wa serikali na vyombo vya habari wanahusika na utapeli huu ambao unafanywa bila kificho kwa matangazo kwenye redio.
Mimi ningetspeliwa ningewabana waliotoa tangazo kupitia redio yao, wanajua waliko.
 
Ndo hapo wizara ya ardhi ijue ina watu wasiostahili kuwepo. Kama nakumbuka vizuri,kuna hotba aliwahi kutoa waziri mkuu,akiwataka watu kutonunua maeneo bila kushilikisha ngazi za uongozi wa juu,unaohusika na ardhi. Labda,hawa walikuwa wameshanunua. Ila sasa, ina maana kitengo hicho hakikupata malalamiko? Je,nchi hii, mtu anapoteleaje kusikojulikana! Mbona wakiamua kumtafuta tu ni masaa kadhaa wanae!
Harafu,kwa nini isitungwe sheria, ili tapeli au fisadi,ajue,ikibainika mali alizopata maelezo hayajitoshelezi, atafilisiwa. Sidhani kama wangeacha familia zao ziteseke.
Je,kama kiongozi,una raia aanyonge hivi, watakuelewa kweli? Je,swali la kujiuliza. Mtu hakuja na kuanza kuuza ardhi,lazima alishirikiana na watu. Itakuwaje watu hao hawajulikani walipo? Bila badhi ya watu kuwajibishwa,lazima mtindo ni huo huo.
Hao wanaotakiwa kuwafilisi nao ni wezi, ngoma ngumu hiyo!
 
Habari wakuu,naandika kidogo hapa maana mambo ni mengi,jana wakati naangalia taarifa ya habari nikaona habari kuwa kuna watu wametapeli wananchi zaidi ya milioni 900 kwa kuwauzia ardhi ambayo ni pori la serikali huko maeneo ya bagamoyo,hadi muda huu wananchi hao wamekwishajenga na ndipo imetoka kauli ya serikali kuwa wananchi wabomoe nyumba hizo kwa mikono yao wenyewe kabla serikali haijachukua hatua.

Mbaya zaidi viongozi wa kampuni iliyowauzia ardhi wametokomea kusikojulikana na bado wanasakwa.

Ninachojiuliza hadi watu wanauziwa maeneo hayo hadi inafika hiyo milioni 900 Wizara ya ardhi iko wapi?jeshi la polisi liko wapi?wale jamaa wa makumbusho ambao wakishalewa wanauliza unaniju mi ni nani wako wapi?je baadhi ya viongozi wakubwa wa serikali wanashiriki katika mipango ya aina hii?
Hiyo ni dhahiri wanashirikiana. Otherwise mtu anajenga Anavuta maji, umeme na huduma zingine za serikali hadi anamaliza serikali inaangalia tu.
 
Hao wanaotakiwa kuwafilisi nao ni wezi, ngoma ngumu hiyo!
Af sasa,watu wanadai demokalasia. Kwamba,mbona nchi furani wao wana demokalasia. Unajiuliza,wao huu ujinga wa matapeli wanaukumbatia? Msemo wa msanii alieimba kwamba wezi wamekumbatiwa. Mtu aanzishe ofisi,awe na nyaraka zote,auze,siku ya kwanza,ya pili,ya tatu na kuendelea,bila kujua ni nani?! Halipo. Mihela yote hiyo,mtu katokomea,hajulikani yuko wapi.
Bila kuongozwa na dikiteta haiwezekani. Sasa,mfano kama aliyenunua na kujenga kwa mkopo, ni mgeni wa nani!?
Serikali,kabla haijakusanya data zote za ardhi na kupimwa,ingetoa uamzi wa bila kununua pasipo mwanasheria. Wakati mwingine,haya matokeo ya madalali. Hivyo mwanasheria akijilidhisha na upatikanaji wa mali hiyo,raia alipie. Na mwanasheria awe anatambulika kweli,ili hata ikitokea amebolonga, mfuko wao uwajibishwe.
 
Back
Top Bottom