1979Magufuli
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 439
- 1,756
Kwanza agenda ya Mbowe na Chama chake anachokimiliki ilikuwa ni Katiba Mpya, wamepambana weeeee hoja yao imekufa kifo cha mende baada ya miswada kupitishwa bungeni na kuwa sheria.
Akawapotezea muda wanachama wenzake kwa kuona njia pekee ni maandamano, ameandamana weeeee wananchi hawamwelewi.Huko kwenye maandamano ameongea hadi amekaribia kupata shinikizo la damu lakini wapi.
Akaona achezee hela za chama wakaitana tena pale Mtwara wakatoka na azimio la maandamano katika miji mikuu ya mikoa na wilaya.Yaani mnasafiri kwenda mtwara mnaazimia kuandamana!
Sasa ameona njia pekee iliyobakia ni uzushi tu, akipanda stejini kulalamikia hali ngumu ya maisha, wabunge wamejiongezea mishahara, sijui Rais Samia kafanya hivi, yaani hana tena hoja.
Naona kuna siku atajichanganya atavunja sheria za nchi atarudi Ukonga kuendelea na maisha yale yale ya wakati ule.
Maana utaendelea kutoa taarifa za uongo hadi lini? Serikali ipi itakuangalia weeee uwe unapotosha na kuleta uchonganishi, hakyamungu Mbowe utayatimba tu.
Kumbuka mahabusu kuna joto sana, hakulaliki huko.Shauri yako.