Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo amewataka mabalozi wa mashina kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2024.
Akizungumza na mabalozi wa mashina katika kata ya Manzese baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wananchi Prof. Kitila amesema kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wananchi na viongozi wanapaswa kujiandaa na kuzungumza mambo yanayofanywa na Serikali.
Prof. Kitila amesema uchaguzi wa awamu hii utakuwa na ushindani mkubwa baina ya vyama vya siasa hivyo ipo haja ya kuweka wagombea wanaokubalika na Wananchi na siyo wanaopendwa na viongozi.
Amesema sheria ya uchaguzi imebadilishwa na hairuhusu mgombea kupita bila kupingwa, hivyo hata kama yupo mgombea mmoja zitapigwa kura za ndiyo au hapana hivyo ipo haja ya kujipanga kwaajili ya uchaguzi.
"Muwachuje wagombea vizuri ili mnaowapeleka kwa Wananchi wawe ni watu wanaokubalika na kuuzika, tusipeane wakati mgumu katika kutafuta kura kwa wananchi" amesema Prof. Kitila Mkumbo
Pia amesema hata ikitokea chama hakimpendi mtu lakini wananchi wanampenda apelekwe ili wananchi wawe na uhuru wa kuchagua, mambo mengine yatarekebishwa mbele na akitokea mgombea viongozi wa chama wanamtaka lakini wananchi hawamtaki huyo naye aachwe
Amewataka wajumbe wa mashina kuwa huru kumuita muda wowote wanaomuhitaji katika maeneo yao ili aweze kushirikiana na wananchi ili kusikiliza changamoto na maoni yao.