Serikali imechelewa kulipa vyama vya ushirika fedha zao, wana ushirika waanza kulalamika kushindwa kukopeshana kwa ukosefu wa fedha

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Ukikaa kwenye gambe lazima uwe na akili nyingi kama siyo maarifa. Walevi sometimes hatuna siri na tukipayuka tunaaminigi watu wote wameziba masikio.

Nimesikia mjadala kwamba serikali imechelewesha kulipa vyama vya ushirika fedha zao. Wanachama wamekuwa wakali kwa kukosa fedha za sikukuu. Wanaolalamika wanaamini mabenki baada ya kuona Saccos na vikoba vinakuja kwa kasi wamepanga njama vyama vya ushirika vife waanze kupata tena wateja.

Siku hizi wakopaji kwenye mabenki hasa watumishi wa umma wamepungua sana kutokana na riba kubwa wanazopigwa. Wengi wameanzisha vyama vya ushirika japo sijui uhusiano wa riba upoje kati ya benki na Saccos au vikoba ila its like kuna faida Saccos kuliko kukopa benki.

Hizi siyo taarifa njema kwa Mhe. Bashe, ushirika nimesoma kwenye website upo wizara ya kilimo. Anaowajibu wakulima vyama vya ushirika na kuvitetea visife kwa malengo ya mabenki na watu wachache wenye tamaa.

Endapo tukianza kucheza na fedha za Saccos na vicoba na mkafanikiwa kuvifulitia mbali kwa namna hawa wanaoitwa wanaushirika wanavyolalamika mtakuwa mmewaumiza na utatokea umaskini mkubwa sana.

Kama kuna mtu ambaye anayepewa mzuri kuhusu Saccos anaweza kutowekea hata tuwalinde watanzania wasipokonywe fursa hii yakusaidiana kwa mabeberu wachache wenye benki kunufaika.

Mabenki yakianza kushindana na Saccos taifa litakua. Tunatakiwa tuwasaidie wanyonge. Wapate mikopo waache kulalamika bar na kwenye mikusanyiko hasa kipindi hiki kigumu

Waziri fuatilia hoja hii uone kama kweli ipo hujuma hasa ikizingatiwa kipindi hiki kigumu cha ukwasi kuelekea desemba mabeberu wanajua piga ua watamishi na wanaushirika watakwenda kukopa benki kwa riba yoyote.

Umofia kwenu.......
 
Back
Top Bottom