Sensa 2012: Yanayojiri

nimeacha namba ya simu MLANGANO mkifika nipigieni 0717........................ mniulize maswali yenu :israel:
 
Anawacheka waislamu wenzake bwana Kikwete...anasema ni mkwara tu hawatakesha misikitini hakuna wapishi huko wakitoka tu wanahesabiwa kwa bluetooth.Anacheka sana bwana.
 
Mbona makarani hawana sare zilizokuwa zinasemwa kwenye vyombo vya habari, huku mpwapwa hawana sare tutawaaminije? vitambulisho pekee yake havitoshi,
 
Ama kweli Rais JK ni kiwango,kawaambia kama waislamu wanaona takwimu cyo sahihi watoe zao ili ngoma iwe droo, awashangaa waislamu kuishutumu serikali yake wakati wao wenyewe wanawajua waliotoa takwimu. Jipange

jk kwa majibu ya kiswahili namkubali anawapatia vizuri sana ndugu zetu, kuanzia pale alipowajibu kuhusu mahakama ya kadhi.!
 
Tena kuna zaidi ya matatizo, just imagine kwa mwaka huu 2012 kunafanyika zoezi la vitambusho na sensa. Kwa viongozi/watendaji wenye akili wangefikiria ku-merge ili fedha nyingine zikanunulie watoto wetu madawati huko shuleni. Ni aibu nchi hii yenye miti kila kona kukosa madawati

haaingii akilini hata kidogo , vitambulisho vya Taifa na sensa ni gharama kubwa sana kwa nchi kama Tanzania kufanya
hayo mambo mawili kwa wakati mmoja. Waalimu hakuna nyongeza ya mishahara , wabunge wao wanapeta tu .
 
Sioni sababu serikali kutoa mishipa ya shingo kukomalia kuhesabu watu kilazima , wakati wameshindwa kutumia nguvu hizo kulazimisha watu kushiriki chaguzi za serikali kuu ambazo ndio muhimili wa kutuletea maendeleo kwa kupata viongozi imara, wasafi na makini kuliko hiki kichuguu cha sensa.
Mfano uchaguzi wa 2010 ni asilimia 40 tu ya watu waliojiandikisha walipiga kura, halikadhalika uchaguzi mdogo wa igunga ni asilimia 33 tu ya wananchi waliojiandikisha walipiga kura na kule arumeru mashariki ni chini ya asilimia 50 ya waliojiandikisha walipiga kura.
Hivi vitisho na nguvu zinazo tumika sasa zilipaswa kutumika kwenye chaguzi husika.
Kama chaguzi kuu ambazo huigharimu serikali mabilioni ya pesa ya wapiga kura zimefanywa ni hiari kwanini sensa ifanywe ni lazima hata kulazimika kuwa tayari kuwapatia nyama pori adimu kama zebra, pombe haramu ya gongo kama wanavyo iita na bangi ili kuwa shawishi wahadzabe washiriki sensa ?

source: http://dailynews.co.tz/index.php/local-news/8801-hadzabes-ask-for-monkey-meat-during-census
 
Huku tumeambiwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wataanza saa tatu. Nimeambiwa wataanzia nyumba yangu, hapa nipo nawaandalia chai kabisa.
Kiongozi hiyo kilo yako ya sukari wawekee wengine hao jamaa wanapata posho, kwanza ukiwapa chai watachelewa kupita huku kwangu.
 
Ni punde Raisi wetu katoka kuelezea umuhimu wa sensa na kuwaomba na kuhimiza watu wahesabiwe. Ila kuna jambo moja kwa upande wangu sijamuelewa vizuri. kaulizwa swali na waandishi wa habari Je, watafanya nini kwa wanaosambaza sms kushawishi watu wasihesabiwe, jibu alilotoa ni rahisi kweli kwa hadhi yake, kasema "nasi tunatuma sms kuwashawishi wakubali kuhesabiwa, tutapambana nao hukohuko kwenye mitandao, tena zinatumwa kwa jina langu (raisi)" kiukweli pamoja na maelezo kuwa hao waliopo msikitini si watatoka tuu kama wamejifungia na wakitoka watahesabiwa. Binafsi naona kama kunamchezo wa kuigiza, kama kweli sheria ya uchaguzi inaelekeza nini cha kufanya kwa waliokiuka hili zoezi si muda wa kubembelezana. Kubembelezana sana huku kwa mambo ya msingi yanapoteza muda na kuchelewesha maamuzi ya msingi! NAPENDEKEZA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA WOTE WALIPOKIUKA WAZIWAZI.

MIMI NIMESHAHESABIWA, NAKUSHAURI NAWE UWE TAYARI KUHESABIWA!
 
lugha ya kiingereza inatafutanini,wameniuliza kama nina fahamu kiingereza.Je ina swii!!!!!!!!??????????
 
Hii ni kauli ameitoa JK WAKATI anahojiwa na tbc live alipoenda kuhesabima.ameulizwa swali na mwandishi wa habari namna ya serikal inavyochukua hatua kwa watu wanaotuma message kuhamasisha watu wasihesabiwe ndipo alipotoa hiyo kaul kwamba wao watume na sisi tunatuma zetu za kuwahamasisha watu kuhesabiwa tena zimeandikwa jina langu(kikwete).Je ni njia sahihi kwa raisi kutumia sms kuhamasisha watu? Je anawasiwasi na hotuba yake kwa wananchi,? Je wasaidizi wake wameshindwa kufanya kazi ipasavyo kutimiza wajibu wao? Nawasilisha.
 
Nachungulia dirishani, my niece kicking football hard na neighbours kids. Water tank is spilling water , jamani zimeni pump! Nasubiri makarani wa sensa.

Lol, siishi kufa mbavu zangu na JF. Mleta mada alikuwa anataka majibu mengine kabisa, ila mada imegeuzwa.
 
NIkishahesabiwa , nitafaidika na nanai Watanganyika . wanaosusia sena nawaunga mkono
 
Kimsingi waliolala nyumba za wageni ndio target mojawapo ya kwanza. Then asubuhi ndo wanapita kwenye makazi ya watu. Midamida wamenigongea, nikatoa ushirikiano.
 
Ni punde Raisi wetu katoka kuelezea umuhimu wa sensa na kuwaomba na kuhimiza watu wahesabiwe. Ila kuna jambo moja kwa upande wangu sijamuelewa vizuri. kaulizwa swali na waandishi wa habari Je, watafanya nini kwa wanaosambaza sms kushawishi watu wasihesabiwe, jibu alilotoa ni rahisi kweli kwa hadhi yake, kasema "nasi tunatuma sms kuwashawishi wakubali kuhesabiwa, tutapambana nao hukohuko kwenye mitandao, tena zinatumwa kwa jina langu (raisi)" kiukweli pamoja na maelezo kuwa hao waliopo msikitini si watatoka tuu kama wamejifungia na wakitoka watahesabiwa. Binafsi naona kama kunamchezo wa kuigiza, kama kweli sheria ya uchaguzi inaelekeza nini cha kufanya kwa waliokiuka hili zoezi si muda wa kubembelezana. Kubembelezana sana huku kwa mambo ya msingi yanapoteza muda na kuchelewesha maamuzi ya msingi! NAPENDEKEZA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA WOTE WALIPOKIUKA WAZIWAZI.

MIMI NIMESHAHESABIWA, NAKUSHAURI NAWE UWE TAYARI KUHESABIWA!

Nyerere wakati anataifisha shule za wakristo, alisema, hawa wenzetu waislamu , hawakusoma, kama tusipowapa elimu ya kutambua zuri na baya, watalisumbua taifa hili. Akataifisha shule zote zikawa za serikali. Huyu Baba wa Taifa aliona mbali. Kinachowasumbua waislamu (baadhi na sio wote tafadhali) ni finyu wa elimu -illiteracy. sidhani kama kuna any educated moslem yupo katika malumbano hayo. Samahani kwa nitakao wakwaza!!! What is wrong with kuhesabiwa?
 
Hata wakati wa utawala wa mfalme Herode walifanya sensa na kila mtu alihesabiwa katika mji aliozaliwa. Mie na familia yangu tutahesabiwa. Ili msiniulize sababu ya sensa wakati wa mfalme Herode maana sikumbuki mpaka nisome hiyo aya

Ilikuwa ni amri ya Octavius Cesar a.k.a Emperor Augustus wa Roma, lengo likiwa ni kujua idadi ya wakazi wote wa himaya ya Roma, kujua dunia nzima ina raia wangapi wa Kaizari.
 
Huyu mzee haish vituko, labda anazo namba za watanzania wote, ngoja nami nisubiri mesej yake
 
Back
Top Bottom