Bungeni: Tanzania imefikia kiwango cha 83% cha kujua Kusoma na Kuandika miongoni mwa Watu wazima

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Kulingana na Ripoti iliyotolewa na NBS, kwa sensa ya 2022 Tanzania imefikia kiwango cha 83% cha kujua kusoma na kuandika miongoni mwa watu wazima yaani miaka 15 na kuendelea ikiwa ni ongezeko la 6.3% toka 78.1% cha sensa ya 2012.

Katika kuhakikisha Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika, Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imeendelea kutekeleza afua mbalimbali ikiwemo kuondoa vikwazo vya kupata elimu kama vile kutolewa kwa elimu ya msingi bila ada, elimu ya lazima sasa kuwa ya miaka 10, kutekeleza programu zenye lengo la kuwafikia Watanzania waliokosa fursa za elimu kwa mfano: Elimu ya Watu Wazima na ujifunzaji endelevu, utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kisomo pamoja na kutoa fursa kwa wanafunzi walioacha masomo kwa sababu mbalimbali kurudi shuleni na kuendelea na masomo (re-entry program) kupitia Waraka Na. 2 wa mwaka 2021.

Pamoja jitihada hizo, Serikali imeendelea kuboresha huduma za maktaba nchini katika ngazi za Mikoa, Wilaya na shule ikiwa ni pamoja na maktaba mtandao ili kuwawezesha Watanzania wengi zaidi katika maeneo mbalimbali kupata huduma ya kujisomea huko waliko.

Aidha, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa lengo la kuongeza fursa kwa Watanzania wengi zaidi kujiunga na Elimu ya Watu Wazima.
 
Kujua kusoma na kuandika ni jambo moja na kuwa na akili nzuri ni jingine.
Kuna changamoto ya kupungua kwa fikra chanya hali ambayo inasababisha kushindwa kwa wasomi wengi kutoa hoja zenye mantiki.
 
Shida ya serikali yeti inapenda kujigamba saaan lakin ukisema ufatilie we mwenyw data official hawana
Mfano mdog tyu ukisema uchukue wanafunzi waliotoka f6 mwakajan na sasa wapo chuon Kam wanafunz wa mwaka wa kwanz
Hao walisifiwa kwamba ufaulu wao wa advance ulikuwa Kwa asilimia kubwa zaidi mpk kufikia 80%+
But nend kaanz kufuatilia kuanzia walipoanz dars la kwanz mwak 2010 hutopewa data kamilii ambayo inaonesh mwenendo wa watoto hao kila mwaka mpk kufikia mwaka 2023
So Kwa Mimi naon Bado Kwa izo data tunazopewa hap na waziri hazina mashiko kbs
 
Back
Top Bottom