Sasa nahama CCM

Unafuata mtu au unafuata sera za chama na utekelezaji wa ilani?Taifa linapoteza muelekeo kwakuwa na watu wa aina yako
 
Nyie ndiyo bendera fuata upepo. Msomi mzima unashindwa kuja na hoja za msingi badala yake unakuja na hoja za chekechea!!!!
 
Hii ndiyo inyokufaa!!We ni sawa na mbwa aliyetapika then karudia matapishi yake!! red card.jpg
 
Ni kwa sababu ya kuridhika na Team iliyochaguliwa kuongoza CCM 2012 - 2017. Na hasa Philip Mangula. CCM OYEEEEEE!!!!!!!

Ni kama ulivyoridhika kwa JK, subiri utaipata, unadhani simba mzee hana meno!

Aliachwa kwenye ulaji, sasa amerudishwa rasmi na yeye akuvune!
 
Nimekuwa mwanachama mfu wa CCM kwa muda mrefu, hasa baada ya kuchoka kuishi katikati ya uozo wa kisiasa ndani ya chama hicho. Nimekuwa nikisita sita kwa kuwa sikuwa na uhakika kama kweli vyama vya upinzani viko 'serious'.

Nilikuwa nasubiri kuvipima kwenye matukio mazito maana bila matukio mazito kila kimoja kilionekana chama cha upinzani. Leo hii baada ya matukio mazito ikiambatana na baadhi ya vyama kupewa rushwa ya madaraka na CCM, ndipo imethibitika kuwa kuna chama kimoja makini cha upinzani nchi hii.

Baada ya leo hii CHADEMA kufanya tukio la kishujaa bila kujali kwamba watakosa madaraka haya au yale bali kwa kuweka maslahi ya haki ya wapiga kura wa Tanzania mbele, sasa nimeamua rasmi kuhama CCM na uanachama wangu mfu na sasa nahamia CHADEMA.

Ninahama na kundi la wapiganaji zaidi ya hamsini tulio kwenye maeneo nyeti sana katika nchi hii.

Buriani CCM, Buriani CUF, Buriani wasaliti wote.


NIMERUDI CCM

Ni kwa sababu ya kuridhika na Team iliyochaguliwa kuongoza CCM 2012 - 2017. Na hasa Philip Mangula. CCM OYEEEEEE!!!!!!!

CCM ni chama sikivu, Mwenyekiti na viongozi wenzake wamesikiliza vilio vya wananchi, CCM imerudishwa kwa wananchi, wajumbe wa NEC tumewachagua tokea vijijini kwetu, kwenye matawi yetu, hata wanyonge tumeshirikishwa kuongoza nchi. Na sasa wakulima wenzetu kina Mangula wako kwenye uongozi. Kwa hekima ya ajabu ya mwenyekiti, ufisadi umebomolewa kabisa, na sikutegemea kabisa kama Jakaya Kikwete angeweza lakini ameweza.

Nyinyi mnaobisha ni kwa sababu mnasimuliwa mambo, mimi nayaona kwa macho yangu. Mimi kamwe sitaingia kwenye uongozi wa siasa na hivyo sina tabia ya kujipendekeza kwa kutaka uongozi. Mimi nina kazi yangu binafsi isiyohitaji kubebwa na mtu na inanitosha, ila sikuzaliwa mtanzania ili kukodolea macho watu wanaoharibu Taifa hili. Hilo siwezi kulikubali kamwe.

Ukweli ni kuwa chini ya uongozi wa Jakaya Kikwete, nilifika mahala nikadhani amekuwa msaliti, sikujua kuwa mbinu zake za kuipigania nchi hii zilikuwa za hali ya juu mno. JK ni kama mchora picha mahiri ambaye anapoanza kuchora unaweza kudhani kuwa anaharibu lakini akimaliza ndiyo unaona picha kamili, picha nzuri, picha iliyojaa ushindi kwa watanzania.

Kwa kweli umahiri wa JK umenifanya nirudi CCM huku nikiona aibu kubwa kwa kumhukumu kiasi cha kumtukana na kumtakia mabaya na kumbe yeye alikuwa akifanya mema kwa ajili ya nchi hii. Furaha niliyo nayo inaizidi aibu niliyo nayo kwa kumchukia bure mtetezi wa kweli wa Taifa langu.

CCM ni chama sikivu, ni chama cha wanyonge. CHADEMA ni chama cha siasa kali, fikira mgando. Ndani ya CHADEMA namewaona watu wachache sana wa maana, mfano Zito Kabwe na Shibuda . Wengine wote ni watu ambao hawataki kufikiri; yaani hata jambo likiwa kwa manufaa ya taifa ili muradi linatoka CCM wao wanalipinga tena hata bila kuboresha.

CHADEMA hawana uwezo wa kutoa hoja bila kuchonganisha wananchi na serikali yao. Kuna watu CHADEMA wanatamani kuhamia Syria au Somalia kwa sababu ya kupenda vita. CHADEMA wanatamani kuingia Ikulu kwa uongo na kwa wale wanaodhani kuwa CHADEMA ni chama cha wakatoliki hiyo siyo kweli, hawa wengi wao ni freemasons, wazee wa ma'casino', watoa kafara mikutanoni wakihakikisha damu inamwagika ili wananchi waone polisi wanaua kumbe wao wametoa kafara kwa mashetani.

CCM pekee ndiyo chama chenye kuweka maslahi ya Taifa mbele.

CCM DAIMA!!!!!!!

Haya wale waongo naoitwa CHADEMA mpoooo?

Kwa wale msiojua maana ya PEEEOPLEEE POWER! Mnashangilia tu. Maana yake ni kuwa wanapotoa kafara ya mtu kwenye mikutano yao wao inawapa nguvu. mashetani sana hawa CHADEMA. Pole ninyi mnaoshangilia CHADEMA kama vipofu.
 
People's Power siyo nguvu ya umma kama CHADEMA wanavyodanganya wananchi. CHADEMA wanaamini katika kutoa kafara wananchi wasio na hatia katika mikutano yao na kuisingizia serikali. Mbinu wanayotumia ni ya hali ya juu mno.

Lengo lao ni kutafuta 'public sympathy', na mimi ni mmoja wa wasomi tuliodanganyika kabisa. Tulihama CCM, tukahamia CHADEMA ile baada ya kuwa CHADEMA tulikutana na madudu ya kufa mtu.

Ikafika mahala nikaona sasa basi tena. Maana niliyoyakimbia CCM yakaonekana matakatifu kuliko uozo nilioukuta CHADEMA. Hapo nikatamani hata kukimbia nchi.

Lakini CCM kumbe ilikuwa ikitengeneza mambo, CCM imeweza, hongera sana wote ambao hawakuhama CCM, Wameonyesha kuwa wao ni majasiri, hawakukumbia matatizo bali wamekaa wakayatatua, wametupa somo kubwa sisi ambao tulikimbia. Wanachama wa CCM ambao hawakutikiswa na nguvu ya soda, bali walikaa wakatatua matatizo ndani ya chama na sasa CCM ni Imara kabisa.

CCM daima!!!!!
 
Wanaoipeleka CDM Magogoni kwa maneno ya kelele za debe tupu lisiloacha kutika hawazipimi nyakati, Kama wanachama wao wanaifagilia CCM kweupe mbele ya kadamnasi wanategemea nini, uteuzi wa Philip Mtu mwadilifu ambaye hana kelele ambaye hata mafisadi walipomuengua hakupiga kelele ni mwanzo wa kufa kwa kundi linalokata mizizi ya CCM. Mbali na utekelezaji wa ilani ya CCM wapinzaji wasubili kuona machine itakayosimamishwa 2015 mwezi May, naamini baadhi ya wanaohama watavitelekeza vyama vyao bila kuaga. nawashauri warudi mapema.
 
Tulikuwa tunasubiri CCM ichague timu yao WANAOIITA YA USHINDI ili na sisi CHADEMA tuanze safari yetu rasmi ya KUELEKEA 2015 muda si mrefu mtasikia kwenye vyombo vya habari MWELEKEO YA CHADEMA 2015!
 
'Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa' Wako radhi kupotosha ukweli kwa kuwa tu wameahidiwa cheo ama kupewa fedha...wanasahau kabisa kwamba kuna mtoto wa mkulima kabla ya huyu mlima nyanya lakini hakukuwa na mabadiliko sana.Ni kujikabidhi kwa shetani kueneza uongo eti watu fulani wanaua watu ili wapate nguvu, je,unapokuwa unasema hayo kisa tu unatumika kisiasa,hufikiri kama CHADEMA wangefanya hivyo wangekimbiwa na wananchi bila kusukumwa wafanye hivyo. Ni kwa nini hatumshirikishi Mungu kwenye maono yetu? Kisa hela tu,upo tayari kujitoa ufahamu kujiita ulikuwa CHADEMA kumbe hujawahi kuwa hata kwa dakika...kumbuka jf haina mpaka.Kwa wasomi kweli na wenye hofu ya Mungu walioko ughaibuni wanapata tabu kujua msomi wa Tanzania anatakiwa aweje? Umasikini,ujinga,maradhi na ufisadi unaolikumba taifa unaishi vichwani mwenu.Je,ulimsikia mfuasi wa democratic akiwatuhusu republican kwa sera zisizoishi freemasons na uchawi nje ya Uchumi,afya,kilimo na biashara?
 
Sina uhakika sana na hayo uliyoyasema kuhusu freemason pamoja na casino maana kabla ya ujio wa vyama hivo vitu vilikuwepo jariau kujenga hoja yenye mantiki
 
Wanaoipeleka CDM Magogoni kwa maneno ya kelele za debe tupu lisiloacha kutika hawazipimi nyakati, Kama wanachama wao wanaifagilia CCM kweupe mbele ya kadamnasi wanategemea nini, uteuzi wa Philip Mtu mwadilifu ambaye hana kelele ambaye hata mafisadi walipomuengua hakupiga kelele ni mwanzo wa kufa kwa kundi linalokata mizizi ya CCM. Mbali na utekelezaji wa ilani ya CCM wapinzaji wasubili kuona machine itakayosimamishwa 2015 mwezi May, naamini baadhi ya wanaohama watavitelekeza vyama vyao bila kuaga. nawashauri warudi mapema.

oops! Kumbe unaimba!
 
Back
Top Bottom