Sasa nahama CCM

Nimekuwa mwanachama mfu wa CCM kwa muda mrefu, hasa baada ya kuchoka kuishi katikati ya uozo wa kisiasa ndani ya chama hicho. Nimekuwa nikisita sita kwa kuwa sikuwa na uhakika kama kweli vyama vya upinzani viko 'serious'.

Nilikuwa nasubiri kuvipima kwenye matukio mazito maana bila matukio mazito kila kimoja kilionekana chama cha upinzani. Leo hii baada ya matukio mazito ikiambatana na baadhi ya vyama kupewa rushwa ya madaraka na CCM, ndipo imethibitika kuwa kuna chama kimoja makini cha upinzani nchi hii.

Baada ya leo hii CHADEMA kufanya tukio la kishujaa bila kujali kwamba watakosa madaraka haya au yale bali kwa kuweka maslahi ya haki ya wapiga kura wa Tanzania mbele, sasa nimeamua rasmi kuhama CCM na uanachama wangu mfu na sasa nahamia CHADEMA.

Ninahama na kundi la wapiganaji zaidi ya hamsini tulio kwenye maeneo nyeti sana katika nchi hii.

Buriani CCM, Buriani CUF, Buriani wasaliti wote.

Hongera kwa uamuzi wa busara na jiandae kushiriki katika mapambano ya kuleta demokrasia ya kweli. Itabidi ufunge mkanda kwani bila kudanganya miaka inayokuja itakuwa ya mapambano makubwa na wale wenye mioyo miepesi watazimia na kuweweseka. Hivyo ni lazima kuwa na moyo jasiri ikiwa ni pamoja na kujisadikisha.
 
HAMENI NYOTE, KWANI MLILAZIMISHWA KUKAA CCM?? OPPORTUNISTS WAKUBWA NYIE.:nono:
Mwalimu alisema "CCM si mama yangu." Sasa kama mwanzilishi anasema CCM si mama yake je wale waliojiunga na wakaamua kuhama wanakosa gani. Naona nikusamehe kwani umazungumza kwa kuhamaki na kukurupuka kwani katika mazingira hayo akili haitumiki ila makamasi.
 
Hii kali, hivi makamasi na akili huwa vimekaribiana eeh!
 
Mshukuru mungu kukuonyesha alama za nyakati na kuacha kuunga mkono mafisadi
 
karibu tena! ila broda ya kikushinda nafasi ipo wazi katika chama tawala! kijani daima
 
CCM ya sasa siyo ile tuliyoijua, ya Wakulima na Wafanyakazi. Ya sasa ni genge tu la walafi na mafisadi.
 
We did not even notice you existed. Its better to die in CCM than being alive in CHADEMA.

Umekosa madaraka and now you are crossing over, uchaguzi umepita unafuata nini huko?

Kukaa ccm ni kupoteza uhuru na kuchagua kuishi maisha ya UNAFIKI siku zote. Wanachama wengi wa ccm wanakasirishwa sana na namna chama chao kinavyoendeshwa lakini kwenye vikao halali vya chama hawasemi. Wanaishia kulalamika vijiweni. Ndiyo maisha ya ccm.
 
Akashube,
Hauko peke yako. Katika matanuzi yangu bongo hivi karibuni nimekutana na wana CCM wengi tu ambao wako disillusioned na chama chao.
Wengi wametoa mchango wa hali na mali kwa CHADEMA na baadhi wanaendelea kutoa mchango wa mawazo na ushauri. CHADEMA is a growing party. CCM is Titanic na wote waliomo kuna wakati watatambua kuwa wamekwaa meli inayozama.
Jasusi... now you understand my signature

i misplace my optimism and gave too much trust on a pact of inhumane selfish dudes... my heart is broken
 
Nimekuwa mwanachama mfu wa CCM kwa muda mrefu, hasa baada ya kuchoka kuishi katikati ya uozo wa kisiasa ndani ya chama hicho. Nimekuwa nikisita sita kwa kuwa sikuwa na uhakika kama kweli vyama vya upinzani viko 'serious'.

Nilikuwa nasubiri kuvipima kwenye matukio mazito maana bila matukio mazito kila kimoja kilionekana chama cha upinzani. Leo hii baada ya matukio mazito ikiambatana na baadhi ya vyama kupewa rushwa ya madaraka na CCM, ndipo imethibitika kuwa kuna chama kimoja makini cha upinzani nchi hii.

Baada ya leo hii CHADEMA kufanya tukio la kishujaa bila kujali kwamba watakosa madaraka haya au yale bali kwa kuweka maslahi ya haki ya wapiga kura wa Tanzania mbele, sasa nimeamua rasmi kuhama CCM na uanachama wangu mfu na sasa nahamia CHADEMA.

Ninahama na kundi la wapiganaji zaidi ya hamsini tulio kwenye maeneo nyeti sana katika nchi hii.

Buriani CCM, Buriani CUF, Buriani wasaliti wote.

Ungehama kabla ya uchaguzi ningekudondoshea kasenksi. unakumbuka shuka alfajiri? we baki huko huko CCM
 
HAMENI NYOTE, KWANI MLILAZIMISHWA KUKAA CCM?? OPPORTUNISTS WAKUBWA NYIE.:nono:

Waacheni watu wahame na kuingia. Itafikia EQUILIBRIAM ambapo wanaotoka na kuingia watakuwa sawa. Hii ndo kusema kuwa, Tanzania itakuwa na vyama viwili tu wakati huo, yaani chama Tawala na chama cha upinzani. Chama tawala chaweza kuwa TLP, PTL, CCM, MCC, CHADEMA, MADECHA, etc... na chama cha upinzani cha weza kuwa mwungano wa vilivyopo au vitakavyokuja.....

NATURE will take its course.....the power of nature is much stronger than TANKS of intercontinental balistic misiles
 
We did not even notice you existed. Its better to die in CCM than being alive in CHADEMA.

Umekosa madaraka and now you are crossing over, uchaguzi umepita unafuata nini huko?

Du! Nadhani mapenzi yako juu ya CCM ni zaidi ya Nyerere aliyesema CCM si baba na si mama yangu.

Sasa ulitaka ahamie kabla ya uchaguzi kwani amekwambia anahamia CHADEMA kwa lengo la kupata uongozi? Hii inadhihirisha kuwa anahamia kwa mapenzi yake na si kwa kutafuta uongozi. Soma tena post yake kwa makini.
 
Wenye mapenzi ya kweli wanahama CCM na kuhamia CHADEMA, wanabaki walioenda kutafuta ulaji. Wao na uchaguzi na uteuzi na takrima...basi. Hata wakati unapohama baadhi wanakwambia subiri huku....kazi ni nyingi, unapowaambia huna haja na ulaji wao hawaamini kabisa.

CCM wa sasa hawa waliochakachuliwa wakiongozwa na JK wao, hawaamini kama mtu anaweza kuwa kwenye chama kwa mapenzi halisi ya nchi yake na chama chake na sio ulaji.

CCM ya sasa imeoza.
 
Ukishajua hivyo ni vyama vya msimu utajirudisha mwenyewe kama ng'ombe anavyorudi zizini kwake.
 
Nimekuwa mwanachama mfu wa CCM kwa muda mrefu, hasa baada ya kuchoka kuishi katikati ya uozo wa kisiasa ndani ya chama hicho. Nimekuwa nikisita sita kwa kuwa sikuwa na uhakika kama kweli vyama vya upinzani viko 'serious'.

Nilikuwa nasubiri kuvipima kwenye matukio mazito maana bila matukio mazito kila kimoja kilionekana chama cha upinzani. Leo hii baada ya matukio mazito ikiambatana na baadhi ya vyama kupewa rushwa ya madaraka na CCM, ndipo imethibitika kuwa kuna chama kimoja makini cha upinzani nchi hii.

Baada ya leo hii CHADEMA kufanya tukio la kishujaa bila kujali kwamba watakosa madaraka haya au yale bali kwa kuweka maslahi ya haki ya wapiga kura wa Tanzania mbele, sasa nimeamua rasmi kuhama CCM na uanachama wangu mfu na sasa nahamia CHADEMA.

Ninahama na kundi la wapiganaji zaidi ya hamsini tulio kwenye maeneo nyeti sana katika nchi hii.

Buriani CCM, Buriani CUF, Buriani wasaliti wote.

karib chadema.
 
Ni kwa sababu ya kuridhika na Team iliyochaguliwa kuongoza CCM 2012 - 2017. Na hasa Philip Mangula. CCM OYEEEEEE!!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom