Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .
Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.
Na alivyojibu Njiwa ndivyo tunavyopaswa kuwa JF Members wote ambao tunajitambuwa, nimemgongea Like lakini Error occurred.Mkuu njiwa tangu umejiunga na JF 16 April 2009 hakuna bandiko la maana kuliko hili Bravo Njiwa.
Amesema kuwa " wananchi wa Mikoa ya Mbeya,Iringa na Ruvuma wasiwe na wasiwasi kwani Tanzania iko tayari kupambana na uchokozi wowote ule kutoka kwa Malawi"
Hii ni kauli nzito ya kuashiria kuwa tayari kwa mapambano na Malawi ni kauli ya kutangaza Vita na ni kinyume na katiba angeweza kusema kuwa tuko macho na tunafuatilia kinachoendelea ila kusema tupo tayari kwa mapambano na uchokozi wowote ni vita hiyo......
najua uzalendo unashuka kutokana na siasa za alijojo ndani ya nchi yetu na mikataba mibovu na wawekezaji lakini hata ikiwa vipi mkuu! mambo yetu ya ndani tutayamaliza mwenyewe iwe siasa au itikadi yoyote ... lakini sio anakuja mgeni wa nchi jirani na kuingilia mipaka ya nchi yako kwa nguvu na hataki kukaa kwenye meza ya maongezi wakati wewe unaumiza kichwa utatue vipi hili tatizo kuna mpumbavu flani anashangilia " bora wachukue eti hainisaidii hata kama ukiwa ni upande wetu .." huo utakuwa ni ukhanithi sasa
Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .
Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.[/QUOTE
IVI UNAJUA KUTANGAZA VITA KUKOJE? SAWA HATUKULAUMU SANA NI KUKOSA ELIMU MAKINI TU HUKO,SASA NA HUU MGOMO WA WALIMU SIJU NA KIZAZI CHAKO KITAFWATA NYAYO ZAKO! au ndo mpaka kieleweke!
malawi wanadai ziwa nyasa ni la kwaoKuna nini kimetokea kwani mpaka atoe kauli hiyo??
We waache... Sie tunawacheki tuuu.. Na hivi wanajeshi wetu hawaja practice vita siku nyingi..
Njiwa,
Ndio maana niliweka bandiko kule nyuma hawa Wamalawi they are arrogant imbecile na ndio maana mnakaa nao katika meza wanasema hili. Wakitoka kurudi kwao wanasema lile. Sasa wafahamu enough is enough hatuwezi kuchezewa masharubu mwanaume mzima ukakaa na kubaki unacheka. Na nimesisitiza Mheshimiwa Rais wetu afahamu ijapokuwa tunatofautiana kiitikadi na kisiasa but linapokuja suala la nchi uzalendo wa kulinda nchi yetu tuko pamoja naye kinguvu kazi na kimaarifa. Tanzania ina jambo moja inajivunia tuna umoja wa hali ya juu hatubaguani na hilo mtu wa nje akituchezea ndio ataliona wazi wazi. Tunalinda nchi yetu kwa lolote.
Mkuu mbona hufundishiki?wenye busara wamejaribu kukuelewesha lakini unang'ang'ania hapo hapo ulipojikwaa! Kauli ya Tanzania iko tayari kupambana na uchokozi wowote toka Malawi si kutangaza vita hata kidogo kwani haiwezi kuidhinisha matumizi ya fedha kugharimia vita wala kuruhusu matumizi ya silaha na lojistics za Jeshi.Amesema kuwa " wananchi wa Mikoa ya Mbeya,Iringa na Ruvuma wasiwe na wasiwasi kwani Tanzania iko tayari kupambana na uchokozi wowote ule kutoka kwa Malawi"
Hii ni kauli nzito ya kuashiria kuwa tayari kwa mapambano na Malawi ni kauli ya kutangaza Vita na ni kinyume na katiba angeweza kusema kuwa tuko macho na tunafuatilia kinachoendelea ila kusema tupo tayari kwa mapambano na uchokozi wowote ni vita hiyo......huku ni kutangaza na sio kwamba namlisha maneno./
Naona yuko bize kutafakari gazeti jngine la kulifungia na jinsi ya kum-ulimboka "mchochezi" wa mgomo wa walimu.Kauli ni safi na ya kishujaa ambayo the chicken jk hawezi kutamka, na sidhani kama sitta katamka kwa kukurupuka but after consultation na ni vema amesema hivyo ili kuonesha tunajali mipaka yetu na tuko tayari kutetea, amiri jeshi mkuu jk alitakiwa aseme kabla but unfortunately he is too chicken even to give a bluff! Bravo mr. Zambi kwa kuibua hoja maana suala hili lilikuwa linatuumiza wengi!
Usimlishe maneno, yule bwana ana busara anajua mwenye mamlaka ya kutangaza vita ni amiri jeshi mkuu pekee; alichofanya ni kuwaweka sawa wanachi kwamba serikali iko macho kuhusu hali hiyo ili kuondoa dukuduku miongoni mwa wananchi.
Tofautisha kauli ya Sitta na hii hapa:
"Sasa tutampiga nduli iddi Amin;
Nia ya kumpiga tunayo;
Sababu ya kumpiga tunayo na
Uwezo wa kumpiga tunao".
J.K. Nyerere; October 1978.