Samwel Sitta: Tanzania iko tayari kupambana na aina yoyote ya uchokozi kutoka Malawi!

Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .

Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.

mi nmegundua kitu kimoja nduguzanguni.upinzani ukizidi sana mwisho mtu unakua KILAZA....sababu ishu ndogo tu utaigeuzaaa ili mradi iwe ya kipinzani.elewa kwanza then ndio ulete hoja.sometimes unaweza hata kuiweka hii thread kikuliza kua mh.sitta alikua anakusudia nn?kuuliza c uhuni wakuu.
 
Mkuu njiwa tangu umejiunga na JF 16 April 2009 hakuna bandiko la maana kuliko hili Bravo Njiwa.
Na alivyojibu Njiwa ndivyo tunavyopaswa kuwa JF Members wote ambao tunajitambuwa, nimemgongea Like lakini Error occurred.
Safi sana. What i can say, Matola says thanks for this useful post.
 
Wakuu hii issue ni nzito ingawa sitegemei izidi ile ya Nduli enzi za Mwalimu. Hata hivyo, sio busara sana ku-under estimate nguvu za hawa jamaa kama tulivyozoea kuchezea ile midebwedo ya pale ng'ambo. Malawi ni dola kamili na hatuwezi kujua wamejiandaa vipi.

Naweka vizuri kale ka cheti kangu ka Makutupora JKT nikisubiri kwa hamu kuitwa front-line kuipigania nchi yangu. Mungu akiwa upande wetu nani atakuwa juu yetu?

Mungu Ibariki Tanzania; Linda na Mipaka Yake. Amen.
 
Amesema kuwa " wananchi wa Mikoa ya Mbeya,Iringa na Ruvuma wasiwe na wasiwasi kwani Tanzania iko tayari kupambana na uchokozi wowote ule kutoka kwa Malawi"

Hii ni kauli nzito ya kuashiria kuwa tayari kwa mapambano na Malawi ni kauli ya kutangaza Vita na ni kinyume na katiba angeweza kusema kuwa tuko macho na tunafuatilia kinachoendelea ila kusema tupo tayari kwa mapambano na uchokozi wowote ni vita hiyo......

Mkuu unajiaibisha tu hapo!!
 
Waache wachukue kwani sisi linatusaidia nin,nchi la kipumbavu hili..
 
Final 6 umevunja ukimya I like it kwa kuwaonya Malawi japo mtoa hoja kapotosha kuwa ametangaza vita. Big up 6
 
Crisis is it real or diversionary tactic kutupumbaza kusahau matatizo ya ndani ya nchi?
 
najua uzalendo unashuka kutokana na siasa za alijojo ndani ya nchi yetu na mikataba mibovu na wawekezaji lakini hata ikiwa vipi mkuu! mambo yetu ya ndani tutayamaliza mwenyewe iwe siasa au itikadi yoyote ... lakini sio anakuja mgeni wa nchi jirani na kuingilia mipaka ya nchi yako kwa nguvu na hataki kukaa kwenye meza ya maongezi wakati wewe unaumiza kichwa utatue vipi hili tatizo kuna mpumbavu flani anashangilia " bora wachukue eti hainisaidii hata kama ukiwa ni upande wetu .." huo utakuwa ni ukhanithi sasa

Njiwa,

Ndio maana niliweka bandiko kule nyuma hawa Wamalawi they are arrogant imbecile na ndio maana mnakaa nao katika meza wanasema hili. Wakitoka kurudi kwao wanasema lile. Sasa wafahamu enough is enough hatuwezi kuchezewa masharubu mwanaume mzima ukakaa na kubaki unacheka. Na nimesisitiza Mheshimiwa Rais wetu afahamu ijapokuwa tunatofautiana kiitikadi na kisiasa but linapokuja suala la nchi uzalendo wa kulinda nchi yetu tuko pamoja naye kinguvu kazi na kimaarifa. Tanzania ina jambo moja inajivunia tuna umoja wa hali ya juu hatubaguani na hilo mtu wa nje akituchezea ndio ataliona wazi wazi. Tunalinda nchi yetu kwa lolote.
 
Nimeshtushwa na tamko ambalo amelitoa muda huu bungeni kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kwa uchokozi wa aina yeyote kutoka Malawi na ametoa tamko hilo kama kaimu waziri Mkuu .

Tamko hili kalitoa kwa niaba ya Serikali sasa hii ni hatari kama Kaimu waziri Mkuu anaweza kutangaza vita na hii ni kinyume na katiba yetu mwenye mamlaka hiyo ni Rais ambaye ni Amir Jeshi Mkuu.
[/QUOTE

IVI UNAJUA KUTANGAZA VITA KUKOJE? SAWA HATUKULAUMU SANA NI KUKOSA ELIMU MAKINI TU HUKO,SASA NA HUU MGOMO WA WALIMU SIJU NA KIZAZI CHAKO KITAFWATA NYAYO ZAKO! au ndo mpaka kieleweke!
 
Wacha amsaidie Pinda na bosi wake. Pinda angeishia kupiga porojo tu na bosi wake angepiga smile tu ili picha zitoke vizuri kwenye magazeti.
 
Njiwa,

Ndio maana niliweka bandiko kule nyuma hawa Wamalawi they are arrogant imbecile na ndio maana mnakaa nao katika meza wanasema hili. Wakitoka kurudi kwao wanasema lile. Sasa wafahamu enough is enough hatuwezi kuchezewa masharubu mwanaume mzima ukakaa na kubaki unacheka. Na nimesisitiza Mheshimiwa Rais wetu afahamu ijapokuwa tunatofautiana kiitikadi na kisiasa but linapokuja suala la nchi uzalendo wa kulinda nchi yetu tuko pamoja naye kinguvu kazi na kimaarifa. Tanzania ina jambo moja inajivunia tuna umoja wa hali ya juu hatubaguani na hilo mtu wa nje akituchezea ndio ataliona wazi wazi. Tunalinda nchi yetu kwa lolote.

Mdondoaji, nakubaliana na wewe kabisa. Hapa watanzania wote tunatakiwa kuungana na kukomesha huu uhuni wa Malawi. Serikali iweke kambi ya nguvu huko Kusini na kama issue ni bora wananchi tukachanga ili kuwezesha hili.
 
Kauli ni safi na ya kishujaa ambayo the chicken jk hawezi kutamka, na sidhani kama sitta katamka kwa kukurupuka but after consultation na ni vema amesema hivyo ili kuonesha tunajali mipaka yetu na tuko tayari kutetea, amiri jeshi mkuu jk alitakiwa aseme kabla but unfortunately he is too chicken even to give a bluff! Bravo mr. Zambi kwa kuibua hoja maana suala hili lilikuwa linatuumiza wengi!
 
Amesema kuwa " wananchi wa Mikoa ya Mbeya,Iringa na Ruvuma wasiwe na wasiwasi kwani Tanzania iko tayari kupambana na uchokozi wowote ule kutoka kwa Malawi"

Hii ni kauli nzito ya kuashiria kuwa tayari kwa mapambano na Malawi ni kauli ya kutangaza Vita na ni kinyume na katiba angeweza kusema kuwa tuko macho na tunafuatilia kinachoendelea ila kusema tupo tayari kwa mapambano na uchokozi wowote ni vita hiyo......huku ni kutangaza na sio kwamba namlisha maneno./
Mkuu mbona hufundishiki?wenye busara wamejaribu kukuelewesha lakini unang'ang'ania hapo hapo ulipojikwaa! Kauli ya Tanzania iko tayari kupambana na uchokozi wowote toka Malawi si kutangaza vita hata kidogo kwani haiwezi kuidhinisha matumizi ya fedha kugharimia vita wala kuruhusu matumizi ya silaha na lojistics za Jeshi.
 
Kauli ni safi na ya kishujaa ambayo the chicken jk hawezi kutamka, na sidhani kama sitta katamka kwa kukurupuka but after consultation na ni vema amesema hivyo ili kuonesha tunajali mipaka yetu na tuko tayari kutetea, amiri jeshi mkuu jk alitakiwa aseme kabla but unfortunately he is too chicken even to give a bluff! Bravo mr. Zambi kwa kuibua hoja maana suala hili lilikuwa linatuumiza wengi!
Naona yuko bize kutafakari gazeti jngine la kulifungia na jinsi ya kum-ulimboka "mchochezi" wa mgomo wa walimu.
Nasikia juzi wahariri (Wenye njaa?) walitii "amri" ya kwenda Magogoni "kumpongeza" kwa hatua aliyoichukua dhidi ya mwenzao. Cheja na njaa veve?
 
Usimlishe maneno, yule bwana ana busara anajua mwenye mamlaka ya kutangaza vita ni amiri jeshi mkuu pekee; alichofanya ni kuwaweka sawa wanachi kwamba serikali iko macho kuhusu hali hiyo ili kuondoa dukuduku miongoni mwa wananchi.
Tofautisha kauli ya Sitta na hii hapa:
"Sasa tutampiga nduli iddi Amin;
Nia ya kumpiga tunayo;
Sababu ya kumpiga tunayo na
Uwezo wa kumpiga tunao".

J.K. Nyerere; October 1978.

Sasa mkuu, Malawi wakisema tuko tayari kupigana vita kuhakikisha ziwa Malawi niletu. Tusiichukulie kijuu juu hiyo kauli ya cta.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom