Samuel Chitalilo anapokuwa M/Kiti wa Kamati ya Bunge

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imekikataa kwa mara ya pili kitabu cha hesabu za mapato na matumizi ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha baada ya kubaini mapungufu, ikiwa ni pamoja na udanganyifu.

Kamati hiyo pia imewapa adhabu ya kukatwa asilimia 15 ya mishahara ya watendaji sita wa halmashauri hiyo kwa kosa la kuidanganya kamati hiyo ilipowatembelea Januari mwaka huu.

Kamati hiyo ilianza kupitia taarifa za mapato na matumizi ya serikali za mitaa kuanzia Jumatatu wiki hii na imeshapitia hesabu za halmashauri za mkoa wa Dodoma na jana ilipitia halmashauri za mkoa wa Arusha.

Awali kabla ya kukataliwa kwa kitabu hicho, mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Cyprian Oyier alionekana kushindwa kutoa maelezo ya kutosha kwa wabunge kuhusu makosa waliyofanya na mapungufu yaliyojitokeza katika kitabu chao.

Oyier alikiri mbele ya wajumbe wa kamati hiyo na wageni waalikwa kuwa waliidanganya kamati ilipoenda kuwatembelea wilayani kwao kwa kuwaeleza kuwa halmashauri ilijenga nyumba ya walimu kwa Sh30 milioni, jambo ambalo halikuwa la kweli.

Nyumba hiyo iliyogharimu zaidi ya Sh 30 milioni ilibainika kuwa imejengwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa) na wao kukabidhiwa funguo tu baada ya wajumbe kufanya ziara shuleni hapo.

Baada ya kukitaa kitabu hicho, wakuu wa halmashauri hiyo na waandishi, walitakiwa kutoka nje kwa muda, ili kuwapa nafasi wabunge kupanga adhabu.

Baada ya dakika 20, kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo, Samuel Chitalilo alisema kuidanganya kamati ni kosa la jinai, lakini kamati imewaonea huruma.
Alisema wangeweza kuwataka kurudi tena mbele ya kamati, lakini wanawasamehe kwa kuwakata asilimia 15 mishahara yao ya mwezi wa tano mwaka huu.
“Tunawarudisha mkaandae tena kitabu chenu... hiki tunakikataa kwa mara ya pili. Angalieni wenzenu wa Same walivyoandaa vizuri ili mkija tena tusije kukikataa tena,” alisema Chitalilo na kuongeza:

“Mmeidanganya kamati na mmekiri kosa, hili ni kosa la jinai, lakini kamati imewaonea huruma kwa kuwapa adhabu ya kujifunza na ili iwe fundisho kwa wengine”.

“Mkurugenzi wa halmashauri, mhandisi, ofisa mipango, mkaguzi wa ndani, mweka hazina na ofisa elimu aliyekuwapo wakati huo tutawakata asilimia 15 ya mishahara yenu ya Mei.”

Naye mbunge wa Kinondoni na mjumbe wa kamati hiyo, Idd Azzan alisema halmashauri hiyo ilitoa taarifa za uongo kwa kamati na kwamba walipokwenda kuitembelea shule hiyo walipewa taarifa tofauti kutoka kwa mkuu wa shule hiyo.

Alifafanua kwamba wanatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa halmashauri zinazotoa taarifa za uongo.

“Adhabu hii tunataka iwe fundisho kwa wengine, kwa kuwa fedha za serikali hazitumiki ipasavyo katika ngazi za halmashauri, zinatumika kwa safari na posho za viongozi jambo ambalo ni kinyume na malengo ya fedha hizo,” alisema Azzan.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo alikataa kuzungumza na Mwananchi baada ya kupewa adhabu hiyo, huku mwenyekiti wa halmashauri hiyo, David Pelo akisema kuwa hiyo ni bahati mbaya na hakuna aliyekusudia kutoa taarifa za uongo.

“Tutajitahidi kufuata maelekezo yenu, tunawashukuru kwa kutoturudisha tena katika kamati kwa kuwa fedha za halmashauri zingetumika pia kwa usafiri,” alisema Pelo.
“Haya ni ya kawaida na yanaweza kutokea kwa halmashauri yoyote, pia tutarudia kuandika kitabu kama tulivyoelekezwa na tutaenda kwa wenzetu wa Same kwa kuwa wao wamefanya vizuri.”

Kamati mbalimbali za bunge zinaendelea na vikao vyake kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kuanzia Jumatatu wiki hii.
SOURCE: Mwananchi 09/04/2009

Ama kweli hii nchi imejaliwa kuwa na viongozi wababaishaji...
 
Samuel Chitalilo ni yule aliye na vyeti vya darasa la saba sijui sekondari vya kugushi?
 
Samuel Chitalilo ni yule aliye na vyeti vya darasa la saba sijui sekondari vya kugushi?
Yup ndie yeye haswaaa... Amenikera kweli Watu wametafuna 30M yeye anawasamehe anawakata asilimia 15 tu aaaah yaani hii nchi hii sijui tuna laana
 
Samuel Chitalilo ni yule aliye na vyeti vya darasa la saba sijui sekondari vya kugushi?

yea ndo huyo huyo kweli sisiem imekosa watu wakuwapa kamati..mtu aliyefail sijui tena anapewa kamati yaa bunge ya hesabu za serikali ya mitaa..hapa kidogo haiingi akilini...
 
Sijui hata kama hiyo 15% ya mishahara yao kama itafikia upotevu huo wa uongo ambao wamesema wametumia kwenye ujenzi kumbe kwenye matumbo yao!! bongo kweli hatuna commited leaders zaidi ya kila mtu na interests zake anapokuwa kwenye madaraka..
 
Hawa wenyeviti wa hizi kamati za bunge wanachaguliwaje? Yaani wabunge wetu ni mbumbumbu kiasi kwamba wakamuona Chitalilo anafaa kuwaongoza kama mwenyekiti wao!! Ama kweli wabunge wa CCm wanavituko; ndio wabunge wa CCm si ndio wengi humo!! Kuna umuhimu wa kuwaondoa hawa vilaza wa CCm humo bungeni mwaka 2010.
 
NDIO HUYO HUYO cHITALILO ANAWAKEMEA WENGINE KWA KUDANGANYA...YEYE AMEFANYAJE NA VYETI VYAKE FAKE???KWELI KAZI IPOO DUUU.....KWELI TUMEKOSA WATU KABISA?SIDHANI....
 
Hii nchi ukiifikiria sana inatia hasira kishenzi.kuna watu waadilifu,wamekwenda shule vizuri na uwezo wa kuongoza wanao lakini wakijitokeza kugombea huko ccm majina yao hayarudi badala yake tunaletewa watu mambumbumbu kina chitatilo ndiyo watuongoze.
tanzania haitakaa iendelee mpaka yesu atakaporudi!
 
Kigezo cha kugombea ubunge ni Kujua kusoma na kuandika basi.
Ila kughushi ni kosa la jinai.
 
Hawa wenyeviti wa hizi kamati za bunge wanachaguliwaje? Yaani wabunge wetu ni mbumbumbu kiasi kwamba wakamuona Chitalilo anafaa kuwaongoza kama mwenyekiti wao!! Ama kweli wabunge wa CCm wanavituko; ndio wabunge wa CCm si ndio wengi humo!! Kuna umuhimu wa kuwaondoa hawa vilaza wa CCm humo bungeni mwaka 2010.

Mkuu Bulesi, Chitalilo hajachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati, ila baada ya viongozi mahsusi wa kamati, Mwenyekiti na Makamu, kutokuwepo, wabunge wengine wakamwomba aendeshe kikao kama Mwenyekiti wa muda which is totally wrong maana huyu jamaa ana kesi mahakamani ya kughushi vyeti! Kumteua yeye kuwa kaimu Mwenyekiti hata kwa muda mfupi tu ni kulidhalilisha Bunge! Chitalilo ni wizi mtupu!
 
We Fataki; Kesi ya Chitalilo imeisha na kwa habari nilizonazo mlalaikaji wake Bwana Alfred Ngotezi alilipwa ubani wake wa kusumbuka kufuatilia kesi (Milioni Kadhaa toka katika mradi wa Pikipiki) So, kwanini asifute kesi, kafuta.

alichofanya aliandika barua ya kuomba kufuta kesi na mahakama ikaipokea kwa mikono mitatu sasa Chitalilo siyo mtuhumiwa tena wala mshitakiwa.
 
Mbona niliwahi kusoa sehemu fulani kuwa bado washitaki wake wanahangaika na rufaa mahakamani?
 
Back
Top Bottom