chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,003
- 20,679
Kuna msemo unaosema kwamba, mchawi aliyeua, hulia kwa sauti kubwa na kugaragara siku ya msiba" wabunge wanalia ubadhirifu, upande wa pili, wamelamba fedha ya Wana ilemela, ambayo ingenunua madawati, dawa, kujenga madarasa.
Kamati ya LAAC inaongozwa na mbunge wa Chadema Halima Mdee.
Katika taarifa ambayo Halmashauri ya Ilemela imeweka katika ukurasa wake wa instagram, wameeleza kwamba wametumia milioni 74 kuwezesha taarifa ya kamati ya Bunge inayohusika na serikali za mitaa.
Nadhani hapa panahitaji ufafanuzi, waliwezesha vipi? Waliwalipa posho akina Mdee? "waliwapoza" ? Ni gharama za stationery?
Nadhani hiki kimefanyika Halmashauri zote nchini. Tukipata mzizi wa nini kiliwezeshwa, tutakuwa tunakaribia kulifikoa tatizo.
Nadhani wakurugenzi huchekecha hesabu zao mpaka Wanapata hati chafu ili kuwawezesha, si wabunge tu, Bali hata wakuu wanaohusiana na Halmashauri hizo, hoi inaenda kwa mashirika yote ya umma.
Piga hesabu, kamati ikitembelea Halmashauri 100 kwa mwaka ....karibu bilioni 10. Hawa watu watakosa hati chafu?
Bunge la Tanzania linashindwa kujigharamia mpaka liwezeshwe na ka Halmashauri ka ilemela? Kwa Kodi za wauza sangara, nyanya, mchele?
Huwa Kuna tetesi kwamba ukiwa katika baadhi ya kamati za Bunge, ikiwemo LAAC, unakuwa uko vizuri kwa kuwa Kila Halmashauri hukutengea fungu ili usiiseme vibaya, na Kuna baadhi ya kamati ukipangiwa, unaenda kufa njaa.
Kwako Halima Mdee.