Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,338
- 9,766
Ndugu zangu Watanzania,
Kamati ya Bunge Utawala, Sheria na Katiba imependekeza kuwa isiwe lazima kwa Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji na Majiji kusimamia Uchaguzi.
Pia kamati imependekeza kuwa badala ya kuitwa Tume ya Taifa ya uchaguzi iitwe Tume huru ya uchaguzi.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
==============
Kamati ilikuwa ina maoni kwamba Sheria isiweke ulazima kwa Mkurugenzi Mtendaji kusimamia Uchaguzi na badala yake, kuwepo na masharti ya Mtumishi wa Umma mwandamizi ama mtu mwingine yoyote mwenye sifa kuteuliwa kuwa Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi.
Serikali iliona kuwa upo umuhimu wa Wakurugenzi Watendaji kutajwa kwenye sheria kwa kuwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwenye kesi ya madai na. 138/2019 na Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu kwenye kesi ya madai na ziliamua kuwa Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi haukiuki masharti ya Katiba wala Mkataba wa Afrika wa Watu na Haki za Binadamu mtawalia.
Ibara ya 6(1) inaeleza kuwa kila Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya atakuwa Msimamizi wa Uchaguzi kwa madhumuni ya kuendesha uchaguzi katika Jimbo au Kata
Hawakubaliani na Wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma kusimamia uchaguzi kwa kuwa hawawajibiki kwa tume ya uchaguzi bali wanawajibika kwa Rais na Chama Tawala hivyo wanakosa sifa ya kuwa mamlaka ya uchaguzi huru na haki. Vifungu hivyo vifutwe na Tume iajiri watumishi wake wenyewe
Kamati bado ina maoni kuwa hakuna ulazima wa sheria kuweka sharti kwa Mkurugenzi wa Jiji, Manispaa, Mji na Wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi au wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa kuwa uzoefu unaonyesha wapo Wakurugenzi kwa sababu mbalimbali wanapoteza sifa za kuwa wasimamizi wa uchaguzi.