SAMATA: Atapotea kwenye Soka

Ndio kashaenda Europa..., na ni yeye ndie kaifikisha ile timu huko. Tusubiri makubwa zaidi kutoka kwake
 
Maana ya kuwa mfungaji nini? Watanzania nifunzeni kupenda vya kwenu hakuna mfungaji anayefunga Bila kuvizia
 
Kila mchezaji ana style yake ya uchezaji, wapo waviziaji nguli dunian niliopata kuwaona kwenye mpira, na wamecheza kwa mafanikio tu.. Na kocha anasajili kutokana na mahitaji uwanjani.. Wapo wanaohitaji waviziaji

Ila samata si mviziaj kama unavyodai mleta mada, samata anashirik karbia hatua zote uwanjan, ila kinachokuchanganya wewe ni yale magoli yake unayoyaona mepesi.. Na yale anayafunga kwasababu samatta anajua kujipanga mbele ya goli la mpinzani, kifupi anajua kujiposition thats why anafunga kimdebwedo.. Jaribu kumtizama kwa jicho la tatu samata tofaut na waviziaji wote unaowajua wewe duniani..
 
Mleta mada unazidi kuumbuka kwa unafiki wako kwa samata kijana ndo anang'ara balaa na keshamuweka bench kereles
 
Hii ndo taabu ya kuwa mtoto wa pekee kijijini unayesoma sekondari! Ndo kwanza umeenda kuanza Form I, ile kurudi likizo ya kwanza tu; Mwenyekiti wa Kijiji anakuuliza "unasomea uganga au ubwana shamba?"
 
MTU akisoma heading yako ni ya kukatisha tamaa. Huenda heading ingesomeka hivi "" Areas of improvement for Samatta" tafsiri isiyo rasmi ' mambo ambayo Samatta anatakiwa kuboresha ili aendelee kuisadia timu yake"
Tuwasaidie vijana wetu badala ya kutangaza mapungufu yao. Vijana wetu ni binadamu.
Ni Maoni tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom