Sakata la gesi Mtwara: Kauli ya Profesa Muhongo

Huyu Prof. anashusha hadhi ya taaluma.

Wakati anahoji uelewa wa watu wa Mtwara, na yeye anatakiwa ajihoji iwapo anailewa jamii anayoiongoza.

Nilikuwa na imani naye sana, lakini yaelekea amelewa sifa, kiburi na kujiona anajua. Anakosa sifa za uongozi wa kijamii.Hafai kuwa kiongozi wa jamii. Anadharau watu, tena watu wanyonge na maskini. Hili ni kosa kubwa kiuongozi.
Kwa bahati mbaya sana, tabia yake inafanana na ya katibu mkuu wake, kazi ipo.

Halielewi kabisa, jukumu lake kama kiongozi, kuondoa huo ambao yeye anaona kuwa ni ujinga wa wana Mtwara!
Haoni wajibu wake katika kuisaidia jamii hiyo.Pity!
 
Hii ndo Tanzania, kauli ya profesa haina tofauti na kauli itakayotolewa na mtu wa darasa la saba! Ni jambo la ajabu sana kuona Waziri mzima, tena Profesa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu, anafananisha usafirishaji wa Korosho na usafirishaji wa gesi. Waziri Muhongo anataka kutuambia kuwa usafirishaji wa hiyo gesi uko sawa na namna korosho inavyosafirishwa kutoka Mtwara? Ama kweli dunia ina mambo! Yangu macho, ngoja tuone wanapotupeleka!

Kwa kusaidia tu korosho analima mtu binafsi, anauza na kupata kipato chake hapohapo. Na hata akisafirisha anafaidika yeye. Pengine tumkumbushe kuwa wanamtwara wanayo malalamiko pia kuhusu korosho zao. Nilifikiri angelilijua hili kwani siyo Siri.
 
Tatizo linajirudia, unasoma ili ubishe badala usome ili unielewe niliandika maandishi yooote haya. Ndugu yangu Chungurumbira, acha ushabiki wa kijinga. Kama maji kiwanda kiko Ruvu, je bomba linaloenda nyumbani kwako linatokea Ruvu moja kwa moja au kuna Bomba kubwa limekuja hadi mjini na distribution inaanzia hapo kuja kwako?

Shida yetu hatupendi kuambiwa ukweli. Yaani kujaribu tu kukueleza kuwa haya yoote unayodai tayari yako hivyo, wewe umeshawahi kusema NATUMIKA.

Usinichoshe, ashakhum si matusi, wewe ni MPUMBAVU. Hiyo kwenye red ndicho ambacho mimi nimetoka kusema. Nimekuita mpumbavu kwa kuwa mpumbavu ni mtu asiyependa kujifunza. Hebu soma kwanza nilichoandika halafu utakubaliana na mimi kuwa wewe ni wa hovyo kabisa.

Unatoa mifano ya RUVU kipumbavu kabisa. Kama maji yanachakatwa Ruvu, yanabebwa kwa bomba kubwa mpaka Ubungo, yanaingia kwenye tank, hapo yanatoka mambomba tena makubwa kwenda hili Kurasini, hili Mabibo, hili Keko na kadhalika, sasa hiyo inatofauti gani na nilichosema kuwa Gesi itachakatwa Mtwara, itasafirishwa hadi Dar, hapo itagawiwa kwa watumiaji, au wewe unabishana nini sasa?

Naona unatukana sana kama vile suala hili wewe ndio baba yao. Nchi hii imepitia kati ya watu wema na wabaya. Namaanisha watafuna nchi(wabaya). Kwa matusi yako utakuwa mmojawao. Uko mwerevu bali wewe huna tofauti na nyoka pia.

Hapa hakuna ushabiki, mbona hujajibu hoja ya mkataba wa huu mradi wa gesi???? uko kivipande vipande tu! wabunge wamekuwa wakipiga kelele kuwa ni vema mikataba hii iwe inapita katika mikono yao ili kulinda mali ya watanzania kwa sababu ya waliyotokea huko nyuma. Mbona wameziba masikio na huu mradi ni sehemu ya ufisadi.

Kwa jinsi ulivyo nitukana eti mjinga ohh mpumbavu yaonekana ndo waficha pesa Uswisi.
 
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza katika kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo, amesema anawaeleza Watanzania kuwa, uchumi wa Dunia wa sasa ni wa ushindaji, hivyo “sisi” Watanzania tumetaka tuifanye Bandari ya Mtwara kituo kikuu cha utafiti na uendeshaji wa shughuli zote za gesi. Kwa hivyo, wawekezaji waliotaka kuwekeza wakiondoka, bandari ya Mtwara kutokana na sababu zozote za kushindwa utulivu wa kufanya kazi zao, watahamishia shughuli zao bandari za Beira au Mombasa.

Mwandishi: Tatizo la wakazi wa Mtwara ni lipi?

Waziri: Mimi sielewi, inabidi wao waulizwe. Watu wa Mtwara kitu walicho nacho haki ni Korosho... Hizo korosho ni mali zao kabisa, mbona hizo korosho zinasafirishwa? Watanzania tuwaulize kwa nini korosho zao zinasafirishwa kutoka Mtwara.

Mwandishi: Huoni vyema nyie Serikali mkakaa na wananchi kutoa elimu kuhusiana na suala la gesi?

Waziri: Serikali na TPDC tumefanya vikao vingi sana na viongozi wa Mtwara na Lindi... wakiwemo Wabunge wao hadi wale wa Halmashauri wamepelekwa nje ya nchi kujifunza umuhimu unaotokana na hiyo gesi asilia.

Isitoshe, wananchi wa Lindi na Mtwara wamepunguziwa bei ya umeme... Je, wanavyounganishiwa huo umeme kwa bei nafuu kuliko wananchi wengine, hawajiulizi? Pili, vijana wao tumewachukua wanakwenda kusoma VETA...

Mwandishi: Upi ni wito wako kuhusiana na vurugu, migororo?

Waziri: Kwanza naomba kuwaambia wananchi wa Mtwara, kuwa wasicheze ngoma wasiyoijua. Wasiimbe nyimbo wasizozijua wala hawajui wanaotunga tenzi za nyimbo hizo.

Pili, Watanzania wote kwa miaka mingi tumepata matatizo ya umeme, suluhisho la umeme linapatikana sasa.

Shukrani za dhati ziende kwa wavuti.com kwa kuyaweka hayo mahojiano kwenye maandishi. Unaweza kumskiliza Mh. Muhongo mwenywe hapa: audio:-Kauli ya Waziri wa Nishati na Madini & Taarifa za habari Januari 27, 2013 - wavuti.com
Nimeshajiridhisha sasa kuwa huyu Muhongo Uprofesa wake ni wa darasani (Nadharia) zaidi kuliko ku-deal na watu direct. Aondolewe kwenye baraza la mawaziri haraka kwa sababu huyu anaonekana kuwa ni hatari kwa usalama wa taifa na arudi darasani akafundishe
 
Kwenye nchi inayojua uwajibikaji Waziri kusema hajui watu wa Mtwara wanataka nini ni sababu tosha ya kujiuzulu.

Sasa kama Waziri hajui nani atajua?

Rais hajui kwa nini nchi maskini, waziri hajui watu wa Mtwara wanataka nini. Unafikiri tutaendelea kwa uongozi huu?

Ina maana tangu mgogoro huu uanze hamna brief hata moja inayoelezea tatizo kwa Waziri?

Ina maana Waziri kashindwa kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa, Mbunge na watendaji wengine wa serikali mkoani kujua tatizo? Siku zote hizi?

Na kama kashindwa kufanya hili kwenye hili swala linalotishia usalama wa taifa kwa nini aendelee kuwa waziri?

Ina maana wizara haina intelligence gathering mechanism at all?

Huyu Muhongo ni muongo, ama mzembe. Quite possibly muongo na mzembe.

Ina maana hata hii risala aliyosomewa PM hajaiona?

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tamko-la-shura-ya-maimamu-mkoa-wa-mtwara.html
 
Sasa kama hajui unataka adanganye? :cheer2:

Kama hajui ajiuzulu tu.Possibly ashitakiwe kwa fraud.

Ni kama dereva ahojiwe baada ya ajali halafu aseme hajui kuendesha gari.

Watu wamekufa, mali zimechomwa moto, usalama wa taifa uko hatarini, waziri anasema hajui tatizo ni nini?

Ningeweza kumuelewa kama angesema anajua tatizo ni nini lakini hakubaliani na njia ya utatuzi ya watu wa Mtwara, au hata angesema anajua tatizo/ wanachotaka watu wa Mtwara ni nini lakini hajui kulitatua.

Lakini huyu waziri hajui hata tatizo ni nini, hajui hata watu wa Mtwara wanataka nini.

Ataanzaje kutatua tatizo asilolijua?

Kwa nini huyu mtu aendelee kuwa Waziri?
 
Kwa sababu Rais aliyemteuwa pamoja na yeye Waziri, wote ni DHAIFU.
Kama hajui ajiuzulu tu.Possibly ashitakiwe kwa fraud.

Lakini huyu waziri hajui hata tatizo ni nini, hajui hata watu wa Mtwara wanataka nini. Ataanzaje kutatua tatizo asilolijua?

Kwa nini huyu mtu aendelee kuwa Waziri?
 
Kwa sababu Rais aliyemteuwa pamoja na yeye Waziri, wote ni DHAIFU.

Tofautisha "anaendelea" na "aendelee".

Jibu lako linahusiana na "kwa nini anaendelea". "Kwa nini aendelee..." ni swali pana zaidi.
 
Tusipende kuwa Wakomunisti wa maneno wakuu, alichosema Waziri ni sahihi. Nchi hii haina utaratibu wa ukanda au majindo, kwa hiyo kauli ya Waziri ni kuwakumbusha wakaazi wa Mtwara kuwa, kuna tofauti ya Korosho uliyolima na Gesi ambayo ni MALI YA ASILI.

Kuwa darasa la 7 haimaanishi kuwa huna akili, tazama wewe na madarasa yako umeshindwa kuelewa suala dogo sana. Waziri hafananishi usafirishaji, Waziri anahoji 'Korosho za Mtwara zinaenda sokoni, gesi ya Mtwara itashindwaje kwenda sokoni?' Shida ni kwamba unajaribu kutumia hisia kuelewa.

Haya anayoyasema Waziri Muhongo hata Zitto Kabwe aliyasema BBC (simaanishi hizo mnazoziita kejeli) kwamba kuna viongozi wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Halmashauri na Wabunge wa mikoa ya Kusini walipelekwa nje kujifunza mambo kadhaa juu ya gesi. Kama nia ni kuweka maazimio wazi kwa Wanamtwara, mbunge wa Mtwara mjini ambaye nasikia naye ni kinara wa maandamano, anataka kuieleza nini Tanzania juu ya ushiriki wake katika ziara na vikao hivyo?

Shizukan

Kwa mawazo yangu madogo nilifikiri wanamtwara na viongozi wao waliofundishwa na kupelekwa ziara za mafunzo walipaswa kuelimika na kufanya maamuzi sahihi, kumbe la ilikuwa ni hongo wakubali mawazo ya Serkali. Professor aache kutumia hili Kama argument anawadhalilisha siyo wanamtwara tu Bali hata Serkali.
 
Kwa nini aendelee? Kwa sababu Boss wake ambaye ni DHAIFU, haoni tatizo kwa dhaifu mwenzake.

Chama Dhaifu, hakioni tatizo kwa Waziri wake. Na ndiyo wengi Bungeni.

Wewe na mimi tunaona Udhaifu huo ila hatuna ubavu wa kumgusa. Kibaya zaidi, hao watu wake wanaona ndiyo Waziri Bora Tanzania, msomi.

Swali lako ni zuri na lingelikuwa na maana hiyo unayoisema kama ingelikuwa nchi za dunia ya kwanza. Ila kwa Tanzania ambapo Rais ndiyo KILA KITU, maswali yote mawili ya "anaendelea" na "aendelee" yanakupeleka kwa mtu mmoja, KIKWETE. Na Kikwete kwa katiba ya Tanzania ni UNTOUCHABLE labda CCM na wao waanze kuhisi joto kwenye makalio yao.
Tofautisha "anaendelea" na "aendelee".

Jibu lako linahusiana na "kwa nini anaendelea". "Kwa nini aendelee..." ni swali pana zaidi.
 
Hivi kuna anayejua kwa nini Tanzania ni maskini?

Sababu ni nyingi. Mojawapo ni too much respect for authority/status quo/ dini/ utamaduni/mungu.

Katika system yenye too much respect for status quo progress is hard.People do what they have always done for fear of innovation.
 
Sababu ni nyingi. Mojawapo ni too much respect for authority/status quo/ dini/ utamaduni/mungu.

Katika system yenye too much respect for status quo progress is hard.People do what they have always done for fear of innovation.

Sasa kama sababu ni nyingi na zinajulikana kwa nini hatuziondoi ili tuweze kuendelea?
 
Kwa nini aendelee? Kwa sababu Boss wake ambaye ni DHAIFU, haoni tatizo kwa dhaifu mwenzake.

Chama Dhaifu, hakioni tatizo kwa Waziri wake. Na ndiyo wengi Bungeni.

Wewe na mimi tunaona Udhaifu huo ila hatuna ubavu wa kumgusa. Kibaya zaidi, hao watu wake wanaona ndiyo Waziri Bora Tanzania, na tena msomi.

Swali lako ni zuri na lingelikuwa na maana hiyo unayoisema kama ingelikuwa nchi za dunia ya kwanza. Ila kwa Tanzania ambapo Rais ndiyo KILA KITU, maswali yote mawili ya "anaendelea" na "aendelee" yanakupeleka kwa mtu mmoja, KIKWETE. Na Kikwete kwa katiba ya Tanzania ni UNTOUCHABLE labda CCM na wao waanze kuhisi joto kwenye makalio yao.

Bado hujaelewa tofauti ya "kwa nini anaendelea" na "kwa nini aendelee"

Ukisema "Kwa nini aendelee? Kwa sababu Boss wake ambaye ni dhaifu, haoni tatizo kwa dhaifu wenzake" unatoa hilo kama rationale ya yeye kuendelea.

"Kwa nini aendelee?" Ni swali linalotafuta a logical rationale.

"Kwa nini anaendelea" ni swali linalotafuta an explanation on the reason he is still ticking.

Unatoa jibu with an explanation on why is he still ticking to a question that does not ask for an explanation on why is he still ticking.

The question asks for a logical rationale, a justification on why should he continue to be a minister.

Ni kama kaitwa mahakamani jaji anataka kumpa hukumu, anaulizwa kwa nini wewe tusikutoe uwazirini.

Hawezi kujibu "kwa sababu boss wangu ni dhaifu, haoni tatizo kwa dhaifu wenzake"

Atakuwa katoa sababu ya kutolewa uwaziri, si sababu ya kutotolewa uwaziri.

Mie natafuta sababu kutoka kwa yeyote anayemtetea huyu Waziri, kuna sababu gani itakayofanya watu rational wasitake kumtoa huyu mtu uwazirini?
 
Back
Top Bottom