Sakata la gesi Mtwara: Kauli ya Profesa Muhongo

Haki ya nani tena, Msigwa alikuwa sawa. Prof. mzima anaongea kama mtoto wa darasa la Pili :(

 
Last edited by a moderator:
mahela ya uswis ni noma, yaani waziri profesa haelewi, lakini wanamtwara tukikomaa, mbona wataelewa!!!!
 
Kwa haya basi, kuanzia leo ninamwomba msamaha Ndg Philipo Mulugo (aka Amim) kwa mitusi na hasira nilizoporomosha kwake kwa kuonesha ukilaza wakati yeye ni waziri wa elimu. Nimeamsha mikono - Bongoland imelaaniwa. Yaani lijitu lina title ya Prof halina hata haya kubwabwaja utumbo!!!!
 
Tanzania inachekesha kweli...sasa waziri kama hajui hivi meya na madiwani si watakuwa wametoa macho tu kwa mshangao!!!!


Haki ya mungu mi tanzania nahama..nitarudi watanzania kakiweka watu wenye akili madarakani....hapana nimeghairi sihami.ngoja nikomae niwe mmoja wa wakombozi wa taifa hili
 
Maprofesa wana dharau sana,ila sometime huwa hawamaanishi! Profesa ni mtaalam na sio kiongozi! Wanafikiri wanachowaza wao tu ndio sahihi! Tusubiri tuone
 
Wakati Muhongo alipotoa maelezo bungeni kwamba mgao wa umeme ulikuwa wa kutengeneza, nguzo za umeme za TZ kupelekwa Mombasa na kupigwa Mihuri ili zionekane zimetoka SA, etc watu walimuona kama kiongozi shupavu na anayefaa hata kuwa Rais. Lakini kwa hili la gesi na mgao wa umeme unaoendelea, inaokena hafai hata uenyekiti wa mtaa.
 
Ukweli ni kwamba viwanda na shughuli zitokanzazo na gesi Kama usafishaji na usambazaji zilitzkiwa zifanyikie Mtwara. Mambo ya Almasi ya Mwadui kwenda kukatiwa Iringa halina sababu katika duniani ya leo
 
Yaani nchi hii vioja vitupu, kama hajui alikuwa anakomalia nini hadi kuja na matakwimu na ma asilimia kibao povu likawa linammwagika utadhani ameambiwa 'hebu jitetee kwa nini usinyongwe?' Kumbe hata hajui wanachodai wala anachokitetea., shame on dis GOMENT
 
Pr ya nini na hao wendawazimu! Hivi kweli tunataka kulea huu -----! Yaani serikali ikitataka kufanya miradi ya kimaendeleo eti iende kuwa bembeleza wananchi wa eneo hilo. Hiyo ges ni ya wanamtwara? Kwa taarifa yako hawana hata nusu lita hiyo gesi ya serikali ni ya wantazania wote!
 
Acheni umbumbumbu, raia wa mtwara wanalishwa sumu wasizozijua, binafsi nimefatalia sana matakwa ya raia wa Mtwara, na kwa zaidi ya asilimia 99% matakwa yao yameshaelezwa ni jinsi gani yatatekelezwa na ambayo yameshaanzwa fanywa kwa upendeleo!!
Hivyo mimi nasikitishwa na watu mnaocomment ujinga wakati ukweli wa mambo unafahamika, fuatalieni mambo kwa pande zote mbili ndipo mtakaporealize kuwa raia wa Mtwara hawajui hata wanachopigania!!!!!!
Profesa na crew yako yote endeleeni kuchapa kazi kwani ipo siku watanzania wataelewa juu ya hiki mnachowaeleza leo!!!
 
Shida ya watu kama hawa ni arrogance. Moto unawaka yeye anaongea kauli za ajabu. Mikutano na wabunge wa CCM unadhani inasaidia nini? Wabunge wao wote ni wagonga meza na wachukua posho hawana interests za wananchi hata siku moja.
 
kosa kubwa alilposema gesi ni ya watu wa Mtwara Vijijini hivyo watu wa Mtwara Mjini haiwahusu
kauli ambayo ilikuwa inawagawa watu hawa maana alichokizingatia yeye ni maandamano kufanyikia Mtwara Mjini na si vijijini alishindwa kugundua kuwa hata watu Mtwara vijijini walikupo kwenye hayo maandano

ZZK amewaambia jana wasiongoze nchi kwa press conference wasione aibu waende Mtwara
 
Huwezi amini kama Muhogo ni profesa,hana tofauti na jamaa wa Zimbabwe na pemba!!
 
Back
Top Bottom