Hii ndo Tanzania, kauli ya profesa haina tofauti na kauli itakayotolewa na mtu wa darasa la saba! Ni jambo la ajabu sana kuona Waziri mzima, tena Profesa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu, anafananisha usafirishaji wa Korosho na usafirishaji wa gesi. Waziri Muhongo anataka kutuambia kuwa usafirishaji wa hiyo gesi uko sawa na namna korosho inavyosafirishwa kutoka Mtwara? Ama kweli dunia ina mambo! Yangu macho, ngoja tuone wanapotupeleka!
Jk akiwaanamuachiachia huyu waziri aongeeongee ataharibu kabisa, yaani nje ya hayo ma jeolojia yake huwezi amini kama jamaa ni profesa inaonekana haelewi isues kabisa.
Hii ndo Tanzania, kauli ya profesa haina tofauti na kauli itakayotolewa na mtu wa darasa la saba! Ni jambo la ajabu sana kuona Waziri mzima, tena Profesa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu, anafananisha usafirishaji wa Korosho na usafirishaji wa gesi. Waziri Muhongo anataka kutuambia kuwa usafirishaji wa hiyo gesi uko sawa na namna korosho inavyosafirishwa kutoka Mtwara? Ama kweli dunia ina mambo! Yangu macho, ngoja tuone wanapotupeleka!
JK: kwa kweli sielewi tatizo la umasikini Tanzania linasababishwa na nini.
mramba: mtakula nyasi lakini ndege ya Rais lazima ininuliwe
Malecela: mkikoboa, hizo pumba mzihifadhi mtazitumia wakati wa njaa.
Msekwa: wana wivu wa kike
Chenge: ni vijisent tu
pombe J.M: Kama hamna nauli pigeni mbizi.
Muhongo: sielewi matatizo ya watu wa Mtwara
Mwema. Kesi ya Ulimboka ni siri ya Taifa.
Baba wa Taifa: ccm si mama yangu...!!!
Hii ndo Tanzania, kauli ya profesa haina tofauti na kauli itakayotolewa na mtu wa darasa la saba! Ni jambo la ajabu sana kuona Waziri mzima, tena Profesa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu, anafananisha usafirishaji wa Korosho na usafirishaji wa gesi. Waziri Muhongo anataka kutuambia kuwa usafirishaji wa hiyo gesi uko sawa na namna korosho inavyosafirishwa kutoka Mtwara? Ama kweli dunia ina mambo! Yangu macho, ngoja tuone wanapotupeleka!
Nathani Mhe. WAziri haelewi pia kwanini yupo madarakani,Mwandishi: Tatizo la wakazi wa Mtwara ni lipi?
Waziri: Mimi sielewi, inabidi wao waulizwe. Watu wa Mtwara kitu walicho nacho haki ni Korosho... Hizo korosho ni mali zao kabisa, mbona hizo korosho zinasafirishwa? Watanzania tuwaulize kwa nini korosho zao zinasafirishwa kutoka Mtwara.
Ukweli ni kwamba viwanda na shughuli zitokanzazo na gesi Kama usafishaji na usambazaji zilitzkiwa zifanyikie Mtwara
Mambo ya Almasi ya Mwadui kwenda kukatiwa Iringa halina sababu katika duniani ya leo
Kinachonishangaza nyinyi wenye mawazo haya ndio mnaothubutu kumuita Waziri kilaza aliyeishia darasa la saba. Sasa angalia ni nini umeandika:
Si ndio haya Waziri anayaeleza saa zote kuwa yatafanyika huko? Watanzania hebu tuache ushabiki wa kijinga na angalau mara moja kwa mwaka tuwe serious na reasonable badala ya kupenda sifa za kijinga. Hivi kuna shida gani ya kutafuta facts badala yake tunaongea kishabiki tu na kusifiana mitandaoni?
IPECACUANHA, natural gas exploration ni shughuli ya kitaalam na ina principles zake. Ungejisumbua tu kutafuta elimu ya gesi ikichimbwa huwa ikoje usingekuwa na maswali kama itachakatwa Mtwara au Dar. Shida yetu ni kukurupuka na kutopenda kusikiliza. Kama tungemsikiliza Waziri kwa umakini, naamini tusingekuwa na mabishano ambayo mimi binafsi nayaona ni ya kipuuzi.
Waziri kasema, uchimbaji, uchakataji na usindikaji utafanyika huko huko Mtwara. Na mimi nakuongezea kuwa: hata kama Serikali ingetaka hayo yafanyike Dar es Salaam, ISINGEWEZA. IPECACUANHA, sour gas (as it comes from the well) ni corrosive, kwa hiyo kwa usalama wa mabomba na sababu zingine za kiuchumi, lazima ichakatwe ndio iwe salama kusafirishwa kwenye mabomba. Na ndio hicho Waziri anachokirudia kila mara kukisema. Hebu soma hii link kwa faida yako mwenyewe uone kwa nini ni lazima gesi ichakatwe Mtwara na sio tu Mtwara, bali inalazimu shughuli hiyo ifanyike karibu na mahali ilipochimbwa kadiri iwezekanavyo NaturalGas.org
Kaka unataka usambazaji wa gesi ufanyike Mtwara? Kama mawazo ya Waziri ni ya darasa la 7 haya ya kwako ya darasa la ngapi?
1. Twiga Cement watandike bomba la inchi 1 toka Mtwara mpaka Wazo Hill DSM ili kupata Gesi
2. Kwanza Bottlers watandike bomba lao toka Mtwara hadi Kawe Industrial Area
3. Murzah Oil Industries watandike bomba toka Mtwara hadi Port Access Industrial Area
4. East Coast Oils watandike bomba toka Mtwara hadi Kurasini
5. Serengeti Breweries watandike bomba toka Mtwara hadi Chang'ombe....
Au mimi sijaelewa usambazaji upi unaomaanisha wewe?
Ushabiki wa kijinga unatunyima nafasi ya kusikia facts, kwani wakati muda mtu anaongea sisi tuko bize kutafuta kitu cha kubisha mara atakapomaliza kuongea. Sasa linakuja hili suala la KINYEREZI. Hata hili jambo dogo tu nalo lizue debate?
Kinyerezi kunajengwa Power Plant (Mtambo wa kufua umeme). Uhusiano wa Gesi na Project ya Kinyerezi ni kwa kuwa huo Mtambo unaojengwa Kinyerezi utatumia gesi kufua umeme. Sasa ukisikiliza watu wengi hapa JF wanakwambia kwa nini gesi itolewe Mtwara ipelekwe Kinyerezi, sasa swali la kujiuliza nyie wenyewe, hiyo gesi tunanufaika nayo kwa kuiangalia au kwa kutumika?
Kuna mambo ya kuzingatia hapa, si kuongea tu kwa kuwa hakuna kodi ya mdomo. Unaweza kuniambia kwa nini NG'OMBE wasichinjiwe Dodoma, Singida na kwingineko wanakopatikana badala yake wanaletwa Dar wakiwa hai? Nauliza hivi kwa kuwa, tukiwa tunaangalia sababu moja tu kati ya 20 zinazo-determine business location tutakuwa watu wa ajabu. Ng'ombe wangechinjiwa Dodoma ni kweli machinjio yangetoa ajira kwa wenyeji wa huko, sasa kwa nini wanasafirishwa hai kuja Dar?
Hana tofauti na Mulugo. Anaongea kwa kiwango kinachokatisha tamaa kabisa hana hata uwezo wa kupanga hoja na huyu ndiye tuliyeambiwa kwamba ni kichwa. Anaendelea kutoa kauli zilizojaa vitisho. Serikali bandia, Rais bandia na mawaziri bandia.
Wakati Muhongo alipotoa maelezo bungeni kwamba mgao wa umeme ulikuwa wa kutengeneza, nguzo za umeme za TZ kupelekwa Mombasa na kupigwa Mihuri ili zionekane zimetoka SA, etc watu walimuona kama kiongozi shupavu na anayefaa hata kuwa Rais. Lakini kwa hili la gesi na mgao wa umeme unaoendelea, inaokena hafai hata uenyekiti wa mtaa.
Isitoshe, wananchi wa Lindi na Mtwara wamepunguziwa bei ya umeme... Je, wanavyounganishiwa huo umeme kwa bei nafuu kuliko wananchi wengine, hawajiulizi? Pili, vijana wao tumewachukua wanakwenda kusoma VETA...
Kinachonishangaza nyinyi wenye mawazo haya ndio mnaothubutu kumuita Waziri kilaza aliyeishia darasa la saba. Sasa angalia ni nini umeandika:
"Ukweli ni kwamba viwanda na shughuli zitokanzazo na gesi Kama usafishaji na usambazaji zilitzkiwa zifanyikie Mtwara"Si ndio haya Waziri anayaeleza saa zote kuwa yatafanyika huko?