Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Labda siku nikiwa kwenye laptop nitafanya editing, nilitamani sana kufanya hivyo. Shukrani sana
Muulize hapo ni wapi!

IMG-20211219-WA0039.jpg
 
Mbona picha nyingi ni za Njombe M
Habari za wakati huu, nimeona niwashirikishe kidogo Wazee wenzangu wa Road trip haka kamsafara kangu kadogo.

Nilipanga kuwa mwaka huu nizunguke kwa gari baadhi ya mikoa, LENGO ikiwa ni kupunzisha ubongo tu na kujionea huko kwingine...LENGO ilikua nianzie Dar-Lindi-Songea-Njombe- Mbeya-Rukwa-Katavi-Kigoma-Bukoba-Mwanza-Mara-Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma-Moro-Dar ila baada ya kuwaza sana nikaona kwa mwaka huu nijaribu route fupi kidogo.

Safari yangu ilianza tarehe 5/12/2021 kutoka Dar mchana kwenda Njombe, niliondoka Dar saa kumi jioni, nikapumzike Moro kidogo then nikapumzika Mafinga Kisha nikamalizia safari Hadi Njombe, nikifika muda wa saa tisa usiku, nikaenda giraffe pale nikamalizia usiku hapo.

Siku iliyofuata nikatembea hapa na pale kidogo ila kesho yake Ikawa nataka kwenda Kitulo kupitia Makete nikalale Kitulo Kisha nidondokee Mbeya, kwa bahati mbaya sana baada ya kufika Makete almost two or three kilometers kutoka Makete nikapotea njia... nilikuta junction sasa baada ya kwenda kulia nikapita kushoto. Nikatembea mwendo mrefu tu huku Barabara ikiwa mbaya, ikafika mahali mlimani na msituni nikakwama, nikaamua kurudi, ndio nikauliza wenyeji wakasema nimepotea sana. Nikaghadhibika nikarudi Njombe Mjini. Siku Ikawa imeisha.

Siku iliyofuata mchana nikaamua kuondoka Njombe, kuanza safari ya Kigoma. Saa nane mchana baada ya kupata lunch pale Glory Hotel nikaondoka taratibu sana.

Nikafika Dodoma usiku wa saa Tano, nikaamua nisogee Hadi Manyoni. Nikapumzika Manyoni pale Pretoria Hadi saa Moja asubuhi nikaondoka zangu.

Saa nne nikafika Tabora, nikapumzika one hour nikapata supu. Muda wa saa Tano nikaondoka sasa kuitafuta Kigoma, Barabara ilikua mbaya baadhi ya maeneo, kuna maeneo kuna lami na kwingine hakuna lami Hadi uvinza. Nikafika Uvinza saa 11 jioni.

Nikatembea sasa kwenye lami Hadi Kigoma, Nikalala Mwitongo Hotel, asubuhi nikazunguka mjini nikaenda kuonana na wadau wangu siku Ikawa imeisha.

Asubuhi nikaondoka kwenda Kasulu, nikafika Kasulu nikatafuta kifungua kinywa nikaendelea na safari, kuanzia Kasulu Hadi Kibondo mjini ni rough road Moja matata sana, lami Iko Pale mjini tu, nikaonana na Wadau wangu hio ni saa tisa mchana sasa nimeshapunzika. Jamaa wakanishauri nisiondoke, tukabadilishana mawazo pale na networking.....

Asubuhi nikaondoka kutoka Kibondo na penyewe ni rough road ya maana tu sema Kuna Ujenzi inaendelea kwa MKOPO kutoka AfDB. Lami nikaikuta Kakonko sasa, nikasimama nikapiga picha kuagana na rough road.

Nikatembea Hadi Nyakanazi, Runzewe, Masumbwe to Kahama. Kahama nikapumzika kidogo maeneo ya kule kwenye maegesho ya serikali, Kahama Pana starehe aiseeee.

Nikatembea zangu saa tisa mchana Shelui, nikapata Company nikajivuta Hadi Singida. Nikalala sikutaka kuendelea na ligi na yule kijana, alinikuta kule mizani namwaga Maji kidogo, akasimama tukaagana nikamwambia sitaweza kuendelea na safari.

Asubuhi nikaanza safari Hadi Dodoma nikapumzika, mchana nikaanza safari Tena Hadi nafika Dar ilikua saa sita usiku.

Hivi ndivyo nilivyoitumia Likizo yangu ya December 2021 kwa kutembelea maeneo hayo kujenga network na kubadilisha mazingira kidogo.

View attachment 2050099

View attachment 2050102

View attachment 2050103

View attachment 2050106

View attachment 2050107

View attachment 2050109

View attachment 2050110

View attachment 2050112

View attachment 2050113

View attachment 2050114

View attachment 2050115

View attachment 2050116

View attachment 2050118

View attachment 2050121
Ak

Mkuu naona picha nyingi ni za kuanzia Mpongo hadi kipengele hapo.... Au uliipenda Njombe?
 
Hongera sana. Nami pia nilikuwa likizo, almost njia hiyo hiyo, ingawa mimi nilipitia mbeya, Rukwa, Katavi, kuingilia uvinza.

Niseme ukweli, Mkoa wa Kigoma umesahauliwa sana, na hasa kwenye Miundombinu! Kile kipande cha Kaliua-Nguruka na Malagarasi-Uvinza kina zaidi ya miaka 5 kiko vile vile,

Kiukweli kabisa inauma mnoo, kwakuwa haikupaswa mpaka muda huu kiwe vile, sababu imekuwa muda sana na kiasi kwamba mtu unajiuliza je, Sirikali ina agenda ya siri juu ya watu wa Kigoma juu ya maendelo yao??

Lakin pia wakati narudi nilipitia njia ulosema kwa maana ya kasulu-Nyakanazi! hali ya barabara inatisha mnoo!

Serikali iwakumbuke wakazi hawa, maana nadhan umebaki mkoa pekee ambao haujaunganishwa kwa lami hapa Tanganyika.
Mie huwa nawaza kwamba, pengine wakikamilisha hizo barabara kwa wakati TRC watakosa soko kwenye treni lao
 
Mbona picha nyingi ni za Njombe M

Ak

Mkuu naona picha nyingi ni za kuanzia Mpongo hadi kipengele hapo.... Au uliipenda Njombe?
Njombe ni pazuri sana sana. Nilitaman sana kufika Kitulo, kwenye Bustani ya Dunia.... Njombe inanikumbusha mengi. Njombe is the best acha kabisa
 
Duhhhh hiyo IST ndo umepiga nayo masafa marefu hivyo.. anyway nzur sana mkuu nakumbuka mwaka jana nilipiga road trip dar-arusha-karatu-babati-hydom-singida-dodoma-dar n nzur kwa kwel especially upo na kampan ya watu wawil ...
Naiheshimu IST tofauti na zamani japo wakati mwingine unanyanyasika sana barabarani. Wiki mbili zilizopita niliitumia toka Morogoro mpaka Kibondo na kurudi bila shida pamoja na kupita barabara ya vumbi Kakonko mpaka Kibondo
 
Hongera sana, hazina shida mbona? Niliwahi kusafiri na Suzuki Kei CC 990
 
Hii ni kawaida sana kwa Wabongo, huwa hatukosi Cha kukosoa, it's okay nimeanzia safari Ubungo Hadi Kibaha nikageuza Dar
Hivi kama kote ulipiga picha maana ni utalii, naziomba na hizo za Manyoni na Dodoma, si mbaya na Tabora pia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom