Safari yangu ya Dar-Njombe-Iringa-Dodoma-Tabora-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi-Kahama-Singida-Dom-Dar

Hongera kutalii.

Siku nyingine jaribu route hizi

1. Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Songea - Mbinga hadi Nkata bay Nyasa ziwani, kisha rudu Dar kupitia Njombe - Iringa - Moro.

2. Dar - Moro - Iringa - Makambako - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga hadi Katavi (Mpanda) Kisha rudi Dar kupitia Stalike - Majimoto - Muze - Mtowisa hadi utokee Mlowo ili uende Mbeya kisha Chunya - Makongolosi hadi Tabora ndio uende Dar kupitia Itigi - Manyoni - Dom - Moro.

Amini nakuambia, ukimaliza route hizo, utakuwa umejifunza mengi sana.

Tembea kwa saa kumi au kumi na moja kwa siku. Kisha pumzika kwenye mji, furahia maisha kisha siku ya pili uendelee. Usitembee usiku kwa safari za kitalii.
Mkuu hiyo number 1 next year lazm niipige trip hiyo.. me huwa nasema utalii wa ndani sio lazm kwenda kuangalia wanyama Serengeti au Ngorongoro hata road trip ni utalii mzur mnoooo
 
Hii taarifa sio sahihi kabisa ndugu zangu, nimeiona kwenye mitandao nikacheka sana. Hakuna sehemu kama hio kwa sababu Barabara Iko chini ya mkandarasi ambaye anakua responsible na issues zote kuhakikisha Barabara inapitika kama kawaida. Sio kweli
Unamaanisha nini ukisema sio kweli? unafaham hapo ni wapi? tuambie
 
Mkuu hiyo number 1 next year lazm niipige trip hiyo.. me huwa nasema utalii wa ndani sio lazm kwenda kuangalia wanyama Serengeti au Ngorongoro hata road trip ni utalii mzur mnoooo
Saaaana sana!
 
Nilipenda nione picha za akiwa
Dodoma na Manyoni Ila sijaziona
Hapo ndiyo kwenu? Ndiyo maana unazitaka hizo itakuwa kaanza na hizo si unajua hatujamtuma kaamua mwenyewe kwa mapenzi yake , Dodoma kwenyewe hakuna hata misitu yakuvutia bali ni jangwa tu vile vindama wanavyo chunga barabarani
 
Nilipenda nione picha za akiwa
Dodoma na Manyoni Ila sijaziona
Hii hapa ni Dodoma baada ya kujaza Mafuta. Hope umeridhika Mpwa. Unaweza kuangalia tarehe na muda niliokua Dodoma. Nimeongeza na details Mpwa. Hope umeamini sasa.

IMG_20211219_210841.jpg

Screenshot_2021-12-19-21-12-59-481_com.miui.gallery.jpg
 
Hongera kutalii.

Siku nyingine jaribu route hizi

1. Dar - Lindi - Mtwara - Masasi - Songea - Mbinga hadi Nkata bay Nyasa ziwani, kisha rudu Dar kupitia Njombe - Iringa - Moro.

2. Dar - Moro - Iringa - Makambako - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga hadi Katavi (Mpanda) Kisha rudi Dar kupitia Stalike - Majimoto - Muze - Mtowisa hadi utokee Mlowo ili uende Mbeya kisha Chunya - Makongolosi hadi Tabora ndio uende Dar kupitia Itigi - Manyoni - Dom - Moro.

Amini nakuambia, ukimaliza route hizo, utakuwa umejifunza mengi sana.

Tembea kwa saa kumi au kumi na moja kwa siku. Kisha pumzika kwenye mji, furahia maisha kisha siku ya pili uendelee. Usitembee usiku kwa safari za kitalii.
Sio nkata bay ni mbamba bay,nkata bay iko Malawi
 
Ila kusema ukweli hii nchi kuna watu wanakula maisha, mtu mwenye uwezo wa kupiga ruti yote hii tena kwa usafiri binafsi ni wazi keshavuka kabisa level za shida ndogo ndogo. Hongera mkuu nasi tupambane inshaallah! Kufanikiwa kukwepa mabasi na mslori pia ni umakini mkubwa.
 
Ngoja nikutafutie wimbo wa Dolly Parton wa Coat of Many Colors
 
Ila kusema ukweli hii nchi kuna watu wanakula maisha, mtu mwenye uwezo wa kupiga ruti yote hii tena kwa usafiri binafsi ni wazi keshavuka kabisa level za shida ndogo ndogo. Hongera mkuu nasi tupambane inshaallah! Kufanikiwa kukwepa mabasi na mslori pia ni umakini mkubwa.
Joseph, naomba usome huu wimbo, concentrate kwenye ubeti wa mwisho anapozungumzia suala la Umaskini.... that's a brotherly advice to you.

Back through the years
I go wonderin' once again
Back to the seasons of my youth
I recall a box of rags that someone gave us
And how my momma put the rags to use
There were rags of many colors
Every piece was small
And I didn't have a coat
And it was way down in the fall
Momma sewed the rags together
Sewin' every piece with love
She made my coat of many colors
That I was so proud of
As she sewed, she told a story
From the Bible, she had read
About a coat of many colors
Joseph wore and then she said
Perhaps this coat will bring you
Good luck and happiness
And I just couldn't wait to wear it
And momma blessed it with a kiss
My coat of many colors
That my momma made for me
Made only from rags
But I wore it so proudly
Although we had no money
I was rich as I could be
In my coat of many colors
My momma made for me
So with patches on my britches
And holes in both my shoes
In my coat of many colors
I hurried off to school
Just to find the others laughing
And making fun of me
In my coat of many colors
My momma made for me
And oh, I couldn't understand it
For I felt I was rich
And I told 'em of the love
My momma sewed in every stitch
And I told 'em all the story
Momma told me while she sewed
And how my coat of many colors
Was worth more than all their clothes
But they didn't understand it
And I tried to make them see
That one is only poor
Only if they choose to be
Now I know we had no money
But I was rich as I could be
In my coat of many colors
My momma made for me
Made just for me
 
Habari za wakati huu, nimeona niwashirikishe kidogo Wazee wenzangu wa Road trip haka kamsafara kangu kadogo.

Nilipanga kuwa mwaka huu nizunguke kwa gari baadhi ya mikoa, LENGO ikiwa ni kupunzisha ubongo tu na kujionea huko kwingine...LENGO ilikua nianzie Dar-Lindi-Songea-Njombe- Mbeya-Rukwa-Katavi-Kigoma-Bukoba-Mwanza-Mara-Simiyu-Shinyanga-Singida-Dodoma-Moro-Dar ila baada ya kuwaza sana nikaona kwa mwaka huu nijaribu route fupi kidogo.

Safari yangu ilianza tarehe 5/12/2021 kutoka Dar mchana kwenda Njombe, niliondoka Dar saa kumi jioni, nikapumzike Moro kidogo then nikapumzika Mafinga Kisha nikamalizia safari Hadi Njombe, nikifika muda wa saa tisa usiku, nikaenda giraffe pale nikamalizia usiku hapo.

Siku iliyofuata nikatembea hapa na pale kidogo ila kesho yake Ikawa nataka kwenda Kitulo kupitia Makete nikalale Kitulo Kisha nidondokee Mbeya, kwa bahati mbaya sana baada ya kufika Makete almost two or three kilometers kutoka Makete nikapotea njia... nilikuta junction sasa baada ya kwenda kulia nikapita kushoto. Nikatembea mwendo mrefu tu huku Barabara ikiwa mbaya, ikafika mahali mlimani na msituni nikakwama, nikaamua kurudi, ndio nikauliza wenyeji wakasema nimepotea sana. Nikaghadhibika nikarudi Njombe Mjini. Siku Ikawa imeisha.

Siku iliyofuata mchana nikaamua kuondoka Njombe, kuanza safari ya Kigoma. Saa nane mchana baada ya kupata lunch pale Glory Hotel nikaondoka taratibu sana.

Nikafika Dodoma usiku wa saa Tano, nikaamua nisogee Hadi Manyoni. Nikapumzika Manyoni pale Pretoria Hadi saa Moja asubuhi nikaondoka zangu.

Saa nne nikafika Tabora, nikapumzika one hour nikapata supu. Muda wa saa Tano nikaondoka sasa kuitafuta Kigoma, Barabara ilikua mbaya baadhi ya maeneo, kuna maeneo kuna lami na kwingine hakuna lami Hadi uvinza. Nikafika Uvinza saa 11 jioni.

Nikatembea sasa kwenye lami Hadi Kigoma, Nikalala Mwitongo Hotel, asubuhi nikazunguka mjini nikaenda kuonana na wadau wangu siku Ikawa imeisha.

Asubuhi nikaondoka kwenda Kasulu, nikafika Kasulu nikatafuta kifungua kinywa nikaendelea na safari, kuanzia Kasulu Hadi Kibondo mjini ni rough road Moja matata sana, lami Iko Pale mjini tu, nikaonana na Wadau wangu hio ni saa tisa mchana sasa nimeshapunzika. Jamaa wakanishauri nisiondoke, tukabadilishana mawazo pale na networking.....

Asubuhi nikaondoka kutoka Kibondo na penyewe ni rough road ya maana tu sema Kuna Ujenzi inaendelea kwa MKOPO kutoka AfDB. Lami nikaikuta Kakonko sasa, nikasimama nikapiga picha kuagana na rough road.

Nikatembea Hadi Nyakanazi, Runzewe, Masumbwe to Kahama. Kahama nikapumzika kidogo maeneo ya kule kwenye maegesho ya serikali, Kahama Pana starehe aiseeee.

Nikatembea zangu saa tisa mchana Shelui, nikapata Company nikajivuta Hadi Singida. Nikalala sikutaka kuendelea na ligi na yule kijana, alinikuta kule mizani namwaga Maji kidogo, akasimama tukaagana nikamwambia sitaweza kuendelea na safari.

Asubuhi nikaanza safari Hadi Dodoma nikapumzika, mchana nikaanza safari Tena Hadi nafika Dar ilikua saa sita usiku.

Hivi ndivyo nilivyoitumia Likizo yangu ya December 2021 kwa kutembelea maeneo hayo kujenga network na kubadilisha mazingira kidogo.

View attachment 2050099

View attachment 2050102

View attachment 2050103

View attachment 2050106

View attachment 2050107

View attachment 2050109

View attachment 2050110

View attachment 2050112

View attachment 2050113

View attachment 2050114

View attachment 2050115

View attachment 2050116

View attachment 2050118

View attachment 2050121

Next time karibu Kigoma wenyeji tupo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom