Safari bungeni dodoma

Apr 29, 2012
81
4
Ndugu wana Jf natumai hamjambo!Leo nipo Dodoma kwa ajili ya mualiko nilioupata pamoja na wenzangu kuja bungeni dodoma,safari yetu imeanzia Iringa majira ya saa mbili asubuhi kwa usafiri wa basi la UPENDO lenye namba T839-ASN na tumefika Dodoma saa moja jioni.Mwenyeji wetu ni mbunge wa Iringa mjini Mh.Mchungaji Peter Msigwa,bado hatujaonana nae kwani bado ana majukumu ya kibunge na bila shaka kesho mimi pamoja na wenzangu tutakuwepo bungeni kujifunza mambo kadhaa yahusuyo mstakabali wa taifa letu.Safari yetu hata hivyo njiani imekumbana na vikwazo vingi 1:Mwenzetu mmoja alivamia na vibaka pale Iringa stand na amejeruhiwa mikononi na shati yake kuchanwa,hata hivyo hali yake inaendelea vizuri na tupo nae hapa Dodoma 2:Basi limepata pancha mara mbili 3:Vumbi,kwani tumepita njia ya Iringa-dodoma kutokana na uchumi.Mwisho nina mshukuru mwenyezi mungu kwa kutufikisha salama!
 
Poleni sana. Siku nyingine mshukuru mungu kwanza ndipo uendelee na mambo mengine usimshukuru mwishoni mwa mapenzi yako.
 
Pole mdau nadhan wakat mwingne ukipata fursa ni bora ukapita ya kuzunguka utatumia muda mfupi kuliko hiyo njia fupi kwani nadhan serikali imeshasahau kabisa umuhmu wake kila siku imekuwa ahadi hewa
 
Ahsanteni jamani!Pia nimesahau kuwambieni kioja kimoja,kijana mmoja akataka kutuuzia maji machafu sh.500/=kazi kwelikweli.
 
Back
Top Bottom