Simulizi: Nyumba ya maajabu

winston20

JF-Expert Member
Jun 21, 2020
1,117
2,256
SURA YA KWANZA

28/3/1989
Ulikuwa ni msafara wa watu watano, wawili kati yao, pamoja na mimi mwenyewe,
tukiwa ni waandishi wa habari waajiriwa wa kampuni ya Film Tanzania ambayo
ilikuwa ni kampuni ya habari na matangazo iliyojihusisha pia uchapaji wa
magazeti ya Tabasamu na Sunday, wakati wale wengine wawili walikuwa ni
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao walikuwa wanafanya tafiti
kwa ajili ya shahada yao ya pili pale Mlimani.
Tulikuwa ni watu wenye furaha kubwa kutokana na namna ambavyo kazi yetu
ilivyo kwenda sawa bin sawia, ilituchukua zaidi ya wiki mbili tukiwa mkoani Geita
tulikokwenda kikazi, ambapo kampuni ilituteuwa kwenda huko kuangazia matukio
yaliyokuwa yakiendelea kutokea katika mkoa wa Geita ambayo kwa kiasi
kukubwa yalikuwa yakigusa hisia za watu wengi nchini na hata duniani kwa
ujumla…migogoro ya wakulima na wafugaji.
Siku hii ya Jumatano ya tarehe 28/3/1989 ni tarehe ambayo haiwezi kufutika katika
akili yangu kwa miaka mingi mno.
Safari ilikuwa ndefu mno kiasi fulani ilinichosha, lakini hata hivyo kila nilivyo
fikiria matunda ya kazi iliyotupeleka huko kwa kweli nilipata nguvu kubwa.
Mwendo mkali wa Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na bwana Magembe
Matiku tulitazamia kati ya saa mbili ama saa tatu tutakuwa tumekwishawasili jijini
Dar es Salaam.
Tulindoka mkoani Geita mapema alfajiri. Awali wakati tunaanza safari ndani ya ile
Land Cruiser kulirindima maongezi vicheko na utani mwingi miongoni mwetu,
lakini kadri muda ulivyozidi kuyoyoma ndivyo zile bashasha zilivyozidi kuyeyuka,
hii ni kutokana na umbali mrefu wa safari yetu uliosababisha kukinaiwa na safari
ile ndefu.
Saa tisa juu ya alama tuliingia mkoa wa Dodoma, hapo bwana Magembe Matiku
dereva wa ile Land Cruiser alitutaka tupate chakula cha mchana kabla ya
kuendelea na safari ile, tuliingia katika hoteli iliyokuwa ndani ya kituo cha mafuta
cha Gapico na kujipatia chochote.
3
Jua lilikuwa ni kali mkoani Dodoma tofauti na mikoa tuliyopita huko nyuma, jaketi
nilililokuwa nimevaa halikuwa na nafasi tena katika maungo yangu.
Nililivua.
Wakati naliondoa lile jaketi maungoni mwangu nililiweka katika mgongo wa kiti
nilicho kuwa nimekalia kisha nikaendelea kushambulia chakula kilichokuwa
mezani kwangu kwani njaa ilikuwa ikiniuma kisawasawa.
Katika meza niliyo kuwa nimeketi, sikuwa peke yangu tuliketi wawili mimi na
Loveness huyu alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu tuliyekuwa pamoja katika ule
msafara wa Geita.
Hatua chache kidogo kulikuwa na meza iliyokaliwa na watu watatu yanii bwana
Magembe Matiku ambaye ni dereva wa kampuni yetu, pamoja na john, na
mwenzake Fidelix hawa ni wale wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam
waliokuwa katika utafiti wa masomo yao.
Sambamba na hilo, katika viti vingine vilivyokuwa mule katika hoteli ile kulikuwa
na watu wengine wengi tu ambao walikuwa wakijipatia chakula mchana ule,
Upande wa mbele wa meza niliyokuwa nimekaa kulikuwa na meza nyingine
iliyokaliwa na mkaka aliyekuwa akinitumbulia macho pindi tu nilivyosaula jaketi
katika maungo yangu.
Macho yetu yaligongana mara mbili, awali nihisi imetokea bahati mbaya na
nikaendelea kushughulika na kula, macho yakiwa katika sahani.
Angalau sasa tumbo langu lilishiba, nikanyanyua uso wangu kuangaza eneo la
kunawia mikono. Lakini wakati nafanya hilo, bahati mbaya tena nikagonganisha
macho na yule mwanaume kwa mara nyingine tena, hapo nikagundua kuwa yule
kaka alikuwa akinitizama muda wote. Pia alikuwa akiniangalia katika namna
ambayo ilinielewesha kitu gani kilikuwa kinapita katika akili ya yule mtu.
Ajabu ni kuwa, pindi nilivyopata kugonganisha macho na yule mtu kwa mara hii
ya tatu nilipatwa na kitu fulani cha ajabu katika mwili wangu hali iliyonifanya
nistajabu.
Nilipapatwa na ganzi chini ya mapaja yangu lakini wakati huohuo nikajikuta
naingia katika siku zangu japo nilikuwa na wiki moja tangu nitoke katika hedhi na
siku zangu za hedhi huwa hazina kawaida ya kubadilika kiasi kile.
4
Upesi akili yangu ikaanza kufikiri kuhusu mkoba wangu ulio kuwa ndani ya ile
Land Cruiser ambao ndani yake kulikuwa na pedi ambazo huwa natembea nazo
wakati wote.
Nazipiga hatua kwenda kunawa mikono, kabla ya kuendea mkoba kwa ajili ya
kujihifadhi na damu iliyokuwa inachafua nguo yangu ya ndani.
Wakati nikiwa nanawa mikono, niligeuza shingo kumwangalia yule mtu, nikaona
bado ananitizama katika namna ile ile. Nafikiri macho yake yalikuwa yakivutiwa
na uzuri wa sura niliyojaliwa na Muumba, na pengine labda macho yake
yalivutiwa na umbo langu lililokuwa kama namba nane, ningekuwa nimevaa blauzi
ya kubana ningesema labda yale macho yalikuwa hayajiwezi kwa sababu ya
maziwa yangu saizi ya embe dodo bichi, lakini kwa bahati mbaya au nzuri
nilikuwa nimevaa shati lilionikaa vizuri ikiwa kwa ndani ya kifua changu nikiwa
nimeyabana maziwa yangu kwa sidiria ndogo.
Sasa vipi huyu mtu anitumbulie mimacho kiasi kile..!
Anajua yeye mwenyewe.
“Zahara vipi tena mbona hivyo?” Loveness alinistua wakati nikitoka ndani ya
hoteli ile kuelekea mahala lilipokuwa gari.
“Aah!. we acha tu shosti niko kwenye siku zangu mwenzio nafuata mkoba garini
nichukue pedi nijistiri”
Nilimjibu haraka haraka kwa sauti ya chini, kisha nikazipiga hatua upesi kwenda
lilipokuwa gari. Lakini wakati huo huo bwana Magembe Matiku na Fedelix
pamoja na John nao walikuwa wanatoka mule hotelini.
“Jamani hatuna muda wa kupoteza wapenzi inabidi tufike Dar es Salaam kabla ya
saa tatu usiku” alisema bwana Magembe akichezeshachezesha lundo la funguo
mkononi mwake.
Niliongeza mwendo hadi katika ile Land Cruiser nikachukua mkoba wangu
uliokuwa na pedi kisha kikaelekea maliwato na kujihifadhi.
Wakati huo, yule mtu aliyepatwa na ugonjwa wa kuniangalia angalia hovyo
nilikuwa nimekwishamsahau katika akili yangu.
Dakika kumi zilizofuata tulikuwa ndani ya gari tukiuacha mji wa Dodoma na joto
lake, gari lililokuwa likiendeshwa na bwana Magembe likiwa katika mwendo
mkali hatari.
5
Kulikuwa na maongezi ya hapa na pale ndani ya gari. Lakini wasaa ule niliishia
kuelekeza macho yangu huko nje nikiangalia vijumba vifupi na vidogo vya makuti
vilivyokandikwa kwa udongo, yakiwa ni makazi ya wanakijiji wafugaji jamii ya
Wagogo.
Dakika arobaini baadae watu wote walikuwa wanasinzia isipokuwa mimi na
bwana Magembe. Kulirindima ukimya garini zaidi ikiwa ni mlio wa gari uliokuwa
ukilalama kutokana na vile bwana Magembe alivyokuwa akilivuta kisawasawa.
Ni hapo nilipo kumbuka radio yangu ya CD kifaa nilichokitumia kusikiliza muziki
mbalimbali niliyoihifadhi katika CD…..na wakati nakumbuka kifaa kile ndipo
hapo moyo wangu ulipopiga “paaaaaaa” kila kitu kilipita katika akili yangu kama
tamthilia.
Nikajikuta napiga ukulele wa fadhaa. “Jaketi languuuuuuu!!..” Nikamstua kila mtu
aliyekuwa amelala.
Na sasa nikakumbana na maswali lukuki kutoka kwa wenzangu. Vipi nibwate kwa
sauti kubwa kiasi kile kwa ajili ya jaketi. Thamani yake ni kubwa kwa kiwango
gani hata nibweke namna ile na kuondoa kabisa utulivu wa watu mule garini.
Nilibaki nimeganda nimekodoa macho, mdomo wangu ukiwa wazi,lakini mkono
wangu wa kushoto ukiwa umefunika domo lile, sura yangu ikiwa imejaa mshangao
mkubwa.
“Zahara kwani hilo jaketi la kazi gani tena ilihali Dar es Salaam lingeenda kukaa
katika begi, tena pengine lingeishia kuwa chakula cha mende na panya”.
Alisema John akimaanisha hapakuwa na sababu ya kujutia kulisahau jaketi ilihali
mahala ninakokwenda ni sehemu ya joto kali ambapo uhitaji wa masweta na
majaketi haupo.
“Naenda kufanya nini Dar es Salaam bila lile jaketi jamani? ndani ya hiyo nguo
kulikuwa na kila kitu ambacho kilitupeleka Geita. Kitabu chenye taarifa zote kipo
katika mfuko wa jaketi, kamera ndogo yenye picha za video pia ipo katika mfuko
wa jaketi, kinasa sauti kilichokuwa na sauti za mahojiano tulizofanya na wale
jamaa waliokuwa wanagombana kuhusu mipaka, kifaa kile kimo katika mfuko wa
jaketi, na hata zile karatasi za maswali na majibu ya mkuu wa mkoa zooote zimo
katika mfuko wa jaketi. Lakini pia, hata vitambulisho vyangu vyote vimo katika
lile jaketi”.
6
“Nooooo!!.” Nini tunafanya jamani!!. nini hiki aah” bwana Magembe alipiga
kelele baada ya kutoa maelezo yale. Na mwisho alikanyaga breki ghafla na gari
likasimama katikati ya barabara huku tairi za gari zikijiburuza katika lami na kutoa
mlio mkali wa mburuzo.
Kwa kweli maelezo yangu yalimchanganya kila mtu hasa wale wafanyakazi
wenzangu, vifaa vilivyokuwa katika jaketi vilikuwa ni vitu muhimu kwa
mustakabali mzuri wa ajira zetu.
Kamwe mkurugenzi isingeweza kutuelewa kama tungerudi bila taarifa yoyote ya
Geita ilihali ofisi iligharamia gharama zote za utafiti wa makala ile na hata kutulipa
pesa nzuri tu kwa kipindi chote ambacho tulikuwa mkoani Geita.
“Sasa tunafanya nini jamani” aliuliza Loveness.
“Unajua kama huu ni uzembe wa kipuuzi ulio ufanya wee Zahara” badala ya
kujibu bwana Magembe Matiku aliyekuwa amefura kwa hasira alinitupia lawama.
Nilijisikia vibaya mno kwa maneno yale ya bwana Magembe lakini sikuwa na la
kufanya kwani kweli kosa lilikuwa langu japo sikukusudia kulitenda. Sikujibu
chochote zaidi ya kuwa kimya nikingoja maamuzi ya wenzangu juu ya ni kitu gani
watafanya.
“Hatuna chaguo jingine zaidi ya kurudi Dodoma” Fidelix aliyekuwa kimya muda
mwingi alishauri, Ushauri ulioungwa mkono na John na hata Loveness, bwana
Magembe alikuwa amevimba kwa hasira alitizama saa yake ya mkononi na kuona
ilikuwa ni saa kumi na mbili na robo za jioni.
Aliachia breki na kuingiza gia kisha akaliondoa gari kwa kasi na kukata kona kwa
kasi na kulielekezea kule tulikotoka.
Safari ya kurudi Dodoma ikaanza.
Ilituchukua dakika arobaini na tano nyingine kufika Dodoma mjini na hapo
tukanyooka na barabara kama tunaelekea Singida na kilometa moja nyingine
tukawa tumefika katika kile kituo cha mafuta ambacho kilikuwa na huduma ya
mgahawa.
Hapo ilikuwa yapata saa mbili kasorobo usiku.
Nilikuwa wa kwanza kushuka katika gari na kukimbia ndani ya ule
mgahawa,nilipo ingia ndani macho yangu moja kwa moja katika kiti nilichokuwa
nimekalia ambapo ndipo nilipoweka lile jaketi.
7
Moyo wangu ulinidunda kwa nguvu kutokana na kile nilichokiona, kiti kile
kilikuwa kitupu. Lile jaketi halikuwepo mahala pale.
Sasa nilianza kuona dalili ya kupoteza kibarua chuangu kinachoniweka mjini mimi
na familia yangu.
Kwa muda wa nusu dakika niliweza kuona maisha ambayo nitakwenda kuishi
muda mfupi ujao baada ya kufukuzwa kazi katika kampuni.
Nilimwona mama mwenye nyumba wangu (mama Leila) namna atakavyokuwa
akinisumbua juu ya kodi yake ambayo ilikuwa ikielekea ukingoni, niliona namna
wazazi wangu watakavyokuwa wakinipigia simu mara kwa mara na kuhitaji
msaada wa kifedha kutoka kwangu hali ya kuwa wakati huo mifuko yangu itakuwa
imetoboka kwa kutokuwa na ajira yenye kuniingizia pesa.
Lakini pia, niliona namna mdogo wangu Nasri namna anavyositisha masomo yake
kwa kushindwa kuendelea kumsomesha kwa kukosa ajira yenye kuniingizia fedha.
“Vipi dada yangu kulikoni?” nilistushwa na sauti ya muhudumu wa mgahawa ule
aliyekuwa amesimama nyuma yangu na kunishangaa namna nilivyokuwa
nimeganda mithili ya sanamu.
Lakini kabla sijamjibu, muda huohuo akina Loveness nao wakaingia.
“Vipi umeliona” wote waliniuliza kwa pamoja kana kwamba waliambizana.
“Hapana, kiti ni kitupu, jaketi halipo”
“Shuuuuph” bwana Magembe alishusha pumzi huku mikono yake ikiwa kiunoni.
“Kwani kuna nini jamani” Muhudumu wa ule mgahawa aliuliza.
“Kuna jaketi nililisahau katika kiti hiki wakati tulipo kuja kula chakula hapa kama
lisaa limoja hivi limepita”
“Jaketi la rangi ya kaki..?”
“Ndiooo” niliitikia upesi upesi nikihisi kuna uwezekano wa kulipata ile nguo kwa
kuona muhudumu yule analifahamu.
“Hiyo nguo niliichukua na kuipeleka ofisini lakini alikuja mkaka mmoja jina lake
nimelisahau alisema lile jaketii ni la mwenzenu ambaye mpo nae katika safari
moja mkitokea Geita na ulikuwa umelisahau na mmemtuma yeye aje kulichukua
hapa”
8
“ Whaaat!.”
Wote tuliuliza kwa mshangao, kwa pamoja.
“Kwani ninyi huyo mtu hamjamtuma na hamjui?!” Muhudumu aliuliza tena kwa
mshangao.
“Hicho kitu unacho sema kigeni kabisa. Hatumjui huyo mtu” John alisema.
“Na kwani huyo mtu yukoje” niliongezea kwa kuuliza.
“Mkaka mweusi mrefu ana kitambi kidogo, wakati ninyi mnakula chakula yeye
alikuwa amekaa katika kiti hicho hapo” Hapo taswira ya yule mtu aliyekuwa
akinikodolea mimacho yake mibaya hadi nikaingia katika siku zangu, sura yake
ikanijia mbele yangu
“Blood fool mijitu mingine sijui ikoje kudada’deki ni lile likaka lililokuwa limekaa
hapo likiniangalia hovyo” nilisema kwa ukali huku nikihisi huzuni isiyo na kifani
“Basi huyo mvulana atakuwa ni mwizi” Loveness alisema pia kinyonge.
“Sasa tutafanya nini?” mtu mwingine aliuliza, mie nguvu zilikwisha, niliona
nilichokuwa nimebakiza ni kufukuzwa kazi na kuingia uraiani na kupambana na
ukali wa maisha kwa namna nyingine.
“Kuna kituo cha polisi hapo mbele kama hamtojali tuongozane tukafungue kesi”
alisema yule mfanya kazi wa ule mgahawa.
Tulikubaliana na ushauri wa yule muhudumu tulikwenda kituo cha polisi na
kufungua kesi kisha tukapewa RB.
Baada ya hapo safari ya Dar es Salaam ikaanza tena.
 
SURA YA PILI

SAA sita na nusu za usiku tuliingia jijini kila mtu alikuwa amechoka vibaya.
Baadhi ya watu walishukia Ubungo ila kwa kuwa mr Magembe alikuwa akiishi
Gongo la mboto na mimi nilikuwa nikiishi Buguruni Malapa alinisogeza hadi
Buguruni Sheli na kuniacha pale.
Pale nilichukua bajaji usiku ule na kumtaka dereva anipeleke Malapa.
Njaa ilikuwa inauma lakini sikuwa na hamu ya kula chakula chochote, nilikuwa
mnyonge mno.
Usiku ule nilikuta geti la nyumbni kwangu limefungwa nilizunguka katika dirisha
la mama mwenye nyumba na kumgongea anifungulie mlango.
“Eeh Zahara huyoo!”
“Ndiye mimi mama”
“Karibu mwanangu, za huko”
“Salama tu mama za hapa”
“Hapa kwema mwanangu sijui mnatunyima nini huko”
“Mvua, matope na baridi”
Nilisema kwa utani, na hapo mama akacheka huku mimi nikifungua komeo la
mlangoni kwangu na kuingia ndani.
“Halafu….we Zahara ”
“Abee mama”
“Kuna baba mmoja amekuja hapa leo kukuulizia mara kumi kumi” alisema mama
mwenye nyumba.
“Baba yupi huyo?”
“Hajaniambia jina lake ila anasema mlikuwa wote huko Usukumani huko uliko
kuwa na mlikuwa katika safari moja leo”
“Unasema!!” moyo wangu ulipiga mkumbo kama mdundo wa nyimbo za Marijani
Rajabu, taswira ya yule mtu kule katika mgahawa ikanirejea tena usoni mwangu.
10
“Unasema kweli mama?”
“Ndio..kwanini nikuongopee mama”
“Hakuacha chochote hapa”
“Ameacha”
“Kaacha nini?”
“Namba ya simu”
Kidogo nilipata nguvu nikaona tumaini jipya la maisha yangu. Kwani niliamini
nitavipata vifaa vyangu,na kwa mara ya kwanza nilijikuta naomba toba kwa
Mungu wangu kwa kumuhisi vibaya yule mtu. Kwa kweli hakuwa ni mtu mbaya
angekuwa mwizi kama ambavyo tulimuona kamwe asingefika pale nyumbani
kunitafuta ilihali akiwa ameiba vitu vyangu.
“Mungu wangu nisamehe kwa kumuhisi vibaya huyu kaka” nilisema kimoyomoyo
huku nafsi yangu ikiwa na furaha.
Jambo moja ambalo sikuwahi kujiuliza muda ule ni vipi mtu yule alinifahamu
mimi kuwa nilikuwa Geita na pia kujisema kuwa alikuwa na mimi pamoja huko
Geita, lakini kubwa kuliko yote ni vipi alipajua nyumbani kwangu ninapoishi.
Nikiwa bado ni mwenye faraja moyoni, mama mwenye nyumba alinipa kipande
cha karatasi kilichokuwa kimeandikwa namba ya simu.
Kwa mara nyingine nilishukuru mno, niliingia ndani mwangu na kuwasha taa
kisha nikaketi kitandani, kabla ya kufanya lolote nilitoa kadi yangu ya posta na
kutoka nje kutafuta vibanda vya simu.
Sikupata tabu kupata kibanda cha simu,.niliandika zile namba kisha nikazipiga
Simu ilita upande wa pili kwa muda kidogo kisha ikapokelewa na sauti nzito yenye
mkwaruzo.
“Halow”
“Habari yako kaka” nilisalimia
“Sijambo. Ooh Zahara, hujambo bibie” alijibu yule mtu, nilistuka kidogo, vipi
huyu mtu anijue namna hii amejua vipi jina langu?
“Safi tu, nafikiri ni wewe uliyekuja kunitafuta nyumbani kwangu?”
11
“Bila shaka”
“Na bila shaka ni wewe uliyeondoka na jaketi langu kule Dodoma?”
“Haswaaa” alijibu tena yule mtu, nilishusha pumzi ndefu nikahisi furaha
ikiongezeka moyoni kwa kulipata jaketi langu lililokuwa na vitu muhimu. Sikujali
wala sikuwa na habari tena na namna yule mtu alivyotumia utaratibu wa
kulichukua lile jaketi kule katika mgahawa, kilichokuwa katika akili yangu wakati
huo ni kuhakikisha naipata ile nguo yangu hususani vitu vilivyokuwa ndani ya lile
jaketi
“Sasa nalipata vipi hilo jaketi?” niliuliza.
“Njoo mtaa wa Aggrey, Kariakoo”
“Sasa hivi?” niliuliza kwa mshangao huku nikitizama saa na kuona ilikuwa yapata
saa saba na nusu usiku.
“Ndio lazima iwe sasa hivi vinginevyo unaweza kulikosa, mie kesho asubuhi
naondoka na basi la Chakito kuelekea Mlalo huko Lushoto.
Nilisimama wima nikapatwa na taharuki ya kulikosa jaketi, japo sikuwa tayari
kabisa kulikosa tena lile jaketi.
Niliagana na yule mtu na kumuhakikishia kuwa nitakuwa mtaa ule wa Aggrey
muda mchache ujao.
Nilikurupuka na kutoka mule ndani bila hata kumwaga mama mwenye nyumba
usiku ule na kutokomea mtaani.
Nilipanda daladala inayoenda mjini kwa miaka hiyo yalikuwa ni yale mabasi ya
kizamani kabisa yenye kuitwa “Chai Maharage” lililonipeleka hadi mtaa wa
Aggrey, Kariakoo.
Hapo nilisimama mbele ya stendi ya mabasi ya Tabata na Buguruni kisha nikaingia
katika kibanda cha kupiga simu na nikampigia simu tena yule mtu.
“Shuka mbele kidogo huku, kama unakuja Mnazi Mmoja, tizama upande wa
kushoto utaona mashine ya kutolea pesa ya NMB kisha ingia katika ghorofa
inayofuatia, panda juu hadi ghorofa ya nne, utanikuta katika korido ya milango ya
lifti nakungoja..”
Baada ya kupewa maelekezo hayo nilizipiga hatua kuelekea eneo lile
nililoelekezwa, bahati ni kuwa hapakuwa mbali.
12
Dakika chache nyingine nilikuwa katika lifti ya jengo lile ambalo sikujua ni jengo
linalojishughulisha na nini, kilichonistajabisha ni kuwa hapakuwa na mlinzi katika
jengo lile.
Lakini hata hivyo sikujali sana kwani kilichonipeleka pale ni vitu vyangu vya
ofisini na si vinginevyo.
Sekunde kumi nyingine milango ya lifti ilifunguka, tayari nilikuwa ghorofa ya nne,
Nilitoka ndani ya ile lifti.
Hapo nikakutana na yule mtu mwenye kupenda kunitizama. Aliponiona aliachia
tabasamu ambalo nililiona kule Dodoma, lile tabasamu liliongea kitu, nafikiri
lilisema “nimekutana na mwanamke mrembo”.
“Karibu Zahara” alinikarimu huku akinipa mkono tabasamu lake likizidi kustawi
usoni mwake.
“Nashukuru sana”.
Nilijibu huku na mimi nikimpa zawadi ya tabasamu, akanionyesha ishara nimfuate,
wakati naongozana nae, macho yangu yalikuwa yakisaili ile nyumba ilikuwa ni
kama hoteli ya kisasa kwani kila tulipopita katika korido, niliona vyumba
vilivyoandikwa namba mithili ya vyumba vya hoteli ya kisasa, sikuwa na uhakika
sana na hisia zangu kuwa huenda ile nyumba ikawa hoteli kwani nilivyoingia
katika ile nyumba sikuona mapokezi wala sikukutana na mtu yeyote mbali na yule
mbaba mwenyeji wangu.
Safari yetu ilishia mbele ya mlango mmoja ulioandikwa Room No 104. Alisukuma
mlango wa chumba kile na kujitoma ndani.
“Karibu Zahara, pita ndani”
“Asante”, niliingia ndani ya chumba kile, kilikuwa ni chumba nadhifu ndani
kukiwa na kila kitu cha thamani kinachotakiwa kuwapo chumbani.
Niliketi katika kochi huku macho yangu yakizidi kusaili mule ndani,.sikuwa na
wasiwasi na lolote.
Kitu kimoja ambacho sikuwahi kukijua wasaa ule ni kuwa uwepo wangu eneo lile
ungeweza kunisababishia madhila makubwa mno ambayo nisingeweza kuyasahau
kwa milongo mingi juu ya mgongo wa ardhi.
13
Yule mtu alisogea katika kabati la nguo na kufungua, kisha alitoa jaketi langu na
kunikabidhi, nilifurahi, muda huo huo nilianza kulipekua ili kuona kama vifaa
vyangu vipo salama.
Naam vitu vyangu vyote vilikuwa salama, nilishusha pumzi ndefu na kuhisi furaha
nyingi moyoni.
“Asante sana kaka yangu, sina cha kukulipa kwa kweli, ila nashukuru mno kwa
wema wako vitu hivi ni muhimu mno”
Yule mtu alitabasamu, lakini hakufumbua mdomo, alitizama pembeni bila kujibu
shukrani zangu kwa sekunde sita au saba kisha akasema,
“Usijali Zahara ilikuwa ni lazima hili litokee ili upate kunifahamu”
“Ndiyo, ni kweli, hakika Mungu ndio mpangaji wa kila kitu ulimwenguni”
“No, no,no hili halihusiani na mipango ya Mungu Zahara, huu ni mpango wa sisi
wanadamu”
“What!!”
Niliuliza kwa mshangao, maneno ya yule mtu yalinichanganya.
Yule mtu alinisogelea pale sofani na kuketi mkabala na mimi.
“Huu ni mpango wangu mahsusi” alisema tena kwa utulivu huku akinitumbulia
macho yake makali pasina kupepesa kando.
Nilifikiri kwa muda, nikaona kwa dakika nyingine tena nashindwa kabisa
kumuelewa yule mtu yale maneno yake.
“Any way, acha niseme tu nashukuru na sasa wacha mie niondoke maana usiku
ushakuwa mkubwa”
Hatimaye niliona ni kheri niage na kuondoka maana sikuwa na sababu nyingine ya
kuumiza kichwa kwa maneno ya yule mtu ambayo nilihisi alitamka pasina kufikiri,
aidha hisia zingine zikaniambia pengine alikuwa amekunywa pombe kidogo na
kuvuruga kidogo ubongo wake.
Nilisimama na kuzipiga hatua kuelekea mlangoni,
“Sawa kila kheri mrembo” yule mtu alisema.
Sikumjibu zaidi ya kuachia tabasamu lililosema,
14
“Tuko pamoja”
Nilipita katika ile korido na kukata kulia kuelekea katika lifti. Pale katika korido ya
lifti nilikuta lifti zote tatu zikiwa zinatumika, hivyo nilisisima na kusubiri kwa
muda kidogo.
Dakika moja badae mlango wa lifti moja katika zile tatu ukafunguka, bila
kuchelewa nikajitoma ndani.
Nilibonyeza kitufe kilicho andikwa G1, lifti ilishuka chini na sekunde tano tayari
taa ya kijani ikaonyesha nimeshafika G1, nilitoka ndani ya lifti ile nikiamini sasa
naweza kutoka nje ya jengo lile na hatimae kurejea nyumbani usiku ule.
Ajabu ni kuwa, pale lifti ilipo simama na mimi kutoka nje, nilikutana na mazingira
mageni machoni mwangu. Halikuwa eneo la nje ila nilipochunguza vizuri
niligundua nilikuwa ghorofa ya kwanza, hapo nikagundua nilifanya makosa wakati
nilipokuwa mule ndani ya lifti ile, sikutakiwa kubonyeza ‘G1’ badala yake
nilitakiwa kubonyeza ‘G’ pekee, hiyo ingenipeleka hadi chini kabisa ya ghorofa
lile.
Lakini hata hivyo sikuona tabu kwani chini hapakuwa mbali ni kiasi cha kushuka
ngazi kama nne na kuweza kuwa nje ya jengo lile.
Nilizifuata ngazi na kuanza kushuka chini. Eneo lile lilikuwa kimya, kulikuwa na
taa za bulbu kubwa zilizotoa mwanga hafifu wa rangi ya njano, nilishuka ngazi ya
kwanza na sasa nikashika ngazi ya pili. Chini ya ile ngazi ya pili, nilipata kuona
kitu.
Eneo lilikuwa kimya kama nilivyopata kusema. Mwendo wangu wa kasi wa
kushuka ngazi ukabadilika na sasa nilishuka taratibu nikitupia macho kitu
nilichoweza kuona, na hapo nika jua alikuwa ni mtu.
Alikuwa amejikunyata pembezoni mwa zile ngazi, alikuwa amejifunika shuka
nzito la rangi nyekundu mwili wote kasoro kichwani.
Jambo moja lilipita kichwani mwangu, kwa vyovyote vile yule mtu atakuwa ni
mlinzi, wazo hilo lilizidi kustawi katika akili yangu baada ya kutizama saa na
kuona ilikuwa yapata saa nane kasoro dakika kumi za usiku, “hawezi kuwa mtu wa
kawaida eneo hili, tena muda huu pasina kuwa ni mlinzi”.
15
Hatua zangu zikiwa za kawaida kabisa nilifika eneo lile ambapo mtu yule alikuwa
amejikunyata, nilimpita pasina kumsemesha lolote na kukuta kushoto kwa ajili ya
kuanza kushuka ngazi zinazo fuatia.
Ila ghafla.
Sauti ilitoka kwa yule mtu ilinifanya nitishike vibaya mno,yule mtu alisema,
“Usiku mwema Zahara”
Niligeuza shingo na kutupa macho yangu na kumwangalia yule mtu, hapo
nikakutana na kitu ambacho kilinifanya hali ya mshangao, niliduwaa, macho
yamenitoka, midomo imefumbuka kama lango la daladala aina ya UDA la
Mbagala, nikaanza kutokwa na jasho, kitu kisicho cha kawaida nikaona
kinanyemelea maisha yangu.
Alikuwa ni yule mtu aliyekuwa na jaketi langu lililokuwa na vitu muhimu vya
ofisi.
Nilijikuta nataka kutimua mbio ila miguu ilikuwa mizito nikabaki nimeganda
namtizama yule baba.
“Hivi Zahara pamoja na kusaidia kibarua chako hujataka kunifahamu hata jina
langu bibie?” Yule mtu aliuliza huku akisimama kwa tabu eneo lile.
“We umefikajefikaje hapa?” badala ya kujibu nilijikuta namtupia swali huku
nikiendelea kumshangaa na sasa haukuwa mshangao tu bali ulikuwa ni hofu kubwa
iliyochanganyikana na mshangao.
Yule mtu alisimama wima akiwa bado amejifunika lile shuka jekundu, miguuni
akiwa peku.
“Katika maisha yangu ya kichawi sijawahi kuona mwanamke msomi lakini wakati
huo huo ni zumbukuku wa mwisho kama wewe!” Yule mtu alisema, kauli ile
ilinifanya mwili wote uingiwe na baridi na kuwa kama mithili ya mtu
aliyemwagiwa maji ya baridi.
Pumzi zilinitoka kwa kasi sasa nikaona kumbe nimekutana na kiumbe kisicho cha
kawaida, sikutaka zaidi kuyatafakari maneno mengine ya yule mtu, neno
“mchawi” lilitosha kabisa akili yangu kuiamrisha miguu yangu ikimbie kwa kasi
eneo lile.
16
Nilitoka mbio nikiwa nimekumbatia jaketi langu kifuani nikitoa yowe dogo la
msaada, nilizishuka ngazi upesi upesi upesi huku nikiyumba hovyo.
Nikamaliza zile ngazi sasa nikashika ngazi za mwisho na kuwa chini ya jengo lile,
wakati nashuka ngazi ya kwanza, ngazi ya pili ile nashuka ngazi ya tatu tu.
Nilijikuta nikifunga breki ghafla na kubaki nimesimama huku nikiweweseka.
Yule mtu alijitokeza kutokea kona ya mwisho ya ile ngazi, alitembea kikakamavu
kunisogelea huku mwendo wake ukifanana kabisa na viumbe aina ya Saibogi,
alikuwa akinijia kwa mwendo wa kunyata lakini akijiamini, macho yake yakiwa
makali, huku sura yake kwa ujumla akiifinya na kufanya awe na mwenekano wa
kutisha, alichanua vidole vya mikono yake na kutanua mikono yake huku akitoa
ngurumo ndogo mithili ya mtu aliyepandisha mashetani na akawa ananisogelea.
Kwa kweli niliogopa mno.
Kwa muda wa sekunde zisizozidi tatu, nilibaki nimebung’aa nikishangaa yale
mambo yaliyo kuwa yanajiri mbele yangu katika jumba lile kabla ya kujikuta
nikipiga kelele kwa nguvu.
“Mamaaaa, mamamaaa nakufaaaa uwiiiiii nisaidieniii” nilipiga kelele nyingi huku
nikitoka mbio kupandisha ngazi kurudi juu.
Nilikuwa nahema kwa kasi, nikizidi kupiga kelele huku nikijitahidi kuzipanda
ngazi za jengo lile kujitenga na yule mtu wa ajabu, mashaka makubwa yalikuwa
kifuani kwangu.
Sikumbuki vizuri nilipanda ngazi hadi ghorofa ya ngapi, ila ninachokumbuka ni
kuwa ilifikia hatua mapafu yangu yalichoka, nilichoka kupiga mayowe kwa nguvu
huku nikizipanda ngazi tena nikiwa nakimbia.
Niliangaza nyuma yangu na kuona niko peke yangu, hapakuwa na mtu yeyote aliye
kuwa akinifuata lakini pia hakujitokeza mtu kunisaidia, pamoja na kwamba
nilikuwa nikipiga makelele ya hali ya juu, lakini hata hivyo sikumwona tena yule
mtu wa ajabu.
Sasa nikiwa najisukuma kwa mbele kwa mwendo wa kutembea nikiendelea
kuzipanda zile ngazi, nilikuwa nahema kwa kasi, machozi na kamasi vilikuwa
vikinitoka kwa pamoja, woga wa kuingia katika mikono ya mchawi ulikuwa
mkubwa.
17
“Mungu wangu wa mbinguni uko wapi sasa muda huu! Huoni ninavyoingia katika
madhila haya? Sasa unangoja nini kunisaidia yarabii” nilijikuta nikitamka yale
maneno huku nikiwa nimepagawa katika kiwango cha mwisho.
Nilizidi kuzipanda ngazi bila kuona dalili yoyote ya kufatwa ama uwepo wa mtu
katika jengo lile, eneo lote lilikuwa kimya, ilikuwa ni sauti ya vishindo vya hatua
zangu kupanda zile ngazi ndio zilizosikika. Yaani ilikuwa ni kama kwamba kile
kilichotokea muda mchache kilikuwa hakijatokea.
Ni hapo nilipo ingiwa na fikra hizi, kuwa huenda ndani ya ghorofa hili kulikuwa na
mtu mmoja tu yanii yule mtu mchawi.
 
SURA YA TATU

WAKATI nalitafakari hilo akilini mwangu wazo jingine likanijia, “kwanini
nazidi kuelekea juu ama ndani zaidi ya jengo hilo?” nilijiuliza mwenyewe swali
hili lakani jibu lake lilikuwa ni jepesi tu, nikajipatia jibu mwenyewe kuwa
“naelekea juu ama ndani zaidi ya jengo lile kwakuwa namkimbia yule mtu asiye
wa kawaida” lakini nikajiuliza tena, “kama namkimbia yule mtu asiye wa kawaida
kwa kuingia ndani zaidi ya jengo lile eneo ambalo inavyoonyesha ndio himaya
yake na anajua kona zote za jengo lile, je zile hazitakuwa ni sawa na mbio za
siafu? Na hiyo si ni sawa na kujiingiza ndani ya kichaka cha adui?.”
Nilijiuliza.
Lakini ubongo wangu haukupata jibu. Ni hapo nilipo hisi sauti fulani
ikinitahadhalisha kuendelea kuzipanda ngazi za jengo lile.
Nilisimama ghafla na kubaki nimeganda. “Sasa nifanye nini Mungu wangu”
nilisema kwa sauti ya ya kunong’ona. Mwisho niliazimia lazima nitoke nje ya
jengo hili liwalo na liwe lakini lazima niwe nje.
Kwa mara nyingine nikajikaza kama mwanamke nikageuka nyuma na kuanza
kuzishuka ngazi tena, wakati nikiwa nashuka chini kwa bahati upande wangu wa
kulia mwa ukuta niliona kuna mtungi wa gesi lakini pembeni ya mtungi huo
kulikuwa na shoka ndogo ya chuma yenye rangi sawa na ile ya ule mtungi wa gesi.
Bila kujiuliza mara mbili niliifyatua ile shoka iliyokuwa umepachikwa katika
kishikizio chake pale ukutani, sasa nikawa tayari kupambana na yule baba mchawi
pale itakapobidi.
Nikaendelea kuteremka taratibu nikiwa na tahadhali kubwa, wakati huo ilikuwa
yapata saa saba na dakika hamsini.
Kitu kingine ambacho ningependa ndugu msomaji ufahamu, ni kuwa, tangu niingie
katika jengo lile nilipata kutizama saa yangu ya mkononi mara mbili, ajabu ni
kuwa muda ulikuwa ikienda taratibu zaidi ya kawaida.
Kwa kipindi ambacho nimetumia kuwasili katika lile jengo hadi kutokea kwa
sintofahamu, kwa makadirio ilikuwa yapata kiasi cha dakika thelathini lakini saa
yangu ilinionyesha ni kiasi cha tofauti ya dakika tatu tu toka niingie hadi sasa.
19
Sikufikiria zaidi hilo kwani akili yangu ilifikiria zaidi ni kwa namna gani nitatoka
Mule ndani.
Nikiwa bado nashuka zile ngazi kwa mbali nikahisi kuna chakarachakara za mtu
kutokea huko chini niliko kuwa naelekea, nilipunguza mwendo nikauvaa ujasiri na
sikuwa tayari kurudi nyuma, sasa nikaelewa kuwa kutokea kule chini kulikuwa
kuna mtu aliye kuwa akipanda ngazi kwa kasi, zaidi ni kuwa mtu huyo alikuwa
akitweta huku akitoa sauti kama ya mtu aliyepagawa kutokana na taharuki fulani.
Sauti iliendelea kunikaribia na ilikuwa ni sauti ya mwanamke, nilisogea pembeni
na kutupa macho kule chini, nilimwona mwanamke mnene kiasi, akizipanda ngazi
kwa kasi lakini akiwa ni mtu aliyechanganyikiwa vibaya mno.
Nilipata hofu moyoni, nikalewa kwa vyovyote vile mwanamke yule lazima
atakuwa amekutana na yule baba mwenye kujisema kuwa yeye ni mchawi.
Nilisimama pale katika ngazi kumngoja yule mwanamke nikiamini kwa vyovyote
vile maswahibu yaliyomkuta yanafanana na yangu hivyo sina budi kuunguna nae
na kuangalia njia ya kutatua sintofahamu ile.
Yule mwanamke sasa alianza kupanda ngazi moja kabla ya kuanza ngazi ya pili
niliyokuwa nimesimama mimi.
Na wakati anamaliza zile ngazi ile anaanza tu kupanda, alisimama ghafla na kupiga
ukulele mwingi wa hofu baada ya kuniona mimi.
“Nyamaza,..nyamaza..tulia tafadhali, mie sio mtu mbaya”, nilisema kwa sauti ya
juu, yule mwanamke alitulia kidogo akawa ananiangalia kwa mashaka makubwa.
“Tulia tafadhali mimi pia nina matatizo kama yako” niliendelea kumsihi yule
mwanamke. Alibaki akihema huku akiliangalia lile shoka nililokuwa
nimelikamata, kwa kweli ilimchukua sekunde kadhaa kabla ya kuniamini.
“Wanakuja” yule mwanamke alisema huku akihema kwa kasi.
“Akina nani!”
“Wanakuja kuniua tukimbie… wako wengi… wanakuja” alisema yule mwanamke
wa makamo pasina kunipa taarifa vizuri.
“Wako wapi akina nani?” nilimuuliza.
20
Lakini hakujibu zaidi ya kusonta kwa kidole kuonyesha kuwa wako huko aliko
toka na kabla sijasema kitu kingine yule mwanamke alitoka mbio na kuzidi
kupanda juu.
Moyo wangu ulipiga paaaa, nilihisi tumbo linapata joto huku mate mepesi yakijaa
mdomoni lakini pia jasho jembamba lilinitoka maungoni mwangu
Nikabaki nimesimama pale moyo wangu ukishindwa kabisa kwenda mbele lakini
pia akili yangu haikuwa tayari kabisa kurudi nyuma nilibaki nimegenda kama
sanamu la askari pale Posta.
Yule mama alizidi kuziparamia ngazi na kutokomea kabisa kule juu. Sasa
nikaelewa kuwa kumbe kuna watu zaidi ya mmoja katika hili jengo, si kama
nilivyokuwa nikifikiria hapo awali.
Nikiwa bado pale, shoka langu likiwa mkononi, nilitupa macho yangu kule chini
nilikokuwa naelekea, nilichokiona kilinitisha sana.
Watu wanne wanaume walikuwa uchi wa mnyama, walikuwa wamebeba mwili wa
mtu aliyekuwa kama mtu aliye ungua na moto,mwili wa yule mtu aliye kuwa
amebebwa katika machela ulikuwa na nyama nyekundu iliyoonyesha kama mtu
yule amebabuliwa na mafuta ya moto. Wale watu walikuwa wamejipaka masizi
meusi usoni mwao na kufanya waonekane kama vinyago vya Kimakonde.
Walikuwa wakizipanda ngazi kuja juu nilikokuwa mimi huku wakiimba nyimbo
fulani kwa lugha ambayo sijawahi kuisikia hapa duniani.
Kwa kweli nilijikuta nikipiga kelele nyingi na kutoka mbio huku nikitupa kile
kishoka na kupanda juu mradi nijiweke mbali na jambo lile la kutisha.
Niliendelea kwenda kasi, atimae nikafika mwisho kabisa wa ghorofa lile, nilikuwa
niko juu kabisa ya lile jengo pale juu kukiwa na eneo kubwa la wazi, kulikuwa na
mitambo mbali mbali ya vitu kama satelaiti pamoja na antena.
Nilisogea mwisho wa ukuta na hapo niliweza kuona mandhari ya jiji la Dar es
Salaam, jiji lilikuwa kimya, mataa ya umeme yakifanya mji kunga’aa na kuvutia.
Kwa kweli machozi yalinitoka.
Nilijikuta nalia kama mtoto mdogo, sasa niliona kama ndio naiona nchi kwa mara
ya mwisho na badae kushikwa na wale watu na kufanywa mbuzi wa kafara.
Niliangalia chini nikaona niko umbali mrefu kutoka ardhini kiasi kwamba kama
ikitokea umeanguka kutoka kule juu basi ukifika chini mifupa yote huna.
21
Nililia mno, sikujua kwanini yote haya yananitokea mimi, nilijiona ni mwanamke
mwenye bahati mbaya katika siku za ukubwa wangu.
Niliikumbuka familia yangu, nikawakumbuka wafanyakazi wenzangu hususani
timu nzima niliyokuwa nayo kule safarini Geita. Kwa kweli nilihuzunika mno,
nilitamani nipaze sauti yangu na iwafikie watu ambao wangeweza kuja kunipa
msaada lakini sikuweza.
Na mwisho mawazo yangu yakakita kwa Thabit Twalib Mwaikimba ni mpenzi
tuliyekuwa na ndoto kubwa ya pamoja, ndoto ya kufunga ndoa ndogo tu ya mkeka,
tuwe na biashara yetu ndogo itakayoleta matokeo makubwa, kisha tuzae mtoto
mmoja mzuri ambaye tutamsomesha hadi chuo kikuu.
Lakini kila kitu hadi wakati huo, niliona kinaeleka kubaki kuwa hadithi tu kama
zile za mwandishi Shafi Adam Shafi.
Nikiwa bado nafikiria mambo yale mara nikasikia vishindo, nilikurupuka upesi
nikajisogeza karibu na lilipokuwa sinki kubwa la maji aina ya “Simtank” kwa
lengo la kujificha.
Niliposogea tu pale katika lile sinki mara moyo wangu ukapiga mkumbo na
kujikuta naruka hatua moja kwa pembeni kisha nikabaki nimebung’aa.
Yule mwanamke niliyekutana nae kule ndani alikuwa amejificha pale, alikuwa
amejikunyata miguu yake ameikumbatia karibu kabisa na kifua chake huku kichwa
chake akiwa amekiegemeza katika magoti yake.
Ajabu ni kuwa yule mama alikuwa ameganda hatikisiki wala hasemi lolote, wakati
huo huo wale watu waliokuwa uchi huku wamebeba machela iliyokuwa na mwili
wa mtu aliyekuwa amebabuka mwili wote waliwasili eneo lile.
Hapo hapo nilikurupuka na kusogea upesi pale alipokuwa amejikunyata yule
mwanamke. “wa..wa.me..fika” nilisema kwa kunong’ona kumwambia yule
mwanamke.
Nilikuwa natetemeka vibaya mno, nilichungulia kidogo, nikaona wanashusha
mwili wa yule jamaa aliyekuwa katika machela ambaye bila shaka alikuwa
amekwishafariki na kuuweka chini.
“Uu..wiii leo..mamaa..ya..ngu weeee!!” nililia, mwili wote ukiingiwa ubaridi,ila
yule mwanamke alibaki akiwa vile vile ameganda hasemi wala hajibu lolote hata
ile hofu yake haikuwepo.
22
Nikahisi kitu kisicho cha kawaida kwa yule mwenzangu, nilimtizama nikamwona
uso wake ukiwa ni wenye hofu kubwa ila macho yake yamekodoa sehemu moja
bila kope za macho yake kupepesa.
Hakuna kiungo katika mwili wake kilichokuwa kinatikisika. “Hey..hey” niliiita.
Kimya.
“Hey wee ma..ma” niliita tena kwa kunongo’na.
Kimya tena, hakukuwa na jibu.
“Wewe..mbo..na hu,.semi ki..tu?” nilimsemesha kwa kunongo’ona.
Kimya kwa mara nyingine.
Nilimsogelea nikamgusa, hapo hapo yule mama akaanguka chini kama mzigo.
Niliruka hatua moja nyuma kwa woga.
Hapo nilipata kujua kuwa yule mama alikuwa amekufa. Nilichanganyikiwa sana.
Nililia nikifinya sauti yangu kwa chini ili wale watu wasinisikie.
“Wewe mama sasa unafanya nini hivyo!” nilisema kibwege huku nikitetemeka
kama mtu mwenye degedege, yule mtu alikuwa amekufa huku akiwa amekodoa
macho kama kwamba kabla ya kifo chake aliona tukio baya la kuogopesha.
“Halow Zahara” ghafla..sauti ilitokea nyuma yangu…nilistuka, “uwiii”,niliruka
kwa hofu huku nikiachia ukulele kisha niligeuka, macho kwa macho nikakutana na
yule baba.
“Uwiiiiiiiiiiiii” nilipiga kelele nyingi za hofu.
Na bila ya kutarajia nikajikuta nazungukwa na wale watu wanne waliokuwa na
masizi usoni mwao mithili ya vinyago vya Kimakonde.
“Toka..to..ka..to..ka” nilisema kwa fadhaa kama kwamba nafukuza nyani
shambani. Wale watu wakawa wananisogelea taratibu huku wakiwa wamekodoa
macho yao na vidole vya mikono yao wamevichanua kama majini, lakini yule baba
mchawi mwenye shuka jekundu yeye alikuwa amesimama vilevile.
Kadri walivyokuwa wakinisogelea ndivyo nilivyoona kifo changu kinazidi kuwa
karibu yangu.
23
“Mamaaaaaaa” nilipiga ukulele mkubwa wakati wale watu wanne waliponifikia,
na sauti yangu ikasambaa katikati ya jiji usiku ule, huku mwangi ukiniitikia kwa
mara ya pili masikioni mwangu.
Sasa mikono ya wale viumbe ikanikamata, ikaushika mwili wangu kwa pamoja,
nilihisi mwili wote unakufa ganzi punde baada ya kuguswa na wale viumbe. Lakini
wakati huo huo nikabebwa kwa nguvu ya ajabu na wale watu wakawa
wamenining’iniza juu juu kunipeleka mahala nisipopajua.
Nilipiga ukulele mwingi kujaribu kufurukuta na kujinasua kutoka katika mikono
ya wale watu lakini mikono yao ilikuwa na nguvu za ajabu kadri nilivyozidi
kufurukuta ndivyo mikono ile ilivyozidi kunibana kwa nguvu hadi nikawa napata
maumivu.
Walinipeleka ndani ya lile jengo kisha wakaniingiza ndani ya chumba kimoja
miongoni mwa vyumba vingi vilivyokuwapo katika nyumba ile ya ghorofa.
Bila kutarajia nikajikuta narushwa hewani, niliachia ukulele wa kuogofya baada ya
tukio hilo lakini nikajikuta naangukia sehemu laini yenye kunesanesa. Ilikuwa ni
kitandani.
“Waiiii..uwiiiii” nilipiga kelele nyingi huku nikikurupuka pale nilipoangukia na
kujiweka sawa. Akili yangu niliona kama inazunguka kwani nilikuwa ni mtu
mwenye mashaka makubwa vibaya mno. Wale watu wanne walisimama
kukizunguka kile kitanda kisha sura zao wakazielekeza juu huku macho
wameyatoa vibaya.
“Ninyi ni akina nani na mnataka nini kwangu?” nilijikaza na kuuliza jasho
likinitoka katika maungo yangu.
Hapakuwa na majibu niliyoyapata, wote waliniipuza kama kwamba hawakusikia
swali langu. “nini hiki?” Kitu gani kinatokea katika maisha yangu mimi? Kwanini
yote haya yananisibu mimi?” nilijiuliza mwenyewe lakini sikuwa na majibu na
sikuona mtu wa kunipa majibu yale.
Wale watu wakiwa wanatizama juu na kuwa kama wanazungumza maneno fulani
kwa kunong’ona mara mule ndani ulianza kutoka moshi mweupe, niliona moshi
mzito mweupe lakini sikujua ni wapi moshi ule unatokea,ule moshi ukasamba
mule ndani na kuacha halafu fulani nzito nisiyoweza kuielezea.
Aisee haya mambo endelea kuyasikia tu yanahadithiwa katika riwaya kwa kweli ni
mambo yenye kutisha si kawaida.
24
Kwa dakika nilikuwa nimejikunyata katika kona ya kitanda kile kilichokuwa
kimetandikwa mashuka mekundu huku rangi ya kuta za chumba kile ikiwa ni rangi
ya maziwa.
Nilijaribu kukisaili kile chumba haraka haraka nikaona kile kilikuwa ni chumba
kikubwa tu kilichokuwa na vitu vichache tu, kabati la nguo, televisheni ndogo ya
Hitachi, saa ya ukutani aina ya Ajanta, meza ndogo ya kioo iliyobeba simu ya
mezani, na pangaboi lililokuwa limefungwa darini ambalo lilikuwa likizunguka
kwa kasi na kutoa upepo mkali mule ndani.
Kwa kweli nilikuwa ni mtu mwenye hofu kuu, niliendelea kujikunyata pale katika
kona ya kitanda huku nikilia na kumuomba Mungu wa mbinguni kimyakimya.
Mara macho yangu yakashuhudia tukio jingine lililonifanya nipige kelele nyingi,
*****
Aliingia yule baba akiwa na vazi lake lile lile, sura lake amelichafua kwa mikunjo
mikunjo iliyojipinda kama mkeka wa kisukuma huku akionekana ni mtu mwenye
hasira kubwa, lakini kubwa kuliko vyote alikuwa ameshikilia kichwa cha yule
mwanamke niliyekutana nae katika ngazi kabla ya kumkuta akiwa amekufa pale
mafichoni.
“Mme..mchi..nja mtu.. na kumnyofoa kichwa?” nilisema kwa kitetemeshi, uzito
wa kile nilicho kiona kilinielemea na kuniwia vigumu kuamini, nilikuwa
nimeduwaa macho nimeyatumbua kwa yule baba huku mdomo wangu ukijikuta
unaachama mshangao uliochanganyikana na hofu vikishika hatamu, kwa kweli
tukio lile lilikuwa kubwa mno kwangu.
Toka nizaliwe sikuwahi kushuhudia tukio baya na la kuogopesha kama lile, akili
yangu haikuwa tayari kuamini tena kama wale walikuwa ni binadamu waliozaliwa
na mwanamke, “bila shaka ni majini haya, mashetani, mizuka”, sikuona sifa stahiki
za wale viumbe.
Mwisho niliishia kulia kwa uchungu na kusubiri zamu yangu ya kuchinjwa na ile
mizuka.
Yule baba alisogea na kile kichwa kilichokuwa kinatiririsha damu kisha ile damu
akawa anainyunyuzia katika kile kitanda nilichokuwa nimekalia.
Nilijikuta najitapikia hovyo huku nikihisi kichefuchefu cha hali ya juu.
25
Baada ya kufanya tukio lile yule baba aliwapa wale watu kile kichwa na mara wale
watu wakaanza kukigombania kile kichwa kwa kukitafuna na kunyonya damu
iliyokuwa inatoka katika shingo.
Kwa mara nyingine nikajikuta natapaika hadi nikahisi nguvu zikiniishia. Wale
watu wenye masizi na miilini mwao wakiwa uchi walitoka mule ndani huku
wakiendelea kukishambulia kile kichwa cha binadamu.
Nikaelewa kitu,
Kwa tukio lile nikapata kunga’amua kwa wale viumbe wenye masizi ndio vile
viumbe vyenye kuitwa misukule, ama wengine wanaita ndondocha, lakini pia
nikapata kuelewa kuwa yule baba mchawi wale misukule walikuwa ni viumbe
vyake anaowafuga.
Kwa faida ya wale wasioelewa, misukule ama mandondocha ni wale binadamu
walioaminika kuwa wamefariki dunia lakini badala yake wanakuwa
wamechukuliwa kichawi na wachawi kwa dhumuni maalumu.
Nililifahamu hili upesi kutokana na habari za viumbe wa namna hii niliwahi
kusoma katika vitabu hasa vile vya Ally Mbetu na pia hata kupata bahati ya
kusikia hadithi zao kutoka kwa watu tofautitofauti.
Sasa mule ndani tulibakia wawili tu, mimi na yule baba.
“Sijawahi kufanya jambo lolote baya” nilisema huku nikimtizama yule mtu kwa
huruma, mtu ambaye muda mfupi uliopita tulikuwa marafiki tena rafiki
aliyenisaidia kuvipata vitu vyangu, lakini sasa kawa mtu mbaya na hatari kwa
maisha yangu.
Yule mtu hakujibu kitu, alinyanyua mikono yake juu na kuanza kuzungumza vitu
fulani kwa lugha nisiyoijua wala kuwahi kuisikia katika popote pale katika
ulimwengu huu. Na kadri alivyokuwa akizungumza maneno fulani hali yangu
ilikuwa ikibadilika.
Nilikuwa nikijisikia kitu kama usingizi mzito ukizikumba mboni za macho yangu.
“Mungu wangu ndio nakufa hivyo…” usigizi mzito ulikuwa ukinijia kwa kasi,
wakati yule mtu akikazana kutamka maneno yale kwa nguvu tena kwa
kuyarudiarudia.
“Kumbe ndivyo hivi mtu akitaka kufa inavyo kuwa” niliwaza wakati giza la ajabu
likinipitia katika ufahamu wangu.
 
SURA YA NNE

SIKU moja katika maisha nilidhani kubadilisha ndoto zangu na kuvurugikiwa
ilihitaji miaka mingi jambo hilo kutokea. Nilidhani kuisha kwa uzuri wangu na kila
nilichokianzisha toka nilipokuwa mdogo ilihitajika miaka mingi kama ile
niliyokuwa nayo sasa. Nilikuwa msichana wa miaka 24 tu mwenye ndoto kubwa
ambazo tayari sasa zilikuwa zinaeleka kutimia asubuhi ya siku inayofuatia.
Nilitarajia kuendesha gari zuri la kifahari na familia yenye furaha mchumba mzuri
nitakayefunga nae ndoa ndogo tu ya mkeka itakayojumuisha watu wachache sana,
ndicho kitu nilichokiwaza katika muda wote wa maisha yangu. Kwa kweli hatima
ya maisha yetu anayeijua ni Mungu na kamwe huwezi kumuona na kumuomba
muda zaidi maisha yafikapo tamati, kila kitu huvurugika pale jioni ya maisha yako
ifikapo. Milango ya ndoto zako hufungwa na giza nene hutanda mbele, hata fimbo
ya kukuongoza njia hupotea.
Mwanga hufifia na woga hukusonga. Hiyo ndiyo hali iliyonipata katika usiku wa
giza ni baada tu ya kupoteza jaketi langu lililokuwa na vitu muhimu vya ofisini
ambalo liliokotwa na mtu wa ajabu.
Kichwa changu kilikuwa kizito, nilipofumbua macho, hata macho nayo yalikuwa
mazito, kwa mbali niliona ukungu mbele yangu huku nikiona kufifia kwa vitu
vilivyoonekana mbele yangu.
Nikiwa nimelala, chali macho yangu yakiwa yanitizama katika dari ya chumba
nilichokuwepo huku fahamu zangu zikiwa hazijakaa sawa nilihisi chakarachakara
ubavu wangu wa kulia. Nikageuza shingo yangu.
Mtu mwanaume alikuwa uchi huku akichezea sehemu zake zilizokuwa wima kama
ukuni mkavu, alikuwa akiniangalia huku akilamba lamba lipsi za midomo yake.
Sasa mtiririko wa matukio yote yaliyotokea kabla ya kupitiwa na usingizi mzito
yakarejea tena upya, nikajikuta nataka kupiga kelele, lakini ajabu sikuwa na nguvu
hata ya kufumbua mdomo.
Ni wakati huo huo pia nilipogundua kuwa hata mimi pia nilikuwa uchi wa mnyama
pale nilipokuwa nimelala chali.
27
“Nataka kubwakwa “Yallah”, uko wapi wewe Mungu? Basi Mungu nakuomba
ufanye miujiza yako,.sitaki kubakwa na mashetani mimi” niliomba kimoyomoyo
huku nikijaribu kujitikisa pale kitandani, lakini nilikuwa kama mtu aliyepigwa
nusu kaputi.
Machozi yalinitoka baada ya kugundua sina namna ya kuzuia kile kinachoonekana
kutaka kutokea muda mfupi ujao.
Kama nilivyotegemea yule baba alipanda kitandani akawa mbele ya mapaja yangu
huku sehemu zake zikinitizama kwa uchu!.
Yule mtu alichukua chupa ndogo nyeusi, kisha akafungua mfuniko na kutoa dawa
fulani iliyokuwa na mafuta kama ya “Gliseline” ila yale yalikuwa ya njano. Kisha
akayanuia kwa sauti ndogo yale mafuta, kisha akajipaka katika lile jogoo lake
kubwa.
Baada ya hapo akanisogelea na kunitanua mapaja yangu,.kwa kweli ndugu
msomaji huwa kila nikifkiria tukio hili, akili yangu inashindwa kabisa kulifuta na
kusahau jambo hili la kinyama.
Niseme tu kuwa huwa najihisi haya (aibu) kuelezea eneo hili, lakini kwakuwa
nahitaji ulimwengu wote utambue juu ya maisha yangu na ukweli kuhusu mimi
sina budi kuficha jambo hata moja katika yale mengi yaliyonisibu.
Mara zote nimekuwa ni mtu ninayehitaji uhuru wangu, labda kuna watu wanaweza
kuona ninajidhalilisha katika hili na niseme tu nimekuwa mwanamke ninaeamini
katika zile falsafa za bwana Thomas Sankara nilizowahi kusoma katika vitabu
nilipokuwa chuo kikuu pale Mlimani alisema “ili kuleta mabadiliko na mitazamo
chanya ni lazima kuwa na hali fulani ya uendawazimu.” I
la tusiufikirie uendawazimu huu wa kuokota makopo bali ule ukichaa mzuri wa
kuamini katika mambo au misingi fulani na kuisimamia kwa dhati pamoja na
changamoto nyingi. Kwa kuamini kwa dhati katika mabadiliko haya na kutaka
kuboresha maisha,” hivyo sina budi kueleza ukweli mtupu bila kujali nani ataniona
mwendawazimu.
Wazungu wana msemo usemao, “To be healthy you have to share your problems
with others!”
Yule baba alipokuwa akiniingilia kwa kweli nilihisi maumivu makali mno kiasi
kwamba niliona kama utumbo unataka kutoka, maumbile ya yule mwanaume
yalikuwa ni makubwa mno.
28
Aliniumiza.
Alikuwa akiingiza na kutoa upesi upesi, huku pumzi zake zikimtoka kwa kasi,
alikuwa katika mahaba mazito juu ya mwili wangu.
Na mara zote wakati ananizini nilikuwa nikiona dunia inazunguka kwa kasi huku
mimi nikiwa ndani yake, yalikuwa ni mateso yasiyomithilika.
Yule mtu alinibaka hadi hamu yake ilipokwisha, nilikuwa nasikia sehemu zangu
zote zinawaka moto.
Sikujua kama yule mtu aliningiza katika maswahibu yale yote kwa sababu ya
tendo lile, lakini pia sikuwa na uhakika wa asilimia zote kama mtu yule anaweza
kuishia kunifanya vile kisha akaniachia uhai wangu.
Nilikuwa nikitweta huku maumivu makali yakinisulubu, hasira zilikuwa
zimenipanda vibaya mno, lakini sikuweza kuongea kila nilivyohitaji kufanya
hivyo.
Yule mtu alikuwa ameniroga na kunifanyia ukatili ambao sikustahili kabisa,
sikuona kama nilikuwa na kosa la kutendewa unyama ule.
Kwa kweli sikuona hata faida ya kuishi.
Yule mtu alipotoka mwilini mwangu, alifungua kabati lililokuwa mule ndani na
kutoa shuka jekundu kisha akajifunika, halafu akasogea mbele ya kitanda changu
kisha akaanza kufanya vitendo vile alivyokuwa anafanya kisha nikapitiwa na
usingizi wa ajabu.
Namna nilivyokuwa nimelala chali machozi yalikuwa yakinichuruzika pembeni ya
macho yangu na kutiririka hadi masikioni.
Yule mtu alikazana kuzungumza maneno yale ya ajabu, na hata yale maneno yake
yalipoingia ndani ya ngoma za masikio yangu nilianza kukumbwa na hali ile kama
ya awali.
Usingizi mzito ulikuwa ukininyemelea kwa kasi, hazikufika sekunde kumi na tano
tayari nilikuwa nimekwishazama katika bahari ya usingizi.

*****
29
Sikujua fahamu zilinirudia baada ya muda gani au baada ya siku ngapi kwani
kichwani mwangu nilikuwa nikipitiwa na taswira nyingi za ajabu ambapo
zilifuataiwa na vipindi virefu vya kiza na utupu mrefu akilini, Miongoni mwa yale
yaliyopita ni tukio la kuingiliwa kimwili na yule baba, nilikuwa nikimwona namna
alivyokuwa akikazana kuniingilia huku akitokwa na pumzi nzito za huba huku
mimi nikipatwa na maumivu yasiyoweza kuelezeka.
Nakumbuka, kuna wakati nilijihisi kuchoka mno kutokana na kulala muda mrefu
nilifumbua macho na kuona mwanga hafifu,. Mule ndani kulikuwa kimya hakuna
kilichosikika zaidi ya mishale ya saa ya ukutani iliyokuwa ikizunguka taratibu
huku ikilia “ta,ta, ta, ta” nilijaribu kuamka nikaona nina nguvu za kutosha.
Niliamka pale kitandani na kukaa kitako, nilikuwa myonge mithili ya teja wa
madawa ya kulevya mwenye kuhudhurua clinic.
Macho yangu yalitizama ile saa ya ukutani kwa kweli sikuamini kile nilicho kiona.
Ile saa ilionyesha ilikuwa yapata saa kumi usiku. “Inamaana kulala kote kule bado
hakujakucha asubuhi” nilijiuliza huku nikijikagua mwili wangu uliokuwa
umevalishwa tena nguo zangu zote ikiwa ni pamoja na lile jaketii lililokuwa na
vitu vya ofisini vyote.
“Au nimelala siku mbili humu ndani huyu baba akiwa amenigeuza mkewe”
niliendelea kujiuliza, lakini sikuwa na jibu kamili japo nilihisi kuwa kuna
uwezekano niliishi mule ndani kwa muda wa siku mbili nikiwa usingizini.
Nilipokuwa najikagua mwili wangu ndipo nilipoona jambo jingine lililonifanya
nitishike vibaya mno.
Tumbo langu lilikuwa kubwa kama kwamba nilikuwa na ujauzito wa mizezi tisa
na muda wowote naweza kujifungua. “Mungu wangu nini hii tumboni
mwangu.,nina mimba! Nimebakwa na nimepata mimba.. Lakini..hii mimba
inakuwaje iwe kubwa kwa siku mbili tu.!”
Nilinong’ona peke yangu machozi yakinitoka, “ni ukatili wa kiwango gani
natendewa mimi Zahara..nabakwa hadi napewa mimba..kwanini msiniue
tu..kwanini sijafa ..kwanini mniacha hai hadi sasa.. mshenzi wewe” nililia mno,
jambo lile lilikuwa ni kubwa mno. Nilijiona ni kiumbe nisiye na faida ya kuishi
duniani tena.
30
Mwili wangu ulikuwa mnyonge mno, nilihisi kabisa ndani ya tumbo langu kuna
kiumbe. Lakini jambo lililokuwa la kustajabisha ni kuwa ile mimba iliwezaje
kukuwa kiasi kile kwa siku mbili tu ambazo niliamini nilikaa mule ndani.
Nilinyanyua mkono wangu na kutizama saa yangu ndogo niliyowahi kupewa
zawadi na mpenzi wangu Thabit Twalib Mwaikimba, kwa mujibu wa saa yangu ya
mkononi ilinionyesha ilikuwa ni saa kumi kama ambavyo ile ya ukutani
ulivyosema, lakini katika kutaka kupata uhakika zaidi nilibofya ile saa ili nione
ilikuwa ni siku gani na tarehe ngapi maana siku ya mwisho kuingia mule katika lile
jengo ilikuwa ni usiku wa saa saba siku ya Alhamisi ya tarehe 29/3/1989.
Saa yangu ilinionyesha kitu kilichonifanya kuanza kupata hisia kuwa huenda nipo
katika ndoto mbaya usingizini.
Ile saa ilinionyesha kuwa ilikuwa ni siku ya alhamisi ya tarehe ya tarehe hiyo hiyo
29/3/1989, yanii ilikuwa ni usiku ule ule.
“Sasa hii miujiza gani tena jamani yaani kulala kote kule kumbe hata masaa matatu
hayajakwisha!.” Lakini hilo lilikuwa ni dogo katika kubwa lililoumiza mtima
wangu.
Vipi niwe na mimba kubwa kama ya miezi tisa ilihali niliingiliwa kimwili lisaa
limoja tu lililopita.
Niliona ninalo bomu kubwa ambalo linalokuja kulipuka katika maisha yangu muda
mchache ujao.
“Sasa nifanye nini” nilijiuliza, wazo la kutoroka mule ndani lilinijia, nilisimama
wima nikasogea pale mlangoni, bado ukimya wa ajabu uliendelea kushika hatamu.
Nikashika kitasa na kukinyonga kushoto, kitasa kiliachia “kwachaa” nikatoka kwa
kunyata nikiwa na tahadhari kubwa.
Niliangalia kulia na kushoto nikaona nipo katika kikorido kirefu kilichokuwa na
vyumba vingi vilivyofungwa pembeni yake.
Nikatizama mazingira yale kisha nikashika uelekeo ambao nilihisi ni uelekeo
sahihi wa kunitoa nje ya jumba lile.
Tumbo langu lililokuwa na kiumbe ndani yake lilikuwa zito na lilikuwa likiuma,
nilikuwa nikisikia kitu kilicho kuwa tumboni ambacho bila shaka alikuwa ni mtoto
akicheza cheza tumboni.
31
Niliendelea kujisukuma kwa mbele huku nikiwa na tahadahli kubwa, sikuwa na
woga tena, sikuogopa kifo kwani hata hivyo sikuona faida ya kuishi katika dunia
ilihali nikiwa ni binadamu niliye na kovu baya moyoni mwangu ambalo siwezi
kulisahu hadi siku naingia kaburini.
Nikiwa nazipiga hatua mara ghafla nilianza kusikia sauti kwa mbali.
Ile sauti ilipenya masikioni mwangu na kunifanya nipate kizunguzungu, sauti ya
yule baba akizungumza maneno ambayo huwa yananifanya nizingirwe na usingizi
mzito.
Yale maneno yalizidi kupenya katika masikio yangu pasina kuelewa mzungumzaji
yupo sehemu gani, lakini kwa namna nilivyokuwa nikisikia ilikuwa ni kama
mzungumzaji yupo maili nyingi kidogo kutoka pale nilipokuwepo mimi, kwani ile
sauti ilingia katika masikio yangu kama mwangwi.
Nilianza kupepesuka nguvu zikiniishia huku giza la ajabu likivaa mboni za macho
yangu.
Na wakati huo yule mtoto tumboni mwangu alikuwa akicheza, giza liliendelea
kutanda mbele yangu na kujikuta nguvu zinaninishia na kuanguka chini kama
mzigo.
Baada ya muda mrefu kupita nikiwa katika dimbwi la usingizi, mara nilistuka
nilipohisi sauti kali ikililia masikioni mwangu, ilikuwa ni sauti ya mtoto mchanga.
Nilifumbua macho yangu na kujikuta nipo katika kile kile chumba mtoto mdogo
wa mwaka mmoja akiwa pembeni yangu katika kitanda.
Na niliporejewa tu na fahamu zangu, tukio baya la kubakwa na yule baba ndio
ilikuwa kitu cha kwanza kupita katika ubongo wangu.
Nilijinyanyua kitako na kuketi pale kitandani. Mtoto mzuri wa kike alikuwa
pembeni yangu.
Yule mtoto hakuwa analia tena baada ya mimi kuamka, nilijiangalia tumbo langu
na kuona mabadiliko, sikuwa na mimba tena, nilijiona niko tofauti katika maungo
yangu.
Matiti yangu yalikuwa makubwa na yaliyolala ilihali awali matiti yangu yalikuwa
wima.
32
Lakini hata sehemu zangu za siri, kwa kweli vile nilivyokuwa najiskia awali si
sawa na muda ule. Hapo nikaelewa kuwa ile mimba iliyoingia kimaajabu nilikuwa
nimejifungua tena kimaajabu, na inavyoelekea nilijifungua wakati ule nimepoteza
fahamu.
Lakini ajabu nyingine mbele yangu ni yule mtoto pembeni yangu. Alikuwa ni
mtoto mkubwa wa mwaka mmoja ambaye swali kuu likawa yule mtoto amewezaje
kukua upesi kiasi kile. Wakati nalifikiria hilo saa yangu ya mkononi bado
ilinionyesha ilikuwa ni tarehe 29/3/1989, siku ya Alhamisi.
“Inamaana haya mambo yanenda haraka hivi kwa dakika ama ni kwa kutegema
siku miezi na miaka”
“Hapana lazima niondoke eneo hili, leo lazma niondoke siwezi kuishi humu! Nini
hatma ya maisha yangu? Kama kufa na acha nife tu, lakini siwezi kuendela kuishi
kifungoni kiasi hiki” nilendelea kuwaza nikiwa nimeketi kitako mule ndani tukiwa
wawili tu, mimi na yule mtoto mchanga.
Sasa nikawa nafikiria namna ya kukabiliana na mazingaombwe yale ambayo
yamekuwa yakindelea kutokea.
Kitu kingine ambacho nimesahau kukueleza mpenzi msomaji, ni kuwa toka siku
ile nibakwe na yule mbaba sikuwahi kumwona yeye wala mtu mwingine yeyote
mule ndani hadi siku nilipoamka na kujikuta nipo na yule mtoto mchanga wa
miaka miwili.
Nikaendela kuwaza namna ya kutoroka katika lile eneo nililoamini ni kifungo
kwangu. Swali dogo likaja kichwani mwangu. Je nitoroke na yule mtoto ambaye
niliamini ni wangu?
Nikapata kidogo kigugumizi katika hilo lakini sauti fulani ikanambia na
kunitahadharisha kuwa sitakiwi kuondoka na yule mtoto kwani kufanya vile ni
kutengeneza mazingira ya kuandamwa na wale viumbe kwani kwa namna yoyote
ile kupewa kwangu ujauzito ilikuwa ni mipango yao.
Lakini sauti nyingine ikanambia kamwe nisimwache mtoto wangu, kwani pamoja
na kwamba upatikanaji wake haukuwa mwema lakini bado yule malaika atabakia
kuwa damu yangu, na ni mimi mwenye jukumu la kuhakikisha usalama wa yule
mtoto unakuwepo kwani mimi ndiye mama yake mzazi.
Sasa nikawa nakinzana na nguvu mbili, kuondoka na yule mtoto ama kumwacha.
33
Nilifikiria kwa muda mwisho nikazimia kumwacha yule mtoto mchanga.
“Sikuja na mtoto hapa, vipi niondoke na mtoto, kwanza si mtoto huyu, mtoto gani
anaingia tumboni siku hiyo hiyo na kuzaliwa siku hiyohiyo kisha anakuwa siku
hiyo hiyo..hapana siwezi kubeba matatizo haya.” Nilinong’ona peke yangu
nikiteremka kitandani.
Msomaji pengine haya nikuelezayo unaweza kuhisi kabisa ni hadithi za kubuni,
lakini amini nakwambia hakuna hata moja la kubuni katika hayo niliyokwisha
kueleza.
Kuna wakati hata mimi sikuwa naamini wakati yananitokea lakini amini
nakwambia katika huu ulimwengu kuna mengi ya ajabu ambayo yanatokea katika
jamii ya siri (secret society) ambayo ukisimuliwa unaweza usiamini asilani.
Sasa nikiwa pale, nilipoangaza chini nikaona raba zangu zikiwa chini ya kitanda,
upesi nikavaa na kuwa tayari kuondoka.
Lakini ghafla.
Nilisikia ile sauti, sauti ya yule baba, alikuwa akizungumza yale maneno yenye
kunifanya nipatwe na usingizi wa ajabu.
Sauti ile kama ilivyo kuwa awali, ilitokea maili nyingi, ilifika pale kama mwangwi.
Na mara ilipopenya katika masikio yangu nikahisi kizunguzungu, nikaelewa kitu
gani kinaenda kutokea, safari hii sikuwa tayari kabisa kuendela kulala lala pale
huku wale wachawi wakinichezea kama shangazi yao, nilidhamiria kabisa
kuondoka mahala pale, ile sauti ikakazana kuyatamka yale maneno, hali yangu
nayo ikaendela kubadilika, kizunguzungu kikazidi kunielemea huku giza la ajabu
likinizingizira.
“No no siwezi kuendelea kubaki hapa..” nilijikuta kinibwata kwa hasira wakati ile
sauti ikizidi kugonga ngoma za masikio yangu.
Sasa akili yangu ikafanya kazi upesi upesi, kwakuwa ile sauti ikisikika masikioni
mwangu ndio huleta madhala ya kupoteza fahamu nikaona njia pekee ya kuzuia
hali ile ni kuziba masikio ile sauti nisiisikie.
Niliingiza vidole vya shahada ndani kabisa ya masikio yangu na kukandamiza kwa
nguvu kuzuia ile sauti kupenya katika masikio yangu.
34
Sikusikia chochote zaidi ya mvumo fulani katika masikio ambao huwa unasikika
pale unapoziba masikio. (Wanazuoni wa tauhidi husema ule ni mvumo wa moto
wa jehanamu).
Kwa muda wa dakika mbili niliendelea kuziba masikio pasina kusikia yale
maneno, niliondoa taratibu vidole katika masikio, sikusikia kitu chochote zaidi ya
sauti ya yule mtoto aliyekuwa akilia kwa nguvu.
Nilibaki nimesimama nisijue kitu gani nifanye, mara nikiwa bado nimesimama
nilihisi nyayo za mtu akija kutokea nje akielekea mule ndani
Akili yangu ikaendela kufanya kazi upesi upesi, niliruka kitandani na kulala
gubigubi na kujifanya nipo katika usingizi mzito.
Zile nyayo ziliendelea kusogea mule ndani na hatimae nikahisi kitasa cha mlango
kikiguswa na kisha akaingia mtu, kupitia pembe ya jicho niliweza kumwona
mwanaume mzee mno akiwa amevalia kanzu nyekundu.
Nilipomtizama vizuri mtu yule nikagundua mtu yule alikuwa ni mzee kati ya
miaka themanini, lakini nipo mtizama kwa uzuri zaidi nikagundua yule mzee
alikuwa akifanana mno na yule baba aliyenibaka, nikahisi pengine huenda wale
watu walikuwa ni watu wa familia moja, familia gani hii washenzi wa tabia kiasi
hiki, niliwaza.
Alikuwa amekamatia vibuyu viwili vilivyofungwa hirizi nyeusi na nyekundu.
Yule mtu alisogea hadi pale kitandani kisha akazungumza maneno fulani nafikiri
ya kichawi kisha akafungua vile vibuyu vyake, mara moshi mweusi ulitokea katika
vile vibuyu na kusamba mule ndani, baada ya hapo alimsogelea mtoto kisha
akambeba na kutoka nae nje.
Nilitaka kufanya kitu baada ya tukio lile lakini nafsi nyingine ikanionya juu ya
hilo.
Niliendelea kutulia kwa namna ile ile kwa muda wa dakika tano nikitegemea yule
babu anaweza kurejea. Lakini dakika tano nyingine zilipita yule babu hakutokea,
nikajiongeza dakika tano nyingine za ziada ili kujilidhisha kuwa yule mtu hawezi
kurejea, zilipita tano nyingine lakini hakurejea.
Nilisimama kwa ungalifu nikavaaa raba zangu, kisha nikauendea mlango, wakati
huo ilikuwa yapata saa kumi na nusu ya tarehe 29/3/1989, na majira hayo
muadhini alikuwa akiadhini kule katika jumba la ibada.
35
Nilitoka nje ya chumba kile na kunyata taratibu, nilitembea upesi upesi katika ile
korido eneo lote bado lilikuwa kimya kabisa, niliongeza mwendo nikawa natembea
kwa kasi kubwa, hatimaye nikawa nakimbia.
Nilipopiga hatua kadhaa nikiwa mbali kidogo kutokea katika kile chumba, nikaona
korido ndogo ambapo pembeni yake kulikuwa na lifti, nikaona hiyo inaweza kuwa
njia nzuri ya kunitoa upesi katika lile jengo.
Mara ghafla nikasikia ile sauti ya ajabu, lakini safari hii sikukubali kabisa
kuendelea kubaki mule katika lile jengo, niliziba masikio nikatimua mbio.
Nilikimbia kuelekea eneo lile, upesi nikajotoma ndani ya lifti moja katika tatu
zilizokuwa pale, kisha nikairuhusu inishushe chini, sekunde kumi tayari mlango
wa ile lift ulifunguka na nilikuwa chini kabisa ya ghorofa lile..ile sauti ilikuwa
ikipotea kwa mbali kabisa.
Bila kuzubaa nikakimbia kuufuta mlango wa kunitoa nje, kama masihara
nikajikuta nipo nje ya jengo lile.
Kwa kweli ilikuwa ni furaha kwangu, nilijiona ni kama mfungwa niliyekuwa na
kufungo kikubwa gerezani na sasa nimekuwa huru.
 
SURA YA TANO

PAMOJA na kwamba nilikuwa ni mtu mwenye furaha ya kuwa nje ya jengo lile
lakini nilijikuta nikisimama na kuduwaa hatua chache mbele ya jengo lile katika
mtaa wa Aggrey, Kariakoo kutokana na kile nilichokiona mbele yangu.
Nilikutana na mji mgeni mpya tena mpya kabisa mbele ya macho yangu, mji
uliokuwa umejengwa ukajengeka maghorofa mengi, mazuri tena marefu kwenda
juu.
“Nipo wapi hapa” sauti moja iliniuliza mawazoni mwangu, japo mtaa ulikuwa ni
ule ule nilioufahamu miaka yote tena palikuwa ni Dar es Salaam ninayoijua kabisa.
Lakini asubuhi hii jiji hili lilikuwa tofauti kabisa, nilizipiga hatua kuelekea Mnazi
Mmoja nikizidi kushangaa mandhari mazuri ya jiji la Dar es Salaam.
“Kitu gani kinatokea katika maisha yangu huku nipo katika dunia gani tena?”
nilijiuliza mwenyewe bila kuwa na majibu.
Wakati naelekea Mnazi Mmoja tayari ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja
alfajiri katika Dar es Salaam hii mpya majira yale kulikuwa na watu wengi mno
mida hiyo tofuati na Dar es Salaam niliyokuwa ninaijua mimi. Watu hawa
walionekana wako ‘bize’ kila mtu alikuwa ni mwenye kujali mambo yake.
Nilifika Mnazi Mmoja na kuelekea katika kituo cha basi, bado niliendelea
kupagawa na namna mandhari yalivyobadilika ghafla kiasi kile.
Lakini pamoja na kuwa mji huu mpya machoni mwangu kuwa na majengo mapya
yenye kuvutia bado kuna baadhi ya majengo niliona yako vilevile mathalani jengo
la Ushirika pale Mnazi Mmoja, jengo la Chama cha Mapinduzi, pamoja na nyumba
za Taifa (NHC) ambazo nyingi zilikuwa zikikaliwa Wahindi.
Hali ilinisukuma kuuliza tofauti ile ninayoiona mbele ya macho yangu kama na
wezangu pia wanaona kama nionavyo mimi, ama ni maono yangu tu, kwani
kusema ukweli toka hapo sikuwa najiamini hata kidogo, niliamini kwa vyovyote
vile wale wachawi niliokutana nao katika lile jengo kuna namna watakuwa
wamenifanya katika ufahamu wangu wa akili.
“Kaka samahani”
“Bila samahani dada yangu”
37
“Hivi mbona naona leo mji umebadilika mno tofauti na siku nyingine za nyuma
nini kimefanyika usiku wa leo?” niliuliza mkaka aliyekuwa anangojea usafiri
kituoni.
“Labda sijalielewa swali lako dada yangu, mji umebadilika kivipi yaani uonavyo
wewe?”
“Kwani wewe huoni huu utitiri wa haya maghorofa?, huoni namna barabara
zilivyo za kuvutia? Huoni kama leo watu ni wengi tofauti na siku
zingine?..Huoni?” nilisema kwa kulalama kidogo, nikionyesha sura ya kumaanisha
kile nilicho kuwa nakizungumza.
Yule mtu alinitizama kwa kina kidogo kichwani mwake akahisi anazungumza na
mlevi wa pombe aina ya mataputapu.
“Ndivyo kulivyo kila siku” alinipa jibu moja kisha hakushughulika tena na mimi,
nilimwona katika uso wake akinisoma mimi kama mlevi wa mataputapu.
Upesi sauti moja ikanambia inawezekana ulikaa mule ndani kwa masiku mengi
mno ndio maana kumekuwa na mabadiliko makubwa katika mji huu, lakini bado
sauti nyingine ikaniambia hata kama nitakuwa nimekaa mule ndani kwa masiku
kadhaa mji huu hauwezi kuwa umebadilika kwa kiwango hiki., mabadiliko yale
hayakuwa ya miezi sita ukiachilia mbali hata kwa mwaka mmoja tu ingehitaji
miaka zaidi ya ishirini ndio kuwe vile.
Lakini sauti moja ikanijia ambayo niliona kidogo imenipa wazo la kujua utata ule,
sauti ilinambia, angalia saa na tarehe ya leo, upesi niliangalia tarehe katika saa
yangu ya mkononi.
Sikuamini kile ambacho macho yangu yaliona,. “MWAKAA elfu mbili na kumi na
sita..!.” Nilijikuta nibwata kwa nguvu huku nikibaki nimeduwaa.

Hapakuwa na mtu aliyenijali pale kituo cha basi cha Mnazi Mmoja, nilihisi huenda
saa yangu ilikuwa mbovu, kwani kabla ya kuitizama muda ule nilikwoshaitizama
wakati nipo ndani ya jengo lile na ikanionyesha ilikuwa ni tarehe 29/3/1989, sasa
vipi huku nje inionyeshe ni mwaka mwingine wa mbele kabisa, ambao sikuwahi
kufikiria kama uhai wangu unaweza kufika huko.
Mambo mawili yakawa katika ubongo wangu, jambo la kwanza inawezekana ile
saa yangu niliyo kuwa nimeivaa mkononi ikawa ni mbovu, na jambo la pili
inawezekana saa ile isiwe mbovu ila tu nikawa nipo katika ulimwengu mwingine
kabisa wa kichawi.
38
Lakini bado wazo hilo nililipinga kabisa kwani pale nilikuwa katika mji
ninaoufahamu sana, mji wa Dar es Salaam, japo ulikuwa umebadilika mno.
“Samahani kaka yangu eti leo ni siku gani? Tarehe ngapi? na mwaka upi?”
niliuliza mshangao mkubwa ukiwa usoni mwangu, nilishaanza kuhisi kuna bomu
linaninyemelea katika maisha yangu.
Yule mtu ambaye hakuwa anavutiwa na maswali yangu, alionekana kukereka kwa
maswali yangu ambayo yalionekana ni ya kipuuzi kwake.
“Nakujibu, lakini hili ni jibu langu la mwisho sintokujibu tena maswali yako ya
ajabu.” Alisema yule jamaa.
“Leo ni Jumatatu ya tarehe nne mwaka 2016.”
“Nini!. Siamini macho yangu.”
“Shauri yako..Ni macho yako mwenyewe. Ukiyaamini sawa, usipoyaamini sawa,
sitaki usumbufu zaidi.”
Alisema yule jamaa na kuingia katika basi lililokwishawasili pale stendi.
Kwa mara nyingine nilijikuta nipo katika taharuki siyo na kifani, niliwauliza watu
wengine kama watatu kuhusu tarehe ya siku hiyo. Kila mtu alinihakikishia kuwa
ilikuwa ni mwaka wa elfu mbili na kumi na sita (2016) ya tarehe nne siku ya
Jumatatu.
“Nimekuja kwenye dunia gani hii sasa mimi” niliongea peke yangu, kila mtu
aliyekuwa pale stendi aliniona kama mwehu, wakati mimi naishangaa hii dunia
mpya na watu wao ambao walionekana ni watu walioendelea mno kuanzia mavazi
yao hata mwonekano wao, lakini pia na wao pia walikuwa wakinishangaa mimi na
kuona ni binadamu niliyetokea sayari ya mbali mno na kuangukia katika dunia
yao.
Wakati huo ilikuwa ni saa moja, watu walizidi kuwa wengi katika hili jiji jipya la
Dar es Salaam asubuhi hiyo.
Niliangalia katika lile jaketi langu na kuiona ile kadi yangu ya TTCL sasa nikaona
njia nzuri ni kuwasiliana na ndugu zangu kwanza akiwa ni pamoja na mchumba
wangu Thabit nikiamini angalau kutoka kwao nitaweza kupata suluhu ya matatizo
yaliyokuwa yananikabili.
39
Sasa kazi ikawa ni kutafuta kibanda cha TTCL, kwa kweli nilizunguka sana pale
Mnazi Mmoja kutafuta kibanda cha TTCL lakini niliambulia patupu.. ilikuwa ni
jambo jingine lilionistajabisha awali kabla sijakumbwa na mazingaombwe yale
vibanda vya kampuni ya simu ya TTCL pale Mnazi Mmoja vilikuwa vimetapakaa
tele kama uyoga ajabu ni kuwa mwaka huu nilio ambiwa ni elfu mbili na kumi na
sita hapakuwa na kibanda hata kimoja.
Japo sikuwa nataka kuuliza jambo lolote kwa mtu yeyote kutokana na kuonekana
taahira, lakini ilinibidi niulize.
“Vibanda vya kupiga simu vimehamishiwa wapi” Nilimuuliza fundi viatu
aliyekuwa akifungua ofisi yake majira yale.
“Vibanda gani?”
“Vya TTCL”
“Mmh!. sijawahi kuviona hivyo vibanda maeneo haya” alijibu yule jamaa.
Sasa nikaona nisizidi kuwapa watu faida ya kuonekana hamnazo kutokana na
maswali yangu.
Nilirejea stendi na kupanda basi lililokuwa likieleka Buguruni., nikaona ni vizuri
nifike nyumbani kwangu kwanza nioge, kisha nile chakula kwani toka chakula
nilichokula kule Dodoma na wenzangu akina Loveness na bwana Magembe
Matiku sikuwa nimekula chochote hadi asubuhi hii, niliona hilo ni jambo zuri
kulitekeleza kabla ya kuendelea kutafuta ufumbuzi wa maswahibu niliyo kuwa
nayo.
Kwani hadi wakati huo ilibidi niamini kuwa huenda mimi pengine ndio
nimekumbwa na jinamizi kichwani mwangu linalo nifanya nijione nipo katika
karne ya 21 mwaka elfu mbili.
Hata basi lile la mjini lilikuwa ni basi la kisasa sana katika Dar es Salaam hii mpya
ukilinginisha na yele yetu.
Nikiwa nimezama katika bahari ya mawazo nilistushwa na sauti ya konda
aliyekuwa akidai nauli yake, niliingiza mkono katika lile jaketii langu na kutoa
shilingi tano na kumpa konda.
“Hii nini unanipa?” Konda aliniuliza kwa ghadhabu.
“Si nauli ama unadai nini?”
40
Hiyo ndio nauli? Kitu gani hicho unanipa wewe sista?” alijibu yule konda kwa
ukali huku akiwa amenitolea macho yake mekundu.
Hata abiria aliyekuwa pembeni yangu pia alinishangaa, “hizo pesa za zamani sana
anti hakuna anetumia tena pesa hizo we uko dunia gani” abiria wa pembeni
alisema.
“Oyaa lipa nauli we sista kama huna shuka chini,.. asubuhi hii.. tusianze kutiliana
nuksi taimu hizi” alisema tena yule konda kwa ukali. Niliendelea kustajabu
mazingaombwe yale yaliyokuwa yananitokea katika maisha yangu.
Niseme tu, pengine hiki ninachokieleza hapa wengi wenu mtafikiri ni hadithi za
kubuni, lakini napenda nikwambie ndugu yangu unaesoma maandishi haya,
kwanza napenda uelewe kuwa uchawi upo kwani hata vitabu vyote vitakatifu
vimeeleza juu ya uwepo wa uchawi, hivyo katika haya nikuelezayo hakuna neno
hata moja nililoongezea chumvi katika hayo ambayo nimekwishayaelezea, na
nitakayoyaeleza yote yaliyo nitokea mimi Zahara katika maisha yangu.
Kila kitu ni ukweli mtupu, na nimeona sina namna ya kuelezea haya katika jamii
na jamii ikanielewa tofauti na kutumia njia hii ya maandishi.
“Lipa pesa wewe sista” alinistua yule konda.
“Sasa kama ndio hivyo mie sina pesa” nilisema kwa upole.
“Suka eeh, zuia hapo mtu ashukie maana nishaona naletewa za kuleta hapa”
alisema yule konda akimtaka dereva asimamishe gari kisha nishushwe.
Lakini yule abiria aliyekuwa kiti cha pembeni alitoa noti mpya mchoni mwangu,
noti ya shilingi elfu moja na kulipia nauli za watu wawili, zogo la mimi na konda
likaisha.
Niliendelea kushangaa namna pesa ilivyokuwa haina thamani, kwenye hii dunia
mpya . noti ya shilingi mia tano ni nauli ya mjini!. Pesa hiyo ilikuwa ndio posho
yangu ya katikakati ya mwezi katika dunia yangu niliyotoka.
Lakini sikujali sana kwani kadri nilivyo endelea kuwa na jamii ndivyo nilivyozidi
kuonekana mtu wa zamani, hali ambayo nilianza kuchukia.
Ilinichukua dakika ishirini na ushee kufika Buguruni Malapa, napo huko kwa kiasi
kikubwa mandhari yalikuwa yamebadilika mno, nyumba zilikuwa zimerundikana
kila mahali mithili ya siafu.
41
Taratibu nilianza kutembea kuelekea nyumbani kwangu, nilikuwa nikitembea
lakini nikiamini muda wowote lolote linaweza kutokea mbele yangu na kuibua
taharuki nyingine moyoni mwangu.

*****
Mbele ya macho yangu, nilishuhudia jumba bovu lililokuwa limegemea upande
mmoja, uchakavu wa jumba hilo ukiwa wa kiwango kikubwa, kulikuwa na
nyumba nyingi mtaa ule ambazo zilijengwa bila mpangilio mzuri wa kiramani.
Mtaa ule ulikuwa na nyumba nyingi ambazo sio nyumba bora, takataka zikiwa
zimetapakaa eneo lote, kulikuwa na pitapita za watu wengi, kelele nyingi kila
mahala.
Ni uswahilini.
Maeneo yaliyokaliwa na watu wa kipato duni.
Macho yangu yaliendelea kuganda katika lile jumba bovu ambalo pengine ndio
lilikuwa jumba baya na bovu katika nyumba zote zilizo kuwa mtaa ule.
Nyumba hii ndio ile nyumba iliyokuwa nyumba nzuri mtaa wote siku moja kabla
ya siku hii, lakini leo ndio ilikuwa nyumba mbovu kuliko zote.
Nilipiga hatua kusogea katika nyumba ile. Kulikuwa na watoto waliokuwa
wakicheza pembeni ya nyumba ile hatua chache palikuwa na bibi aliyekuwa
amejilaza katika mkeka, niliendelea kusogea pale kwa yule bibi.
Moyo wangu ulikuwa ukipiga mkumbo nikiwa nimekata tamaa kwa kiwango cha
mwisho,
“Shikamoo bibi..mama” nilimwamkia yule mwanamke mzee, baada ya kumfikia,
hakuwa mzee sana kama nilivyomuona kwa mbali, alikuwa katikati ya umama wa
makamo na uzee.
“Marahaba mjukuu wangu hujambo” aliitikia, nilimwangalia vizuri yule bibi
mama na kugundua jambo lililozidi kuustua moyo wangu, yule alikuwa ni mama
mwenye nyumba wangu (mama Leila) ambaye jana kabla ya siku hii ndiye aliye
nipatia namba ya mtu aliyekuwa ameokota vifaa vya ofisini kwangu vilivyokuwa
katika jaketi langu, mtu aliyeniingiza katika maisha ya mazingaombwe.
42
Jana kabla ya leo alikuwa ni mwanamke wa miaka kati ya thelathini na thelathini
na tano hivi, lakini siku hii ambayo kwangu ilikuwa ni siku ya pili tangu niachane
nae, tayari alikuwa ni bibi wa miaka kama sitini ama sitini na tano.
“Mama Leila kitu gani kinatokea katika maisha mbona sielewi, jana tu tumeachana
ukiwa kijana, leo nakuona umekuwa mzee, nini kinatokea mama, eeh..kwanini
mambo haya yanakuwa hivi,” niliuliza huku machozi yakinitoka, nguvu nazo
nikihisi zinakwisha mwilini mwangu.
Yule bibi alitayahari kwa yale maneno yangu, akakaa vizuri pale mkekani kisha
akanitizama usoni vizuri.
“Wewe ni nani..Za…Za..Zahara” alisema huku akinitizama kwa mshangao
mkubwa.
“Ndio ni mimi mama Leila nimekumbwa na mambo makubwa mama..kila kitu
katika maisha yangu kimeharibika..”
“Ni wewe Zahara ama mwanawe na Zahara!!..”
Yule bibi au mama Leila alizidi kuniuliza kwa mshangao…kisha akaendea
kunisaili kwa maswali.
“Wewe ni Zahara huyu aliyekuwaga’ mpangaji wangu?”
“Ndio mama Leila ni mimi haswaa niliyeondoka jana baada ya kunipa namba ya
yule baba aliyechukua Jaketi langu lililokuwa na vitu muhimu vya ofisini.
“Hata sio wewe,..japo ulichokisema kuna ukweli kidogo lakini sio wewe..labda
useme wewe ni mtoto wa Zahara nitakukubalia..ila sio Zahara huyu niliyekuwa
namjua mimi..halafu hilo unalolisema halikuwa jana” alisema yule bibi,
akionyesha wasiwasi na mimi.
Sauti moja mawazoni mwangu ikanambia, kama nisipokuwa jasiri na imara katika
kueleza ukweli juu ya mambo yaliyonikuta kuna uwezekano wa kuonekana ni mtu
majinuni.
“Mama najua kuna vitu visivyo vya kawaida vimetokea katika maisha yangu,
lakini nahitaji uwe makini kunisikiliza kile nitakachokueleza kisha nione nitapata
vipi msaada dhidi ya maswahibu yangu, kwanza uwe na utayari wa kunisikiliza”
Nilisema nikimkazia macho yaliyoonyesha kuwa sikuwa na mzaha na kile
kilichokuwa kinatoka mdomoni mwangu.
43
“Hebu ngoja… kwanza twende taratibu wewe mwana,.”Alisema yule bibi
akionekana kutoafikiana na mimi moja kwa moja
“Unasema wewe ni Zahara mpangaji wangu?”
“Ndio”
“Ulikuwa wapi miaka yote hiyo?.. Na kwanini umri wako unaonekana upo
vilevile? Kama kweli wewe ni Zahara huyu nimjue mie. Maaana ni miaka mingi
mno imepita kama angekuwa ni Zahara basi pengine sasa hivi ungekuwa mama wa
miaka hamsini lakini.. Zahara wewe unaonekana bado mbichi kabisa binti wa
miaka ishirini na nne tu”
Alisema yule bibi maneno yaliyo niingia kabisa ndani ya mtima wangu, na kwa
kweli niseme tu sasa nafsi yangu iliukubali ukweli kuwa katika maisha yangu
uchawi wa ajabu uliusika kusimamisha umri wangu kwa kujiona nimeishi ndani ya
nyumba kwa siku moja tu, kumbe nimeishi zadi ya miaka takribani thelathini.
Nilifikiri kwa muda kidogo, kisha nikasema , “kama utakuwa tayari kunipa muda
wako nieleze jambo, labda maswali yako na mashaka yako yote dhidi yangu
yatajibiwa katika maelezo nitakayo yatoa kwako.”
Mama Leila aitikisa kichwa kuonyesha ishara ya kukubaliana na ombi nililoomba,
nilianza kumsimulia kila kitu kilichotokea, nilimweleza toka mwanzo tukiwa
safarini tukitokea kule katika mji wa Geita, nilivyomwona yule baba ambaye hadi
wakati huo sikuwa nalijiua jina lake, kusahaulika kwa jaketi langu, kurejea tena
Dodoma na kulikosa kisha kurudi Dar es Salaam na yeye kunipa taarifa za uwepo
wa mtu huyo aliyekuwa akinitafuta na kisha kuingia katika maswahibu mkubwa.
Hadi namaliza kueleza mama Leila alionekana kustaajabishwa na mkasa huo wa
ajabu kabisa, pamoja na kwamba alionekana kunielewa vema lakini bado
alionekana kuwa na maswali lukuki ambayo hakujua ni kwa namna gani
ayapangilie katika kuuliza.
“Kwahiyo wewe unavyoona mwaka ule ulivyondoka hapa kumfuata huyo mtu
ilikuwa ni jana usiku?” aliniuliza mama Leila akiwa amechanganyikiwa kama tu
ambavyo mimi nilivyokuwa katika mkanganyiko wa kifikra siku ile nilivyotoka
nje ya jengo lile kwa mara ya kwanza na kuona mabadiliko makubwa ya mandhari
yaliyotokea mbele yangu kwa masaa machache niliyokuwa mule ndani.
44
“Ndio mama ilikuwa ilikuwa ni jana usiku, tena usiku wa saa sita ama saba kama
sikosei. Yaani kwa namna nyingine naweza nikasema ilikuwa ni usiku wa kuamkia
leo ama ni leo”
Nilisema, na hapo mama Leila akazidi ‘kupalanganyika’ kwa mambo yale
akatikisa kichwa kutokubaliana kabisa na jambo lile.
“Mwanangu kwanza nikupe pole sana.” Alisema Mama leila, akisita kidogo kisha
akaendelea.
“Kwa kweli umenieleza tukio la ajabu ambalo sijawahi kulisikia katika maisha
yangu yote hapa ulimwenguni, nalazimika kukubaliana na wewe kwa namna moja
ama nyingine, lakini pia naweza nisikubaliane na wewe kwa upande mwingine
vilevile..”
Alisema mama Leila, sikuona tena haja ya kuendelea kumfanya yule mama
anielewe maneno yangu kwani kwa vyovyote vile ingemchukua muda mwingi
kunisadiki.
“Sasa mama,kuna vitu nataka kujua, kitu gani kiliendelea kipindi chote ambacho
ninyi mliona ni mimi sipo nyumbani kwa kipindi kirefu.” Nilisema.
“Aagh..sasa huko unako elekea ni mapema sana, kwanza nataka nijilidhishe na
maelezo yako Zahara” alinidakiza, akiwa ni mwenye kutaka kuelewa mambo
mengi dhidi ya yaliyo nisibu.
“Sawa mama uliza tu” nilimjibu.
“Kwanini unafikiri huyo mtu alikupeleka wewe katika hilo jumba la kichwawi na
si mtu mwingine.?”
“Kwa kweli hadi sasa hivi mama Leila hilo swali bado kwangu ni kitendawili”
“Na umesema ulibakwa?” nilijibu kwa kutikisa kichwa huku taswira ya tukio lile
kuingiliwa kimwili na yule baba ikijidhihilisha tena mbele yangu.
“Pole sana”
“Asante”
“Iliwezekanaje uingiliwe kimwili, muda huo huo upate mimba tena mimba kubwa
na muda mchache ujifungue?”
45
“Hilo pia sijui, nisime tu hata mie pia sijui mambo haya yaliwezekanaje kutokea,
na labda tu nikwambie siku ile hata mimi nilishangaa kama wewe unavyo shangaa
sasa” nilijibu, mama Leila alifikiri kwa muda kisha akaniuliza tena.
“Kwani mwanangu uliwahi kuwa na ubaya na mtu katika maisha yako mama?”
“Kivipi mama Leila?”
“Aagh..unajua Zahara katika hii dunia kuna watu wana visasi vya ajabu usije kuwa
uliwahi kukwaruzana na mtu akamua kukufanyia ushenzi huo”
Nilifikiria kidogo maneno yale lakini hata hivyo sikuwahi kuwa na ugomvi na mtu
yeyote katika siku za ukubwa wangu.
“Hata sijawahi kuwa na ugomvi na mtu”
Tuliendelea kuongea mengi na mama Leila hadi kiasi fulani akawa anaamini
hadithi ile ya ajabu niliyompa.
Ilikuwa ni zamu yake kujibu maswali yangu yote niliyo muhoji, kusema ukweli
kila neno lililotoka kinywani mwake lilininyong’onyesha mno,
Alisema; “mwaka 1989 baada ya wewe kuwa umepotea katika mazingira ya
kutatanisha taarifa zako zilizagaa kila kona wakati huo, kulikuwa na uvumi
mwingi juu ya kupotea kwako ghafla kiasi kile,”
Aliendelea kusema;
“Ndugu zako hususani wazazi wako walitumia muda mwingi katika maisha yako
kukutafuta japo wapate hata mwili wako tu, lakini kadri siku zilivyoyoyoma
ndivyo jambo hilo la wewe kupotea lilivyozidi kupotea katika vichwa vya watu
wengi na kuhesabika kama ni miongoni mwa watu walio poteza maisha na mwili
wako kutooneka, kila mtu anajua kuwa wewe ‘ulishakufaga’ siku nyingi tu.”
Mwazoni mwa mwaka 1999 nilipata taaarifa zisizo njema kwa kweli” Alisema na
kunikazia macho, moyo ulikuwa ukinienda kasi, nikaelewa kuna bomu linakuja
masikioni mwangu na kwenda kuupasua moyo wangu, akaendelea kusema.
“Taarifa zisizo njema, nilisikia wazee wako walifariki kwa kuangukiwa na
nyumba, kutokana na mvua kubwa za El Nino zilizokuwa zikinyesha miaka
hiyo..kibaya kuliko vyote. Alisema mama Leila. Akajiweka sawa pale alipokuwa
ameketi, halafu akanisogelea na kunishika bega kama ishara ya kunifariji kwa
taarifa ile aliyokuwa akinipa. Koo langu lilikuwa na donge zito, sikujua machozi
46
yalinitoka muda gani kwani nilistuka tu pale matone ya machozi yaliponichuruzika
na kupenya hadi katika kinywa kilichokuwa wazi kwa mshangao wa taarifa ile, ni
ile chumvi chumvi ya machozi ndio iliyonijulisha kuwa nilikuwa nikitiririkwa na
machozi kwa kasi.
“Kibaya kuliko vyote..” aliendela kusema mama Leila. “yule mdogo wako
uliyekuwa ukimsomesha alikuwa akiitwaje vile?”
“Nasri”
“Naaam.. Nasri.. nilipokea taarifa za kijana huyo kwa kweli hazikuwa taarifa
njema..yupo gerezani anatumikia kifungo cha miaka sitini jela.,inasemekana aliua
kwa bunduki..alifanya uhalifu wa kuvunja na kuua alikuwa jambazi, mwizi,
mtumia madawa ya kulevya na bangi” alisema mama Leila.
Kwa kweli nililia sana siku ile, dunia niliiona ni kubwa mno huku mimi nikijona
mdogo kama nukta..
“Inawezekanaje mtoto wa shule afanye hayo yote?” nililalamika mno, zaidi ya
yote nilimlaumu yule baba mchawi kwani ndiye mtu aliyebadilisha kabisa dira ya
maisha yangu.
 
SURA YA SITA

SIKU ile tuliongea mengi na mama Leila na niseme tu ilifikia hatua yule mama
alinielewa vema juu ya maswahibu yaliyokuwa yamenikuta, na niseme pia kwa
kiwango kikubwa nashukuru yule mama alionekana kunielewa kadri nilivyokuwa
nikiendelea kuzungumza nae..
“Vipi kuhusu Thabit?” atimae nilimuuliza mama Leila juu ya mchumba wangu
Thabit..
“Unamwongelea Thabit Twalib mjukuu wa marehemu mzee Mwaikimba?”
“Ndio”
“Kwa kweli yule kijana ni miaka mingi imepita sijamwona ila niliwahi kusikia
kuwa hivi sasa yupo huko Mwanza japo sina uhakika,”
“Wakati nimepotea yeye hakuwahi kujishughulisha kunitafuta?” niliuliza, japo
sikujua kwanini niliuliza swali lile.
“Hilo kwa kweli sijui, sikuwahi kumwona toka ulivyopotea” alisema mama Leila.
Tangu wakati huo sikuwa na uelekeo maalumu, sikuwa na mbele wala nyuma
katika hii dunia mpya, si Mashariki wala Magharibi, sikuona kama nina lolote
muhimu katika maisha.
Nilikuwa nikiishi nyumbani kwa mama Leila yapata wiki, pale katika ile nyumba
yenye kuegemae upande mmoja.
Nilikuwa ni msichana mgeni kabisa katika jamii ile mpya, hata wale watu
wachache waliokuwa wakinifahamu wengi wao hawakuwa tayari, kuamini kama
mimi ndiye yule Zahara waliyemfahamu toka miaka ile, wengi wao kama sio wote
waliamini kwa vyovyote vile mimi ni mtoto wa Zahara.
“Mtoto wa marehemu Zahara anafanana na mama yake vilevile” mtu mmoja wa
zamani alikuwa akiongea na mwenzake mtaani nilikokuwa nikikatiza.
“Huyo binti mwenyewe anaitwa Zahara na nasikia anadai yeye ndiye Zahara”
“Binti huyo anajitia umajinuni Zahara hawezi kuwa yeye, Zahara alikwishafariki
miaka mingi mno toka mwanzoni mwa mwaka themanini na tisa”
48
Yalikuwa ni maneno niliyowahi kubahatika kuyasikia, kila mtu alikuwa akisema
lake juu yangu kadri alivyo weza kunijua.
Nilikuwa ni msichana wa miaka ishirini na nne tu, nilikuwa ni mtu mshamba
katika mambo mengi mno, kila kitu katika maisha yangu kilikuwa kipya.
Sikuwa mimi tena yule mwandishi wa magazeti maalufu hapa nchini, gazeti
nililokuwa nikiandikia halikuwepo kabisa katika ulimwengu wa magazeti.
Nilikuwa ni binadamu mpweke, marafiki ndugu na jamaa wengi wao niliwapoteza
miaka mingi.
Nilikuwa nikimsaidia kazi za kuuza chakula mama Leila. Kila mara nyakati za
usiku tulikuwa tukibeba meza, majiko na vyombo kisha tunauza chakula gengeni.
Siku moja tulikawia kidogo kumaliza kuuza biashara, ilikuwa yapata kama saa
tano kasoro za usiku, siku hii biashara haikuwa nzuri sana. Hivyo kutokana na
muda kuwa umekwenda ilitubidi tufunge na kurejea nyumbani.
Kwakuwa usiku ulikuwa umekwisha kuwa mkubwa moja kwa moja tulifikia
kitandani na kulala.
Wakati nimekwishapitiwa na usingizi, kwa mbali nilikuwa nikisikia sauti ya mtoto
mchanga ikilia, ilinijia kama ndoto, lakini nikagundua haikuwa ndoto muda wote
ilikuwa ikitengeneza karaha kichwani mwangu, nikafumbua macho kivivu nikihisi
huenda alikuwa ni mtoto nyumba ya jirani aliyekumbwa na maswahibu ya
kutokulala usiku ule.
Lakini nilistuka nilipo gundua sauti ile haikuwa inatokea nyumba ya pili kwa
jirani, isipokuwa sauti ile ilikuwa inatokea chumba cha pili mulemule ndani.
Sasa vipi sauti hii ya mtoto itokee ndani ya nyumba ile wakati, ndani ya jumba lile
tulikuwa tukiishi wawili tu!. Niliwaza.
Sauti ile ilizidi kulia kwa kasi, nilipatwa na mashaka na woga mkubwa, nilianza
kumwamsha mama Leila aliyekuwa akikoroma.
“Mama Leila, we mama Leila” nilimwita huku nikimtikisa, ajabu ni kuwa mama
Leila alikuwa akiendelea kukoroma na kutoonesha dalili za kuamka.
Na nilivyokuwa nikizidi kumwamsha mama Leila kwa nguvu ndivyo sauti ya
mtoto ilivyozidisha kasi ya kulia.
49
Sasa nikawa natetemeka na jasho likinitoka kwani niliona dhahili mazingaombwe
mengine yanakaribia maisha yangu. Niliona hilo ni tukio jingine ambalo linakuja
katika maisha yangu na pengine ni tukio litakalobadilisha tena maisha yangu japo
sikujua safari hii maisha yangu yatakuwa katika hali gani.
Mara sauti ya kichanga ilinyamaza ghafla, halafu muda huo huo vikafuatia vicheko
vingi. Yaani ilikuwa ni kana kwamba wale watu walikuwa wakinicheka mimi
kutokana na namna nilivyokuwa na woga na wasiwasi uliotokana na kusikia sauti
ya yule mtoto akilia.
“Ninyi ni akina nani?” nilisema kwa sauti kali ya kushurutisha.
Vicheko vikanyamaza na kukawa kimya, yanii kimya cha ghafla kama vile
hakukuwa na vicheko.
“Ninyi ni akina nani..eeh?” nilirudia tena kuuliza kwa ukali baada ya kuwa kimya.
Kimya kingine..
Sikusikia chochote wala chakarachakara yoyote, nilitega sikio kwa makini
nikitegemea kusikia labda minong’ono ya wale watu lakini kulikuwa na ukimya
wa ajabu, ukimya ambao hata sisimizi angetambaa chini ungeweza kumsikia, hali
ya ukimya usiku ule ulikuwa ni eneo lote la mtaa ule wa Buguruni Malapa.
Niliogopa sana, kwa muda wa dakika sita hadi kumi, nilibaki nimekaa pale
kitandani nikitegemea kusikia chochote wakati wowote, lakini muda ulizidi
kwenda bila kusikia chochote.
“Inamaana hawa walozi wananiogopa ama?” niliwaza.
Wakati huo mama Leila alikuwa akiendelea kukoroma.
“Hii hali si ya kawaida vimbweka vyote hivi mtu anakoroma kama amekufa!”
Baada ya kukaa kitako kitandani kwa muda mrefu pasina kusikia kituko chochote,
niliamua kulala, wakati huo ilikuwa yapata saa saba na madakika za usiku.
Nilijilaza huku nikifikiria suluhu ya matatizo haya yaliyokuwa yananiandama
katika maisha.
Nikiwa pale kitandani usingizi ukiwa umegoma wasiwasi ukiwa mwingi mara
nikasikia kitu kingine, nilisikia sauti kama ya moto, tena moto mkubwa unao waka
kwa kasi, moto ule ulikuwa ukiwaka nyumba ya pili.
50
Nilikurupuka pale kitandani na kuwasha mshumaa, kisha nikasogea katika dilisha
na kufungua kisha nikatupa macho nje.
Sikuamini nilichokiona moto mkubwa ulikuwa ukiwaka katika nyumba ya jirani,
nyumba ile ilikuwa ikiungua kwa kasi kubwa.
Na mara nikasikia sauti nyingi kutokea nje “moto, moto, moto,moto” sauti za watu
wengi zilikuwa zikipiga kelele.
Ule moto ulikuwa ukiwaka kuelekea katika nyumba yetu, niliogopa mno, na hapo
nikarejea kitandani na kumwamsha mama Leila kwa nguvu zaidi, lakini mama
Leila hakuamka, alikuwa ni kama mtu aliyekunywa pombe nyingi mno na kuwa
hajiwezi. Nilichukua maji ya baridi na kumwagia ili amke na tutoke nje ya nyumba
ile ili kuokoa maisha yetu kwa kuungua na moto uliokuwa unawaka kwa kasi kuja
nyumbani kwetu.
Lakini wapi, mama Leila hakuamka.
Akili yangu ilifanya kazi upesi upesi, niliona ni vema nitoke nje nikaombe msaada
kwa watu waje kumtoa nje mama Leila hata kwa kumbeba ili kuokoa maisha yake
kutokana na moto uliokuwa ukiwaka kuja katika nyumba ile.
Nilifungua mlango na kutoka nje.
Lakini ile natoka tu nje, sikuamini macho yangu, ajabu ni kuwa hapakuwa na kitu
kile nilichokuwa nakiona wakati nimo mule ndani.
Hapakuwa na moto uliokuwa ukiwaka na kuchoma nyumba, na hata zile sauti
zilizo kuwa zikisema “moto, moto moto” HAZIKUWEPO TENA.
Pale nje palikuwa hakuna mtu hata mmoja kulikuwa kimya na eneo lile lilikuwa
shwari kabisa.
Nilihisi mwili ukinisisimka kwa kituko kile, nilijikuta nikiwa nimeduwaa huko
hofu kuu ikiwa kifuani mwangu, mate mepesi yalinijaa mdomoni na hapo
nikajikuta napiga kelele nyingi na kupiga hatua kubwa kurejea ndani.
Nilipoufikia mlango wa kuingia ndani nilipousukuma, haukufunguka, nikasukuma
tena kwa nguvu lakini ulikuwa mgumu, ulifungwa kwa ndani, haukufunguka.
Na wakati huo huo nikasikia vile vicheko vya awali vikitokea mule ndani.
Niliendelea kutishaka pasina kifani.
51
Sasa nikawa sielewi, aidha niingie ndani ambamo kuna viumbe visivyoonekana
ama nibaki pale nje.
Jibu rahisi likaja, ni kheri kubaki pale nje kuliko kuingia mule ndani ambamo kuna
viumbe wa ajabu tena wasioonekana, wenye kutia wasiwasi na mashaka, lakini
bado hofu yangu ilikuwa juu ya mama Leila aliyekuwa akikoroma mule ndani,
sikujua nini hatma ya uhai wake mule chumbani ndani ya lile jumba.
Nilisogea hatua kadhaa kutoka pale mlangoni vile vicheko kutokea mule ndani
nikawa navisikia kwa mbali na badae kidogo vikayeyuka.
Nikiwa pale nje nikawa nasogea katika ukuta wa jumba lile la mama Leila, nikawa
ukingoni kabisa mwa ukuta ule, nikajikunyata, umeme wa Tanesco uliokuwa
ukiwaka wasaa ule mara ukakatika, na kufanya kuwa na giza zito, giza jeusi,
nilizidi kuogopa lile giza kwa kweli sikujua nikimbile wapi, moyo wangu haukuwa
tayari kurejea mule ndani usiku ule.
Nikaendelea kujikunyata nyuma ya jumba lile katika ukuta, joto siku hii lilikuwa ni
kubwa usiku ule. Kwa wakazi wa Dar es Salaam wanaelewa hili.
Nikiwa pale ukutani, mbu walikuwa wakinishambulia vibaya mno.
Bado mashaka yangu yalikuwa makubwa dhidi ya mama Leila mule ndani japo
zile sauti sikuzikia tena kutokea ndani.
Kukawa na kiupepo kidogo, joto likapungua kiasi, kiupepo kile kikaongeza kasi ya
kuvuma, na joto nalo likawa linapungua, hata mbu pia wakapunguza kasi ya
kuniuma.
Ule upepo ulioanza kuvuma kama mzaha ukawa upepo mkubwa ukawa
unapeperusha takataka nyingi mtaani na kuzisukuma hovyo, mapaa ya nyumba za
uswahilini yalikuwa yakilalama kutokana na kuzongwa na upepo ule.
Mimi niliendelea kujikunyata katika ukuta wa lile jumba.
Machozi yalikuwa yakinitoka na kulia, nilia sana kwa uchungu, sikujua nilimkosea
nini Mungu katika maisha hata kukumbwa na mambo yale.
Kila kilichokuwa kinatokea katika maisha yangu kilibakia kuwa kitendawili
ambacho sikujua nani wa kunitegulia.
52
Nilijiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa katika maisha, siku zote niliamini Mungu
ndiye mtatuzi wa mitihani yote migumu kwa waja wake. Bahati mbaya kuliko zote
nilizowahi kuwa nazo katika maisha, sikuwa ni mtu mwenye kumcha Mungu.
Sikumbuki mara ya mwisho kumsujudia Muumba wangu ilikuwa mwaka gani, hili
halina maana kuwa sikuwa na dini ama kuamini katika uwezo wa Mungu lahasha.
Isipokuwa ni kule kujiweka mbali na Mwenyezi wangu, kwani pamoja na mambo
yote hayo bado sikuwa na misingi ama njia na taratibu sahihi ya kumuomba
Mungu wangu kama ambavyo alivyoamrisha katika vitabu vyake vitakatifu.
Mara ule upepo uliokuwa unavuma ulibadilika na kuwa kimbunga. Kimbunga
kilichokuwa kinavuma kwa kuzunguka, kilikuwa kikizunguka kuja katika uelekeo
nilikuwapo mimi.
Niliendelea kujikunyata, nikiwa naogopa mno hali ile, usiku ule ulikuwa ni usiku
mwingine wa kutisha na kuogopesha.
Kile kimbunga kilifika eneo lile nililokuwa nimejikunyata na kuvuma kwa kasi
mbele yangu.
Hata vile vitu vilivyokuwa vikizungushwa na kimbunga kile vilikuwa vikizunguka
kwa kasi kama pangaboi.
Hakikuwa kimbunga cha kawaida, hilo nililielewa, nikiwa nimejikunyata
niliangalia vizuri mbele ya kile kimbunga japo kulikuwa na giza lakini niliweza
kuona kiumbe kilichokuwa katikati ya kimbunga kile.
“Uwiiii, mamaaa ,uwiii” nilipiga kelele nyingi nikiwa nimetoa macho najiburuza
kwa makalio kurudi nyuma, mkono wangu nikiwa nimeiweka mbele kuzuia kile
kiumbe nilichokiona, huku mkono wangu mwingine nikiwa nimeziba mdomo,
macho yenye mshangao na hofu kubwa yamenitoka pomoni.
Kilikuwa ni kiumbe cha kutisha mno, alikuwa ni kama kichwa cha nyati, huku
umbo lake likiwa kama la ndege popo, alikuwa na rangi nyekundu umbo lake lote,
Macho yake yalikuwa makubwa kama bundi huku zile mboni za macho yake
zikiwa zina mg’ao wa rangi ya dhahabu.
Na kadri nilivyokuwa nikijiburula pale chini ndivyo kiumbe yule alivyokuwa
akipiga hatua ndogo kunisogolea akiwa katikati kimbunga kile, kwa hiyo hapo
unaweza kuwa umeelewa, yanii kadiri nilivyokuwa nikijongea nyuma ndivyo kile
kimbunga kilivyokuwa kikinisogelea taratibu.
53
Nikafika mwisho wa kona ya ukuta ule sasa nikawa sina eneo la kusogea, yule
kiumbe akazidi kunikaribia nilikuwa nikilia kama mtoto, nilijikojolea.
Niligundua kitu kingine kwa yule kiumbe, alikuwa na miguu kama ya binadamu
lakini katika kiganja cha mguu alikuwa na kwato kama za ng’ombe.
Mikono yake ilikuwa ya binadamu lakini yenye manyoya mengi na kiganja
kikubwa.
“Uwiiiii” nilipiga ukelele kubwa, akili yangu ilinambia kuwa jini alikuwa mbele
yangu.
Yule kiumbe aliniangalia kwa macho yake ya kuogopesha, mimi pia nikabaki
nikiwa nimekodoa macho mbele ya kiumbe yule na kuwa kama mtu aliyenata
katika rundo la ulimbo.
Mara nikasikia sauti fulani niliyo wahi kuisikia mahala fulani, ulikuwa ni wimbo
usio kuwa na maana ninayoweza kuielewa, na hata wakati ile sauti inaendelea
kupenya masikioni mwangu nikawa nahisi nazongwa na hali fulani ya kupoteza
fahamu.
Ni hapo nilipokumbuka kuwa sauti ile nilipata kisikia katika lile jumba la ajabu
kule mjini, Aggrey, Kariakoo.
Nikazidi kuelekea kuzama katika kina kirefu cha bahari ya usingizi.
Sikuwa tayari kwa hilo, nikakumbuka mbinu niliyoitumia kuepukana na ile sauti
ya ajabu.
Hapo nikasokomeza vidole masikioni mwangu, nikiziba masikio sauti ile isipenye
ndani ya kichwa changu.
Wakati napambana na tendo lile yule kiumbe alikuwa akinitizama huku sura lake
baya likiniangalia kwa hasira kubwa.
Sasa kukawa hakuna ninachokisikia zaidi ya kuona yale yalikuwa mbele yangu.
Upepo wa kimbunga uliendelea kuvuma kwa kasi na kadiri nilivyokuwa nikiziba
masikio yangu ndivyo upepo ulivyokuwa ukiongeza kasi ya kuvuma, na yule
kiumbe akitizima kwa jicho kali la hasira.
Lakini wakati vile vituko vinaendelea kutokea mara nilistuka nilipomwona mama
Leila akitokea nyuma ya nyumba ile.
54
“Wee Zahara” aliniita huku akinitizama kwa mshangao. Nilipomwona nilijiburuza
pale huku nikijiweka mbali na yule kiumbe kusogea mahala alipokuwa
amesimama mama Leila.
Wakati nafanya matukio hayo mama Leila alishikwa na mshangao mkubwa juu
yangu, alionekana ni mtu mwenye kutahayari huku maswali yakiwa mengi
kichwani mwake.
Hapo nikagundua jambo moja, ama mawaili, kwanza mama Leila hakuwa
anamwona yule kiumbe aliyekuwa mbele yangu, pamoja na kwamba kulikuwa na
kimbunga kilichokuwa kikizunguka kwa kasi hatua chache mbele yangu.
Lakini jambo la pili nilielewa kuwa mama Leila alikuwa na maswali mengi juu
yangu, vipi usiku ule mkubwa, usiku wa giza niwe nje kama mwanga, lakini vipi
niwe ni mtu mwenye mashaka woga na wasiwasi kama mtu aliye ona jini mbele
yake.
“We Zahara una nini? Mbona hivyo? na mbona huku sasa usiku huu?”.
Sikujibu lolote, isipokuwa nilijikuta nikipiga ukelele wa hofu na kusimama
kiwazimu kisha nikatoka mbio kuelekea pale alipokuwa mama Leila.
Kitendo kile, kilimwogopesha mama Leila yeye pia aligeuka na kukimbilia ndani,
alisukuma mlango wa ndani na kujichoma ndani hatua chache nyuma mimi pia
linijitoma ndani kwa kasi kisha tukashindilia komeo kwa ndani.
Tukawa tunahema kwa zamu huku mashaka makubwa yakiwa ndani yetu.
“Nini kimetokea?” mama Leila alihoji.
“Hata sijui, ila ni majini, humu ndani kuna majini na wachawi?”nilisema
kimajinuni.
Mama Leila hakunitizama ila alisikiliza kauli yangu kisha akatikisa kichwa
kunikatalia.
“Hayo majini humu ndani yameingia lini, miaka nenda rudi sijawahi kuona japo
unyoya sasa mimi sikuelewi kwa kweli Zahara”
“Mama Leila nimekuamsha mno ila hukuweza kabisa kuamka, vituko vilivyo
tokea humu ndani leo si vya kawaida” nilisema, japo uso wa mama Leila
alionekana kuanza kujutia uamuzi wa kuishi na mimi ndani ya nyumba yake, uso
55
wake ulizungumza zaidi ya kinywa chake.aliona kama mimi nimemletea mabalaa
nyumbani kwakwe.
Tulibaki kimya kila mtu akiwaza lake, huku ule mvumo wa upepo huko nje ukiwa
umepotea.
“Nimeona kimbunga kikivuma kwa kasi mbele yako nini maana yake? Na kwanini
muda huu ukawa nje?” mama Leila aliniuliza.
Nilimweleza kila kitu kilivyo kuwa usiku ule, tangu vile vituko ndani ya nyumba
kutokea chumba cha pili,moto kuwaka nyumba ya jirani na kisha kile kimbunga
cha ajabu.
Ilikuwa ni habari ya kutisha kwa mama Leila lakini bado ilikuwa ni kama hadithi
ya kufikirika kwa upande mwingine.
“Labda naweza kukuelewa kwa huo upepo kwakuwa nimeuona lakini nashndwa
kuelewa maelezo yako kuhusu hiki chumba cha pili ulicho sema kuna sauti ya
mtoto mchanga na vicheko, hii ni stoo na humo hakuna vitu vingi zaidi ya
makorokoro yasiyo na kazi..”
Nilinyamaza kwakuwa sikujua namna ya kuendela kueleza.
“Haya mambo ya kiswahili tuwapelekee waswahili mwanangu au unaonaje?”
alisema mama Leila baaada ya kifiri kwa muda wa nukta kadhaa.
“Sijaelewa mama”
“Ninamaana kuwa kesho kukicha twende kwa mtaalamu huko Bagamoyo.”
Niliifikiri rai hiyo, nikaona siyo wazo baya wala siyo wazo zuri.
Baya lisilokuwa na madhara ni jema lisilo na faida, niliamini hivyo, nikalala
kuisubiri kesho.
 
SURA YA SABA

SIKU iliyofuatia alikuwa mama Leila aliyeanza kuamka.
“Zahara” aliniamsha.
“Abee mama” niliitika usingizi ukiwa bado machoni mwangu.
“Sasa mie itabidi nizungukie madeni yangu, ili tupate senti kidogo tutakayoiacha
huko kwa mtalamu tuendako, maana humu ndani senti iliyopo haitoshi.”
Alisema mama Leila kisha akaondoka. mie nilibaki pale nyumbani nikifanya usafi
wa nyumba na mwili wangu mwenyewe. Si unajua mwanamke mazingira, Saa
saba juu ya arama mama Leila alirejea.
“Pesa imepatikana mwanangu lakini safari ya Bagamoyo itabidi iwe kesho maana
sasa hivi muda umekwenda mno na hili foleni la Dar es Salaam tunaweza kufika
huko saa tatu usiku.” Alisema huku akiangalia saa ya kwenye simu yake na muda
ulionyesha ilikuwa ni saa saba mchana.
“Mie sina neno mama Leila, chochote usemacho ni sawa tu”. Nilisema, na
hatimaye tukakubaliana kesho ndio iwe siku ya safari.
Siku hiyo hatukwenda kuuza chakula usiku gengeni kwani hatukuwa
tumetayarisha chochote.
Nilitumia muda mwingi kuwaza maisha yangu, mambo mengi yaliyopita katika
kichwa changu yaliniumiza mno.
Uhai wangu ulikuwa nusu duniani nusu kuzimu,.niliishi maisha ya dhiki japo
kitaaluma nilikuwa mwandishi wa habari.
Usiku ulipoingia muda wote nilikuwa nikifikiria safari ya kwa mganga huko
Bagamoyo, bado sikuwa na uhakika kama kuna binadamu anaeweza kuwa na
uwezo wa kuzuia viumbe vilivyokuwa vimezingira maisha yangu.
Ulikuwa ni usiku mwingine nikiutafuta usiingizi, huku tumaini langu likiishia
mikononi mwa mganga tutakae kwenda kumwona kesho huko wilayani Bagamoyo
mkoa wa Pwani.

57
*****
Asubuhi ya siku iliyofuatia, tuliamka mapema na kupata staftahi ya chai na
maandazi kisha tukajiweka vema na safari ya kuelekea Bagamoyo ikaanza.
Tulipanda basi hadi Makumbusho kituo kipya cha mabasi ya mjini awali ikiwa
pale Mwenge, hapo tukachukua gari jingine na sasa tukaanza safari ya kuelekea
Bagamoyo kwa mganga wa kienyeji.
Siku hii ya Jumapili hakukuwa na foleni kubwa kwa muda wa nusu saa tulikuwa
tumekwisha pita Tegeta na sasa tulikuwa tukiitafuta Bunju.
Mita kama hamsini mtu mmoja aliyekuwa na gari lake dogo, akionekana kama ni
mtu aliyeharibikiwa na usafiri wake, alilipiga mkono basi letu dogo aina ya Costa.
Mvulana yule aliingia ndani ya basi kisha safari ya kuelekea Bagamoyo
ikaendelea.
Tulipofika kituo kimoja mbele abiria aliyekuwa ameketi siti moja na mimi
aliteremka, na yule kaka aliyepanda basi akiwa ameharibikiwa na usafiri wake
njiani aliketi katika siti.
“Habari yako anti?” alinisalimia. Hata sauti yake ilipotoka kinywani mwake tumbo
langu lilipuka na moyo wangu ukapata mstuko, nikajaribu kuikumbuka ile sauti
niliwahi kuisikia mahala gani.
“Mambo vipi anti?” yule mtu alinisalimia tena
Nilikuwa kama mtu aliyepigwa nusu kaputi,nikabaki nimemkaodolea macho yule
mtu.
“Wewe ni Thabit Talib?”
“Nani…mimi?”
“Ndio”
“Hapana..ila mzee Thabit Talib ni baba yangu mzazi.
Umemjua vipi baba yangu”
Yule kijana alisema, Tumbo lilipata joto nikawa nahema kwa kasi, lakini wakati
nafikiria maneno ya yule kijana tulikuwa tumefika katika kituo cha kijiji cha
Msata, Bagamoyo, na hapo ndio ilikuwa kituo anachoshukia yule kijana.
58
“Any way, tumejuana juu juu, lakini labda siku moja tutafahamiana zaidi, shika
hii” alisema huku akitoa kadi yake ya biashara iliyokuwa na mawasiliano yake na
kunipatia, kisha yeye akateremka katika gari.
Nilibaki katika gari nikitafakari lile tukio na kuona ni kama mkanda wa sinema
unaopita katika maisha yangu.
Tuliendelea na safri na mwendo wa kilometa kadhaa tukawa katika mji wa
Bagamoyo.
Tulivyo shuka katika gari nilimweleza mama Leila juu ya kukutana na mtoto wa
Thabit mvulana aliyekuwa mchumba wangu wa zamani.
Mama leila pia alishangaa sana, lakini hatukuwa na namna ya zaidi ya kuacha
maisha yaende kama yalivyo.
Tulitembea mwendo kiasi sikumbuki ni eneo gani mama Leila alinipeleka pale
Bagamoyo lakini ninachokumbuka safari yetu ilishia katika kijumba kidogo cha
makuti kilichozingirwa na wigo mkubwa wa fensi ya mifenesi.
“Karibuni jamani karibuni..”
Tulikaribishwa na kijana wa miaka kati ya ishirini na nne ama tano, alikuwa
mchangamfu mdada mzuri na mrembo wa kuvutia lakini uzuri wake ulipotezwa na
matunzo duni aliyoyapata katika maisha yake.
“Asante ..asante sana” mama Leila aliitikia huku tukiketi katika mkeka mkubwa
uliokuwa chini ya mti wa mpogopogo.
“Haya mtalaamu tumemkuta?”
“Mmh, hapana kaenda musikitini ila ndio mida yake hii”
Alisema yule mdada chaurembo asiyekuwa na matunzo.
Tulikaa kumngoja mtalaamu na baaada ya kama ya nusu saa alirejea babu akiwa
katika kanzu nyeupe.
“Mwenyewe huyoo anakuja” alisema yule dada chaurembo, na wote tuligeuza
kichwa kumtizama.
Alikuwa ni mzee wa miaka kati ya sitini ama sabini, alijikongoja taratibu kuja
usawa wa pale mkekani tulipo kuwa tumeketi.
59
Alipo karibia mita kama kumi na mbili kutoka pale mkekani, mara alisimama
ghafla na akabaki ameduwaa huku macho ya uwaoga amenitumbulia, akawa
anatetemeka huku ngurumo fulani ya vitu kama maruhani ikawa inamtoka.
“Weweeee!” alisema kwa mshangao akinisonta na kidole.
Kila mtu aliyekuwepo pale alibaki na taharuki kuu, hata yule dada niliyempachika
jina la chaurembo aliogopa.
“Umebeba viumbe wabaya na hatari mnoo sogea mbali na eneo hili
upesi..tokaaa..nasema tokenii hapa!.”
Yule mganga alifoka akinitizama kwa hofu na mshangao akawa ananifukuza.
Niliendelea kushangaa kile kituko huku yule mganga akiendelea kunitaka nipotee
upesi eneo lile.
Hatukuwa na namna zaidi ya kuondoka haraka pale kwa mganga, lakini si mimi
wala mama Leila kila mtu alikuwa na hofu kubwa moyoni mwake.
Na hata nilivyokuwa nikimwangalia mama Leila nilimwona kabisa kuwa alikuwa
akiniogopa mno.
“Sasa nikwambie kitu Zahara” alisema Mama Leila akitoa noti mbili za shilingi
elfu kumi na kunikabidhi
“Niambie tu mama Leila”
“Naomba uniwie radhi sana kwa hili ninano kwenda kuliamua kwa sasa”
“Lipi hilo?”
“Kwa kweli siwezi kuishi na wewe zaidi, niwe tu mkweli ndugu yangu, kwa sasa
nakuogopa, kama mtaalamu ninaye mwamini ile kukuona tu kashindwa hata
kusikiliza tatizo letu kwa vitu ulivyo navyo mwilini mwako.
Vipi mimi niweze kubeba matatizo haya kiasi hicho, kwa kweli ndugu yangu
siwezi?”
“Sasa mama Leila kama wewe ukiamua pia kuniacha wapi pawe kimbilio langu,
kumbuka matatizo haya niliyonayo sijapenda mie kuyapata.
Lakini pia kumbuka kwa sasa sina sehemu yoyote ni nayo weza kusema
nitakwenda kuishi zaidi ya kwako mama Leila…tafadhali” nilisema kinyonge huku
kamasi na machozi vikinitoka kwa pamoja.
60
“Pole lakini sina wazo tofauti zaidi ya hilo nililokwishaamua, nafsi ya uhai wangu
ni muhimu kuliko kitu chochote Zahara.. nasikitika sana lakini sina jinsi”
Alisema mama Leila, kisha akasimamisha bodaboda na kumtaka dereva ampeleke
stendi ya mabasi ya Makumbusho.
Kwa muda wa dakika tano nilibaki nimebunga’aa pale barabarani nikiona maisha
yangu hayana thamani hata kidogo.
Mfululizo wa matukio ya ajabu yaliyokuwa yakinitokea katika maisha yangu
yakawa yanapita katika fikra zangu mithili ya mkanda wa filamu.
Nilifikiria kwa muda kisha nikaona sina namna zaidi ya kurejea Dar es Salaam ili
kuona kama nitaweza kumshawishi mama Leila ili aendelee kunipa hifadhi
nyumbani kwakwe nikiwa natafuta ufumbuzi wa maswahibu yangu.
Nilifika jioni Buguruni, na nilipofika nyumbani kwa mama Leila sikumkuta, zaidi
ni kuwa nilikuta begi dogo lililokuwa na nguo zangu chache likiwa limewekwa
pale mlangoni huku mlango ukiwa umefungwa kwa kufuri kubwa.
Hali hiyo ilimaanisha mama Leila hakuhitaji kabisa kuendelea kushi na mimi pale
nyumbani kwakwe.
Nilishusha pumzi ndefu huku nikijaribu kufikiria wapi pa kwenda jioni ile.
Nilibeba lile begi la nguo na kuondoka pale kwa mama Leila.
Kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi ilikuwa yapata saaa moja za jioni, giza
lilikuwa limekwishafunika nuru ya jiji la Dar es Salaam, nikawa nazipiga hatua
kuelekea mjini, japo sikujua uelekeo ule hatma yake itakuwa ni wapi ila
niliendelea kujisukuma kwa mbele vitendawili vingi katika maisha yangu vikiwa
vimezingira ufahamu wa akili zangu.
Kufumba na kufumbua nikajikuta nimefika mitaa ya Jangwani, hapo nikastuka na
akili yangu ikarudi kufikiria cha kufanya zaidi juu ya hatma ya maisha yangu kwa
usiku ule wa siku hiyo.
Nikawa mbele ya viwanja vya Jangwani, katika nyasi kavu nikaketi kitako huku
macho yangu yakielekea angani na kutizama nyota na mwezi huku nikiwa na wivu
dhidi ya nyota zile, nikaona bora ningekuwa nyota pengine ningekuwa na furaha
na maisha kuliko kuwa binadamu nisiye na mbele wala nyuma huku mitihani
mizito ikiwa imechukua nafasi kubwa katika maisha yangu.
61
Wakti nikiwa katika mawazo yale mara nikajikuta nazungukwa na wavulana kama
sita watatu kati yao wakiwa na panga na visu.
“Leta begi hilo” mmoja alisema akinisogelea na kukwapua lile begi langu la nguo.
Mara moja nikaelewa wale walikuwa ni wezi. Wakati sijajua nifanye nini
mwingine alinifikia na kunipokonya ile pesa niliyokuwa nimepewa na mama Leila.
Lakini nilipotaka kupiga kelele nilijikuta napigwa vibao vikali na kutakiwa kutulia
kama maji ya mtungini.
Walipoona wamemaliza kuninyang’anya kila kitu hawakuniacha hivi hivi.
Wakanipiga na kunitaka nivue nguo zangu zoote huku kila mmoja akionekana
kutaka kunibaka.
“Hapana kaka zangu msinifanyie hivyo ni dhambi kwa Mungu kunifanyia hivyoo”
“Unazijua dhambi wewe., hebu toa hicho kichupi chako upesi kabla
sijakucharanga na panga sasa hivi”
Jamaa alisema kwa ukali macho yake mekundu yaliyoathiriwa na bangi
yaliniogopesha sana.
Nilivua lakini siku tayari kuona nafanya mapenzi na vijana wale wahuni.
“Sasa mnaonaje kama mkifanya kwa hiyari yangu kuliko kuniingilia kwa nguvu?”
“Ni wewe tu utakavyoamua, ukipenda ukubali kwa hiyari yako na utukatie mauno
na ukipenda ukomae kama gogo ni wewe na roho yako sisi tunachotaka ni uroda
tu”
“Sasa naombeni msinikabe kwa nguvu mtafanya mapenzi na mimi kwa zamu hadi
hamu yenu iishe” nilisema kwa kwa sauti ya kubembeleza na huruma kidogo.
Hata nilipopata kusema hayo jamaa watatu katika wale sita wakaonekana kugutuka
kidogo kutokana na rai ile.
“Oyaa masela kama vipi tujikatae huyu demu inawezekana ana moto, vipi akubali
kirahisi hivi tena bila hofu kufanya mapenzi na sisi sote kwa zamu?”
Jamaa mmoja alisema akimaanisha inawezekana kuwa nikawa na Ukimwi hata
nikakubali kufanya nao mapenzi kwa zamu ili pengine na mimi niwaambukize huo
ukimwi.
“Eti wee una Ukimwi?”
62
“Kusema ule ukweli sitaki kuwaongepea kaka zangu,. Mimi kweli nina Ukimwi,
naishi na Ukimwi huu mwaka wa pili sasa”

Nilisema kwa kujiamini nikiona ile fikra ya yule jamaa hakika ndio njia pekee ya
kujinusuru na tatizo lile la kutaka kubakwa na wale wahuni.
Lakini baada ya kusema hilo nikidhani wale jamaaa wataniacha na kuondoka zao
lakini kilicho tokea huwezi kuamini mpenzi msomaji.
Nilikutana na kipigo cha haja kutoka kwa wale vijana wa kiume nilipigika hadi
nikahisi safari ya kuelekea kuzimu inaninyemelea.
“Fala wewe unataka kutuaa kwa ngoma kirahisi hivyo.”
Nilisukumiziwa teke la tumboni na kutoa mguno mkali hapo hapo jamaa mwingine
alinilapua konde la usoni na kunipasua mdomo huku damu zikawa zinanitoka
puani na mdomoni.
 
SURA YA NANE

TA, ta, ta, mshale wa saa ya ukutani ulikuwa ukitoa sauti ndogo katika chumba
kidogo lakini chenye mlundo wa fenicha za kisasa. Kulikuwa na ukimya hakuna
kilichosikika zaidi ya sauti ya mshale wa saa ya ukutani iliyokuwa ikilia ta, ta, ta.
Nilijinyanyua kivivu kutoka katika chumba kile kidogo kichwa kikiwa kinaniuma
vibaya mno. “niko wapi hapa” nilijuliza mwenyewe.
Lakini kabla kumbukumbu zangu hazijakaa sawa bin sawia mlango ulifunguliwa
kisha akaingia mwanamke aliyekuwa amevaa shati la kijivu lililochomekwa vizuri
ndani ya suruali ya rangi ya buluu iliyowiva aina ya ‘jeans’ iliyo mkaa vema na
kulidhihirisha umbo lake la kuvutia ambalo mara moja lilimletea mtu yeyote
aliyekuwa akimtizama yule mwanamke wakati ule hisia ya tarakimu ‘nane’
ukijichora kichwani mwake.
Sura yake mzuri ya kuvutia ulikuwa umejaa wahaka mkubwa baada ya kuniona
nimeketi kitandani.
“Vipi mrembo wajionaje”
“Safi tu”
“Pole sana ilikuwa wakuue wale mafedhuli. Kama sio kuwahi kuwatiamua wallah
sasa hivi ungekuwa mochwari” Alisema yule mrembo sasa sura yake ikawa na
mengi maswali dhidi yangu.
“Waitwaje?”
“Zahara”
“Kwanini usiku ule ulikuwa pale”
“Ni habari ndefu”
“Nieleze kwa kifupi?”
Ilinibidi niongope kuwa nilikuwa mgeni kutokea mkoani ambaye nilikuwa
nikifanya kazi za ndani lakini nikafukuzwa na mwajiri wangu baada ya kutokea
kutoelewana baina yetu Yule dada alikaa kimya kwa muda wa dakika tano kisha
akanigeukia na kusema;
“Kwa hiyo ungependa nikusaidieje”
64
“Nisaidie hifadhi, mahala pa kuishi dada yangu nikiwa natafuta kazi nyingine ya
kufanya”
“Kwanini usirudi kwenu?.. halafu kwenu ni wapi?”
“Kwetu ni Iringa ila hata hivyo sina nauli ya kurudi kwetu”
“Sawa nitakupatia hiyo pesa siku mbili hizi” alisema yule dada ambaye baadae
nilikuja kumfahamu kuwa alikuwa akiitwa anti Latifa. Nikiwa naishi pale kwa anti
Latifa siku mbili badae alinipatia pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini kama nauli ya
kunirejesha mkoani kwetu kama alivyoelewa yeye.
Alfajiri na mapema hiyo baada ya kuagana nae akidhani naelekea Ubungo,
nilipanda basi la Kigamboni na kuelekea Feri , huko niliamini nikifika Feri nitapata
kazi yeyote hata ya kuchuuza samaki kazi itakayoniwezesha kusukuma maisha
yangu yaliyokuwa hayana thamani kwa wakati huo.
Wakati nipo katika gari konda alivyoniomba nauli wakati natoa noti katika mfuko
wa gauni mara nikapata kuona kadi ya yule kijana mwenye kufanana na Abdallah
Twalib. Baada ya kumlipa konda pesa yake nikawa naipitia ile kadi ya yule kijana.
Jina katika ile kadi ilisomeka Mr. Uwesu Twalib Abdallah.
Kulikuwa na jina la kampuni yake na mawasiliano yake. Baada ya kushuka katika
lile basi la mjini nilielekea kibanda cha kuchaji simu na kununua vocha kisha
nikamwomba yule mtu kibandani simu yake kwa muda. Nilipiga namba moja
katika zile zilizo kuwapo katika ile kadi kisha kwa muda mfupi simu ilipokelewa.
“Haloo habari yako?” sauti ilitokea upande wa pili baada ya simu tu kupokelewa.
Alikuwa ni yule kijana niliyekutana nae katika basi la Bagamoyo, Uwesu
Abdallah.
“Ni njema ndugu”
“Nazungumza na nani na una shida gani?”
Kimya.
“Nazungumza na nani na una shida gani?” Alirudia teena kuuliza yule mtu.
Nilijikuta napata kigugumizi, sio kwamba nililokuwa nataka kusema lilikuwa zito..
lahaasha. Isipokuwa sikuwa na la kusema.. “hivi nimempigia ili nimwambie nini
sasa” Nilijiuliza huku nikijiona bwege,
“Nazungumza na nani na una shida gani?” Alinisutua tena.
65
Niliamua kukata simu, halafu nikabaki najishangaa. Swali kuu likiwa ni kwanini
nimempigia simu, nina shida nae ipi. Nilituliza akili yangu kwa muda kidogo
badae nikapata kulewa kitu, kwanini nilimpigia. Nilibonyeza kitufe cha upande wa
kulia chenye rangi ya kijani kisha nikaipiga tena ile namba. “Hivi wewe ni nani
unae nipigia simu halafu huongei?” alizungumza kwa ukali baada ya kupokea.
“Mimi Zahara”
“Zahara..! Zahara gani?” nilimkumbusha kuwa tulikutana katika basi la
Bagamoyo.
Alifurahi baada ya kunikumbuka na kuomba niende nikamtembelee huko Tabata
Kimanga alipokuwa akiiishi. Kwa kuwa niliona Uwesu anaweza kunisaidia kitu
fulani katika maisha nilimkubalia kwenda kumwona siku hiyo hiyo.
“Karibu sana bibie,” alinikaribisha ndani mwake, ndani ya sebule kubwa
lililosheheni thamani ghari.
“Asante habari za siku mbili tatu”
“Safi tu”
Alinikaribisha kinywaji cha baridi kisha tukaendelea na mazungumzo.
“Ulisema unafahamiana na mzee wangu mzee Talib Abdallah?”aliuliza. Nilifikiria
kwa muda nikaona jibu sahihi la kumpaa kijana yule ni hili; “ndio namfahamu
kwakuwa alikuwa mchumba wangu miaka ishirini iliyopita” Uwesu alikunja uso
baada ya kumpa jibu lile kisha akawa ananitizama kwa mtazamo wa kiudadisi,
jicho lake lilitaka kujua kama nakunywa pombe ama natumia madawa ya kulevya.
Nilielewa sentesi yangu ilimchanganya Uwesu ila nikaiacha iendelee kuingia
kichwani mwake.
“Nini unajaribu kuzungumza wewe?” Uwesu alisema tena akinikazia jicho kali.
“Baba yako alikuwa mchumba wangu wa zamani”
“Kwahiyo hilo ndio lililokuleta.. kuja kunieleleza kuwa ulishatembea na baba
yangu mzazi!” Alisema tena kwa ukali lakini kwa sauti ya chini.
“Hapana lililonileta hapa si kuja kuanika yale niliyowahi kuyafanya na baba yako
ila nimekuja kushea matatizo yangu na wewe ili nione vipi nitapata msaada”
“Msaada juu ya nini?” aliuliza tena jicho lake likiendelea kuwa kali usoni
mwangu. Nilianza kumweleza ‘A’ mpaka ‘Z’ juu ya mkasa wa maisha yangu.
66
Kama ilivyokuwa kawaida Uwesu alionekana kushangazwa na mkasa ule wa ajabu
kabisa.
“Aisee!. pole sana simulizi ya maisha yako inasisimua sana”
“Nimekwishapoa”
“Kwahiyo siku ile tumekutana katika basi ndo ulikuwa unakwenda kwa mganga
kutafuta ufumbuzi wa hayo maswahibu?”
“Ndio”
“Inaonesha tatizo lako ni kubwa sana”
“Ndivyo mtaalamu alivyo sema japo sijui ni kitu gani kinachonisibu haswaa”
Uwesu alinyamaza kusema, akatoa pakiti ya sigara na kuipachika mdomoni kisha
akawasha kiberiti cha gesi katika sigara na kuvuta mkupuo mmoja mkubwa kisha
akapuliza moshi mwingi angani halafu akasema.
“Kwahiyo hadi kunieleza yote hayo ulipenda mimi nikupe msaada gani?”
“Waswahili wana msemo usemao zimwi likujualo..”
“Achana na semi za kiswahili nenda kwenye mada husika tafadhali” alinikatisha.
Nilishusha pumzi ndefuu kisha nikasema, “nahitaji kuonana na baba yako” Uwesu
alinitizama kwa kina akashusha pumzi ndefu kifua chake kikapanda juu na
kushuka pindi alipovuta pumzi na kuzitoa nje.
“Pole sana ma mdogo..” alisema akavuta sigara yake kisha akatoa moshi
mwembamba katika tundu za pua yake kisha akaendelea kusema.
“Baba yangu nimekwishamzika miaka mingi sasa”
“Nini!!” nilipatwa na mshangao moyoni huku uchungu ukinishika nikashindwa
kuzuia matone ya machozi katika macho yangu.
Uwesu alizunguka kutokea pale alipokuwa ameketi katika kiti chake cha
kuzunguka na kunifuata.
“Pole sana, kwani ulitaka baba akusaidie jambo gani?” aliniuliza.
“ Baba yako ndio kimbilio langu na tegemeo nililokuwa nimebakiza katika maisha,
sasa nimebaki mimi tu, mimi peke yangu, nani atakae kuwa tayari kushea matatizo
yangu teena” niliongea kwa uchungu machozi yakinitoka.
67
“Pole sana Zahara, usijali nitakusaidia katika kila hali.”
“Huwezi Uwesu.. huwezi, matatizo yangu ni makubwa mno inahitaji mtu anaye
ijua thamni yangu haswaa na si vinginevyo.”
Uwesu alinipiga piga begani kama ishara ya kunifariji, kisha akanitaka niongozane
nae katika lile jumba lake. Aliniongoza hadi katika chumba kimoja kikubwa.
“Karibu na jisikie upo nyumbani kesho nitafanya jambo kwa ajili yako.” Alisema
Uwesu. Tangu hapo nilikuwa nikiishi pale kwa Uwesu kwa muda wa wiki, ndani
ya lile jumba tulikuwa tukiishi watu wanne yanii Uwesu, mimi, ndugu yake na
uwesu aliyeitwa Cholo ambaye alikuwa akisoma kidato cha pili pamoja na mlinzi
wa getini.

*****
Siku moja Uwesu aliniita na kunitaka tutoke na kusema kuwa alikuwa na
maongezi na mimi.
“Tunakwenda wapi?”
“We nifaute tu”
Tuliingia katika gari na kuanza safari nisiyo jua wapi tunakoelekea. Tulishika njia
ya kuelekea mjini lakini tukiwa Manzese Tip Top mita kadhaa tuliingia Magomeni
Mwembe Chai na safari yetu ikaishia mbele ya geti jeusi huku ndani yake kukiwa
na jengo kubwa la kifahari. Alipiga honi mara mbili kisha geti likafunguliwa
tukajitoma ndani.
Tuliishia katika sebule kubwa lilitandikwa zuria kubwa la manyoya, katika sebule
lile hapakuwa na kitu kingine zaidi ya TV aina ya ‘flat screen’ lililogandishwa
ukutani.
“Keti hapo” alisema Uwesu.
Yeye aliingia katika moja ya vyumba vilivyokuwa mule ndani alionekana ni
mwenyeji mule ndani. Sekunde chache baadae alirejea akiwa ameongozana na
mkaka mfupi mweusi.
“Karibu sana bibie” yule mkaka mweusi alinikaribisha kwa uchangamfu.
68
“Asante,” niliitikia pasina kuelewa kwanini nakaribishwa eneo lile nisilolijiua.
“Zahara”
“Abee”
“Siku moja ulinieleza una matatizo..” alisema huku akinitizama usoni. “matatizo
ya viumbe wa ajabu, viumbe wanaochezea maisha yako.” Alisema tena. Nilitikisa
kichwa kumkubalia.
“Sasa leo nimekuleta huku kuangazia ufumbuzi wa maswahibu hayo.” Alisema
huku akiachia tabasamu akinitizama kwa macho yaliouliza
“je umefurahia supraizi hii?”
Niliachia tabasamu huku macho yangu yakimjibu kuwa hakika hii ilikuwa ni siku
niliyokuwa nikiisubiri kwa hamu. “Safi sana kutana na Sheikh Hussein Maalim
huyu ni mtaalamu aliyejikita katika mambo ya nyota na tiba” Alisema Uwesu,
Sheikh Hussein alinipa mkono huku akisema karibu sana Zahara.
“Wakati tumegusana viganja vya mikono yetu mara ghafla nilihisi kama
nimeguswa na waya wa umeme uliokuwa umechubuliwa, kwani nilihisi
nikitetemeshwa mwili wote tendo lile lilitokea si zaidi ya sekunde tatu. Nilipiga
ukelele wa kuogofya huku nikiondoa mkono wangu kwa nguvu na upesi. Uwesu
alishanga nikaoana akinitizama kwa macho ya udadisi.
“Uwesu mgonjwa wetu ana viumbe wengi na hatari mno”. Alizungumza kwa
utulivu akiachia tabasamu jepesi lakini meno yake hayakuonekana, kisha akasema
tena.
“Uwesu nenda kule chumbani na bibie umsitiri mwili wake”, sikujua nataka
kustiliwa kitu gani lakini kwakuwa nilikuwa tayari kupata msaada niliamua kutii
kama nilivyo takiwa. Tuliingia katika chumba,Uwesu alinitolea juba lililokuwa
katika begi la nguo na kunitaka nivae kiheshima kama mwanamke wa kislamu
avaavyo.
“Unaonekana mwenyeji katika nyumba hii Uwesu?” nilimuuliza wakati nikimaliza
kulivaa lile juba.
“Nitakueleza tukitoka hapa.”
Baada ya kumaliza zoezi la kuustili mwili wangu. Tulirejea kule sebuleni
alikokuwa Sheikh Hussein.
69
“Sasa tutakwenda kusoma Surat Al Fatiha mara kumi kisha Surat Al Naas halafu
tutamalizia Surat Al Jinn.
Nafikiri baada ya hapo Allah atatia wepesi inshallah.” Alisema huku akifunua
msahafu na kujiweka vizuri kama kwamba anangojea pilau la nyama. Upesi
alianza kusoma zile aya takatifu yeye peke yake huku akiwa amefumba macho
akionekana amezama zaidi kiroho. Hata kabla ile aya ya kwanza kufika katikati,..
ghafla nilihisi kizunguzungu kikubwa huku nikiona maluweluwe na michoro ya
ajabu isiyo ashiria chochote mbele yangu.
Nikaoana kama dunia inayumba kutoka upande mmoja kwenda mwingine huku
mimi nikiwa juu yake naelea.
“Uwiiii” nilipiga ukelele wa kuogofya baada ya kuona naelekea kuanguka lakini
ajabu nikajiona kama dunia ilivyokuwa ikizunguka na kuyumba yumba huku mimi
nikiwa juu yake chini yake kulikuwa na shimo kubwa ambalo mwisho wake
haukuonekana zaidi ya giza zito. Sasa dunia ikawa inayumba huku ikinisukuma
mimi kuangukia katika lile shimo la giza.
“Uwiii! Nakufaa” nilipiga ukelele mwingine wa nguvu huku nikijaribu kushika
kwa nguvu pale chini ili nisiteleze zaidi na kuangukia katika lile shimo la ajabu.
Lakini kadri yule Sheikh Hussein alivyokuwa akisoma zile aya katika kile kitabu
ndipo nilipokuwa nikijiona ninapata nguvu halafu nikiwa na tumaini kubwa la
kujikomboa kwa kutoanguka katika lile shimo. Hali hiyo ikawa inajirudia kila
mara. Yule sheikh akawa anakazana kusoma ile aya kuu kabisa katika kitabu kile
kitakatifu.
Niseme tu na kadri alivyokuwa akizungumza yale maneno ambayo sikujua tafsiri
yake zaidi ya kujua ni maneno matakatifu ya Mungu yaliyoandikwa katika kitabu
chenye kuitwa Qur-an, nilikuwa nikipata nguvu japo kuna wakati nilikuwa
nabanwa mwili mzima na kitu kama praizi. Ikafikia hatua nikaoana ni heri yule
sheikh asitishe zoezi lake la kutamka yale maneno kwani alivyokuwa akisoma yale
maneno katika kile kitabu ndivyo nilivyokuwa nikizidi kufinywa katika mwili
wangu na vitu nisivyoviona.
Mara zoote macho yangu yalikuwa yanaona ukungu mbele yangu. Nikawa nalia
kwa uchungu lakini sidhani kama sauti yangu ya kilio ilisikika kwa sheikh pamoja
na Uwesu. Hali ile iliendelea hadi nikajikuta giza linazunguka mboni za macho
yangu na sikujua kilichoendelea tena
70

*****
Nilizinduka baada ya lisaa limoja na kujikuta bado nipo pale sebuleni Uwesu na
Sheikh Hussein akiwa pembeni yangu.
“Pole sana bibie”
“Asante” nilijibu huku kumbukumbu zangu zikirejea upesi mno.
“Imekuwaje kwani”
“Mshukuru Allah kwakuwa ndiye daktari wa madaktari, hakika ulikuwa na viumbe
wabaya mno katika mwili wako, viumbe waliokufanya kuwa kifungoni kwa
miongo mingi mno.” Alisema Sheikh Hussein alivuta bilauri ya maji na kuyanywa
kidogo kisha akaendelea kusema.
“Siwezi kusema mengi uzuri ni kuwa kila kitu Uwesu amerekodi katika kamera
hii..” alisema huku akitoa kamera ndogo ya Sony na kuifungua.
“Tizama mwenyewe” Alinipa ile kamera ikiwa ‘On’ tayari kuonyesha tukio zima
lilivyokuwa wakati ule Sheikh Hussein akiwa anasoma zile dua takatifu na mimi
nikiwa katika mkanganyiko mkubwa wa maluweluwe. Nilijiona natutumuka
mwili mzima huku ukelele wa kutisha ukitoka kinywani mwangu, macho nilikuwa
nimekodoa huku uso wangu ukibadilika na kuonekana katika namna kama ya
mzuka.
“Aghaghaagh,” nilikoroma kama mtu anayekata roho mwili umenikakamaa hadi
mishapa ikiwa inaonekana. “Mnataka nini ninyi binadamu” sauti ya ukali ilinitoka
kinywani mwangu, ajabu ni kuwa pamoja na kwamba nilionekana mimi ndiye
ninae ongea lakini sauti iliyosikika ilikuwa ya kiume.
Hapo nilipatwa na mshangao mkubwa nikasogeza karibu ile kamera kisha
nikaendelea kujitizama. “Nasema ninyi binadamu mnataka nini kwetu?” Sheikh
Hussein aliendelea kusoma zile dua, akawa kama kwamba hakusikia wala kuona
chochote kilichokuwa kikinisibu.
“Basi basi basi.. tunatoka.!! Usiendelee kutusomea kisomo hicho kinatutesa,
twatokaa” sauti kutoka kinywani mwangu ilisema. Sasa hapo nikiwa naangalia ile
kamera nikaelewa kuwa kumbe nilikuwa na majini katika mwili wangu.
71
“Ninyi ni akina nani na kwanini mpo kwa huyu binti mkiyachezea maisha yake
huku mkimfanyia mazingaombwe yenye kutisha kiasi hiki?” Hatimaye Sheikh
Hussein aliuliza kwa upole huku akinitizama kwa upole ilihali mimi nilikuwa
nikimtizama kwa jicho kali na la hasira.
“Kwa niaba ya wezangu naitwa Jini Sipra kutoka katika bahari ya mbali niko
mwilini mwake kwa bahati mbaya tu, sio kwa makusudi”
“Kivipi?” Sheikh Hussein aliuliza tena.
Nikiwa nimeendelea kushika ile kamera Sheikh Hussein pamoja na Uwesu
walinitizama kwa jicho lililosema tizima kwa makini hiyo video kuna maelezo
yanayotoa fumbo la maswahibu yako yote. Nilirudisha macho katika ile kamera
iliyokuwa ikiendelea kucheza. Na hapo nikajiona mimi kupitia majini yaliyo kuwa
kichwani mwangu yakisimulia mkasa woote ulio tokea miaka mingi hadi mimi
kujikuta naingia katika mkondo wa kuwa ndani ya viumbe wa ajabu waliobadilisha
dira na mwangaza wa maisha yangu.
Yale majini yaliyokuwa kichwani mwangu yalieeleza hivi…
 
SURA YA TISA

IRINGA, MIAKA MINGI ILIYOPITA
Kundi kubwa la ng’ombe lilikuwa katika malisho katikakati ya misitu ya Kitonga,
kengele ndogo zilizofungwa katika shingo za mifugo hiyo zililindima pande zote
ndani ya msitu huo wenye nyasi nyingi za kijani kibichi na miti mirefu. Jioni hii ya
saa kumi na mbili, Kalindimya kijana mchungaji wa mifugo hiyo alikuwa
akijitahidi kuwaswaga wale ng’ombe wenye kukaribia mia mbili, aliwasukuma
kwa mijeredi ng’ombe wa nyuma, muda ulikuwa umekwisha wa yeye kuendelea
kuwa katika malisho, mbwa wake wawili, waliendelea kuwa kando yake muda
wote wakingojea amri yoyote kutoka kwa bwana wao, jua lilizama na giza
kuchukua nafsi yake.
Kalindimya alikwishafika katika zizi kubwa la ng’ombe lililokuwa ndani ya msitu
ule, pembeni ya zizi kulikuwa na kijumba kidogo cha nyasi ambacho kilitumika
kama hifadhi kwa mchungaji yule mwenye kuitwa Kalindimya.
Baada ya kuhakikisha mifugo yote imeingia katika zizi alielekea katika kijumba
chake kwa ajili ya kupumzika. Ni dhahili mtu yule alikuwa ni mfugaji mwenye
kuendesha ufugaji wake katika mtindo wa kuhamahama kwa ajili ya kutafuta
malisho. Mara tu alipofungua mlango alikutana na harufu nzuri ya manukato
ambayo kamwe hakuwahi kusikia mahala popote.
“Pengine ni mauwa ya mwituni” alijifajiri kwa kuondoa mashaka yaliyo kuwa
moyoni mwake,hata alipogeuka na kukipa mgongo chumba chake kwa
kutengeneza kiegesheo cha mlango wa makuti, ndipo alipohisi kuwapo na ugeni
mule ndani. Aligeuka upesi na macho yake yakakutana na mwanamke mrembo
ambaye hakuwahi kumwona katika hii dunia.
Alibabaika kidogo huku akijiuliza apige kelele, akimbie au akabiliane nae.
Hakuwa na jibu. Alibakia ameduwaa kwa uzuri wa kiumbe yule, binti yule
alimsogelea na kumzunguka pande zote, huku akichezea nywele zake ndefu na
nyeusi tii, macho yake yakizunguka kama goroli mwendo wake ukiwa wa madaha
na pozi za kujinyonganyonga, lakini hata hivyo midomo yake iliachia tabasamu
jepesi la dharau, kisha kwa suti nzuri ya kisichana akasema “naitwa Shakira, ndiye
malkia wa msitu huu wa Kitonga, nitakuona siku nyingine” Hata kabla
73
Kalindimya hajatia neno mtu yule alitoweka kama moshi, jamaa alibaki katika
mashaka makubwa, huku akiamini ametokewa na mzimu wa msitu ule,
Hiyo ilikuwa ni siku ya kwanza Kalindimya kutokewa na kiumbe yule katika msitu
ule mnene… ikaja siku ya pili akiwa katika machungo… ikatokea siku ya tatu
akiwa amelala usiku…ikatokea siku nyingene tena akiwa kajipumzisha, mwisho
ikawa ni mazoea tu, kila mara Shakira akawa anamtokea yule mfugaji wa
ng’ombe.
Mwisho Kalindimya akazoea hali ile, Shakira akawa rafiki yake na Kalindimya,
wakazoeana mno, mazoea yakazaa upendo. Uliibuka upendo wa ajabu mno kwa
hawa watu wawili, Kalindimya alishii na huyu kiumbe kama mke na mume kwa
miaka mingi katikati kabisa ya msitu wa Kitonga. Hatimaye Shakira alishika
mimba na miezi tisa badae alizaliwa mtoto wa kiume, mtoto ambaye alikuwa nusu
jini nusu binadamu aliyefahamika kama Karogoyo.
Watu hawa walitengeneza kijiji chao ndani ya msitu ule, na waliishi kwa upendo
ya hali ya juu, siku moja mtoto huyu alipatwa na ugonjwa wa ajabu, na ghafla
alifariki dunia. Jini mwenye kuitwa Shakira aliumia mno kwa kifo cha mtoto wake
aliyempata kutoka kwa binadamu yule mchungaji. Miaka mingine baadae
alizaliwa mtoto mwingine aliyeitwa Zahara, alikuwa ni mtoto mzuri kuliko hata
uzuri wenyewe.
Siku moja yule mwanamke jini mwenye kuitwa Shakira aliuwawa na waganga wa
kienyeji waliokuwa wanakuja katika msitu wa Kitonga kuchimba dawa za
mitishamba ambazo walikuwa hawazitumii kwa matumizi mazuri katika jamii.
Lakini pamoja na hilo tangu afariki yule jini Shakira ambaye alikuwa ni malkia wa
msitu wa Kitonga ndani ya msitu huo kumekuwa hakuna amani hata kidogo, kila
binadamu anayeingia ndani ya msitu huo uliobarikiwa kuwa na dawa za
mitishamba, lazima apotelee humo daima. Na yule mfugaji na mwanae Zahara
hadi leo hawajulikani walipo.

***
Storage is full, ndio neno lililotokea katika video ile ndani ya kamera na hapo
ukatokea rangi ya bluu kuonesha kuwa ile video iliyokuwa inarekodiwa imejaa.
“Ayaaa imekwishaaa!!” nililopoka kwa fadhaa huku nikimtizama Sheikh Hussein
74
kisha nikarejesha macho upesi katika kamera. Sikuweza kuona tena kwa kuwa
pale ndio ilikuwa mwisho wa ule uzi wa mkanda wa filamu.
Bado sikuweza kuelewa chochote katika yale yaliyosimuliwa na majini waliokuwa
katika kichwa changu zaidi ya kuona kuna uhusiano wa majina tu kati ya jina
langu na la yule kiumbe aliyeelezewa katika simulizi ile. Bado niliona sijapata jibu
kamili la kitendawili hiki, zaidi nilijikuta nasombwa na wimbi la maswali katika
kichwa changu.
Nilibaki nimeduwaa nikiukodolea macho ile rangi ya bluu katika kamera kwa
nukta kadhaa.
“Umeelewa kitu” sauti ya Sheikh Hussein ilinistua.
Nilitikisa kichwa kumkatalia kuwa sijaelewa lolote, nikahamisha macho yangu
katika kile kikamera nikawa namtizama yule Sheikh.
“Huyo Zahara ndio nani aliyekuwa anazungumziwa?” niliuliza wahaka ukiwa
umenijaa.
Yule Sheikh aliachia tabasamu jepesi huku akihesabu tasbihi iliyokuwa mkononi
mwake, kisha akasema.
“Kama sio mkanda wa hiyo divu ya kamera kujaa basi ungepata jibu la kitendawili
chako chote.”
“Lakini kwakuwa sisi tulikuwa mashuhuda wa kile kilichokuwa kikielezwa na
viumbe vilivyokuwa ndani ya mwili wako hatuna budi kukueleza mambo yoote
tuliyoyasikia, ama sivyo bwana Uwesu?”
“Kabisa kabisa” Uwesu aliitikia huku akitikisa na kichwa chake kuafikiana na
maneno ya Sheikh Hussein. Nilijiweka sawa tayari kwa kusikia sababu ya mimi
kuingia katika majanga yale ya ajabu kabisa.
“Historia inaonyesha baada ya kila binadamu anayeingia kwenye ule msitu na
kutokomea kusikojulikana waganga na waganguzi kutoka maeneo mbalimmbali
walikaa na kuweka shauri la pamoja. Lazima suluhu la vifo vinavyotokea katika
msitu wa Kitonga ipatikane ufumbuzi na ufumbuzi pekee ilikuwa ni kuondoa
mzuka na majini waliokuwa wanaangamiza waganga waliokuwa wakienda
kuchimba dawa katika msitu ule ambao unasadikika ndio eneo lenye utajiri wa
mitishamba mingi pengine kuliko eneo lolote katika bara la Afrika. Lakini hadi
sasa ninavyoongea na wewe bado halijapatikana suluhu ya tatizo hilo, bado kuna
75
vita kubwa kati ya majini na waganga wa jadi dhidi ya msitu huo Zahara.”
Alisema Sheikh Hussein na kukaa kimya kidogo.
Nilifikiri kwa muda maneno yake lakini bado katika yote aliyoyasema bado
sikuona jibu la kitendawili changu.
“Bado sijaelewa kitu Sheikh” nilisema huku nikimkodolea macho huku ndita
katika paji langu la uso zimejichora.
“Ni kwamba wewe ndio Shakira, yule jini aliyesadikiwa kuwa ameuawa na
waganga wa jadi.”
“Nini!” mshutuko mkubwa ulinivaa baada ya kauli ile, nikabaki mdomo wazi kwa
nukta zisizohesabika, kope za macho yangu zikikapua, uso wa mshangao usoni
huku tumbo langu likipata joto.
“Mimi ni nani?!..jini..kivipi niwe jini?..kiaje?” nilisema.
Sheikh Hussein alitabasamu kisha akasema,
“Mimi nilitegema ungehoji vipi uwe jinni halafu usumbuliwe mwilini mwako na
majini mengine ilihali wewe ni jini”
“Hapana, hapana sheikh, hata hili la kutaka tu kujua mimi nakuwaje jini ilihali
tangu utoto hadi ukubwa naijua vema familia yangu haikuwa na mambo yoyote
yenye unasaba na mambo haya ya jamii ya siri ni muhimu kuliko hilo ambalo
ungependa nianze kuhoji, na nafikiri hilo litakuwa ni swali la pili baada ya hili la
kwanza kujibiwa maana unaposema kwamba mimi ni jini maana yake ni kwamba
hata wazazi walionizaa nao ni majini ama sivyo basi sio wazazi wangu.” Nilisema
kwa kulalama huku sura yangu bado ikiwa ni yenye kutawaliwa na taharuki isiyo
kifani.
“Utafundishwa elimu za majini na utaelewa hili, kwa ufupi ni kuwa binadamu
hawezi kuua jini, lakini jini anaweza kuua binadamu. Wale waganga
walichokifanya ni kupiga nusu kaputi jini Shakira, kwa miaka mingi mno. Na
wewe ukiwa katika usingizi ndipo unapopata njozi kuwa kuna siku uliwahi kuwa
binadamu, lakini kiasili wewe sio binadamu.” Alisema Sheikh Hussein huku
akiwa amenikazia macho makavu pasina kusema neon.
Nilimtizama yule sheikh kwa sekunde chache nikamwangali Uwesu, yeye pia
alikuwa akinitizama kwa mashaka kidogo huku akimung’unya midomo kama
76
mwenye kumungu’nya tambuu, macho nikayarejesha kwa Sheikh Hussein kisha
nikahoji.
“Kwahiyo unataka kujaribu kusema kila kitu kilichotokea tangu nikiwa mtoto hadi
nakuwa yote ni ndoto niliyokuwa naota nikiwa nimelala?”
“Haswaaa, ni ndoto lakini si ndoto”
“Kivipi ni ndoto lakini si ndoto” niliuliza kwa wahaka.
“Kilichotokea katika maisha yako na kujiona ni mtu mwenye familia, ndugu
jamaa, marafiki na hata mchumba wa dhati ni sahihi kabisa jambo hilo ni la kweli,
lakini si ndoto kwa kuwa kuna siku itakayokuja na kuona, na kugundua kama kuna
mahala uliwahi kutokea na kuishi huko kwa miaka mingi, na siku hiyo
utakapopatwa na hali hiyo ndipo utakapojielewa rasmi wewe ni nani?” Yule
sheikh aliendelea kunieleza vitu ambavyo sio tu kwamba sikumwelewa lakini pia
mambo yale yalikuwa hayaningii akilini hata kidogo.
“Hahahahaha..!! unajua unanieleza mambo ambayo kila nikijaribu kulazimisha
utashi wangu uelewe hilo lakini ubongo wangu unagoma kabisa kuelewa aisee”
Nilisema huku cheko dogo lenye mchanganyiko wa fadhaa likinikitoka.
“Zahara” aliniita Sheikh Hussein huku akinitizama kwa makini zaidi.
“Abee”
“Unaonaje na na sisi akili zetu zishindwe kuelewa kuwa ulitekwa nyara na mzee
aliyeokota jaketi lako wakati unatoka Geita, kisha akakuingiza katika chumba
ambacho alikubaka, siku hiyo hiyo ukapata mamba na siku hiyo hiyo ukajifungua
mtoto, na siku ya pili ulivyotoroka katika jumba ukakuta sio mwaka 1989 bali ni
mwaka 2016, unaonaje na sisi tukubeze kwa maelezo hayo?”
“Lakini mimi huo uliousema hapo ni ukweli uliotokea mbele kabisa ya macho
yangu” nilijibu upesi upesi huku nikiwa nimetoa macho.
Yule Sheikh alinicheka kwa pozi, cheko ambalo ndani yake lilisema ‘acha ubwege
hebu fungua akili yako sasa’
“Sasa huu si muda wa kukulazimisha ukubali haya nikuelezayo jukumu lako ni
kusubiri, muda utaongea zaidi” alisema Sheikh Hussein.
“Kwamba badae nitakuwa jini?” nilimdakiza.
77
“Sio baadae wewe bado ni jini kama majini mengine, kinachotokea na kujiona
wewe ni binadamu hata mimi sijui.”
“Khaa!!”
“Unaonaje ukineleza sababu ya mimi kubakwa, kuzaa mtoto ndani ya lile jumba na
kuingiliwa na viumbe wa ajabu mwilini mwangu na kunitesa kwa miaka yote
hiyo”
Hatimaye niliona niulize swali ambalo pengine jibu lake lingenipa maana ya
matatizo yote yale katika maisha yangu.
“Niseme mara ngapi kwamba wewe ni jini, yale yote yaliyotokea katika lile jumba
ni mwendelezo wa juhudi za waganga kujaribu kukuzuia usizidi kuwaangamiza
wataalamu wanakwenda kusaka dawa kwenye msitu Kitonga kwa kazi zao
mbalimbali. Kuingiliwa kimwili, kuzaa mtoto na kupigwa nusu kaputi kwa miaka
zaidi ya 25 yote hayo ni kinga za kukuzuia Zahara, unajua wewe ni kiumbe hatari
mno Zahara. Kwa kweli kadri nilivyozidi kuambiwa mambo yale na yule baba
nilijikuta hadi mimi najiogopa.
*****
Baada ya mambo yote hayo hakuna binadamu yoyote aliyekubali kuishi ama kuwa
karibu na mimi kwa kuamini mimi ni Jini. Si Uwesu wala mtu mwingine yeyote
aliyekuwa tayari kuwa karibu na mimi, ajabu ni kuwa, taarifa za kwamba mimi ni
kiumbe wa ajabu zilitapakaa mno katika baadhi ya maeneo hapa jijini. Siku moja
niliwahi kuona gazeti la udaku lisilo maarufu likitoa habari juu ya sakata la maisha
yangu japo, mwandishi aliandika ile habari kwa kuipika mengi yakiwa ya uongo na
machache ya ukweli, bado mtu yoyote angesoma habari ile lazima asingeacha
kutishika mno kwa mambo yale yaliyokuwa kama hadithi za kufikirika. Kwa siku
zile za awali nilikuwa nikiishi kwa yule sheikh, naweza nikasema ni Sheikh
Hussein yeye peke yake ambaye hakuwahi kuniogopa katika uhai wangu wa
mwishoni.
Lakini hata hivyo bado sikuona furaha wala tumaini la maisha kama binadamu
yoyote. Sikuwa na kitu muhimu chochote katika dunia, sikuwa na chochote cha
kupoteza katika ulimwengu huu. Nilijiona ni kikatuni tu mbele ya macho ya kila
aliye mbele yangu. Sikuona thamani ya utu wa wangu hata siku moja. Hivyo basi
kutokana na hayo yote yaliyonisibu na yanayoendela kunisibu siioni haja ya
kuendelea kuishi katika huu ulimwengu mpya kwangu. Asihusishwe mtu yeyote
na kifo changu. Naomba maaamuzi yangu yaheshimiwe..
78
By Zahara..
Mwisho wa ujumbe wa marehemu.

*****
Sheikh Hussein alimaliza kusoma kile kitabu cha kumbukumbu, mikono yake
ilikuwa imeloa kwa jasho, huku mwili wake ukitweta vibaya mno. Wakati wote
Mwili wa msichana mrembo Zahara ulikuwa ukining’inia katika kenchi juu ya dari
tayari akiwa ni marehemu. Alijikaza kiume akapiga simu polisi na kutoa maelezo
ya awali, muda si mrefu polisi waliwasili nyumbani kwa Sheikh Hussein tayari
kwa uchunguzi wa awali kabla ya mwili wa marehemu Zahara kuzikwa.
Hii ilikuwa ni 9/5/2016.



MWISHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom