Sababu za JK kumnyima Samuel Sitta na kumpa Anne Makinda nishani hizi hapa!

natafuta joke mtu aliyenayo anipostie... Ni ile ya mashindano ya wanasayansi ambayo Tz ilishiriki. Nasi tukatia fora. Baada ya mtoto aliyezaliwa bila kichwa, na wanasayansi wa kibongo wakamwekea nazi badala yake na leo ni kiongozi mkubwa wa Taifa letu!

Mkuu unataka kufunguka kuwa hilo ndilo linalomsumbua mpaka sasa?
 
You must be out of your freakin mind...ni lini Sitta alifukuzwa uspika ukiwa hauna uhakika na unachoongea ni bora kukaa kimya kuliko kuonekana katuni mbele ya watu

Siyo kikatuni tu mbele ya watu ni kikatuni male ya walioshiba maana ukisema mbele ya watu kutakuwa na wenzake wenye njaa kama yeye
 
****** endelea kuboronga tu namna hiyo ili uudhihirishie ulimwengu kuwa wewe hufa na huwezi hata kidogo kuwa na wadhifa ulio nao. Pia busara kwako haipo na hata chembe ya aibu hauna
 
chama ndicho kinakupa nafasi ya uongozi kama kinaona hujakiwakilisha vema hakina sababu ya kukupa nishani. suala la msingi viongozi hao wanaweza kupewa nishani hata na vyama vya upinzani kama vinaona Siita au Lowassa wanastahili.

Mkuu, unataka kueleza zile nishani zilikuwa za wana ccm, kwanini wasingezitoa kwenye kamati kuu ya chama cha mapinduzi.
 
Mkodoleaji

Sina shaka kuwa observations zako ziko sahihi, lakini ninamashaka na jinsi ambavyo umefanya hitimisho (conclusion) ya observations zako. Kimsingi Mwakyembe ripoti yake sijaujua vema unafiki uliokuwemo, labda kwa kuwa ilikuwa inainvolve significant figure within the government. Lakini pia ifahamike kuwa actions ambazo zililiwa proposed had greater impact on the government in power wakati ule. Yumkini Sitta alihitaji busara za ziada ku-deal na kitu kama hicho, na nina mashaka kama spika wa sasa angeweza kuruhusu hata kusomwa repoti ambayo kwangu naiona ilikuwa so sensitive! Itoshe kusema, kwamba kwa suala la unga ...hakuna aliyekuwa na hakika kama ilikuwa uchawi au sumu..polonium inawekwa kwa viti! Kwa hiyo ili kujiridhisha na kwenda kisayansi ilibidi apewe mkemia mkuu! Hapa si kupima uchawi, bali kuja na uchunguzi wa kisayansi kukubali au kukanusha hisia. Nina imani Sitta na wabunge wote wanajua kuna uchawi, kwa hiyo wangeweza kumtafuta sangoma mmoja na kuja kupunga mapepo hapo Bungeni!!!!

Ninalosema hapa ni kwamba sioni sababu ya kumnyima Sitta kisa ya mapungufu ya richmond na Unga wa uchawi. Hoja ibakie kuwa mbona Makinda kapewa wakati tuzo zilikuwa kwa wastaafu? Huyu mama bado, na ndo kamaliza mwak tuuuuuuuuu


Bube kuhusu unafiki wa hiyo ripoti nimekwambia Mwakyembe mwenyewe alikiri kuwa kuna mambo yamefichwa, kama siyo unafiki ni nini? Ni kweli kama unavyosema kwamba kwa Mkemia Mkuu wangejiridhisha kama ni pollonium au siyo. Lakini siyo kitu kilichotokea wakati ule. Mimi na wewe tunakumbuka kabisa kuwa issue ilikuwa ni uchawi ndiyo maana wakatajana sana majina na wakasema kuna wabunge walikuwa wanawanga usiku. Hayo pia yaliandikwa.

Nikubaliane na wewe kitu kimoja kuwa kisa cha Richmond na Unga wa Uchawi haiwezi kuwa sababu ya kumnyima Sitta nishani. Lakini pia kwa sababu utoaji wa nishani ni suala la utashi wa mwenye kutoa inawezekana yeyey kaona hivyo kama ni vigezo
 
Toka tumetolewa kwenye mjadala wa KATIBA MPYA, tumepewa orodha nyingine ya vitu vya kipuuzi hasa kujadili....
1. Ziara ya CDM kwa JK
2. Maadhimisho ya "serikali ya uhuru wa TZ bara" aka miaka 50
3. Nishani za wateule hao
4.
5.
6.

Endeleaaaaa....
lol hamna KATIBA MPYA hii nchi hapa!
 
Nyerere (R.I.i P) Aliwahi kutoa tuzo nadhani katikati ya miaka ya 80.Nishani hizo zilitolewa kwa watumishi na watu mbalimbali ambao siyo watumishi wa serikali kwa maana ya raia wa kawaida.Kulikuwa na category ya watu waliokuwa majasiri.Hizi za miaka 50, sijui kama categories zilielekezwa zaidi kwenye mchango wa "uhuru" ama vipi.Kama ndivyo basi nadhani kuna watu walipewa hakuchangia kivile kwenye kuleta uhuru.Vinginevyo hizo categories zina utata na kufanya wananchi wa kawaida kuuliza maswali mengi.
 
Kweli huyu jamaa ni kauzu, we utasemaje sitta kafukuzwa uspika wakati muda wake uliisha, This is veri insane!!!!!!!!!!!!!
 
Ubora wa mtendaji au kiongozi sio maneno bali anachosema na kuhubiri kinafaa kitafsiriwe kwa vitendo. Sitta akiwa spika alikuwa na maneno mengi ambayo kimantiki hayakuweza na hayataweza kumwachia legacy. Historia haiwezi kuandikwa kwa kuruhusu mijadala bungeni amabayo ni critical kwa serikali au alleged curruption curprits. No, not all. Kiongozi wa kweli anatakiwa aende zaidi ya hapo kwa kuhakikisha maazimio yanatekelzwa bila chembe ya shaka. Sasa Sitta tunaweza kumpima hivyo? Aliruhusu mjadala wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme-Richmond ukaendelea, kamati ikaundwa, ikafanya kazi yake, ikatumia mamilioni ya walipa kodi kusafiri ndani na nje na muda wa kujadili maswala ya maendeleo ukawa haupo wabunge na watu nje ya bunge wakazama kwenye debate ya Richmond. Lakini cha ajabu mtu huyo huyo akaja kuuzima mjadala wa Richmond ktk kipindi ambacho Tiafa lilihitaji majibu ya kina kuwa haupashwi kujadiliwa tena. Sasa huyu ni mpambanaji wa kweli au tumwite tragic hero? Ni sawa na mtu aliyejilemba vizuri kuelekea kwenye sherehe na karibia na lango na shughuli anaamua kujipaka tope. Sitta hapa historia haiwezi kumsifu maana after all kitu ambacho vizazi vijavyo watataka kujua ni baada ya mjadala nini kilifanyika na kama hakikufanyika nini kilifuata? Sasa waandike spika alizima mjadala?


Pili Sitta kuwa mpambanaji wa ufisadi ni quite questionable maana hajawahi kutuambia aliongoka lini? Wakati Dr.Slaa anataka kuanika list of shame bungeni na kashfa ya EPA alinyimwa nafasi hiyo. Na ushahidi wa kile alichotaka kusema bungeni alipompatia spika-Sitta akaenda navyo kwenye kipindi cha maojiano na TBC kikiendeshwa na Simbeye akaonyesha hizo nyarak kwa dharau na akatishia kuzipeleka polisi. Sasa huyu ni mpamnaji anayeshindwa kuheshimu confidential information alipowa na mbunge? Na ilipokuja kudhihirika kuwa kweli watu walikwapua mabilioni toka BOT Sitta akuwahi kuliomba Taifa msamahaa kwa kuukataa ukweli aliokuwa amepelekewa na Dr.

Ujenzi wa nyumba ya bei kubwa kama ofisi ya spika kwenye jimbo lake. Je alifikiri yeye ni pertual speaker.

Haya pamoja na matukio mengine hayampi sitta uhalari wa kuvikwa nishani

Lowassa atawamaliza marinda mwaka huu kwa mwendo huu
 
wanywaji wanapokuwa na furaha,hugonganisha chupa zao kushangilia mafanikio (cheerz)

Wala nchi wanapokuwa na furaha kwa ulaji wa nchi.hupeana nishani kudhihirisha utendaji kazi wao.
 
Vipi Kuhusu Mzee Malecela?inamaana vigezo alivyovitumia kikwete kuwapa mawaziri wakuu wastaafu yeye hana?

Mytake: Kama Kikwete alijua kwakuwapa Tuzo hizi wachache kungejenga na kuletamshikamano La hasha inaweza kuwa vinginevyo:Maji na mafuta vimeshaanza kujitenga!
 
Angalieni mnapojadili mambo haya mnaposwa kuangalia jinsia zote sio wanaume tu.
Kuna mambo ya kuangalia kigezo cha jinsia, mbona hatujaskiaga Sheikh wa kike??? Tukubaliane kuwa masuala muhimu yatahitji vigezo makin, sio mtu ametoka kunywa chimpumu anakuja na kuanza kuweka vgezo vya kipuuz vya kumpata Spika.
 
Kaka hakuna kitu serious ambacho kinafanywa ni serikali ya CCM. Kila kitu ni comedy tu. Aliyoyafanya mkuu wa kaya ni comedy ya aina yake ambayo inawezwa kuingizwa kwenye Guiness Book of Records. Huwezi kutoa Nishani kwa kuangalia nani unampenda na nani unamchukia. Hiyo haipo kwenye ulimwengu was leo.
Nimeshangazwa na kusikitishwa na Kitendo cha Rais JK kumnyima Nishani aliyekuwa Spika wa Bunge tisa Mhe. Samuel Sitta na Kumpa nishani hiyo Spika wa Sasa Anne Makinda ambaye hana vigezo alivyovitaja Rais. Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa hadi sasa, Anne Makinda hamkaribii na wala haoneshi dalili ya kufikia robo ya utendaji wa Samuel Sitta, mbaya zaidi hata mwaka mmoja bado hajamaliza kwenye hicho kiti, huo utendaji uliotukuka kauonyesha lini ilihali hadi sasa ni mauzauza tu???Kama kwa viwango vya Rais, Anne Makinda ni mtendaji bora zaidi ya Sitta, basi ndugu zangu tujue kuwa nchi hii tunajiongoza wenyewe.

Mhe. Samuel Sitta alipoulizwa sababu za kutopata nishani hiyo, alisema kwa sasa asingependa kulizungumzia suala hilo na kusisitiza, "hilo liache kwanza, sitaki kulizungumzia" Aidha, Rais Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na mawaziri wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madarakani, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Maoni yangu

Kama Fedha za kuwezesha uwepo wa nishani hizi unatokana kodi zetu, nadiriki kusema fedha zetu zimechezewa kwani baadhi ya waliopewa hawana sifa mbele ya Umma ya kupewa nishani hizo zilizotokana na Kodi zetu kwa mfano, Mkapa. Mzee huyu pamoja na kuliongoza Taifa alijimilikisha kifisadi mgodi wa kiwira kupitia kampuni yake na mkewe tena akiwa bado madarakani. Hiyo heshima anayoisema JK huyu mzee anayo anatoka nayo wapi????Nani atamuheshimu kwa wizi alioufanya???Mzee huyu na mtuhumiwa wa ufisadi - Mramba walituingiza mkenge ktk manunuzi ya Rada na mambo mengine mengi ya hovyo hovyo kwa mtu wa hadhi yake kuyafanya. Spika Anne Makinda mara kadhaa amenukuliwa akitaka Posho za wabunge ziongezwe tena kwa hoja za kitoto kabisa za kupanda kwa gharama za maisha huku akijua kuwa Serikali kiuchumi ipo dhohoflihali. Kimsingi huyu mama hana utu na ni mbinafsi, anajijali yeye na tumbo lake. Anapendelea wazi wazi wabunge wa chama chake. Itoshe tu kusema kuwa huyu mama hana sifa za kuwa Spika ila Jinsia yake ndo ilimbeba kama tulivyoambiwa na waliompitisha kugombea nafasi ya uspika.

Kitendo cha Rais kutompa Nishani Mhe. Samuel Sitta, Spika ambaye kwa asilimia kubwa alionyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuruhusu mijadala ya ufisadi kujadiliwa kwa marefu na mapana yake Bungeni, ni dhahiri kuwa Rais wetu yupo kwa ajili ya mafisadi/wezi wa Rasilimali zetu na sio kwa ajili ya Wananchi. Nlitegemea Rais ampe Sitta nishani kwa moyo wa Uzalendo aliouonyesha akiwa Madarakani. Wataalam wa mambo ya kijamii wanaweza wakahusisha kitendo cha Sitta kunyimwa Nishani, pamoja na kutoteuliwa kugombea Uspika kuwa kinatokana na chuki aliyonayo Rais kwa yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika wa Bunge la Tisa. Kimsingi inaonekana Rais hakupenda yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika.

Kwa kuwaacha watumishi wanaostahili kupata Nishani hizo na kuwapa watu wasio na sifa za kupata nishani hizo. Ni dhahiri kuwa Nishani hizo zimepoteza sifa na kamwe haziwezi kuheshimiwa machoni mwa Watanzania.

Source: Mwananchi 12/12/2011
 
Back
Top Bottom