Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
Nimeshangazwa na kusikitishwa na Kitendo cha Rais JK kumnyima Nishani aliyekuwa Spika wa Bunge tisa Mhe. Samuel Sitta na Kumpa nishani hiyo Spika wa Sasa Anne Makinda ambaye hana vigezo alivyovitaja Rais. Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa hadi sasa, Anne Makinda hamkaribii na wala haoneshi dalili ya kufikia robo ya utendaji wa Samuel Sitta, mbaya zaidi hata mwaka mmoja bado hajamaliza kwenye hicho kiti, huo utendaji uliotukuka kauonyesha lini ilihali hadi sasa ni mauzauza tu???Kama kwa viwango vya Rais, Anne Makinda ni mtendaji bora zaidi ya Sitta, basi ndugu zangu tujue kuwa nchi hii tunajiongoza wenyewe.
Mhe. Samuel Sitta alipoulizwa sababu za kutopata nishani hiyo, alisema kwa sasa asingependa kulizungumzia suala hilo na kusisitiza, "hilo liache kwanza, sitaki kulizungumzia" Aidha, Rais Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na mawaziri wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madarakani, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.
Maoni yangu
Kama Fedha za kuwezesha uwepo wa nishani hizi unatokana kodi zetu, nadiriki kusema fedha zetu zimechezewa kwani baadhi ya waliopewa hawana sifa mbele ya Umma ya kupewa nishani hizo zilizotokana na Kodi zetu kwa mfano, Mkapa. Mzee huyu pamoja na kuliongoza Taifa alijimilikisha kifisadi mgodi wa kiwira kupitia kampuni yake na mkewe tena akiwa bado madarakani. Hiyo heshima anayoisema JK huyu mzee anayo anatoka nayo wapi????Nani atamuheshimu kwa wizi alioufanya???Mzee huyu na mtuhumiwa wa ufisadi - Mramba walituingiza mkenge ktk manunuzi ya Rada na mambo mengine mengi ya hovyo hovyo kwa mtu wa hadhi yake kuyafanya. Spika Anne Makinda mara kadhaa amenukuliwa akitaka Posho za wabunge ziongezwe tena kwa hoja za kitoto kabisa za kupanda kwa gharama za maisha huku akijua kuwa Serikali kiuchumi ipo dhohoflihali. Kimsingi huyu mama hana utu na ni mbinafsi, anajijali yeye na tumbo lake. Anapendelea wazi wazi wabunge wa chama chake. Itoshe tu kusema kuwa huyu mama hana sifa za kuwa Spika ila Jinsia yake ndo ilimbeba kama tulivyoambiwa na waliompitisha kugombea nafasi ya uspika.
Kitendo cha Rais kutompa Nishani Mhe. Samuel Sitta, Spika ambaye kwa asilimia kubwa alionyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuruhusu mijadala ya ufisadi kujadiliwa kwa marefu na mapana yake Bungeni, ni dhahiri kuwa Rais wetu yupo kwa ajili ya mafisadi/wezi wa Rasilimali zetu na sio kwa ajili ya Wananchi. Nlitegemea Rais ampe Sitta nishani kwa moyo wa Uzalendo aliouonyesha akiwa Madarakani. Wataalam wa mambo ya kijamii wanaweza wakahusisha kitendo cha Sitta kunyimwa Nishani, pamoja na kutoteuliwa kugombea Uspika kuwa kinatokana na chuki aliyonayo Rais kwa yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika wa Bunge la Tisa. Kimsingi inaonekana Rais hakupenda yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika.
Kwa kuwaacha watumishi wanaostahili kupata Nishani hizo na kuwapa watu wasio na sifa za kupata nishani hizo. Ni dhahiri kuwa Nishani hizo zimepoteza sifa na kamwe haziwezi kuheshimiwa machoni mwa Watanzania.
Source: Mwananchi 12/12/2011
Ni kweli JK ana matatizo sana katika maamuzi yake. Lakini mara nyingine watu tunaowatetea kwa kweli wanatia mashaka. Samuel Sitta unayemtetea ni yeye ambaye alifunika mjadala wa Richmond ili serikali isishughulikiwe. Sitta alikuwa akifokea wabunge kama watoto wadogo na kurekebisha maswali ya wabunge kwa serikali. Ni kipindi cha Sitta huyo huyo ambapo kwa mara ya kwanza tulishuhudia bunge likipeleka unga wa uchawi kwa Mkemia Mkuu (sasa sijui kama Mkemia Mkuu ana vifaa vya kupima uchawi hatujui).
Tunaweza kuwa hatumpendi Anna Makinda labda kwa kwa sababu ya udhaifu wake lakini hapo hapo kwa mapenzi yetu kwa Sitta tukasahau udhaifu wake. Linganisha Ripoti mbili ile ya Mwakyembe na hii ya Ramo Makani. Utakuta ya Mwakyembe imejaa unafiki na uwongo (na hapa sijamsingizia Mwakyembe maana yeye mwenyewe alikiri kuficha baadhi ya mambo) wakati hii ya Ramo Makani imejitahidi kuwa very objective. Cha kushangaza ya Mwakyembe ilikuwa na mwenyekiti ambaye ana PhD hivi alishindwaje kuoanisha njia za utafiti, matokeo ya utafiti na hitimisho? Tofauti kabisa na Ripoti ya Ramo Makani unaona njia zilizotumika, matokeo na hitimisho. Kwenye Ripoti ya Ramo Makani wahusika wote wakuu waliwekwa kiti moto na hitimisho halikuegemea upande wowote. Nimetoa mfano wa hizo Ripoti mbili kuonyesha kwamba wakati tunalinganisha hao maspika wawili tuweke mizani ya haki na wala siyo mizani ya mapenzi na chuki.