Rushwa na uraia wa Siyoi, CCM watafutana uchawi badala ya kujibu HOJA

chachana

Member
Aug 4, 2011
57
92
Rufaa iliyokatwa na chadema kuhusu utata wa uraia wa sioi sumari mgombea wa ccm umeleta mkanganyiko mkubwa kwa viongozi wa ccm.

Inasemekana kwenye vikao nape alionya sana kuwa utata wa uraia wa sioi unaweza kuwaingiza matatani. Idara ua uhamiaji ilishakiri kwa barua kuwa sioi hakuwahi popote kukana uraia wa kenya na mbaya zaidi inasemekana pia kuwa hati mbili za kusafiria zenye kuonyesha uraia wa nchi mbili tofauti.

Mpaka usiku huu mkurugenzi na wanasheria wa serikali walikuwa kwenye kikao kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo inasemekana kuna uwezekano mkubwa sioi akatolewa kwenye kugombea kwa sababu kinyume na hapo ni kuamsha balaa kubwa.
IGP saidi mwema inasemekana usiku huu amefika usa river kwa ajili ya suala hili

Update:
hii siasa wanayo icheza CCM ya Leo ni ya ajabu sana. Maana itakumbukwa kwenye Kikao cha kamati ya siasa ya Mkoa wa Arusha cha kujadili wagombea ubunge wa Arumeru Mashariki, wajumbe wa Kikao walimwomba RC wa Arusha awapelekee nyaraka mbalimbali kuhusu ufafanuzi wa masuala ya rushwa na uraia wa Sioi na hii ni kwa Kuwa kwa mujibu wa taratibu za ccm RC ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa.

Lakini cha kushangaza Mara tu baada ya RC kukabidhi nyaraka hizo tukashusahudia kuvuja kwa nyaraka hizo kwa kasi ya ajabu. Tukajiuliza kulikoni mwenyekiti wa ccm Mkoa wa arusha ndugu Onesmo Nangole ang,ang,anie kuonyeshwa nyaraka hizo? Kumbe yeye na kijana wake mtumwa wa mafisadi James Millya walikuwa na Lao jambo. Walipanga kuvujisha ili ionekane Kuwa Sioi anaonewa na aweze kipata huruma ya wana Arumeru Mashariki. Huu ni upuuzi mtupu. Lazima wajue Kuwa wana Arumeru Mashariki hawadanganyiki.

Hivyo kuna taarifa kwamba Kuwa Onesmo Nangole na James Millya watahojiwa kwa kuvujisha Siri za vikao vya CCM.

Hata hivyo huko ni kutapa tapa kwa CCM maana Chadema hawahitaji kupewa nyaraka maana hao kina Millya na Nangole ni wazembe hawajui kutunza nyaraka na aliyezichukua hata wao hawakutegemea ndio maana wanatapatapa kutafuta mchawi wakati aliyeziiba nyaraka ni mtu wa karibu sana na mzee wa Monduli lakini ni mtu wa Chadema sana anawachota akili kila siku bila wao kujua. wakija kugundua watalia sana. Jamaa alichukua akatoa photocopy na kuzirudisha.
by Joseph Peter
 
Rufaa iliyokatwa na chadema kuhusu utata wa uraia wa sioi sumari mgombea wa ccm umeleta mkanganyiko mkubwa kwa viongozi wa ccm.

Inasemekana kwenye vikao nape alionya sana kuwa utata wa uraia wa sioi unaweza kuwaingiza matatani. Idara ua uhamiaji ilishakiri kwa barua kuwa sioi hakuwahi popote kukana uraia wa kenya na mbaya zaidi inasemekana pia kuwa hati mbili za kusafiria zenye kuonyesha uraia wa nchi mbili tofauti.

Mpaka usiku huu mkurugenzi na wanasheria wa serikali walikuwa kwenye kikao kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo inasemekana kuna uwezekano mkubwa sioi akatolewa kwenye kugombea kwa sababu kinyume na hapo ni kuamsha balaa kubwa.
IGP saidi mwema inasemekana usiku huu amefika usa river kwa ajili ya suala hili

Siyo rufaa, bali ni PINGAMIZI. Iwapo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo [Bwana Kagenzi] atalitupa, ndipo Nasari anaweza kukata Rufaa kwa Tume ya Uchaguzi Makao Makuu Dar es Salaam na hiyo ndio itaitwa ni Rufaa.

Swala la Uraia halimhusu IGP Said Mwema, kama kweli ameenda hapo ni kwamba anaingilia kazi za Idara ambazo sio za kwake. Maswala ya Uraia yanahusu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji ambaye yuko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kama CHADEMA wana barua ya kutoka ofisi ya Uhamiaji mkoani Arusha, basi hapo kuna utata mkubwa. Kwa kuwa kuna baadhi ya wana CCM hawakutaka Siyoi apite, watahujumiana wao kwa wao na huo ndo utakuwa mwisho wa mchezo.
 
Nilidhani CCM wanapiga kelele juu ya ukoo ndani ya Chadema tu kumbe hata wao wana endeleza ? Kuna nini hadi huyu mtoto apiganiwe hivi kuwa Mbunge ?
 
Hii ni shida nyingine ya kugangamalia jambo bila kufikiria madhara yake. Si kila saa Nape ni Mropokaji wakati mwingine huwa mkweli asilimia mia moja. Oneni sasa.
 
Kazi imeanza na hata watakayemweka kama wataamua kumtoa asiyeoa naye watamtafutia sababu tu. Chadema Chama Makini chanjeni mbuga mwenzetu ana msiba kwake
 
Mwanzoni nilidhani ni mizengwe ya ccm jama alivokatwa Bashe kumbe pana weza kuwa madai ya mashiko.
 
Mliambiwa Barua ya UHAMIAJI ilika bidhiwa CHADEMA na vigogo wa CCM mkabisha sasa yako wapi,kazi yenu kupinga bila kutafakari,hata wama CCM hawamtaki siyoi
 
Mwanzoni nilidhani ni mizengwe ya ccm jama alivokatwa Bashe kumbe pana weza kuwa madai ya mashiko.

Kwa mujibu wa Bashe mwenyewe, anasema alizaliwa Tanzania na kwa kujua mizengwe ya sihasa za Tanzania akaukana na uraia wa Somalia kabla ya uchaguzi. Uhamiaji walithibitisha haya lakini Magamba wasipokutaka, hata nyeusi itaitwa nyeupe.
 
Sheria gani inayomfanya Sioi asiwe raia wa Tanzania?.... sheria namba na kifungu plz.
 
Siyo rufaa, bali ni PINGAMIZI. Iwapo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo [Bwana Kagenzi] atalitupa, ndipo Nasari anaweza kukata Rufaa kwa Tume ya Uchaguzi Makao Makuu Dar es Salaam na hiyo ndio itaitwa ni Rufaa.

Swala la Uraia halimhusu IGP Said Mwema, kama kweli ameenda hapo ni kwamba anaingilia kazi za Idara ambazo sio za kwake. Maswala ya Uraia yanahusu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Uhamiaji ambaye yuko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kama CHADEMA wana barua ya kutoka ofisi ya Uhamiaji mkoani Arusha, basi hapo kuna utata mkubwa. Kwa kuwa kuna baadhi ya wana CCM hawakutaka Siyoi apite, watahujumiana wao kwa wao na huo ndo utakuwa mwisho wa mchezo.

Imekwenda shule! Imetulia!
 
rufaa iliyokatwa na chadema kuhusu utata wa uraia wa sioi sumari mgombea wa ccm umeleta mkanganyiko mkubwa kwa viongozi wa ccm.

Inasemekana kwenye vikao nape alionya sana kuwa utata wa uraia wa sioi unaweza kuwaingiza matatani. Idara ua uhamiaji ilishakiri kwa barua kuwa sioi hakuwahi popote kukana uraia wa kenya na mbaya zaidi inasemekana pia kuwa hati mbili za kusafiria zenye kuonyesha uraia wa nchi mbili tofauti.

Mpaka usiku huu mkurugenzi na wanasheria wa serikali walikuwa kwenye kikao kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo inasemekana kuna uwezekano mkubwa sioi akatolewa kwenye kugombea kwa sababu kinyume na hapo ni kuamsha balaa kubwa.
Igp saidi mwema inasemekana usiku huu amefika usa river kwa ajili ya suala hili

kwa hiyo hata baba yake hakuw raia wa tanzania?
 
CCM mercenary politician:
rage
kinana
rostam
and bunch of them are there...

Mkuu inasikitisha sana kuona kuwa watu wengi sana wana uraia wenye utata, lakini serikali iko kimya tu. Utata wa urais wao unaonekana pale wanapokuja kugombea nafasi za uongozi. Kama ni kweli mgombea ana pasi mbili za kusafiria, anakuwa amevunja sheria za nchi, na anatakiwa kuchukuliwa hatua, na kama ana uraia wa nchi mbili moja ikiwa ni Tanzania pia anatakiwa kuchukuliwa hatua, na kama ni mgeni inatakiwa ithibitishwe kuwa amelipia hati zake zote za ukazi na kuwa taratibu zote zinazohusiana na uhamiaji zimefuatwa.

Inaonesha kuwa kuna udhaifu mkubwa sana Uhamiaji. Ni Jambo la aibu kama kweli IGP amekwenda USA RIVER kwa sababu ya utata wam uraia wa mtu mmoja anayeeonekana kuwa mgombea wa CCM, wakati Dar es salaam makao makuu kuna mamia ya mambo muhimu yanayitakiwa kushughulikiwa. Still inaonekana hata ndani ya jeshi letu la Polisi usalama wa raia uko chini ya maslahi ya CCM.
 
Back
Top Bottom