Rufaa Igunga: Kafumu atofautiana na CCM

Aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Dr. Dalali Kafumu-CCM amekaririwa akisema kuwa tayari ameshafanya maamuzi. Taarifa nilizonazo toka chanzo kilicho karibu na Dr. Kafumu zinasema kuwa uamuzi wenyewe ni wa kutokata Rufaa dhidi ya Hukumu ya Mahakama Kuu- Tabora iliyomvua Ubunge. 'Sina nia ya kukata rufaa na wala sitajihusisha kwa namna yoyote ile na rufaa itakayokatwa na yeyote' alisema Kafumu. ' Kuna watu wa ajabu sana...kwanini wanilazimishhe jambo nisilotaka?' alifoka Dr. Kafumu. Picha inaendelea...
 
Eheee yshakua hayo? Kwani si yupo hospital kalazwa huyu? Nashangaa jana nimemuona starTv anaongea au aliongea yale kabla ya ajali? Kama ndio au ndio ajali za ccm?
 
Tatizo hakujua anaingia kula meza moja na wenyer mikono michafu...Kaingia ndani amegundua..
 
Hasira za nini Dr ndo siasa hiyo inafika mahala unaachwa mwenyewe hata wale waliyokuwa nyuma yako wanakimbia.
 
Kafumu amejitambua, anakumbuka damu za wana Igunga ilimwagika kwa uchaguzi uliojaa hila na uonevu dhidi ya maamuzi sahihi ya wapiga kura!
 
Aliyekuwa Mbunge wa
Igunga,Dr. Dalali Kafumu-CCM amekaririwa akisema kuwa tayari ameshafanya
maamuzi. Taarifa nilizonazo toka chanzo kilicho karibu na Dr. Kafumu
zinasema kuwa uamuzi wenyewe ni wa kutokata Rufaa dhidi ya Hukumu ya
Mahakama Kuu- Tabora iliyomvua Ubunge. 'Sina nia ya kukata rufaa na wala
sitajihusisha kwa namna yoyote ile na rufaa itakayokatwa na yeyote'
alisema Kafumu. ' Kuna watu wa ajabu sana...kwanini wanilazimishhe jambo
nisilotaka?' alifoka Dr. Kafumu. Picha inaendelea...

Kafumu yuko sahihi kutokata rufaa,kwani hata siku ya hukumu alisema anaachana na siasa anarudi kwenye kazi yake ya madini.Kina Mwigulu wanalazimisha ili wamtose tena kwenye kesi.
 
Dk kagundua akin mwigulu, wasira na wengineo ndani ya ccm sio watu wa kuwaamini, baada ya kesi kufunguliwa wote walikimbia wakamwachia mwenyewe hata alipowaambia waje kuto ushahidi waligoma. Bora ajipumzikie afanye mambo yake
 
Na kweli amefanya uamuzi wa BUSARA. Sasahivi wanamlazimisha akate rufaa, kesi ikianza hawatamleta Mh.Makufuli na wenzake muhimu kutoa ushahidi ambao hata kama wakija hautabadili matokeo. Kifupi ni kwamba kampeni za CCM zilimwaribia pia, ile kugawa mahindi ya njaa kama rushwa, kutishia wananchi bastola, kuahidi uongo (daraja la Mbutu), kutishia asiyeipigia CCM atakiona, kumtumia DC kisiasa, kuvuruga ndoa za makada wenzie, umafia na mauaji, makada wenzie kujitafutia umaarufu kupitia mgongo wake (hata sasahivi wanaendelea na zoezi hili).
 
Wakati aliyekuwa mbunge wa Igunga Bw Dalaly Peter Kafumu amesema hatakata rufaa kupinga hukumu iliyotengua "ushindi" wake wa ubunge, chama chake kupitia kwa Mwigulu Nchemba kimesema kitakata rufaa hiyo. Mwigulu amesema hivyo kwenye mikutano ya chama hicho inayoendelea jimboni Igunga wakati Kafumu ametoa tamko hilo alipohojiwa na Star Tv.

Source: Star Tv Habari.

My take: Mambo si shwari ndani ya ccm maana tangu Mwigulu aanze mikutano yake Igunga, Kafumu hajawahi kuonekana.
Tunamhitaji Mwigulu atoe majibu hapa, hizo kampeini ni za nini, hapo Igunga anafanya kazi gani ikiwa Dr Kafumu mwenyewe amekataa???

 
Chezea sisiem wewe!!!!!!!!!!!!!sisiem nikama mtoto wa mbuzi,ananyonya nabado anamtwanga mama yake vichwa,nakama kazaliwa dume ndio balaa tupu,akimaliza kunyonya anambashia mama yake.sisiem noma!!!!!!!!!!!!kudadadekiiiiiiiiiiiiiiiiii

Kwa huyo mtoto wa mbuzi ni Mwigulu au Nape??
 
Bora ameona haina maana kupigania kitu ambacho mwisho wa siku sidhani kama kitamlipa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom