Rufaa Igunga: Kafumu atofautiana na CCM

Aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Dr. Dalali Kafumu-CCM amekaririwa akisema kuwa tayari ameshafanya maamuzi. Taarifa nilizonazo toka chanzo kilicho karibu na Dr. Kafumu zinasema kuwa uamuzi wenyewe ni wa kutokata Rufaa dhidi ya Hukumu ya Mahakama Kuu- Tabora iliyomvua Ubunge. 'Sina nia ya kukata rufaa na wala sitajihusisha kwa namna yoyote ile na rufaa itakayokatwa na yeyote' alisema Kafumu. ' Kuna watu wa ajabu sana...kwanini wanilazimishhe jambo nisilotaka?' alifoka Dr. Kafumu. Picha inaendelea...

ndugu yangu naamini katika mengi ya mabandiko yako. Na hili ningependa kuliamini pia
 
Wakati aliyekuwa mbunge wa Igunga Bw Dalaly Peter Kafumu amesema hatakata rufaa kupinga hukumu iliyotengua "ushindi" wake wa ubunge, chama chake kupitia kwa Mwigulu Nchemba kimesema kitakata rufaa hiyo. Mwigulu amesema hivyo kwenye mikutano ya chama hicho inayoendelea jimboni Igunga wakati Kafumu ametoa tamko hilo alipohojiwa na Star Tv.

Source: Star Tv Habari.

My take: Mambo si shwari ndani ya ccm maana tangu Mwigulu aanze mikutano yake Igunga, Kafumu hajawahi kuonekana.

Huyo Mwigulu mchumi namba one wa BOT anajua sheria huyo au ni kuongea tu? akamuliize JEMBE TUNDU!
 
Tu'assume CCM ikishinda rufaa, kafumu atakataa kuwa Mbunge?

Kesi za uchaguzi ZINATAMKA WAZI kuwa pande 2 zinazoshtakiana NDIYO TU ZENYE HAKI YA KUKATA RUFAA!Dr Kafumu na Mwl Kashindye tu ndiye wenye haki ya kukata rufaa na wala sio CHADEMA au CCM; Dr Kafumu akikataa KUKATA RUFAA KESI NDIYO IMEISHA!
 
Haya majamaaa yanapiga kelele za mfa maji. wanajua dhahr kwamba kuwa uchaguzi walishazidiwa ubavu. Mungu wetu aliye hai akiamua wataumbuka mpaka watafikia hatua ya kutembea uchi bila ya wao kujitambua. Hebu fikiria mungu alivyowambua Arumeru Mashariki.. kumbuka pia skendo ya kutaka kumuondoa kamanda MWAKYEMBE, Prof. MWandosya, Zitto. Sasa ona hili la Dr. Ulimboka!!! Haya basi ona na hili la Mwangosi!!!!... eheeeeeee! Haya, ona sasa Mungu anaonyesha utukufu wake kwa kutuonyesha kuwa Kafumu hakuwa mshindi halali wa Magamba.......ya kijani!!! Sasa ndugu yangu subiri uone siku moja wanaumbuka hadharani kama alivyoumbuka huyu jamaaa Naibu waziri wa madini wakati ule (Malima) pale MOR alipotaka kuuza madini yetu hadharani wanjanja wakampoka.....Eeee mungu wetu tunakuomba uzid kuwatia aibu hawa magamba ambao hachoki kutuibia!!!!!!!!
 
CCM wakitaka kupunguza makali ya aibu na kukataliwa mbele ya umma wa Watanzania, waacha kabisa kumtumia Mwigulu. Huyu mtu ni kero machoni na masikioni kwa kila mtu mwenye akili timamu.
 
CCM wakitaka kupunguza makali ya aibu na kukataliwa mbele ya umma wa Watanzania, waacha kabisa kumtumia Mwigulu. Huyu mtu ni kero machoni na masikioni kwa kila mtu mwenye akili timamu.

Kweli kabisa ... hivi ccm hakuna chombo kinacho shughulikia nidhamu na maadili .. au wanaona ni sawa tuu
 
Bora ameona haina maana kupigania kitu ambacho mwisho wa siku sidhani kama kitamlipa.

Alionywa sana na marafiki zake wa ndani na nje ya nchi asijiingize ktk siasa za ubunge,hakusikiliza,akadhani ni mteremko! Toka ametangazwa kuwa mbunge ktk uchaguzi uliojaa damu,amekua hana furaha na sitashangaa akiamua kuachana kabisa na siasa!
 
CCM wakitaka kupunguza makali ya aibu na kukataliwa mbele ya umma wa Watanzania, waacha kabisa kumtumia Mwigulu. Huyu mtu ni kero machoni na masikioni kwa kila mtu mwenye akili timamu.

kwao CCM wanamuona ndie Superb kwakuwa ni kijana kama walivyo akina Mnyika, Zito, Wenje, Mdee na wengineo, a wanaamini kwamba anaweza kuwaokoa lakini bila kujua kuwa ujana pekee hautoshi, bali upstairs uwe safi pia
 
Mkuu , msomi yeyote ataona hiyo ni typo.
Kuhusu signature yako, I always go the full distance katika mdahalo, debate, warsha au mada yoyte or otherwise, iliyoenda shule.
Stupidity and insinuations put me off.
read my signature...............

.........and by the way, stupidity and insinuations put anyone off, sio wewe tu, and probably you have just done what puts you off

Just read my signature once or twice
 
Kumbe mbwembwe zote za Mwigulu Igunga hawajakata rufaa, labda wameenda kupima upepo kwanza.

Hawapimi upepo ndo wameanza kampeni mapema!!! CCM Wenzenu hawezi kukata rufaa, si mmeona Sumbawanga wameongea tuuuu mpaka muda wakukata rufaa umepita.
 
ccm WANAJUA WAKIPIGWA CHINI TENA iGUNGA WATASAMBARATIKA, AIBU TUPU
Aibu imewapata! sasa wanachofanya ni kujibalaguza, hata wenyewe, wanajua hukumu ya yule jaji, ilikuwa sahihi, na wanajua kuwa hata kwenye rufaa hawatashinda, kwa hiyo wanachokifanya CCM, ni kile tunachoweza kukiita delaying tactics!!
 
Alikosa nini kwenye ukamishina wa madini na kukimbilia siasa za magamba? ama alienda kusafisha jina kwa tuhuma za ufisadi na mikataba feki ya madini!! Huyu jamaa ni expert, walau basi atulie afanye kazi ya manufaa kwa taifa siyo kucheza karata ambayo hana ujuzi nayo. Tatizo la wataalamu kuingizwa mkenge na wanasiasa linashika kasi TANZANIA. Professors, Doctors wanataka kuwa wanasiasa ili wapate nini? Na kule wanakotoka wanamuacha nani asaidie kukuza ujuzi na maarifa kwa vijana wetu? Kafumu rudi ufanye kazi uliyobobea achana na siasa kulinda heshima ya taaluma yako. Wasomi njaa zinatusumbua na wanasiasa wanajua kiu yetu, wameshatuteka.
 
Hiyo ndio siasa hata Arusha mjini aliyeshindwa ubunge Dr.Batilda hakufungua kesi mahakamani na ndivyo itakavyokuwa Igunga Dr.Dalali ameishaona ni vigumu kupata ushindi na jinsi chama chake kilivyomuangusha bola akafanye kazi nyingine!
 
Kesi za uchaguzi ZINATAMKA WAZI kuwa pande 2 zinazoshtakiana NDIYO TU ZENYE HAKI YA KUKATA RUFAA!Dr Kafumu na Mwl Kashindye tu ndiye wenye haki ya kukata rufaa na wala sio CHADEMA au CCM; Dr Kafumu akikataa KUKATA RUFAA KESI NDIYO IMEISHA!
Mkuu tafadhali thibitisha hii statement yako, maana najiuliza mbona Arusha mjini Batilda hakufungua mashtaka na ile kesi ikaendelea kusikiizwa na Lema akapigwa chini? Au ni katika stage ya rufaa tu basi? Kama ni katika stage ya rufaa peke yake tukubaliane kuwa hiyo sheria inahitaji marekebisho.
 
Mkuu tafadhali thibitisha hii statement yako, maana najiuliza mbona Arusha mjini Batilda hakufungua mashtaka na ile kesi ikaendelea kusikiizwa na Lema akapigwa chini? Au ni katika stage ya rufaa tu basi? Kama ni katika stage ya rufaa peke yake tukubaliane kuwa hiyo sheria inahitaji marekebisho.

Ni kwenye rufaa tu!Yule aliyeanzisha kesi au yule aliyeshtakiwa NDIYO TU WANAOTAKIWA KISHERIA WAENDELEE NAYO KWENYE HATUA YA RUFAA!Kwa mfano waliomshtaki LEMA wangeshindwa kesi Mama BATILDA asingeweza KUKATA RUFAA hata kama angependa kufanya hivyo maana HAYUMO KWENYE ORODHA YA WASHTAKI na yy aliitwa kama SHAHIDI TU!

Jaji Rwakabalila aliyemvua LEMA ubunge aliongelea chochote kwenye kipengele"cha haki ya mtu asiyegombea ubunge kushtaki kulalamikia uchaguzi ili hali yeye HAKUWA MGOMBEA?Wakili wa LEMA aliweka pingamizi kuomba mahakama iifute kesi kwani Mama Batilda mwenyewe HAJALALAMIKA KAMA ALITUKANWA?Zilionyeshwa hata DVD zozote za LEMA akitukana?

Tuache mahakama ya rufaa iamue lkn mm tayari NIMENUSA KITU!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom