Makonda anauvalisha Ukatibu Mwenezi CCM mamlaka ya Urais na uenyekiti wa Samia

DaveSave

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
440
634
FB_IMG_1700220117607.jpg

MKUTANO wa hadhara upo Geita. Mhitubiaji mkuu ni Katibu wa NEC CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda. Mara, Makonda anaagiza Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, apigiwe simu. Halafu, Makonda mwenyewe ndiye anapiga hiyo simu.

Mavunde ameshapatikana, simu inapokelewa. Makonda anamwambia Mavunde: “Nakupa maagizo ya chama”. Makonda anamwagiza Mavunde, akitumia mwavuli kuwa hayo anayomwagiza ni maelekezo ya chama.

Makonda anauliza: “Leo ni lini?”

Umati unaitikia: “Jumamosiiii!”

Mavunde kwenye simu naye anajibu: “Jumamosi.”

Kisha, Makonda anampa amri Mavunde: “Kesho naondoka Geita, tupishane na wewe ukiwa unaingia Geita.” Ni amri ya Makonda kwa Mavunde, kwenda kushughulikia mgogoro wa ardhi katika vijiji nane mkoani humo.

Mavunde, alijibu kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, alishatoa maagizo ya kushughulikia mgogoro huo. Zaidi ya mwezi mmoja kabla alishakuwepo Geita, akaahidi angerejea tena baada ya mwezi.

Mavunde akasema: “Kesho (Jumapili), nina kikao hapo Geita. Leo usiku nitakuwa Geita na kesho tutakuwa na kikao. Baada ya kikao cha kesho, tukiwa na mkuu wa mkoa, tutatoa mrejesho kwa wananchi.”

Mambo mawili; mosi ni jinsi ambavyo Mavunde alitoa majibu yake. Yupo mtu, nje ya wananchi waliokuwa wakishangilia kwa bidii, yeye aliamini kuwa Makonda alikuwa na ufahamu kuhusu ziara ya Mavunde, kwa hiyo aliamua kufanya siasa.

Hili ni tatizo kubwa. Siasa za kutafuta sifa na kujijenga binafsi. Wananchi wanapiga mayowe kwa matumaini, kumbe mwenzao yupo jukwaani kujenga haiba kupitia wao. Mavunde alipoingia Geita, kuna wananchi walitafsiri au wataendelea kuamini ziara yake ni agizo la Makonda.

Pili ni swali; tangu lini Katibu Mwenezi CCM, akawa na mamlaka ya kumwagiza waziri tena kwenye mkutano wa hadhara? Katiba ya CCM, haitoi mamlaka hayo hata kwa Katibu Mkuu ambaye ndiye Mwenyekiti wa Sekretarieti.

Sasa, ikiwa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, hana mamlaka ambayo Makonda amejivalisha, wapo watu wanawaza pengine Rais Samia, ambaye ndiye Mwenyekiti CCM, ameamua kubadili mtindo wa kushughulika na wasaidizi wake, kwa hiyo anazungumza kupitia kinywa cha Makonda.

Mzee fulani, yeye kwa busara zake na kwa ufahamu wake jinsi nchi inavyoendeshwa, haamini kuwa Rais Samia anaweza kujishusha na kufanya siasa za bei chee, kumtumia Makonda kuzungumza au kuwashughulikia wasaidizi wake.

Kupitia imani hiyo, Mzee huyo mtazamo wake umejikita katika dhana kwamba matamshi, maagizo na amri za Makonda jukwaani, hujituma mwenyewe. Ukichagua “kununua” mtazamo wa Mzee huyo, utajikuta ndani ya hekima za makatibu wakuu wawili wa zamani wa CCM.

Katibu Mkuu CCM mwaka 2012 – 2018, Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana, hivi sasa ni Makamu Mwenyekiti CCM, Tanzania Bara. Katibu Mkuu CCM mwaka 2018 – 2021, Dk Bashiru Ally, kwa sasa ni mbunge wa kuteuliwa.

Oktoba 30, 2023, Arusha, Kinana akiongoza ujumbe wa CCM, katika mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Zelothe Sephen, alisema kuwa uongozi ni tabia. Ujumbe wake ulijikita katika kumsifu Zelothe kwamba alikuwa mwenye tabia njema, hivyo alikuwa kiongozi mzuri.

Ukiuelewa ujumbe wa Kinana barabara, utapata majibu kuwa mtu kama una shida za hulka, hata usome namna gani, upewe mafunzo yapi, abadan, hutakuwa kiongozi mzuri. Mtu yeyote mwenye tamaa ya kukwea nafasi za uongozi na kupata mafanikio, sharti kwanza ajinoe katika hulka. Tabia iwe njema.

Bashiru, alipokuwa Katibu Mkuu CCM, si chini ya mara mbili, alisema Makonda alitakiwa kurudi shule apigwe msasa wa elimu ya uongozi. Kwa matamshi yake, Bashiru alisema Makonda ni kijana aliyekosa weledi wa kiuongozi.

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliiwezesha Tanganyika kupata uhuru akiwa na umri wa miaka 39. Alifanikisha kuifanya Tanganyika kuwa jamhuri, kisha yeye kuwa Rais wa Kwanza, alipokuwa na umri wa miaka 40.

Kutoka wakati huo, Bashiru akisema Makonda ni kijana, anahitaji kulelewa au akue kiuongozi, hadi leo akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, bado ni yuleyule. Makonda haendelei kuwa kijana. Ana umri wa miaka 41 anaitafuta 42. Hulka haibadiliki.

Pengine yakawa makosa kumtathmini Makonda kwa kipimo cha Mwalimu Nyerere kwa sababu Baba wa Taifa ni binadamu maalum Afrika, ila hata kwa viongozi wa zama za sasa, Mavunde ni waziri leo. Ni mbunge muhula wa pili. Ameshawahi kuwa naibu waziri katika wizara mbili tofauti.

Nafasi hizo, alizishika akiwa na umri kuanzia chini ya miaka 35. Pamoja na hivyo, hujamsikia popote akivuka mipaka yake. Kiongozi mzuri utamtambua jinsi anavyoweza kutekeleza majukumu yake ndani ya mipaka ya uongozi wake.

Mathalan, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM ni msaidizi wa Katibu Mkuu CCM. Wajibu wa Katibu Mwenezi CCM ni kukisemea na kukitetea chama, kulingana na maagizo ya sekretarieti, ambayo Mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu.

Makonda anaposimama na kumpa maagizo Waziri Mkuu, inaleta mkanganyiko mkubwa. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kwa nafasi yake, moja kwa moja anakuwa mjumbe wa Kamati Kuu CCM.

Kwa vile CCM ndio chama kinachoongoza dola, Kamati Kuu CCM ina hadhi sawa na Politburo, chombo ambacho nyakati za Soviet, ndicho kilichokuwa kinafanya uamuzi wa juu kuhusu sera na uelekeo wa nchi. Hivyo, Kamati Kuu CCM ni chombo nyeti, si tu kwa CCM, bali pia nchi.

Waziri Mkuu anahudhuria vikao vyote muhimu vya chama, kasoro vile vya kamati tendaji (Sekretarieti). Ni maagizo yapi hayo asipewe na Rais, yasimfikie akiwa Kamati Kuu au hata mikutano ya Halmashauri Kuu Taifa (Nec), aje apewe kwenye mikutano ya hadhara na Makonda?

MAKONDA NA MAMLAKA YA SAMIA

Nyakati za mwanzo baada ya kula kiapo, Makamu wa Rais, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Phillip Mpango, alikuwa akijisahau kwa kutoa maagizo yenye hadhi ya urais, wakati Rais Samia mwenyewe alikuwepo. Siku hizi, Mpango amebadilika.

Mfano mmojawapo, Mpango aliwahi kumwagiza Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba: “Nataka makusanyo ya mwezi yafike Sh2 trilioni.” Pengine sababu ni kuwa Mpango alipanda kuwa Makamu wa Rais kutoka Waziri wa Fedha. Hata hivyo, aliyepaswa kutoa maagizo hayo ni Rais Samia.

Mathalan, Mpango alipotoa maagizo ya kutaka makusanyo kwa mwezi yafikie Sh2 trilioni, kisha Samia alipoisogelea mimbari, angesema matakwa yake ni Sh2.5 trilioni mpaka Sh3 trilioni. Si ingeonekana kuna mgongano baina ya viongozi wa juu wa nchi?

Waziri Mkuu, kikatiba anapaswa kufanya kazi kwa ukaribu na Rais. Waziri Mkuu ni mshauri wa Rais. Waziri Mkuu ndiye mtekelezaji mkuu wa maagizo ya Rais. Juu ya yote, Waziri Mkuu ndiye mtendaji mkuu wa serikali ambayo mkuu wake ni Rais. Imefafanuliwa hivyo kikatiba, Ibara ya 52 na ibara zake ndogo, 1, 2 na 3.

Katiba ibara ya 53, inafafanua kuwa Waziri Mkuu anawajibika kwa Rais. Hivyo, mwenye mamlaka ya kikatiba ya kumwajibisha Waziri Mkuu, kumpa maagizo au kumwita ajieleze ni Rais. Bunge pia limepewa mamlaka ya kumwajibisha Waziri Mkuu kwa kura.

Bunge limepewa mamlaka dhidi ya Waziri Mkuu lakini kwa mzunguko mrefu. Rais ndiye mwenye mamlaka ya moja kwa moja. Inakuwaje Makonda anampa maagizo Waziri Mkuu? Bila shaka, kwa nafasi yake ya kukisemea chama, ameamua kuupa ukatibu mwenezi wake, nakshi za urais wa Samia na uenyekiti wake wa CCM.

Uthubutu huo wa Makonda ni hulka yake. Alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuna wakati alitoa maagizo yenye kuvuka mipaka. Aliwakaripia waliomzidi cheo kuwa yeye aliwapita mbali sana. Alisema: “Wale ambao mnajiona mna cheo kikubwa kuliko mimi, nimewazidi sana.”

Rejea mgogoro wake alipokuwa Mkuu wa Dar es Salaam dhidi ya Mpango, akiwa Waziri wa Fedha. Pitia kauli ya Rais wa Tano, Dk John Magufuli kuwa Makonda alifanya maonesho kuliko kazi. Tazama na anachokifanya sasa. Kumbuka pia kauli ya Majaliwa kwamba Makonda hakuwa akifanya kazi za ukuu wa mkoa.

Novemba Mosi, 2023, Nyerere Square, Dodoma, Makonda anasikiliza kero za wananchi, halafu anamwita Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule jukwaani, anamwambia “kimbia hapa”. Kisha anampa maagizo.

Mama Senyamule anatoa majibu kuwa kero husika imeshafika kwa Makamu wa Rais, ila yeye anatoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, wapigiane simu ili majibu yapatikane. Kisha, Makonda mwenyewe anampigia simu Kamishna Mkuu TRA, Alphayo Kidata. Anamhoji na kumpa maagizo.

Uongozi ni tabia, alisema Kinana. Kihulka, Makonda anaonekana hajui mipaka yake. Anajaribu kufanya kilekile ambacho Magufuli alikifanya alipokuwa Ikulu. Anashindwa kutofautisha nafasi yake ya ukatibu mwenezi na urais wa Magufuli.

Rais Magufuli sio tu alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vilevile alikuwa Mwenyekiti wa CCM. Mwenye mdaraka hayo kwa sasa ni Rais Samia. Ndiye anaweza kumwagiza yeyote ndani ya serikali na chama.

Wapi huku nchi inakwenda, Kamishna wa TRA anapokea maagizo kutoka kwa mjumbe wa Sekretarieti ya CCM? Huku nchi inapokwenda, CCM itapoteza hadhi na misingi yake, kipindi ambacho Makonda anajijenga binafsi kwa wananchi wenye kuamini kupiga mayowe jukwaani na kutoa amri ndio uongozi.

Ndimi Luqman MALOTO
 
View attachment 2816493

Soma Katiba-ya JMT na CCM utaona dhana ya ukuu wa chama
 
Makonda ana baraka zote kutoka juu ndio maana unaona anafanya hayo afanyayo !

Kama ingekuwa anafanya vinginevyo angekuwa ameshaonywa !!
Kwani umesahau ya mwenezi Nape Nnauye na mawaziri mizigo kipindi cha mwisho cha Kikwete ??!!
 
It's all scripted...!

Comrade Kinana alisema hapa majuzi: CCM haiko chini ya serikali bali serikali inamilikiwa na chama...kama unaelewa hiyo kauli hautopata shida kwa hizi theatrics za Makonda.

CCM wameanza kampeni, wanawaonyesha wananchi kwamba serikali hii ni yao...wao wanaweza kuiamuru cha kufanya na ikafanya...it's a campaign strategy...!
 
..kufuatilia yanayotokea ktk ziara za Makonda utakubali kwamba wananchi wana shida kubwa, na dhuluma imepita kiasi.

..mifumo yetu ya kiutawala na kiuongozi imefeli. Hili tatizo lililokuwa na kukomaa kwa muda mrefu hapa nchini. Ziara za Makonda ni kama kumwaga chumvi baharini.

..Matatizo ya Watanzania yamezidi kiwango cha fikra na utendaji kazi wa Ccm.
 
Kuna mahala nimeona gari ya matangazo kuwa wananchi wote wenye migogoro ya Ardhi wahudhurie mkutano wa kutatua changamoto hizo tar 18 kwenye ukumbi wa manispaa fulani!naona maagizo ya Makonda kwa W/Mkuu na waziri wa Ardhi yanaanza kutekelezwa! Ikumbukwe W/Mkuu alipewa miezi 6 kushughulikia migogoro yote ya Ardhi nchini huku waziri wa Ardhi akipewa miezi 3.
 
It's all scripted...!

Comrade Kinana alisema hapa majuzi: CCM haiko chini ya serikali bali serikali inamilikiwa na chama...kama unaelewa hiyo kauli hautopata shida kwa hizi theatrics za Makonda.

CCM wameanza kampeni, wanawaonyesha wananchi kwamba serikali hii ni yao...wao wanaweza kuiamuru cha kufanya na ikafanya...it's a campaign strategy...!
Hata Nape na Kinana walifanya hivyo hivyo na kuwaita baadhi ya mawaziri kwamba ni mizigo awamu ya Kikwete !!
Nchi hii watu wengi hawana memory nzuri !!
 
Kwamba ili utoe Maagizo , unatakiwa kwanza uwe na mamlaka Fulani Fulani ya juu?.

Wee naye kama unajiita Mwanasiasa au Ni kiuongozi, basi Unauongozi ambao Hujui hata uufanyie nn!!.

Ukishakua Kiongozi, unawajibika ,maadam unaona kitu hakipo sawa na unauwezo wa kukisemea , Sema !!! Sema !!.

Kama umeshindwa wewe, Wacha Makonda Aseme.
 
Inaonekana umesoma ukiwa unakimbia, Na umejibu ukiwa unakimbia ,
 
Back
Top Bottom