Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,171
- 3,346
Wana JF epukeni sana lugha za kejeli katika vifo, huwezi jua unaweza kukuta mwanae au mmoja wa wana familia ni mwana JF! Utasikiaje mtu mwana JF mwenzako amefika na baba yake halafu wewe ulicomment heri fisadi kafa n.k! Ni vizuri kujifunza kuwa mtu akifa anakwenda kuanza maisha mapya ambayo wote ni wageni hivyo ni kumtakia marehemu safari njema na kuwapa pole wafiwa.
Hivi unafikiri chuki ya kuwachukia polisi imetoka wapi kama siyo kwenye siasa? Ni bora tukaweka siasa pembeni na kutangaliza utu hata kama marehemu ulikuwa humpendi kwa sababu yoyote iwayo ile jamani.