'Ripoti' ya Mziray na Mabadiliko ya Chadema kuelekea 2010

Mnyika
Chama chenu vilevile kinatakiwa kuwa na financial muscle, mmejiandaa vipi kuhakikisha kuwa chama chenu kina pesa za kutosha? au ndio mnategemea tu michango ya wanachama na membership fee. 2010 inaonekana kama iko mbali, lakini kwa uchaguzi iko karibu, mmeangalia weakpoints (zipo nyingi) ambazo mnaweza kucapitalize kwenye viti vya udiwani na ubunge, walau mkaongeza idadi ya wabunge? Au lengo lenu ni kuendelea kuwa na wabunge hawahawa wachache waliopo?

Hili la finnancial muscle naomba nisiingie kiundani. Yatosha kusema tu, tunajiandaa. Ila haiondoi ukweli pia kuwa chama ni cha wanancha, hivyo michango ya wanachama ni suala la lazima kikatiba. Pia, ni jukumu la kila mpenda demokrasia na maendeleo kuchangia mageuzi hata kama hana kadi ya uanachama. Mnavyoviona vinaelea, vimeundwa!. Ama sivyo, nguvu ya wanamabadiliko inaweza kuzidiwa kupindukia kirasilimali na mafisadi wanaotumia kodi zetu hizo hizo na hatimaye ufisadi kuendelea zaidi na kuchota kodi zaidi. Kwa kila senti ambayo inakosekana katika kuleta mabadiliko na uwajibikaji kuna shilingi kadhaa zinazokwapuliwa na ufisadi ama kufujwa kwa matumizi ya anasa. Kumbuka kampeni za kumwondoa mkoloni, pamoja na kuchangiwa na wanachama, TANU ilichangiwa pia na watu binafsi wapenda ukombozi, vuta fikra ni kwa namna gani Nyerere alipata ile tiketi ya kwenda Umoja wa Mataifa- vyema za kadi za TANU hazikutosha, Rupia akaongeza, lakini unajua pia kwamba kuna fungu lilitoka Tanga toka michango wa watu wengine? Sasa jiulize, leo unataka Mbowe, Dr Slaa, Wangwe, Zitto nk waende vijijini- tunajua kwamba fedha za ruzuku pekee hazitoshi, fedha za michango ya wanachama pekee hazitoshi- unashindwa vipi mwananchi, haswa umbae uko middle class ya kibongo- ndani na nje ya Tanzania, kuunganisha nguvu ya wenzako wachache kufanikisha viongozi hawa kuja kwenye kijiji chako cha asili au jimbo lako ulipotoka ukaleta mabadiliko ya kweli? Wakati umefika sasa wa kusimama na kuhesabiwa ama kunyamaza milele!. Hilo la kuweka mkazo kwa ubunge nimeshalijibu kwenye FOCUS 2010. Kilichobaki ni mwitiko tu kwako na kwa mwingine. Pamoja Tutashinda

JJ
 
Mnyika,

Samahani nilishindwa kuwasiliana nawe tena kwa ajili ya dharura, nitakutafuta baada ya Krismas.

Air, Kasi na Nguvu ya Reforms ni muhimu. Naamini kuwa Chadema ni chama makini, hivyo woga wa kuanguka usiwepo. Kuanguka ni kawaida katika safari, waamka pukuta mavumbi na kuendelea huku ukijiuliza ni vipi ulianguka?

Kama kuanguka, mmeshaanguka, mmejipukutisha, lakini inabidi muongezo kasi ya mageuzi ambayo itawasaidi kung'ara 2010!

Sualal nililoliongelea kuwa ni la ki CCM ni lile la Ukabila na Ukoo ambalo limekuwa likiliandama Chadema tangu kuundwa kwake. Hisia za Watanzania pamoja na kuwa ni kweli si Chama cha Wachaga pekee au ukoo wa Mtei zimetapakaa kwenye mawzo ya Watanzania na CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhakikisha hisia hizo bado zipo na kuaminika.

Ndio maana nasema, mabadiliko ya haraka yanahitajika ambayo yataondoa ukungu wote ambao umekitia chama chenu doa.

CUF wanatatizo moja ambalo ni la wazi na kamwe hawataweza kufanikiwa mpaka wabadilike. Kwa wengi, CUF ni chama cha Kizanzibari na Udini! Ushahidi ni mkubwa hata katika uwakilishi wao katika Bunge na hoja wanazopigania.

Chadema has opportunity to be the only party that will reform the political spectrum of Tanzania and change the structure of Political systems that could lead to real solutions to critical things such as Katiba ya nchi na Muungano.

CCM had that opportunity, lakini they have decided to focus on their tummies and being a big bully who oppresses everytghing under democracy.

I am looking forward to work with you and share our passion for Taifa letu.

Rev. Kishoka

Sina tatizo na Ari, Nguvu na Kasi mpya kama msemo- ndio maana unakumbuka wakati wa kampeni zangu za Ubungo nilikuwa naawambia wanaCCM kama kweli wanaamini kasi mpya basi wanipigie kura mimi kijana wa miaka 25 badala ya Mzee wangu Keenja wa miaka 65 wakati huo!

Lakini ukisoma mfano huo hapo kuu utaona kwamba hii kauli CCM wanaitumia vibaya kwa kweli, ndio maana nikasema Ari, Nguvu na Kasi mpya bila maudhui na mwelekeo- ni hasara kuliko faida.

Ninukuu nilichosema baada ya wewe kutaka CHADEMA ifanye reforms zake kwa Ari, Nguvu na Kasi Mpya:

"Kwa kweli tunaendeleza reforms kwa misingi ya "Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke". Ujumbe wa hizi reforms ni 'CHADEMA- Tumaini Jipya'. Na kauli mbiu yake ni "CHADEMA: Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli"

Ari, NGUvu na KAsi Mpya bila maudhui yanayoeleweka ni mhemko, mabavu na mbio za kufukuzana na upepo, inaweza kuwa ni kwenda mbele au kurudi nyuma ama kujikwaa kabisa na ku- A.NGU.KA."

Kuhusu hilo la uchaga- ni reforms zipi ambazo chama ambacho wewe mwenyewe umekiri kwamba si cha kichaga kinaweza kufanya ili kionekane si cha wachaga? Wewe mwenyewe umekiri kwamba uchaga wa CHADEMA si muundo wake au uongozi wake, au sera zake bali ni hisia zilizopandikizwa na CCM. Tiba ya kisiasa ya hisia si reforms za chama, ni mind reforms kwa hao waliopandikiziwa hizo fikra. Ndio maana mimi nasema, tatizo la propaganda chafu ni kuzikalia kimya bila kuzijibu papo kwa papo- pengine katika baadhi ya maeneo CHADEMA ilichelewa kujibu papo kwa papo, na wananchi nao walipaswa kuwahoji CCM papo kwa papo kutoa ushahidi wa madai yao ya ubaguzi na si kukubali tu hewala na kutishwa mzigo wa lawama kwa CHADEMA wakati chama ni taasisi ya wanachama na umma!

Lakini ukweli unaanza kusambaa na kupambana na uwongo. Kwa kuwa wewe umeshautambua ukweli, naomba uwe balozi mzuri popote ulipo inapojitokeza hoja kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga, uwe wa kwanza kutoa ufafanuzi. Umeutambua ukweli, na ukweli ukufanye huru. Ubarikiwe!

Karibu tufanye kazi, pamoja tutashinda!

JJ
 
Mnyika
Let us face it. Chama chenu kinahitaji reform, ili kiweze kutupatia watanzania alternative tunayoitaka. Mimi naona inawezekana, ikiwezekana kuwe na merger na baadhi ya hivyo vyama mlivyoshirikiana navyo kutoa list of shame, na kuwatikisa mafisadi. Ni vema kama mtaondoka kutoka kwenye politics za umaarufu wa personalities na kuingia kwenye umaarufu wa chama. Sasa hivi CCM kilichomaarufu ni chama na sio individuals hili ni moja kati ya matatizo ya Chadema. Sijui kama mnaliona au hamlioni. This time around mna bahati ya kuwapata hao persnalities wakiisha ina maana Chadema imeisha, and that is not good for Tanzania.
 
Bongolander,

We are ready to face it but what should we face? Umesema chama kinahitaji reforms- ni vyema ukafafua ni reforms gani hizo na namna gani ili tuweze kuchukua hatua.

Kuna personalities nyingi zimepita CHADEMA- wameanza wakina Mtei- wakastaafu, CHADEMA bado inaendelea kusimama. Wakaja wakiMakani, wakastaafu- CHADEMA bado inaendelea kusimama. Wakapita wakinaKaborou, wakatekwa na CCM, CHADEMA bado inasimama. Sasa hivi ni wakati wa kina Mbowe, Wangwe, Dr Slaa, Zitto, Tundu Lissu nk, CHADEMA inaendelea kusimama. Na hapa si mtu mmoja, huu ni umaarufu wa timu ya watu, na si umaarufu tu kama wasanii- ni zaidi ya umaarufu. Ni umashuhuri unatokana umahiri wa hoja. Na hoja zenyewe chimbuko lake ni umakini wa sera za chama. Nakiri kwamba inawezekana personalities za CHADEMA ni maarufu kuliko policies, lakini niseme tu kwamba hata Mwalimu Nyerere mwenyewe alikiri kwamba CHADEMA ni chama chenye sera bora. Kumbuka, genesis ya CHADEMA sio uperisona wa watu kama wakina Mtei, bali kutofautiana na Nyerere kisera. Na hapo ndio chimbuko sera mbadala. Lakini sikatai kwamba bado tunachangamoto ya kuiboresha CHADEMA kuwa chama taasisi zaidi. Na ndio maana tumejikita kutengeneza chama taasisi ni si chama uchaguzi. Ili wengine tutakapoondoka, wanaofuta nao wakute taasisi imesima na inasonga mbele. CHADEMA is a going concern. Ndio mana kuna misingi ya kubadilishana uongozi, kuna misingi pia ya kuboresha muundo na sera ili kuendana na hali halisi na pia kusukuma mbele mabadiliko. Soma waraka wangu kuhusu "dokezo juu ya uzinduzi wa CHADEMA. Tukumbuke pia mfumo wa taasisi ni jambo moja, lakini viongozi katika mfumo huo nalo ni jambo la pekee sana. Ndio maana leo tunazo baadhi ya sheria ambazo kwa hizo tayari kuna haki fulani fulani ambazo raia na taifa kwa ujumla wangepata, lakini chini ya viongozi mafisadi sheria hizo zinatelekezwa badala ya kutelekezwa!

Ndio mana wakati wa uchaguzi tulisema; mabadiliko ya Kweli hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale eti kwa ari, nguvu na kasi mpya. Kwa falsafa ya Chukua Chako Mapema(CCM), Tanzania yenye neema haiwezekani.

Leo miaka miwili imepita toka tuyaseme maneno haya katika Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA- ukweli wa maneno yetu umeanza kudhihirika wazi, na wapo ambao wameanza kujutia ushabiki wao wa mwaka 2005.

CHADEMA is full of reformist- we are open to face it...mpira uko kwako sasa..

JJ
 
Mnyika,

Si unajua watu wa marketing wanatumia neno positioning kuangalia wanawezaje kuteka market share kutoka kwa washindani wenzao au wa concentrate na kundi lipi la customers.

Siku hizi hilo neno limeingia kwenye siasa.

Nikipita kule vijijini naona wazi wanachi wako hapa na wanasiasa wako kule. Mnachotakiwa CHADEMA kufanya ni kuichukua position hiyo iliyowazi karibu na kwa wananchi walio wengi.

Wananchi wengi wana matatizo mbali mbali, mafao yao hayalipwi, wanachangishwa pesa zinaliwa na wezi, wanaahidiwa mbolea ya ruzuku lakini wanalanguliwa au hawaioni kabisa, mazao yao yananunuliwa kwa bei ya chini mno, wakiumwa hakuna dawa hospitali, walimu hawafundishi na badala yake ni tuition kulipia nk. Sasa kwanini msiwe champions wa kuwatetea hawa wananchi wakati huu ambao sio wa uchaguzi ili wajue nyie mko pamoja na wao na ikifika uchaguzi mnakuwa mmejitengenea nafasi ambao wananchi walio wengi hawawezi kuwasahau?

Siasa za kutumia mabilioni kwenye uchaguzi na kisha kila mtu anapotelea mjini, naona itawachukua miaka mingi sana kuchukua uongozi wa nchi. CCM wako vijijini, hata kama hawafanyi kazi nzuri sana lakini angalao wako huko vijijini.
 
MNYIKA

Napenda kwanza kuweka wazi ITIKADI yangu. Mimi ni Mwana CCM.
Nimevutiwa na Mada yenu hii ya chadema must reform, As mwana ccm naamini ktk siasa za ushindani thats why nimeamua kuchangia ktk hili kama tulivokutana ktk mjadala wetu ulopita last week abt jk kuvunja baraza la mawaziri.

Mada hii imenbivutia nikiwa kama mtanzania mwenye itikadi tofauti kidogo na wana ccm wenzangu juu ya Demokrasia ya vyama vingi.

Mchango wangu wa mawazo.
MR KUSHOKA ana mawazo and as kijana na chama you have to accept kama ulivo uliza reforms zipi naomba ni highlit some of the areas.
(1) Mnachanga moto ya ku ainisha vipaumbele vyenu kivipi kama chama cha kisiasa at the end of the day if you dont have reach nzuri hamuwezi kufanikiwa,Chadema Mna mapungufu ya availability yenu kwa wananchi,nikiwa kwetu kijijini i have to travel all most 185km nikutane na ofisi ya chadema while ccm tupo ktk kila kata,kijiji wilaya wakati nye ur not there.
(2) Wangwe had a point ingawa kama chama hamuwezi kukubali kwa statistic za uchaguzi wa 2005 wilaya Tarime mlipata votes nyingi kuliko hata HAI but uwakilishi wa special seats haupo hoja iliyopo ni kua mnachagua kutokana na mchango wa watu husika na chakua hili neno from wangwe i happen to talk to him kua KATIBA inaelekeza kua watateuliwa kwa kuangalia mchango wa mtu,i think si sahihi special seats ziangalie number of Votes na compitence ili muweze kuwapa moyo hao walio wapa kura.
(3)Reforms chadema inatakiwa iangalie kutokana na uchaguzi wenu wa juzi wa kumchagua Vice chair mapungufu ya kiutendaji,kikanuni,kiitikadi yalijitokeza hiyo iwe learning point.

Kwahiyo wafikieni watu kwa kua na Network nchi nzima ofisi ziwepo publications ziwepo operation ziwepo na jaribuni kua more pro active kwani leo naona kabisa kile mlichopata i mean viti vya ubunge kuna majimbo mnapoteza bcs wabunge wenu wameshindwa kuwasaidia wananchi wao Exept SLAA, But Zito Wangwe na Arif (Mpanda) they have not deliverd as per expectation eg watu wa jimbo la zito wanapoteza imani.Nachtaka kuonyesha hapa ni kua Focused.

Upande wa pili najua sisi kama CCM ndo watawala ni jukumu letu kusaidia kukua kwa vyama bcs changa moto mnazotupa it helps in the process ya policy making kwahiyo uwepo wenu ni muhimu kwa ustawi wa jamii ila msipinge kila kitu.Ila imani hii ni yangu si ya chama.

Asante

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

NB;Usije ukabadili kauli mbiu yetu as u did last time kudai KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI nilianza kuhoji ur level of thinking.
 
Mtanzania

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba siasa lazima zikope baadhi ya mambo toka katika sayansi ya biashara; na political marketing is a new concept that is evolving worldwide- just as it is for marketing of products and services, politicians have to see how they brand their political products and services; their policies etc. Positioning, fragmentation etc are all applicable in this regard.

Lakini kama ilivyo katika biashara; si kila wakati ofisi kuu ama mahali ambapo bidhaa zinazaliwashwa wanakwenda kuuza bidhaa mpaka vijijini- ni wazi wanakwenda katika ziara mbalimbali za promotion kubwa kubwa. Lakini all year round, marketing inaendelea kupitia channels mbalimbali, ikiwemo bidhaa zenyewe kujiuza kupitia loyal customers na hata kujiuza kupitia mawakala.

Hata kwa vyama vya siasa- lazima wale loyal members walioko vijijini kama walivyo loyal customers wazitafute na kuzitumia bidhaa zao wazipendazo, ndio maana sishangai mtu wa kijijini akifuatilia kwa makini viongozi wake wa kitaifa wanatoa misimamo gani katika masuala fulani fulani hata kama ni kupitia redio ya kijiji.

Lakini pia kuna agents wa kuuza political product, tena mara nyingi huzi-customize kukidhi mazingira ya eneo lao. Hawa ni viongozi wa CHADEMA wa ngazi husika, issue za kiwalaya zinapaswa zizungumzwe na viongozi wa wilaya wa chama, wananchi wakinyanyaswa ngazi ya kata natarajia watetezi wao wa kwanza wawe ni viongozi wa chama wa ngazi yao. Wakishindwa ndio lipande juu zaidi. Kuna maeneo mengi ambayo viongozi wa CHADEMA ngazi husika wanawatetea wananchi bila kusubiri mpaka Mbowe afanye ziara; juzi juzi umeona maandamano ya wananchi wa Kigoma yaliyoandaliwa na waCHADEMA wenyewe wa huko, bila kusubiri Slaa au Zitto wafanye ziara. Mambo kama haya yanaendelea pia Tarime ambapo all politics is local, kule watu wanashindana na Barrick kupata haki zao bila kusubiri kamati ya Bomani itatoka na nini. Changamoto ni kufanya kila eneo katika nchi yetu waielewe falsafa ya 'people's power' , nguvu ya umma na kukuchukua hatua za kuwawajibisha viongozi wa ngazi zao, kupinga ufisadi katika maeneo yao na kutetea rasilimali zinazowazunguka.

Na kwa kweli, siasa hizi si za wakati wa uchaguzi pekee- ni siasa za wakati watu.

Naelewa ukisemacho, tunafanya katika maeneo inapowezekana- kufanya kila kijiji yataka muda wa kuendelea kujenga chama taasisi katika ngazi zote. Na suala hili linahitaji kuungwa mkono na wote wapenda mabadiliko, kuanzia Februari 2008 tunaanza uchaguzi wa chama nchi nzima tukianzia Msingi, Tawi, Kata na kuendelea mpaka Taifa. Ni lazima kila mpenda demokrasia na maendeleo ahakikishe katika eneo lake analotoka, chama mbadala kinakuwa na uongozi thabiti wenye kuweza kuwatetea wananchi na kuwa kama serikali mbadala katika eneo lake la kiutawala hata kama ni kijiji au mtaa. Ni kwa kufanya hivi ndipo tutajenga oganizesheni ya ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2008 na hatimaye uchaguzi mkuu 2010. Inawezekana, timiza wajibu wako.

JJ
 
Ndugu zangu asalaamu aleykum,

Nawapongeza sana hawa vijana na wazee wa CHADEMA kwa kazi nzuri wanayoifanya na kwa kweli tunapaswa wote kwa ujumla wetu tuweze kuwunga mkono kwani ni watu ambao wameonyesha nia ya kutaka kuutenganisha uongo na siasa kwani wamekuja na facts.

Napenda kumpongeza sana kijana Mnyika na wenzake na huwa namfahamu kijana Mrema John ambaye alikuwa ni mwanafunzi wangu pale mlimani wakati wa semina za PS political science alikuwa na changamoto nyingi sana na huwa alikuwa anaonekna ni kijna mwenye msimamo usioyumba.N pia namkumbuka kijana huyu wakati akiwa ni katibu mkuu wa DARUSO pale mlimani hakukuwahi kutokea jaribio la kuwapindua kama tulivyozoea kwa wale tuliowahi kupitia mlimani UDSM, naambiwa pia kijana huyu yupo CHADEMA na kwa sasa ndio mkurugenzi wa masuala ya Bunge la jamhuri na huwa anashiriki kupika hoja za wabunge wa CHADEMA na kwa kweli kwa mwaka huu kama ni kweli alishiriki basi sote tumeweza kuona changamoto kubwa za wabunge hao ndani ya Bunge, namtakia kheri na kama yupo hapa tafadhali wasiliana nami kwenye PM yangu kuna mambo nataka kujadili naye.

Naona kwa sasa suala la kufanya reforms labda tuliache hadi watakapomaliza uchaguzi wao kama mnyika alivyosema kuwa unaanza mwakani then tuweze kuangalia mfumo wao mpya wa kiutawala unavyofanya kazi na naamini walifanya research ya kutosha kabla ya kuamua kubadili katiba yao .
 
MNYIKA

Napenda kwanza kuweka wazi ITIKADI yangu. Mimi ni Mwana CCM.
Nimevutiwa na Mada yenu hii ya chadema must reform, As mwana ccm naamini ktk siasa za ushindani thats why nimeamua kuchangia ktk hili kama tulivokutana ktk mjadala wetu ulopita last week abt jk kuvunja baraza la mawaziri.

Mada hii imenbivutia nikiwa kama mtanzania mwenye itikadi tofauti kidogo na wana ccm wenzangu juu ya Demokrasia ya vyama vingi.

Mchango wangu wa mawazo.
MR KUSHOKA ana mawazo and as kijana na chama you have to accept kama ulivo uliza reforms zipi naomba ni highlit some of the areas.
(1) Mnachanga moto ya ku ainisha vipaumbele vyenu kivipi kama chama cha kisiasa at the end of the day if you dont have reach nzuri hamuwezi kufanikiwa,Chadema Mna mapungufu ya availability yenu kwa wananchi,nikiwa kwetu kijijini i have to travel all most 185km nikutane na ofisi ya chadema while ccm tupo ktk kila kata,kijiji wilaya wakati nye ur not there.
(2) Wangwe had a point ingawa kama chama hamuwezi kukubali kwa statistic za uchaguzi wa 2005 wilaya Tarime mlipata votes nyingi kuliko hata HAI but uwakilishi wa special seats haupo hoja iliyopo ni kua mnachagua kutokana na mchango wa watu husika na chakua hili neno from wangwe i happen to talk to him kua KATIBA inaelekeza kua watateuliwa kwa kuangalia mchango wa mtu,i think si sahihi special seats ziangalie number of Votes na compitence ili muweze kuwapa moyo hao walio wapa kura.
(3)Reforms chadema inatakiwa iangalie kutokana na uchaguzi wenu wa juzi wa kumchagua Vice chair mapungufu ya kiutendaji,kikanuni,kiitikadi yalijitokeza hiyo iwe learning point.

Kwahiyo wafikieni watu kwa kua na Network nchi nzima ofisi ziwepo publications ziwepo operation ziwepo na jaribuni kua more pro active kwani leo naona kabisa kile mlichopata i mean viti vya ubunge kuna majimbo mnapoteza bcs wabunge wenu wameshindwa kuwasaidia wananchi wao Exept SLAA, But Zito Wangwe na Arif (Mpanda) they have not deliverd as per expectation eg watu wa jimbo la zito wanapoteza imani.Nachtaka kuonyesha hapa ni kua Focused.

Upande wa pili najua sisi kama CCM ndo watawala ni jukumu letu kusaidia kukua kwa vyama bcs changa moto mnazotupa it helps in the process ya policy making kwahiyo uwepo wenu ni muhimu kwa ustawi wa jamii ila msipinge kila kitu.Ila imani hii ni yangu si ya chama.

Asante

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

NB;Usije ukabadili kauli mbiu yetu as u did last time kudai KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI nilianza kuhoji ur level of thinking.

Mtoto wa Mkulima

BTW: Unaweza kutueleza kwa nini uko CCM? Ni maboresho gani yamefanyika CCM ambayo yamekuvutia mpaka uko huko badala ya CHADEMA? Unadhani, kati ya CCM na CHADEMA ni chama gani ambacho kinahitaji mchango wako wa mawazo wa kukiboresha?

Nirudi sasa kwenye maswali yako:

1. Kuna ofisi za CCM kila kijiji au kata kwa kuwa maeno mengi CCM ilipora viwanja na majengo vilivyopatikana na wananchi wote kabla mfumo wa vyama vingi kuanza. Tungejua uwezo wenu wa kujenga hayo maofisi kama mwaka 1992 mngerudisha majengo na viwanja vyote serikali vyama vyote vikaanza sawa. Kwa hiyo, hamuwezi kujisifia kwa kupora mali za umma na kuziita mali za chama. Pia unajua kwamba ofisi zenu za ngazi ya chini nyingine zimejengwa kwa nguvu ya chama dola- kwa maana ya wafanyabiashara kulazimika kuchangia na viongozi wa serikali kuchangia wakati wa ziara zao. Kwa hiyo hapo si suala la kujisifia sana, chama chochote kikiamua kutumia vibaya madaraka yake wakati kikiwa tawala kinaweza kufanya hivyo. Katika hizi hela, zipo pia hela za mafisadi zinazochotwa katika ngazi mbalimbali lakini wakishachangia wanapigiwa makofi. Na wakishasema wamejenga ofisi eneo fulani, ni takrima ya nguvu na hapo ndipo mnapoanza kusitasita kuwachukulia hatua. Ni wazi yapo maeneo machache sana ambayo wananchama wa CCM wamejenga kwa nguvu zao wenyewe, ila ni machache. Ukweli ni kwamba pamoja na CCM kupokea ruzuku ya milioni 60 kwa siku, inakaribia milioni 2000 kwa mwezi ukichanganya ruzuku ya ubunge na udiwani kwa mwezi zinakwenda CCM, na hizi ni fedha za walipa kodi. Pamoja na mafedha yote hayo bado ni aghalabu kwa mgawo huo kupelekwa kwenye kata au matawi. Kwa hiyo nashangaa kama mtu kama wewe wa CCM ukisema CHADEMA ipeleke igawe ruzuku yake ya milioni 60 kwa mwezi kwa kila kijiji nchini. Wewe unajua kwamba nchi hii ina zaidi ya vijiji elfu 10,-kwa ruzuku ya CHADEMA hata ikiacha kufanya kazi zote za kisiasa- ziara, kusambaza bendera na kadi nchi nzima, kutoa mafunzo kwa viongozi nk- zote kabisa zikichwa na fedha kugawanya bado kila kijiji kitapata at most elfu 6 kwa mwezi. Sasa hapo kazi itafanyika kweli? Ndio maana chama kinapaswa kuwa cha wanachama- ruzuku inachangia tu, pale inapoweza kulipia ofisi inafanya hivyo kwa mujibu wa maamuzi ya pamoja ya vikao. Pale inaposhindikana, nguvu ya umma lazima ifanya kazi. Ukweli ni kuwa wanachama 1000 tu katika kijiji wakilipa ada ya mwezi ya around shilingi 100, hii ni sawa na laki moja; je kipi bora kuweka mikakati ya kujipatia laki 1 kwa kutengenezewa kadi, bendera, mafunzo ya viongozi, ziara za hamasa nk au kusubiri ruzuku ya mwisho wa mwezi ya shilingi elfu 6? You talk about priorities!

2. Uwe unasoma, nimeweka hapa katiba ya CHADEMA- hakuna kipengele chochote kinachosema hayo uliyoyasema! Na suala la viti maalumu nimelifafanua hapa sasa kwenye thread mbalimbali- http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=113490#post113490, hii imehusa kidogo tu. Lakini nimetoa maelezo maeneo mbalimbali. Soma kwanza urejee na maswali mahususi. Ila nimeweka bayana kwamba viti maalumu majina hupelekwa kabla ya uchaguzi(hii ni kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na chama chako CCM ambayo mimi sikubaliana nayo kwa kweli), kwa hiyo majina yalipelekwa huku tukiangalia matokeo ya 2000; hakuna ambaye angeweza kubashiri kama Mara, au Rukwa chama kingefanya vizuri kama kilivyofanya. Na niliweka bayana kwamba kama sheria ingeruhusu uteuzi baada ya uchaguzi ni wazi Mara au Rukwa lazima angetoka mbunge wa viti maalumu. Na ni sheria hii hii iliyotungwa na serikali ya chama chako CCM ndio iliyofanya UVCCM walalamike kwamba kwanini nafasi ya marehemu Amina Chifupa haikuzibwa na Mbunge toka UVCCM badala yake ametoka kwingine? Lakini ni sheria ndio iliyowafanya tume watangaze toka kwenye orodha waliyopatiwa kabla ya uchaguzi! Na orodha ni ya chama kwa ujumla haina makundi maalumu. Ndio maana nasema Sheria hii ibadilishwe twende kwenye PR pana, kwa hiyo kama ni reforms kuhusu hili. Waambie CCM waanzishe mchakato.

Nashukuru, tuendelee na mjadala

JJ
 
Mtanzania

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba siasa lazima zikope baadhi ya mambo toka katika sayansi ya biashara; na political marketing is a new concept that is evolving worldwide- just as it is for marketing of products and services, politicians have to see how they brand their political products and services; their policies etc. Positioning, fragmentation etc are all applicable in this regard.

Lakini kama ilivyo katika biashara; si kila wakati ofisi kuu ama mahali ambapo bidhaa zinazaliwashwa wanakwenda kuuza bidhaa mpaka vijijini- ni wazi wanakwenda katika ziara mbalimbali za promotion kubwa kubwa. Lakini all year round, marketing inaendelea kupitia channels mbalimbali, ikiwemo bidhaa zenyewe kujiuza kupitia loyal customers na hata kujiuza kupitia mawakala.

Hata kwa vyama vya siasa- lazima wale loyal members walioko vijijini kama walivyo loyal customers wazitafute na kuzitumia bidhaa zao wazipendazo, ndio maana sishangai mtu wa kijijini akifuatilia kwa makini viongozi wake wa kitaifa wanatoa misimamo gani katika masuala fulani fulani hata kama ni kupitia redio ya kijiji.

Lakini pia kuna agents wa kuuza political product, tena mara nyingi huzi-customize kukidhi mazingira ya eneo lao. Hawa ni viongozi wa CHADEMA wa ngazi husika, issue za kiwalaya zinapaswa zizungumzwe na viongozi wa wilaya wa chama, wananchi wakinyanyaswa ngazi ya kata natarajia watetezi wao wa kwanza wawe ni viongozi wa chama wa ngazi yao. Wakishindwa ndio lipande juu zaidi. Kuna maeneo mengi ambayo viongozi wa CHADEMA ngazi husika wanawatetea wananchi bila kusubiri mpaka Mbowe afanye ziara; juzi juzi umeona maandamano ya wananchi wa Kigoma yaliyoandaliwa na waCHADEMA wenyewe wa huko, bila kusubiri Slaa au Zitto wafanye ziara. Mambo kama haya yanaendelea pia Tarime ambapo all politics is local, kule watu wanashindana na Barrick kupata haki zao bila kusubiri kamati ya Bomani itatoka na nini. Changamoto ni kufanya kila eneo katika nchi yetu waielewe falsafa ya 'people's power' , nguvu ya umma na kukuchukua hatua za kuwawajibisha viongozi wa ngazi zao, kupinga ufisadi katika maeneo yao na kutetea rasilimali zinazowazunguka.

Na kwa kweli, siasa hizi si za wakati wa uchaguzi pekee- ni siasa za wakati watu.

Naelewa ukisemacho, tunafanya katika maeneo inapowezekana- kufanya kila kijiji yataka muda wa kuendelea kujenga chama taasisi katika ngazi zote. Na suala hili linahitaji kuungwa mkono na wote wapenda mabadiliko, kuanzia Februari 2008 tunaanza uchaguzi wa chama nchi nzima tukianzia Msingi, Tawi, Kata na kuendelea mpaka Taifa. Ni lazima kila mpenda demokrasia na maendeleo ahakikishe katika eneo lake analotoka, chama mbadala kinakuwa na uongozi thabiti wenye kuweza kuwatetea wananchi na kuwa kama serikali mbadala katika eneo lake la kiutawala hata kama ni kijiji au mtaa. Ni kwa kufanya hivi ndipo tutajenga oganizesheni ya ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2008 na hatimaye uchaguzi mkuu 2010. Inawezekana, timiza wajibu wako.

JJ

Mnyika,

Hoja yangu ilikuwa maoni yangu na ushauri wangu kwa kuangalia kule wilayani ambako wengine tunatoka.

Kama mnaona mna njia zingine za kuwafikishia wananchi ujumbe wenu ni sawa tu na mafanikio mema.

Huenda tukagongana kwenye kampeni 2010 hata kama tutakuwa pande tofauti.
 
Nashukuru.

Maoni yako uliyotoa nayo yana umuhimu wake. Ndio maana unaona viongozi wetu wa kitaifa wanafanya ziara maeneo mbalimbali, ningefahamu wilaya yako ningepata picha kamili ya nyuma ya swali lao.

Kuhusu uchaguzi wa mitaa, mkono uliteleza kidogo- ni mwaka 2009; mwaka 2008 ni uchaguzi mkuu wa CHADEMA.

Nakutakia heri katika maandalizi yako ya kampeni za 2010.

JJ
 
Mjadala huu hakika umeenda shule, damn- nachota mengi sana hapa kama vile niko darasani.
J.J. Mnyika, tutawasiliana mkuu naona kazi ipo na mada hii itafungua milango mingi sana.
 
Mkandara,

Karibu bwana, twaelimishana. Twatafuka njia zote kuleta mageuzi ya kweli ka Taifa letu.
 
Mnyika kwanza nikupongeze kwa kasi nzuri uliyoionesha pale Ubungo mwaka 2005, kwa kweli pamoja na mzee Keenja kushinda cha moto alikiona na ninaamini kama mwaka 2010 kama utajitosa kupambania tena jimbo, hakika uwezekano ulio mkubwa utajitwalia kiti mwanangu.

Nionanvyo mimi watanzania wengi wameamka kisiasa japo chini kwa chini. wanachotafuta haswa ni mwana mageuzi gani wamwamini kiasi cha kumpa ruhusa ya kuingia jumba jeupe la magogoni kwa miaka 5 kuanzia 2010. Bado Upinzani haujatoa mtu ambae kwa kweli atauzika 2010. CCM walimuandaa JK wao kwa takribani miaka kumi, ilipofika uchaguzi wala hawakupata shida. Chadema mgombea wenu Bwana Mbowe aliibukia from no where japo alileta mtikiso na changamoto kwa JK lakini lakini akawa kama mwanafunzi aliyeanza kusoma mwezi mmoja kabla ya mtihani.

Chadema mnamuandaa nani kushindana na Kikwete 2010? au ndo zile zile za 2005 za kutuacha dilema hadi mwezi mmoja kufikia uchaguzi? Mimi sioni vibaya kama kuna technic za kisisiem zilizo nzuri zikaigwa. kwa mfano wao tayari wagombea wao wengi hivi sasa wameshaanza kujipanga na mikakati mingi ya 2010 imeshaanza, na wameshaanza kujishaua kwa wananchi ki aina.

Viogozi ama office za chadema za ngazi za chini haziko karibu na wananchi. Msipoweza kupajenga huku chini kwa wasioijua JF wala kuwa na uwezo hata wa kupata nauli ya daladala piga ua hamtakaa muiongoze hii chini haijalishi mko wazuri au mna uchungu na mapenzi kiasi gani kwa nchi yetu.

2005 hamkuwepo kwenye majimbo mengi hususani zanzibar. hata kampeni zenu za urais sina hakika kama zilifika zanzibar, tuelewe nini hapo? Maana kama nguvu yenu inaelekezwa upande mmoja tu wa nchi kuna hatari kuchukua kwenu chini kunaweza kutia chachu za kuvunjika Muungano.

Sera ya chadema ni Serikali ya majimbo, Je Zanzibar inaichukulia kama jimbo?

Demokrasia ndani ya chama chenu:

Wakati mwingine kwa mtu wa kawaida ni ngumu sana kutofautisha demokrasia na mgogoro, haswa inapotokea demokrasia hiyo inapokuwa imakaa ki malumbano zaidi. Kuonesha tofauti zenu kupitia vyombo vya habari hilo ni kosa kubwa ambalo iko siku CHADEMA mtalijutia. si watu wote tunaoamini demokrasia za malumbano kama yenu. sana sana tunaona kama kila mmoja wenu analinda maslai binafsi. Tafuteni utaratibu mzuri wa jinsi ya wanachama kucheua yanayowakera bila kufaidisha wapinzani wenu. Ni aibu viongozi wakubwa kama Wangwe na Zitto kulumbana au kupingana magazetini.

Bwana Mnyika bado mna safari ndefu. Nasikitika kwa watu alioanza kuaminika kama Zitto mapema hivi wanaanza kutangaza kuwa hawana mda mrefu kwa utumishi kwa wananchi kisiasa. Kama wewe mwenyewe ulivyosema muda si mrefu hatutakuona tena si ajabu ikawa jumla jumla. hatuna reliable people from you guyz. siasa haifai kubeep ukiingia ingia full. Mbona viongozi wengi wa ccm wanasoma na bado wapo ulingoni? inakuwaje Elimu zenu hadi na jukwaa ya siasa inabidi muweke pause?

Demokrasia Daima kaka, Sorry kama nimeteleza mahala.
 
Endelea,

Tatizo la Chadema na upinzani si kukosa kufahamika, bali ni jinsi gani wanavyotaka kufahamika kwa nguvu.

Nilipoanzisha mjadala wa Focus 2010, nilipinga hii tabia ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari kutafuta umaarufu. Sana sana wananchi watakwambia tunaijua Chadema kwa ajili ya Zitto kaleta Buzwagi na Slaa na Mafisadi.

Ukiuliza jee sera za Chadema ni nini? hakuna jibu kutoka kwa mwananchi wa kawaida.

CCM pamoja na kuwa mabepari na manyang'au, ukienda vijijini sera ni "Ujamaa na Kujitegemea" si mkiki mkiki kati ya Salim, Mwandosya na Kikwete au kuwa CCM ndio walitutangazia hadharani ya Chupini ya Mbowe na Slaa.

Mwanakijiji kaleta mada nzuri sana inayoonyesha mapungufu ya wakuu wa Chadema (Chadema kama chama) kwa kupenda kukimbilia magazeti. Sasa wanaonekana kama majuha na wajinga. Jee, ikifika 2010 na upuuzi kama huu, unafikiri ni nani atashinda Tsunami?
 
Mtoto wa Mkulima

BTW: Unaweza kutueleza kwa nini uko CCM? Ni maboresho gani yamefanyika CCM ambayo yamekuvutia mpaka uko huko badala ya CHADEMA? Unadhani, kati ya CCM na CHADEMA ni chama gani ambacho kinahitaji mchango wako wa mawazo wa kukiboresha?

Nirudi sasa kwenye maswali yako:

1. Kuna ofisi za CCM kila kijiji au kata kwa kuwa maeno mengi CCM ilipora viwanja na majengo vilivyopatikana na wananchi wote kabla mfumo wa vyama vingi kuanza. Tungejua uwezo wenu wa kujenga hayo maofisi kama mwaka 1992 mngerudisha majengo na viwanja vyote serikali vyama vyote vikaanza sawa. Kwa hiyo, hamuwezi kujisifia kwa kupora mali za umma na kuziita mali za chama. Pia unajua kwamba ofisi zenu za ngazi ya chini nyingine zimejengwa kwa nguvu ya chama dola- kwa maana ya wafanyabiashara kulazimika kuchangia na viongozi wa serikali kuchangia wakati wa ziara zao. Kwa hiyo hapo si suala la kujisifia sana, chama chochote kikiamua kutumia vibaya madaraka yake wakati kikiwa tawala kinaweza kufanya hivyo. Katika hizi hela, zipo pia hela za mafisadi zinazochotwa katika ngazi mbalimbali lakini wakishachangia wanapigiwa makofi. Na wakishasema wamejenga ofisi eneo fulani, ni takrima ya nguvu na hapo ndipo mnapoanza kusitasita kuwachukulia hatua. Ni wazi yapo maeneo machache sana ambayo wananchama wa CCM wamejenga kwa nguvu zao wenyewe, ila ni machache. Ukweli ni kwamba pamoja na CCM kupokea ruzuku ya milioni 60 kwa siku, inakaribia milioni 2000 kwa mwezi ukichanganya ruzuku ya ubunge na udiwani kwa mwezi zinakwenda CCM, na hizi ni fedha za walipa kodi. Pamoja na mafedha yote hayo bado ni aghalabu kwa mgawo huo kupelekwa kwenye kata au matawi. Kwa hiyo nashangaa kama mtu kama wewe wa CCM ukisema CHADEMA ipeleke igawe ruzuku yake ya milioni 60 kwa mwezi kwa kila kijiji nchini. Wewe unajua kwamba nchi hii ina zaidi ya vijiji elfu 10,-kwa ruzuku ya CHADEMA hata ikiacha kufanya kazi zote za kisiasa- ziara, kusambaza bendera na kadi nchi nzima, kutoa mafunzo kwa viongozi nk- zote kabisa zikichwa na fedha kugawanya bado kila kijiji kitapata at most elfu 6 kwa mwezi. Sasa hapo kazi itafanyika kweli? Ndio maana chama kinapaswa kuwa cha wanachama- ruzuku inachangia tu, pale inapoweza kulipia ofisi inafanya hivyo kwa mujibu wa maamuzi ya pamoja ya vikao. Pale inaposhindikana, nguvu ya umma lazima ifanya kazi. Ukweli ni kuwa wanachama 1000 tu katika kijiji wakilipa ada ya mwezi ya around shilingi 100, hii ni sawa na laki moja; je kipi bora kuweka mikakati ya kujipatia laki 1 kwa kutengenezewa kadi, bendera, mafunzo ya viongozi, ziara za hamasa nk au kusubiri ruzuku ya mwisho wa mwezi ya shilingi elfu 6? You talk about priorities!

2. Uwe unasoma, nimeweka hapa katiba ya CHADEMA- hakuna kipengele chochote kinachosema hayo uliyoyasema! Na suala la viti maalumu nimelifafanua hapa sasa kwenye thread mbalimbali- http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=113490#post113490, hii imehusa kidogo tu. Lakini nimetoa maelezo maeneo mbalimbali. Soma kwanza urejee na maswali mahususi. Ila nimeweka bayana kwamba viti maalumu majina hupelekwa kabla ya uchaguzi(hii ni kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na chama chako CCM ambayo mimi sikubaliana nayo kwa kweli), kwa hiyo majina yalipelekwa huku tukiangalia matokeo ya 2000; hakuna ambaye angeweza kubashiri kama Mara, au Rukwa chama kingefanya vizuri kama kilivyofanya. Na niliweka bayana kwamba kama sheria ingeruhusu uteuzi baada ya uchaguzi ni wazi Mara au Rukwa lazima angetoka mbunge wa viti maalumu. Na ni sheria hii hii iliyotungwa na serikali ya chama chako CCM ndio iliyofanya UVCCM walalamike kwamba kwanini nafasi ya marehemu Amina Chifupa haikuzibwa na Mbunge toka UVCCM badala yake ametoka kwingine? Lakini ni sheria ndio iliyowafanya tume watangaze toka kwenye orodha waliyopatiwa kabla ya uchaguzi! Na orodha ni ya chama kwa ujumla haina makundi maalumu. Ndio maana nasema Sheria hii ibadilishwe twende kwenye PR pana, kwa hiyo kama ni reforms kuhusu hili. Waambie CCM waanzishe mchakato.

Nashukuru, tuendelee na mjadala

JJ
MNYIKA

Kwanza nianze na salaam ,Pili nisingependa kujadili maboresho ya ccm bcs si hoja yetu hapa lakini uhuru wa kujadili haya ni matokeo ya ccm.

Nikirejea ktk mada Hoja yako ya pili kua majina ya viti maalum hupelekwa kabla ya uchaguzi naamini ni uchaguzi mkuu ni si wandani ya chama,hapa ndipo palipo na tatizo manyapataje,yanateuliwa vipi,au manawachukua majina ya magirlfreand zenu na kupeleka (joke lakini in ukweli ingawa wako hayupo kati ya wabunge wa viti maalum)
Tatizo ni hilo tu utaratibu wenu hauruhusu mfumo amboa utaonyesha na kupelekea maamuzi ya wengi yachukue mkondo wake, 2005 unless unakua unamatatizo maaeneo ambayo mlikua mpate kura nying yalifahamika eg MBOGORO Songea,Chacha Tarime,Kigoma,Mpanda,etc sasa tatizo si sheria bali ni kanuni zenu for the First time chadema imechagua kiongozi kwa kufata mfumo wa kuwapa sauti watu wake ni uchaguzi wa WANGWE ambao vigogo wenu hamkumtaka.

About hoja yako ya kwanza imejaa hisia tupu ndugu yangu bcs sijaona kosa mwanachama au kiongozi kuchangia ujenzi wa ofisi naamini hata nyie mnafanya hivo kwahiyo si hoja,ila ni ngejibu kua hoja ya ccm kupata ruzuku kubwa nimatokeo ya kura nyingi tulizopata kutoka kwa wananchi,Hoja kua hatupeleki pesa ktk matawi kuanzia october 2007 tunapeleka pesa ktk kata,matawi na tumeanza kuwapa posho wenyeviti wetu wa mikoa,wilaya,kata,matawi together with makatibu wa uenezi na itikadi kwahiyo dont comment when u dont have Facts.

Hoja kua tumepora mali nyingi i belive si kweli but kama ni kwelu why msifate mkondo wa sheria ku claim mali hizo zirudi kwa serekali nyie kama chama instead ya kuhoji vitu visivikua na impact kwetu wananchi i think kama chama cha kisiasa piteni na helkopta tena mtuambie mali zilizoporwa na ccm ili tuwaunge mkono,ila tangu 1992 unataka kujua majengo tulojenga,nakupa machache ktk miji mikuu bcs vijijini hamfiki,SINGIDA jengo gorofa 3,HAI jengo gorofa 2,Tabora wilaya ya Nzg,Jengo linaendelea la gorofa 1,Kishapu jengo gorofa moja linaendelea,etc si kweli kua hatuna majengo labda huna taarifa.

Ungesoma nilicho malizia mara yakwanza kua kanuni,taratibu zenu zina matatizo na hapa umetuonyesha mapungufu ambayo unataka tukubali kua ni ya kisheria kua majina ya viti maalumu hupelekwa kabla ya uchaguzi mkuu lakini umesahau kua majina hayo yanapatikana vipi mpaka kufikishwa ktk tume ya uchaguzi ni kinanani wanachuja,pendekeza na mnapo yapeleka yamepatikana vipi hapa ndipo kwenye tatizo.

Asante KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Majina ya Viti Maalumu ya CCM mlipeleka lini Tume ya Uchaguzi? Wakati mnayapeleka mlikuwa mnajua matokeo ya uchaguzi 2005? Umewahi kusoma sheria ya uchaguzi inasemaje kuhusu uteuzi wa wabunge wa viti maalumu na muda wa kuwasilisha majina?

He, toka CCM ianze kupata ruzuku mwaka 1995 ndio mmeanza kupeleka ruzuku Oktoba 2007 kwenye kata na matawi, miaka yote hiyo mlikuwa mkipeleka wapi fedha hizo?

Unakumbukuka ni wakina nani walichagia ofisi ya CCM mamilioni ya shilingi kule Zanzibar juzi juzi? Hebu tupe majina na kiasi maana walitolewa gazetini. Si unajua jinsi wakina Manji walivyokimbelembele kununua maofisi ya CCM?

Heeh, yani miaka yote hiyo mnajenga majengo machache hivyo? Lakini mbona CCM inamiliki majengo mpaka kwetu Jang'ombe? Mliyapata wapi kama si kupora mali za ASP na TANU tulizochuma watu wote na kuziweka kwa CCM?

Hebu rudisheni mali zetu huko; ama sivyo tutaendelea kuwasuta wapenda dezo dezo

Asha
 
ASHA

Hapa hatusutani this forum ya kujadiliana,abt kua kina nani wananchangia si hoja bcs as far as ni mwana ccm na analipa ada na ni mtu safi ( hata manji ni safi bcs hajawa convicted na mahakama or hao mnao waita mafisadi) we dont have problem na mchango wake.

Hoja ya kua ni office chache dada yangu nadhani huku elewa nilichosema i said baadhi sijui kikwenu ningekuelewesha,Pia ustadha hujanielewa hoja yangu si lini tumepeleka hoja yangu ni namna gani wanapatikana sisi hata tukipeleka leo mfumo wetu unahusisha watu wengi kufanya maamuzi hatuchagui wale wamakao makuu tu.

Abt majengo ya ASP na TANU hujui muungano wao ndo ulioform CCM?

Nadhani unasahau mada yetu,ila kua sasa hivi ndo tumeanza kupeleka tulikua na vipau mbele vingine.

Kwahiyo ni vizuri isilete TAARABU humu ndani
 
Back
Top Bottom