'Ripoti' ya Mziray na Mabadiliko ya Chadema kuelekea 2010

kuna watu wanachangia, na wakati mwingine natoa mfukoni mwangu mwenyewe. Halafu huo mchango wenu wa kutaka kuchangia ili nifanye kitu fulani itakuwa ni kuninunua nitimize malengo yenu.

Kama unataka kuchangia, wewe changia tu. Kuna watu kadhaa wanachangia na hata mara moja hawajawahi kuniambia nani nimhoji au nisimhoji.

Tatizo ni kuwa huwezi kuchangia.
 
MBOWE, WANGWE NA SIASA ZA KIHUNI CHADEMA

Mtanzania Julai 6, 2008

Na Mzee Yusuf Halimoja

Nianze kwa kusema kweli.
Nimetumia muda mrefu kufikiria kichwa cha habari cha makala yangu kiwe kipi. Niliamua shoka kuliita shoka. Hakuna kuficha. Hakuna cha kuzungusha. CHADEMA INAONGOZWA KIHUNI.

Blah blaha.....

.

Hivi haka kazee si ndio kalikokuwa kakiuza habari na majungu kuhus CHADEMA (kabla ya kufukuzwa) katika lile gazeti la makuwadi wa USALAMA linaloitwa HOJA....Gazeti linalo endeshwa na funds za serikali na hata kusambazwa na magari ya UMMA......

Tanzanianjema
 
WAPINZANI WANAJIMALIZA WENYEWE KUTOKANA NA HISTORIA YA MIGOGORO YAO

Nimekuwa nikifuatilia kwa makini juu ya wanasiasa wetu, hususan viongozi wa vyama vya upinzani na migogoro ya mara kwa mara ya ndani ya vyama hivyo.

Hivi karibuni umezuka mgogoro mkubwa kwenye kambi ya upinzani ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Kamati Kuu ya chama hicho, imemuondoa madarakani aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake, CHACHA WANGWE, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime.

Uongozi wa CHADEMA katika kufikia hatua hiyo, unadai kwamba WANGWE ameondolewa kutokana na makosa kadhaa, ikiwemo kile wanachokiita “kutumiwa na chama tawala cha CCM kuhujumu chama chao ili kukigawa chama na pia kueneza madai ya uwongo dhidi ya uongozi wa CHADEMA.

Kwa upande wake WANGWE amedai yeye hakubaliani na uamuzi huo, na kwamba kutokana na hilo, atakata rufaa kwenye Baraza Kuu na hata Mkutano Mkuu wa chama hicho. Aidha, WANGWE amekaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba atalifikisha suala hilo mahakamani, na kwa wanachama wa CHADEMA kupitia mikutano atakayoifanya nchi nzima.

Hiyo ni harufu mbaya inayoashiria kuwapo kwa mgogoro mkubwa wa kisiasa ndani ya CHADEMA, mgogoro ambao kama hautadhibitiwa, unaweza kukidhoofisha au hata kukisambaratisha kabisa chama hicho, kutokana na kila upande kukataa kushindwa na wala kukubali kufanya suluhu na upande mwingine.

Migogoro kama hiyo huko nyuma iliwahi kuvisambaratisha vyama vya NCCR – Mageuzi na TLP, kiasi cha kusababisha vipoteze wabunge wake wote, ikiwa ni pamoja na kukosa kura za wananchi. Hatujui CHADEMA itaishia wapi!!!!

Kwa mfano, NCCR – Mageuzi ilikuwa na viti 19 ndani ya Bunge mwaka 1995 – 2000 lakini kwa sasa chama hicho hakina hata mbunge mmoja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa upande wa TLP kilikuwa na wabunge 5 mwaka 2000 – 2005 lakini kwa sasa hakina hata mbunge mmoja. Aidha, Kura za vyama hivyo zimekuwa zikipungua kila uchaguzi mkuu unapofanyika.

Mwaka 1995, NCCR – Mageuzi kilipata asilimia 28 ya kura zote lakini mwaka 2005 kilipata asilimia 3.5 ya kura zote. Hali hii ya kudidimia kwa vyama hivyo imetokana na migogoro mikubwa iliyovikumba na ambayo bado inaendelea kuviandama, ikiwemo CHADEMA.

Utafiti uliofanywa na Taasisi binafsi ya Utawala Bora na Maendeleo nchini (CEGODETA),umeonyesha kwamba migogoro isiyokwisha ndani ya vyama vya upinzani inatokana na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:-

!!!!

Yaani wewe na akili yako ukachukua kile unachoitwa UTAFITi uliofanywa na hii NGO ya mikobani ya hao wazee wako kina NGAWAIYA walifilisika kisiasa na kiuchumi na kutaka watu wachukulie kama reference ya kuelewa hali ya demokrasia ya upinzani nchini....

Ujinga huu una mahala pake pamoja tu...katika kile kigazeti chenu cha HOJA za makuwadi wa ufisadi na labda RAI ya mafisadi kama sio MTANZANIA hovyohovyo au MAJIRA ya ufisadi....

Tanzanianjema
 
WanaJF,
Nilikuwa tu ndio nimemaliza kuyachapa haya majibu yangu kwa Kitila, nilipoona thread ya kifo cha wangwe. Nimeamua niiache kama ilivyo ili iwe kama kielelezo cha jinsi baadhi yetu tulivyomthamini sana marehemu Chacha Wangwe kama mwanamageuzi, licha ya mapungufu yake au hata wakati ilipoonekana yuko peke yake. Mwenyezi Mungu ailaze pema peponi roho yake.

KJ: Nina mambo matano ya kukwambia kuhusu maneno yako hapo juu na katika post zako zingine:

i) Ni wazi kuwa wewe husomi post za watu sawasawa na unapoandika kujibu hoja unaandika tu yale yaliyopo kichwani mwako bila kuzingatia alichosema yule unayemjibu. Kwa kukusaidia tena kuelewa nilichokisema kwenye post yangu ni kwamba kamati ya Mziray ilishindwa kuthibitisha madai ya kuwepo upendeleo katika ajira za wafanyakazi wa makao makuu na uteuzi wa wakurugenzi wa idara mbalimbali ndani ya chadema, na badala yake waliobua hisia mpya za ubaguzi wa kikabila na kidini. Hakuna mahala niliposema eti "hakuna upendeleo wowote uliotokea na ni coincedences tu zilizosababisha mgawanyo mbaya wa madaraka". Sasa unapoamua kujibu hoja za watu jibu hoja zao, sio kuibua hoja ambazo hazikuwepo. Inaonekana una kile wanasaikolojia wanaita self fulfilling prophecy-which is huge personality issue needing urgent attention!!

Mkuu Kitila,
Sio lazima mtu aseme exactly kama nilivyoandika, ila nimeangalia kwa ujumla wa yote uliyoandika ambapo inaonyesha wazi kabisa kuwa ulijaribu kutushawishi tuone kuwa hakuna upendeleo wowote uliotokea kwenye ajira (kwa mfano eti Mwakagenda alikataa ajira ya kuteuliwa, very difficult to believe) halafu eti kuwa replacement yake imekuwa tu by coincidence, Mrema akawa wa Kilimanjaro. Either huelewi unachoandika kwa vile na wewe ni kati ya ‘sort of the accused’ (Kilimanajaros), au unadhania wengine ni wajinga kutoelewa tafsiri ya maelezo yako.

ii) Nikutoe wasiwasi kuhusu kama ninamuunga mkono Mbowe au la. Kwanza nikwambie tu kwamba mimi sio miongoni mwa watu ambao huficha utashi wao kwa jambo ambalo wanaliamini. Nikikikubali na kukiamini kitu huwa sina uwezo wa kuficha hisia zangu na hiyo ni moja wa udhaifu nilio nao. Sasa nakwambia tu kwamba mimi namuunga sana mkono Mbowe kama Mwenyekiti wetu, sio kwa sababu yeyote ingine bali kwa kuwa ninaamini kwamba ni kiongozi imara na ana dira anapotaka CHADEMA ifike. Above all, as far as I am concerned, ana commitment kubwa sana kwa maendeleo ya chadema kuliko kiongozi mwingine yeyote ninayomjua ndani ya chadema. Hii haina maana kwamba Mbowe kama kiongozi hana mapungufu; anayo na yanazungumzika na itakuwa ni ujuha kudhani kwamba kuna kiongozi duniani asiye na mapungufu.

Sidhani kila anayesoma maandiko yako anaona uungaji wako mkono kwa Mbowe ni wa kichama tu. Wengine tunaona ni zaidi ya hapo na sidhani kama kati yetu kuna anayeweza kuhakikisha vizivyo mtazamo wa mwingine.

iii) Binafsi sina matatizo na Wangwe au Mziray. Kuhusu Wangwe nimekwisha kusema awali katika post zangu kwamba huyu ni kiongozi imara sana na ni muhimu sana kwa maendeleo ya chadema. Lakini nikasema pia kwamba moja ya tatizo la Wangwe ni kushindwa kuelewa mipaka ya uwezo wake. Mara nyingi hutaka mambo makubwa kuliko uwezo wake, na ni wazi kwamba cheo cha umakamu uenyekiti kilikuwa kizito mno kwake na ndio maana kimemshinda ndani ya muda mfupi alichokishikilia. Katika post zangu huku nimekemea sana tabia ya baadhi ya viongozi wa chadema kujaribu kumrushia matope na ku-demonise Wangwe na nikasema wazi kwamba kitendo hicho sio tu kwamba kinamshushia hadhi Wangwe kama mbunge mbele ya watanzania na wapiga kura wake huko Tarime, lakini pia haikisaidii chadema kwa lolote na linatuweka katika wakati mgumu wa kushinda tena kiti cha ubunge huko Tarime katika uchaguzi ujao.

Kuhusu Mziray, mimi binafsi sina matatizo naye kama mtu, kiongozi na mjumbe wa kamati kuu ya chadema. Ninachosema ni kwamba huyu naye alipewa kazi ambayo ni wazi kwamba ilikuwa juu ya uwezi wake, na matokeo yake kazi aliyeifanya imeonyesha udhaifu wake zaidi kuliko kutatua tatizo alilokwenda kulichunguza.

Tatizo lililopo kwa baadhi ya wana CHADEMA ni kutofuata demokrasia ndani ya chama na badala yake kubagua baadhi ya wanachama, aidha kutokana na elimu zao ndogo au sababu nyinginezo, wakidhani kuwa mafanikio ya darasani tu ndio yanayoonyesha uwezo wa mtu kuongoza. Hili ni kosa kubwa na ndio maana badala ya kupanua mjadala wa aliyoleta mbele Mziray, mnaanza kumkosoa kitaaluma.

Kuna woga ndani ya CHADEAM wa kumpa Wangwe uenyekiti wa chama ikidhaniwa kuwa labda atavuruga na sababu nyingine binafsi za wahusika. Kwani akipewa uenyekiti si bado atawajibika kwa kamati mbalimbali? Kwa nini wanachama wasiamue nani awe nani badala ya kupangana ndani ya Chama na Bungeni kulingana na sababu zisizo za kidemokrasia? Binafsi nafikiri Wangwe anao uwezo na mawazo mazuri mengi tu ambayo kama yakipatiwa msaada badala ya kupingwa tu kila anapofungua mdomo wake, yanaweza kusaidia sana Chadema. He always thinks out of the box, unlike most of the so called learned CHADEMA leaders.

iv) Ni mara chache nimesoma posts zako ambapo humtaji Mbowe. Na kwa kweli, ni mara chache nimekuona ukichangia thread ambayo haihusi mambo ya CHADEMA na hasa Mbowe, sasa on a light touch, may I ask you do you have any personal issue na Freeman Aikael Mbowe?

Nafikri hujasoma postings zangu nyingi sana. Kwa kawaida sina muda wa kuzunguka kwenye kila thread, ila ninapolikamata jambo ni mpaka nione mwisho wake au angalau lifikie sehemu inayoridhisha. Hili la uongozi wa CHADEMA tumelipigia kelele lakini wahusika wamekuwa wakijificha bila kutoa majibu ya kueleweka mpaka data mpya zinapoibuliwa kama hii ripoti ya Mziray.

Kwa mawazo yangu, Mbowe ndio kiini cha mgogoro ndani ya CHADEMA na kwa bahati mbaya wale wanaomzunguka hawalioni hilo. Mbowe is ambitious like any other politician, lakini na yeye pia hajui upeo wake. Nina uhakika anataka kugombea tena uraisi ingawa kwa mawazo yangu ni kuwa hafai hiyo nafasi zaidi ya kupoteza muda kugombea na pia resources za chama. Kwa hiyo anavyokiendesha CHADEMA hivi sasa ni katika mtazamo wa yeye na yeye tu kuweza kuwa mgombea 2010 na sio katika misingi ya kukipanua chama.

Kwa hiyo tunapojadili CHADEMA sijui tujadili nini zaidi ya Mbowe ingawa mhusika mkuu amefanywa kuwa kama vile ni mini-god asiyewajibika kwa mtu yeyote. Hahojiki, hakosoleki n.k., kwa ujumla ni kuwa Mbowe hakosei wala hakuna kibaya anachofanya. Sasa wengine wetu hatuko tayari kuona vyama vya wananchi vinageuzwa kuwa NGOs au falme za watu binafsi.

v) Mimi ni mpinzani mkubwa sana wa watu wanaomwaga sweeping statements au kwa maneno mengine wanaoropoka mambo huku wakijua hawana chochote cha kuthibitisha kauli zao. Sasa unaweza ukaisaidie hii forum kueleza ni kwa vipi mimi ni beneficiary wa teuzi ndani ya chadema kufuatia kauli yako hii: "Only wale ambao ni kati ya beneficiaries, kama Kitila n.k. ndio wanaoweza kuzikubali hizi teuzi zinasoshabihiana na ukabila kuwa ni coincedences".

Sihitaji kwenye hili kuleta solid evidence, ila kwa yeyote yule aliyefuatilia huu mjadala na mingine inayohusu CHADEMA na Mbowe in particular au anayefahamu unakotokea au uhusiano wako na Mbowe, historia ya uanachama wako n.k. ataelewa wazi kuwa kwako wewe kumtetea Mbowe ni zaidi ya ulivyosema hapo juu kwenye kipengele cha (ii). Tutaendelea kukukumbushana kwenye hili kwani sio ajabu hujielewi ili uweze kubadilika na kuangalia demokrasia kwenye misingi yake na sio sababu nyingine zozote.
 
Political structure of Chadema resembles CCM! It stinks!

For CHADEMA to be effective on its drive to bring mageuzi, it needs to revamp its leadership structure and organization.

What Chadema has done is to follow the leadership structure and organization blue print of CCM inch by inch. As a result of this, it has failed to separate itself from CCM and thus being ineffective to bring solid changes to political spectrum fo Tanzania!

Mageuzi si kuingia Ikulu pekee, bali ni mabadiliko ya mfumo mzima wa siasa na uendeshaji wake. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kinabidi kiwe cha kwanza kufanya hivyo,ndipo wengine watafuatilia na Wananchi wanweza kuanza kutofautisha Pumba na Mchele.

Nimewahi kuhoji miaka kadhaa iliopita kuwa siasa za Tanzania ni za mrengo gani baada ya Azimio la Zanzibar na kuja Mageuzi, sikupata jibu la maana zaidi ya watu kudai sisi sasa ni Mabepari na tuna Siasa za vyama vingi!

Mwanzo wa kweli wa mageuzi ya Siasa za Tanzania, utaanzia kwenye mabadiliko ya mfumo na miundo ya vyama vya siasa.

Chadema kiwe cha kwanza kuondokana na mfumowa ki-CCM ambao umelea tabaka la kundi maalum kutawala daima na kufanya maamuzi kwa Taifa zima (wanachama wake)!

Mbowe alipata bahati kuja Marekani wakati wa Uchaguzi wa 2004, je alijifunza yapi? je aliona mkutano mkuu wa chama kupitia kamati kuu na halmashauri kuu za Republican au Democrats zikipanga ni nani awe mgombea uwakilishi wa jimbo u uraisi? Nope!

Structure ya kwetu ni ya Kikomnisti, ile ile ya Wachina, Korea na hata Urusi. Sasa ni vipi mifumo hii ya utendaji italeta maendeleo na demokrasia ya kweli ikiwa Wenyeviti wa Vyama na wale "wateule wakuu" wanapewa nguvu za kufanya maamuzi makubwa kwa kutumia nyadhifa zao?

Kwa mnaoishi Marekani, mwaelewa mfumo wa siasa za vyama. Nguvu za chama na wawakilishi zipo majimboni na si Mkutano Mkuu au Kamati na Halmashauri Kuu!

Ikiwa Chadema itakubali mawazo yangu na kubadilisha mfumo wake ambao umeanza kuleta migooro na ulalamishi wa upendeleo, ukabila, udini na udugu na kuachia nguvu za wawikilishi kukamilishwa na wanachama wake katika ngazi za kata, wilaya hata mkoa, hapo ndipo mageuzi ya kweli katika siasa za Tanzania yatatoka na hiyo itakuwa njia pekee ya kuleta Demokrasia na Maendeleo kwa Taifa.

Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika, Makani, nasubiri vitendo!

Nilichokiongelea Disemba ya 2007, ndicho kilichotokea majuzi kwa Chadema. Swali ni je tulichokuwa tukiongea hapa kilipotelea wapi masikioni mwa Chadema na viongozi wake ambao wote wako humu ndani JF?
 
Mnyika,

Kwa mtaji huu wa uamsho mpya unaniambia kuwa mtaondokana na Kamati na Halmashauri Kuu kufanya maamuzi yote ya kiutendaji katika kata, wilaya na Mikoa?

Jee wnaotaka kugombea uchaguzi katika Kata, Wilaya na Mikoa hawatakuwa na hofu ya majina yao kuchujwa kwenye kikao cha siri cha "Wateule"?

Ni nguvu gani wenyeviti wa Chama wa Mikoa walizonazo katika maamuzi ya Kitaifa na uongozi wa Chama Kitaifa?

Je Watendaji wa Chama katika Wilaya na Mikoa watakuwa huru kuchaguliwa na wanachama wao au watakuwa ni Wateule wa Mwenyekiti na kamati yake?

Je Katiba yenu inasemaje kuhusu kutenganisha kofia? Does the Chairman have to be Presidential Candidate? je Kutafuta Ugombea uraisi, maamuzi ni ya wanachama kupitia nguvu zao za kata, wilaya na mikoa au kila kitubado kitakuwa rolled up to Kamati na halmashauri Kuu ambazo zitawasilisha majina ya mchujo kwa Mkutano Mkuu?

Je hata kama mtabakia na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, mchujo wa wagombea uwakilishi kupitia Chadema utaachwa kwa ngazi husika au kwa wagombea waliopita michujo yote kujinadi mbele ya Mkutano Mkuu na si "Wateule" kuchuja na kuweka watu wanaowataka?

Tuendelee kuelimishana!

Mapendekezo haya yalipuuzwa, sasa mmekivuna mlichokipanda!
 
Sad day for Chadema today. This issue of Wangwe and Mbowe needs to be resovled in Western style, a revolver with five empty chambers!

Sorry for distasteful comment, however I think Chadema needs to restracture its leadership, from the Chairman to the way down.

The appearance of Chadema being a party of Friends and Family of Mtei is going to be the natural cause of Death of Chadema.

Wangwe carries a big constituence and despite the differences, I believe Chadema has failed to sit down and ask itself tough questions what is the fate of their credibility and popularity with this move.

Buriani Chadema, unless the sort of obvious story is that Mwenyekiti is an associate of CCM and he is in CCM payrol!

A day before Zitto could unleash a big speech, and a fight against Ufisadi to carry a momentum, Chadema dares Watanzania by pulling such a foolish stunt!

For the next 180 days, the talk will be about Chadema infighting and not Richmond, IPTL, EPA or Meremeta and CCM will own the debate on Ufisadi!

Kuna swali ambalo Mnyika aliniuliza na sikuwahi kumjibu.

Tetesi kwua Chadema ni chama cha Wachaga hakijaanza jana au juzi. Ni la siku nyingi. Mimi sikioni kuwa ni chama cha Wachaga kwa kuwa binafsi, sina tatizo na Uchaga wala yale ya CUF kuwa cha Wazanzibar na Waislamu, maana sina tatizo na Wazanzibari au Waislamu.

Lakini,taswira ya Chama kuwa ni cha kabila, kundi au dini fulani, si jambo zuri katika uwanja wa Kitaifa kwa maana si kila mtu ataangalia jambo kwa mtazamo wangu. Kupuuzia kwangu ukabila na udini na kuweka nyenzo yangu kwenye ufanisi, si lazima Masanilo, Masatu na Engineer wawe na msimamo sawa na wangu.

Sasa nikirui kwenye hili la Chadema na Uchaga, hili ni kama kidonda sugu na dugu. Limekalia Chadema tangu kilipoundwa na mpaka leo hii, na hivyo linaaminika.

Tofauti na CCM (TAA/TANU-ASP) ambavyo viliundwa kwa msukumo wa Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar waliokuwa wakipigania uhuru na hivyo kuwa na umoja na kuwa Chama cha Watanzania, CHADEMA kiliundwa kwa mkusanyiko wa Marafiki ambao walikuwa wameshibana na waliotumia fursa ya kuanzishwa kwa vyama vya Upinzani, kuunda Chama chao cha Kisiasa ambacho kitawakisha mawazo yao.

Kama Chadema kingekuwa kimeundwa kama TANU na hata CCM ilivyokuwa, ingekuwa ni rahisi sana kuondokana na hisia kuwa ni mali ya Mtei na familia.

Hata pamoja na kuwa CCM kuna mizengwe na kuna wateule, Chadema imeshindwa kujivua Taswira ya Uchaga na Umtei na ukweli umeonekana katika Uchaguzi mkuu uliofanyika majuzi.

HIvyo basi, ile nafasi ya kuwa Chama cha Demokrasia, imepotea kwa kuwa Waasisi na marafiki walioanzisha CHADEMA, hawako tayari kwa Chasaka aje kukiongoza chama chao hata kama wangekuwa na mfumo bora wa kidemokrasia.

Sina tatizo na Freeman, Mtei, Makani hata Zitto kama mtu mmoja mmoja, bali tatizo langu kwao ni wao kama Viongozi wa Chama na jinsi wanavyoshindwa kukijenga Chama chao kiwe ni chama Bora kuliko CCM.

Ndiyo maana matokeo ya Uchaguzi wa CHADEMA 2009, yaminipa jibu moja, kuwa CHADEMA ni chama cha Wababaishaji, sawa na CCM!
 
Mkuu Mkandara,
Kuhojiwa kwa Mbowe ni muhimu sana, sio tu katika kuweka fairness kati ya Wangwe na Mbowe, ambao ndio kiini cha mgogoro wa hivi karibuni, bali pia kutuondolea maswali mengi ambayo yapo vichwani mwetu. Kwa mfano;
  1. Inasemekana Mbowe hakumtaka Wangwe tokea siku nyingi. Akihojiwa atapewa nafasi ya kueleza sababu za chuki yake.
  2. Mbowe inasemekana ndie aliyechomekea suala la kumsimamisha Wangwe. Ni vema akapewa nafasi ya kulielezea hili.
  3. Mbowe ndie anashutumiwa kuteua watu katika misingi ya kikabila, anaweza akaelezea hili.
  4. Ubadhirifu wa fedha nao amelaumiwa Mbowe, anaweza akawasilisha hata balance sheet kujikosha.
  5. Mziray ripoti yake ikakataliwa kwa nguvu ya Mbowe, anaweza akaeleza
Kwa ufupi ni kuwa yapo mengi ambayo Mbowe anatakiwa kuyaelezea ili kuondoa minong'ono na kuweka mambo sawa.

Nimemuahidi MMJJ kumchangia ili aweze kuandaa hayo mahojiano na ningeomba wanaJF tusiyazuie pasipo na sababu. Tumpe nafasi Mbowe aweze kujibu hoja zilizopo na pia kuondoa hii hali ya kumuona yeye kama vile hagusiki.

Mbowe ameiyumbisha CHADEMA toka siku nyingi, sasa imefikia kutumia ubavu wake ndani ya CHADEMA kuondoa wapiganaji kama Chacha, Zitto, Dr. Slaa n.k, na kuwaingiza wala rushwa wenzake, Lowassa, Masha n.k. Ukimlea nyoka lazima akudunge sumu yake siku moja.
 
Hii thread tulijadili 8 years ago na in a very matured way bado nikiwa mwanafunzi. Sasa kuiunganisha na post ile ya leo haifai kama baadhi ya watu wanavyodai kule kwingine
 
Mnyika,

Kwa mtaji huu wa uamsho mpya unaniambia kuwa mtaondokana na Kamati na Halmashauri Kuu kufanya maamuzi yote ya kiutendaji katika kata, wilaya na Mikoa?

Jee wnaotaka kugombea uchaguzi katika Kata, Wilaya na Mikoa hawatakuwa na hofu ya majina yao kuchujwa kwenye kikao cha siri cha "Wateule"?

Ni nguvu gani wenyeviti wa Chama wa Mikoa walizonazo katika maamuzi ya Kitaifa na uongozi wa Chama Kitaifa?

Je Watendaji wa Chama katika Wilaya na Mikoa watakuwa huru kuchaguliwa na wanachama wao au watakuwa ni Wateule wa Mwenyekiti na kamati yake?

Je Katiba yenu inasemaje kuhusu kutenganisha kofia? Does the Chairman have to be Presidential Candidate? je Kutafuta Ugombea uraisi, maamuzi ni ya wanachama kupitia nguvu zao za kata, wilaya na mikoa au kila kitubado kitakuwa rolled up to Kamati na halmashauri Kuu ambazo zitawasilisha majina ya mchujo kwa Mkutano Mkuu?

Je hata kama mtabakia na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, mchujo wa wagombea uwakilishi kupitia Chadema utaachwa kwa ngazi husika au kwa wagombea waliopita michujo yote kujinadi mbele ya Mkutano Mkuu na si "Wateule" kuchuja na kuweka watu wanaowataka?

Tuendelee kuelimishana!
 
Political structure of Chadema resembles CCM! It stinks!

For CHADEMA to be effective on its drive to bring mageuzi, it needs to revamp its leadership structure and organization.

What Chadema has done is to follow the leadership structure and organization blue print of CCM inch by inch. As a result of this, it has failed to separate itself from CCM and thus being ineffective to bring solid changes to political spectrum fo Tanzania!

Mageuzi si kuingia Ikulu pekee, bali ni mabadiliko ya mfumo mzima wa siasa na uendeshaji wake. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kinabidi kiwe cha kwanza kufanya hivyo,ndipo wengine watafuatilia na Wananchi wanweza kuanza kutofautisha Pumba na Mchele.

Nimewahi kuhoji miaka kadhaa iliopita kuwa siasa za Tanzania ni za mrengo gani baada ya Azimio la Zanzibar na kuja Mageuzi, sikupata jibu la maana zaidi ya watu kudai sisi sasa ni Mabepari na tuna Siasa za vyama vingi!

Mwanzo wa kweli wa mageuzi ya Siasa za Tanzania, utaanzia kwenye mabadiliko ya mfumo na miundo ya vyama vya siasa.

Chadema kiwe cha kwanza kuondokana na mfumowa ki-CCM ambao umelea tabaka la kundi maalum kutawala daima na kufanya maamuzi kwa Taifa zima (wanachama wake)!

Mbowe alipata bahati kuja Marekani wakati wa Uchaguzi wa 2004, je alijifunza yapi? je aliona mkutano mkuu wa chama kupitia kamati kuu na halmashauri kuu za Republican au Democrats zikipanga ni nani awe mgombea uwakilishi wa jimbo u uraisi? Nope!

Structure ya kwetu ni ya Kikomnisti, ile ile ya Wachina, Korea na hata Urusi. Sasa ni vipi mifumo hii ya utendaji italeta maendeleo na demokrasia ya kweli ikiwa Wenyeviti wa Vyama na wale "wateule wakuu" wanapewa nguvu za kufanya maamuzi makubwa kwa kutumia nyadhifa zao?

Kwa mnaoishi Marekani, mwaelewa mfumo wa siasa za vyama. Nguvu za chama na wawakilishi zipo majimboni na si Mkutano Mkuu au Kamati na Halmashauri Kuu!

Ikiwa Chadema itakubali mawazo yangu na kubadilisha mfumo wake ambao umeanza kuleta migooro na ulalamishi wa upendeleo, ukabila, udini na udugu na kuachia nguvu za wawikilishi kukamilishwa na wanachama wake katika ngazi za kata, wilaya hata mkoa, hapo ndipo mageuzi ya kweli katika siasa za Tanzania yatatoka na hiyo itakuwa njia pekee ya kuleta Demokrasia na Maendeleo kwa Taifa.

Mbowe, Slaa, Zitto, Mnyika, Makani, nasubiri vitendo!
 
Rev. Kishoka

Kuhusu mageuzi ndani ya CHADEMA tulishaitika mwito huo tayari; mara baada ya uchaguzi mkuu 2005 tulifanya tathmini ya kina na hatimaye tukaandaa Mpango Mkakati(Strategic Plan) ya miaka mitano. Kama sehemu ya Mpango huo tukaamua kubadili Katiba ya chama na kuchukua muundo tofauti kidogo(unaweza kuitazama kupitia www.chadema .net) na kuilinganisha na ya CCM. Ndio maana baada ya hapo tuliamua kuzindua chama upya( bonyeza hapa utapata maelezo yangu kuhusu uzinduzi huo na ni kwa vipi unakifanya CHADEMA kuwa chama tofauti na CCM):

http://www.chadema.net/blogu/mnyika/2006/09/dokezo-kuhusu-uzinduzi-mpya-wa-chadema.html

Kwa hiyo uliyoyaona yametokea 2007 ni matokeo ya mipango na malengo sio bahati nasibu.

Mwaka 2008 ni mwaka wa uchaguzi ambapo tutaunda oganizesheni ya chama kuanzia ngazi ya msingi mpaka taifa, na hata kimataifa; na tutafanya hivi mijini na vijijini. Ni changamoto kwa wanaCHADEMA sasa kuifahamu ratiba husika na kushiriki michakato hii ya uchaguzi na kujenga chama katika maeneo yao.

Kwa kweli tumeamua kabisa kupeleka nguvu zaidi majimbo na hata kupanua uwakilishi wa majimbo kwenye baraza kuu; lakini nguvu za kichama sasa ni katika vitovu vya kimapambano.

Ni hatua nzuri; naamini mabadiliko yanayofuata ya katiba yatatoa mamlaka zaidi kwa ngazi za chini katika kujitawala; ila katiba hii mpya ya mwaka 2006 naamini itawezesha kuwa na muundo na mfumo bora zaidi. Haionekani sasa kwa kuwa mpaka sasa bado tunatumia katiba ya mwaka 2004. Katiba mpya itaanza kutumika mwaka 2008 mara baada ya uchaguzi. Kwa meneno mengine, uchaguzi utakaonza mwezi Februari utaendeshwa kwa katiba mpya ya CHADEMA ambayo imeshazingatia sehemu ya ushauri ambao umeutoa.

Lakini kazi hii si ya kina Mbowe, Makani, Zitto na Mnyika pekee. Ni yako pia wewe na yule. Pamoja tutashinda.

JJ
Mkuu siku hizi "umejificha"..unatumia ID fake kuchangia humu JF.Imekuwaje Lowassa ndiye mjenzi mpya wa chama huku nyie mpo pembeni?
 
Back
Top Bottom