John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
Mnyika
Chama chenu vilevile kinatakiwa kuwa na financial muscle, mmejiandaa vipi kuhakikisha kuwa chama chenu kina pesa za kutosha? au ndio mnategemea tu michango ya wanachama na membership fee. 2010 inaonekana kama iko mbali, lakini kwa uchaguzi iko karibu, mmeangalia weakpoints (zipo nyingi) ambazo mnaweza kucapitalize kwenye viti vya udiwani na ubunge, walau mkaongeza idadi ya wabunge? Au lengo lenu ni kuendelea kuwa na wabunge hawahawa wachache waliopo?
Hili la finnancial muscle naomba nisiingie kiundani. Yatosha kusema tu, tunajiandaa. Ila haiondoi ukweli pia kuwa chama ni cha wanancha, hivyo michango ya wanachama ni suala la lazima kikatiba. Pia, ni jukumu la kila mpenda demokrasia na maendeleo kuchangia mageuzi hata kama hana kadi ya uanachama. Mnavyoviona vinaelea, vimeundwa!. Ama sivyo, nguvu ya wanamabadiliko inaweza kuzidiwa kupindukia kirasilimali na mafisadi wanaotumia kodi zetu hizo hizo na hatimaye ufisadi kuendelea zaidi na kuchota kodi zaidi. Kwa kila senti ambayo inakosekana katika kuleta mabadiliko na uwajibikaji kuna shilingi kadhaa zinazokwapuliwa na ufisadi ama kufujwa kwa matumizi ya anasa. Kumbuka kampeni za kumwondoa mkoloni, pamoja na kuchangiwa na wanachama, TANU ilichangiwa pia na watu binafsi wapenda ukombozi, vuta fikra ni kwa namna gani Nyerere alipata ile tiketi ya kwenda Umoja wa Mataifa- vyema za kadi za TANU hazikutosha, Rupia akaongeza, lakini unajua pia kwamba kuna fungu lilitoka Tanga toka michango wa watu wengine? Sasa jiulize, leo unataka Mbowe, Dr Slaa, Wangwe, Zitto nk waende vijijini- tunajua kwamba fedha za ruzuku pekee hazitoshi, fedha za michango ya wanachama pekee hazitoshi- unashindwa vipi mwananchi, haswa umbae uko middle class ya kibongo- ndani na nje ya Tanzania, kuunganisha nguvu ya wenzako wachache kufanikisha viongozi hawa kuja kwenye kijiji chako cha asili au jimbo lako ulipotoka ukaleta mabadiliko ya kweli? Wakati umefika sasa wa kusimama na kuhesabiwa ama kunyamaza milele!. Hilo la kuweka mkazo kwa ubunge nimeshalijibu kwenye FOCUS 2010. Kilichobaki ni mwitiko tu kwako na kwa mwingine. Pamoja Tutashinda
JJ